Mwanamke usimdanganye mumeo hujazaa!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Muda huu tunapoongelea uhuru wa miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, kuna mwanamke hapa Chan'ombe Dodoma limemshuka, tena looooooooooooooote! Ameolewa ana miaka 9 ktk ndoa yake ingawa hajabahatika kuzaa ktk ndoa yake hii. Mumewe siku zote hakujua kuwa kabla ya kuoana alishazaa mtoto wa 'ujanani'. Hakumueleza mumewe wakati wa urafiki, uchumba na baada ya ndoa. Juzi huyo mtoto wake wa ujanani alokuwa akiishi na bibi alifariki hapa dodoma, hivyo ilibidi mama na mumewe waje dodoma, huku mume akijua kuwa mtoto aliyefariki alikuwa ni wa kaka wa mkewe. Hakukuwa na jipya lililoendelea zaidi ya hali ya majonzi miongoni mwa wafiwa.

Hali libadilika leo asubuhi wakati wa maandalizi ya kwenda kuzika wakati wa kuaga mwili. Mama alipoenda kwa jeneza, si ndo akaanza kulia kwamba anamuachia upweke kwani yeye ndiye alikuwa mwanawe pekee, ataishije bila kuwa na mtoto. Siku zote alikuwa akijivunia kuwa mzazi sababu ya yeye ingawa alikuwa akisemwa hazai na watu na majirani. Minong'ono ikawa mingi pale msibani baada ya kuona ameng'ang'ania kwa jeneza zaidi ya dk 5 ambapo ililazimu watu waende kumuondoa ili taratibu za mazishi ziende kama ilivyopangwa.

wakati minong'ono ikiendelea ndipo mumewe alipojua na kuthibitish kwamba kumbe mtoto aliyekuwa akimjua kama mpwa wa mkewe, ukweli alikuwa ni mtoto wa mkewe. Jamaa alimaindi sana, na nusura aondoke msibani ila busara ya wazee ilisaidia jamaa abaki msibani na kuendelea na mazishi. Ajabu mara baada ya kurudi mazishini, pamoja na juhudi za wazee na ndugu kumuomba baki ili waliongelee hilo, jamaa alifungasha vitu vyake na kurudi dar, pamoja na juhudi za mkewe kumsihi ili wamalize issue hii kabla ya kurudi zao dar na mumewe. Hakuna nayejua nini kitafuatia baada ya 'aibu' hii kujulikana.

My take: Chondechonde kina dadana wanaume pia, kama mtu kakupenda epuka kumdanganya issue ambazo ziko wazi kama hii au kabila yako. Mambo hayo hayana kificho yatakuja julikana tu. Na ukweli utakapojulikana utakosa pa kuuficha uso wako.
 
Kuna kabila moja so far ndio nimekuja ku conclude wana hiyo tabia saaana. Wakizaa ujanani wanaficha kuanzia mimba mpaka mtoto. Jirani yetu alikuja kujua mtoto wa mkewe siku binti anafunga ndoa; MC akasema mama wa bibi harusi, kasimama mama ambaye sote tulijua ni dada yake na ndo alomlea watu wakabaki midomo wazi. From there ndo tukajua kumbe alikuwa mtoto wake. Mumewe alimind kishenzi ila ndio hivyo walishakaa kwenye ndoa more than 20 years na wana watoto wengine.

Nina rafiki yangu nae watu wanasema chini chini (wamejua from reliable source) ana mtoto alimzaa akiwa form two; nayo ni siri sirini. Na alikuja kuolewa na kuachika bila ku mention kuwa ana mtoto. Sasa ana mtoto mmoja kwa ex hubby wake.

BUT it is not fair kwa hao watoto wanaonyimwa haki ya kuita mama zao "Mama" very selfish behavior indeed!
 
dunia bado inakua na sijui huwa kama wana amani moypni maana ni kama wamejibebesha mzigo mzito ktk maisha yao. Muda wote wanakaa wakipanga mikakati ukweli usijulikane huku mtoto naye akinyimwa haki yake ya kujua ukweli wa maisha yake
 
Yaani mi kila siku nasema wanaume huwa wanajidai wajanja ila wakitendwa wanajiskia wameonewa! With current relations, mi sizimii wala kustuka aisee. Nina ndugu aliwahi kuacha shule form 2, akaishi na mwanaume na kuzaa twins bahati mbaya wakafariki na wakaingilia kumrudisha yule dada shule.

Yuko married, mume ana wivu kama kichaa na ndugu tunaambiwa tukae mbali tusije tukamfundisha mkewe tabia mbaya na tamaa. Yeye mwenyewe huwa anacheka anasema ' hajui mie ndo mwalimu mkuu wa tabia mbaya maskini'.

Mshkaji wangu alioa mzulu, alikuja gundua kumbe mtoto alieambiwa ni wa dada alikua ni wa mumewe baada ya mama mkwe kufariki na kuwalazimu kukaa nae.

Ndyoko, cases ni nyingi tu! Binamu yangu alikaa russia na married woman for 5 yrs, wakazaa na mtoto. Dada akija likizo kwa mumewe kimyaa, mwanaume anabaki na mtoto.

Bahati mbaya lakini nzuri kwao yule kiddo akafariki. Wamerudi nchini kimya as if nothing happened! Issue ni usipate wazimu na mwenzio. Siku yakifunuka u cross the bridge there and then, period. Maisha mafupi haya, usijitie wazimu.
 
Issue nayoona hapa si kumdanganya mwanaume ila ni kumyima haki mtoto ya upendo wa mama; that's all. Wanaume wala siwahurumii kihivyo maana wako wengi wanazaa nje, ambao huwezi linganisha na kosa la wanawake wanaoficha watoto wa ujanani.
:mvutaji:
 
ni makabila gani yanaongoza kwa kuficha ukweli? hili ni muhimu kulifahamu ili mtu unapotafuta mchumba ukidondokea kwenye hilo kabila ufanye full check up....nyumbakubwa tufahamishe pls..
 
Nikiwataja watantoa roho, lakini nawajua several wa kabila hilo hilo.

ni makabila gani yanaongoza kwa kuficha ukweli? hili ni muhimu kulifahamu ili mtu unapotafuta mchumba ukidondokea kwenye hilo kabila ufanye full check up....nyumbakubwa tufahamishe pls..
 
Huyo mwanaume nae hovyoooo......kususa msibani maana yake nini sasa?? Au alidhani yale aloambiwa ndo yatageuka miujiza?? Atleast hata mwanamke hakughasi kwa malezi, kuna mijanaume mingine inasubiri mpaka ikishakuweka ndani ndo unaanza kuletewa orodha ya watoto, mmoja baada ya mwingine utadhani unasajili wacheza mpira bana!!! Sio issue kabisa waungwana, kutakiana lawama tu!
 
Nikiwataja watantoa roho, lakini nawajua several wa kabila hilo hilo.
hakuna kukutoa roho maana hapa tunajadiliana na kusaidiana pia. kama ukiwataja hata wao watafurah maana watajua kuwa udhaifu wao umefahamika na wataanza kujifunza na kuwa wawazi kwa wapenzi wao kabla ya kufunga pingu. tafadhali funguka....
 
ni makabila gani yanaongoza kwa kuficha ukweli? hili ni muhimu kulifahamu ili mtu unapotafuta mchumba ukidondokea kwenye hilo kabila ufanye full check up....nyumbakubwa tufahamishe pls..

We ndo ushaanza kuogopa hivyo! Sasa ukitajiwa kabila na ukakuta mpenzi wako amehusu huko, ndo kusema unapiga tipa?? LOL
 
Kuna raha ya kuoa mtu Bikira,au uwe wa kwanza, ukiacha hzo za kichina ile Original yenyewe. Mambo kama haya utayasikia kwa wengine tu.
 
siku hizi hata wanamme wanaficha watoto.
Kuna case moja wameoana, kaka ana mtoto wa nje hajamwambia mkewe. Bahati mbaya hadi leo hawajajaliwa kupata mtoto kwenye ndoa. Yule kaka kauza mechi mtaani kwa manamke mwingine naya kapata ujauzito.
Mkewe hajui chochote hata yule wa ujanani hajui.
duh yaan mie sielewi hii ya kuficha watoto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom