Mwanamke: Unatoka mtoko wa kwanza halafu unakutana na karaha hizi….!

1. Si mkweli ntampotezea baada ya hapo
2. Mh anamatatizo huyo!
3.Bado anampenda X wake
4.Ntamueleza kuwa tumbo ngashtuka labda menu haikuwa sawa
5.Ni mtu wa watu au hajachukulia serious mazungumzo yetu, au anawathamini sana marafiki, hana prog settled
6.Hapo ?? kwa mazoea yapi?
7.Nampotezea ghafla
8. mh hapo napo !
9.Labda off Dar zone kwa Dar si rahisi kukosa sehem kabisa
10. Mh hapo pagumu!
 
Nakuwa mpole na makini kumsikiliza
Ingawa moyoni nishakeleheka Namba 1,2,3..............................
Huo ndio utakuwa mtoko wangu wa kwanza na wa mwisho
Nakata mawasiliano
 
Mtambuzi
Namba moja inahusu sana nakupa wakati bado sijawa mrs sweetheart nilipata kidate kama hicho
oooh mama sitaki kukumbuka
 
Last edited by a moderator:
1,6,7 aisee unatamani ungekuwa umevaa bomu ulipuke nae..
1. Et nnae but sina future nae,huku anapigiwa simu unamuona anavyo-vibrate!
6. Yan hachelewi kukukiss na kukuita bby,wkati hata hujamkubalia, mara akiongea na simu nipo na myheartbeat(aisee nilimkata jicho,nlitaman kumpgia ukunga wa mwizi)! Na hivi alishaniboa!
7. Akaanza story oh mymom,blah blah mydad fyoko fyoko,mara mimi nlikuwa wamwisho darasani!.
Nlipolegea, oh gari ya shemeji(mmewe dadake)ananiazimaga!
Aisee wakat ukimuangalia unasema juan miguel,ver smart,kumbe kichwa kina popcorn!
Wat i did, nlmtxt mtu anipigie kuna emergence,nkatimka kama Ambulance iliyobeba majeruhi!

Hahahahahhaaa!!!!umenikumbusha mbali sana eti mke wangu hakua chaguo langu alipata mimba bahati mbaya ikabidi niishi nae SASA MBNA UMEVUA PETE??? unajua nlijua nkikuambia nimeoa ungekataa kutoka na mm..!!!yn hapo ni samahani kaka ndo ushaharibu kwa herii...huyooo!!!!!
 
Aaaah wapi enzi zetu tulizoea sarakasi za chagulaga na niangusage unadhani hayo mambo ya kukaa na mwanamke bila kupiga game kwa miaka ile ya 70, ungeonekana joka la kibisa, lakini tofauti na miaka hiyo ya 70, siku hizi vijana hunachukulia mambo kistaarabu baada ya kujifunza kwa kuangalia tamthilia... vijana wa siku hizi wanaweza hata kulala kitanda kimoja na mwanamke bila hata kugusana... Si unajua vijana wa siku hizi mpaka kupasha kwa supu ya pweza, wakati enzi zetu ngoma ilikuwa inasongesha kwa nguvu zake naturally bila kutumia miundo mbinu...... LOL

mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
black-couple-at-lunch-madame-noire-e1348545911944.jpeg


Mtoko wa kwanza huwa unawaweka wanawake katika wakati mgumu ukilinganisha na wanaume. Wakati wanaume kwao sio tatizo kubwa la kuwaumiza vichwa, kwa wanawake huwa wanajiuliza maswali mengi sana kuhusiana na huyo mtu anayekwenda kuonana naye.Hebu tuchulie mwanamke ametoka na mwanaume kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufahamiana na kuangalia kama anaweza kuwa na muafaka na mwanaume huyo kwa matarajio ya kujenga familia bora. Lakini kinyume chake anakutana na karaha hizi zifuatazo. Je kama ni wewe mwanamke unakabiliana na hali hii utafanyaje?

1. Unagundua kwamba mwanaume uliyetoka naye ana mke au ana mpenzi wake..

Baada ya kufika kwenye mgahawa kwa ajili ya kupata mlo wa usiku pamoja, katikati ya maongezi yenu mwanaume huyu anakushika mkono kama ishara ya upendo wakati mkiwa mmekaa mezani. Unapochunguza vidole vyake unagundua kwamba ana alama ya pete ya ndoa, unapomdadisi anakanusha, lakini baada ya kumbana sana anakiri kwamba anaye mke lakini ndoa yake ina vurugu na inalegalegakiasi kwamba siku oyote itavunjika. Au wakati wa maongezi yenu anakiri kwamba anaye mchumba wake, lakini hadhani kama atamfaa ingawa bado wako pamoja. Je utafanya nini?
Hiyo ndio itakua date ya kwanza na ya mwisho

2.
Anakunywa kupindukia mpaka anashindwa kumudu mazungumzo…

Baada ya kupata mlo mnahamia kwenye baa ili kupata vinywaji kidogo kabla ya kuachana, mkiwa hapo baa, mwanaume huyo anakunywa pombe kupita kiasi mpaka anaashindwa kumudu mazungumzo na kuongea pumba tupu.
Mlevi wa kunipa pressure wa kazi gani> Ikiwa kashindwa kuji control ulevi siku ya kwanza, mbele ya safari itakuaje? Hafai...


3. Anatumia muda wake mwingi kumzungumzia mpenzi wake waliyeachana..

Inawezekana katika mazungumzo yenu unamuuliza sababu ya kuachana na mpenzi wake wa zamani.. mwanaume huyo anatumia muda mwingi kumzungumzia mpenzi wake huyo na anaonyesha dalili za dhahiri kwamba ana m-miss
Hafai pia... ndicho alichotaka kuniona ili anisomee mashairi ya mpenzi wake wa zamani. Nitamwambia apotee kwanza hadi amsahau huyo wa zamani ndio anitafute
4. Baada ya kupata mlo, tumbo lako linaleta kisirani
Labda chakula ambacho umekula hapo mgahawani hakikupatana na tumbo lako, ghafla unapatwa na tumbo la kuhara kiasi cha kujikuta ukipiga trip kadhaa kwenda maliwatoni, mpaka mwanaume huyo anakuuliza kama una tatizo. Je ungejibu nini? Nitamjibu tumbo limechafuka maana sioni kwanini nimfiche wakati naumwa

5. Marafiki zake wanajiunga nanyi..
Wakati mnapata chakula na kuongea kwa bashasha, mwanaume huyo anapigiwa simu na marafiki zake ambapo anawaelekeza mlipo. Ghafla marafiki hao wanakuja na kujiunga nanyi kwa ajili ya kupata mlo mkiwa pamoja. Je ungefanyaje? Nitakaa, lakini baada ya hapo lazima nimpe za uso, marafiki wanahusu nini first date..?

6.
Anakuwa na shauku kubwa na mwili wako.

Wakati mkiendelea kupata vinywaji baada a kumaliza kula, mwanaume huyo anaanza kukushika shika mwili wako mara kwa mara hususan sehemu zako za faragha huku akikupiga mabusu motomoto kiasi cha kukukera. Je utafanya nini? Nitaachana naye maana interest yake nitaona ni hiyo. Mwanaume mwenye nia nzuri na wewe hawezi kukufanyia uhuni huu

7. Unagundua kwamba siye uliyemtegemea..
Mlipokutana kwa mara ya kwanza ulimuona alikuwa ni mwanaume mzuri wa sura na umbo, mpole kiasi, mcheshi, mwenye utani mwingi na mwenye uelewa mpana. Na hizo sifa ndizo zilizokuvutia kwa jicho la kwanza na ndio ikawa ni sababu kwako kukubali kutoka naye ili mpate kufahamiana zaidi. Lakini mkiwa hapo kwenye mghahawa unagundua kitu tofauti. Wakati wa mazungumzo yenu unagundua kwamba si lolole wala chochote. Jamaa ni mweupe hajui kujieleza ana ubishi usio na maana na anayependa kujikweza tofauti na hali aliyo nayo. Lakini pia unagundua kwamba ni mwongo na asiyepima uzito wa kauli zake. Kwa kifupi ni mropokaji…. Je ungefanyaje? Roporopo wa nini asojua anachooongea. that will be the first and last date. Akatafute mbishi mwenzie.

8. Mpenzi wako wa zamani mliyeachana kwa kisirani ni mjomba wake…!
Wakati wa mazungmzo yenu hapo mghahawani unagundua kwamba ni mwanaume mwenye muafaka na anayefaa kuitwa mume. Ni mtu ambaye mnaendana kwa kila kitu, ni msikivu na mwenye subira na asiye na papara. Lakini katika mazungumzo yenu kuhusu familia zenu unagundua kuwa mpenzi wako wa zamani ambaye mliachana miaka kadhaa iliyopita kwa vurugu kubwa na kuwekeana visasi ni mjomba wake. Huyo mjomba wake anaishi mkoa mwingine na ulikutana naye wakati ulipokuwa ukifanya kazi katika mkoa huo kabla ya kuacha na kuhamia mkoa mwingine. Je utafanya nini? Sioni sababu ya kutoendelea nae kama nimehisi ananifaa maana huyo ndugu ni mjomba na si kaka ywa kuzaliwa nae. Labda yeye ndio abadili mawazo

9. Kila kitu kinaenda kinyume na matarajio yenu…
Kuna wakati huwa tunakutana na visirani mpaka tunajiuliza tulikanyaga mdudu gani siku hiyo… Inaweza kutokea mpenzi wako kafanya booking ya meza kwenye mghahawa kwa ajili ya dinner, lakini mnapofika mnaambiwa meza yenu wamepewa watu wengine, mnaona kuliko kulalamika itakuwa ni kupoteza muda bure kwa kuwa maji yameshamwagika. Mnaamua kwenda katika mghahawa mwingine, lakini kwa mshangao mnakuta napo pamejaa, manaanza kuingia mghahawa mmoja baada ya mwingine lakini kote mnakuta kumejaa. Je mtaahirisha au mtaamua kwenda nyumbani kwa mmoja kati yenu kwa ajili ya kuendelea na mtoko wenu? Tutaahirisha siku hiyo, kila mmoja arudi kwake, tutapanga mtoko siku nyingine, maana mabalaa mengine mnaonyeshwa mapema, huwezi jua mbele ya safari kungetokea nini. Hivyo bora kila mmoja arudi kwake kulala

10. Unagundua kwamba pamoja na kuwa na mwili mkubwa kumbe jamaa ni mdogo sana kiumri ukilinganisha na umri wako…
Kuna watu wamejaaliwa kuwa na miili mikubwa, ukilinganisha na umri wao. Hiyo iko kote kote, si kwa wanawake wala wanaume. Kwa mfano inatokea mwanaume uliyetoka naye wakati wa mazungumzo yenu unakuja kung’amua kwamba umri wake ni mdogo sana tofauti na muonekano wa mwili wako. Mwanaume huyu anazo sifa muafaka za kuweza kuitwa mume, lakini umri umemzidi sana kiasi cha miaka mitano. Je utaendelea kuwa na uhusiano naye au utajitoa mapema…?.” Kama yeye hatojali kuhusu umri, sioni sababu ya mimi iwe sababu, umri ni namba tu, most important ni tutaelewana vipi.
 
Baby Boy anaendelea vizuri tu kachangamka kama mimi baba yake...
Nashukuru kama hamna njama hizo maana kina gfsonwin, BADILI TABIA, Madame B, lara 1, nyumba kubwa, sweetlady, na viherehere wengine wameniambia itabidi nisubiri mpaka miezi sita ndo nisongeshe... Si nitakufa jamani...
We fikiria nili stop hako kamchezo three months before, ukimjumlisha na miezi sita jumla miezi tisa.....mama weee nafa mwaka huu............LOL



hahhahahaaa miezi sita mingi mno, akipona vizuri miezi mitatu tu unapiga mzigo
 
Last edited by a moderator:
ooh yah...nimekumbuka kweli uliwahi kuweka......lakini kitu hiki huwa kinakera sana.....
unatoka na mtu first date.....tuseme ndio mwanaume ameitisha hicho kikao.....then wakati wa kulipa anaanza kuzungusha macho kama kinyonga....hii kitu huwa inaniput off kabisa........

Preta,
mwanaume akizungusha macho na wewe zungusha macho......
Ukinialika kidate shurti ulipe, nitalipa kama tu mimi ndo nimekualika......

Na kama akijifanya hamnazo nitalipia nilichokula mie tu then nasepa, baada ya hapo asahau, hata salamu hatopata
 
Last edited by a moderator:
BADILI TABIA yaani hapo umejibu vizurije, yaani hapo mia ya mia.......
Kuna swali nitakuuul;iza baadae, ngoja nakunywa kahawa kwanza.........LOL[/QUOTE]

poa poa
 
Last edited by a moderator:
Ndio shida ya kudate tayari mtu ukiwa kazini....

Ni ngumu kujuana na mtu through outing...

Ni ngumu kujua details za mtu anayefanya kazi next office...

Mi sijawahi kutana na hii changamoto kwani wangu tulikutana chuoni...hivyo haikuwa tabu kupata full details...ukizingatia vyuoni kuna wambea wa kutosha.

Kwa wasiojali mambo ya ku chop his money...college ni mahala pazuri pa kupata wenza.
 
Baby Boy anaendelea vizuri tu kachangamka kama mimi baba yake...
Nashukuru kama hamna njama hizo maana kina gfsonwin, BADILI TABIA, Madame B, lara 1, nyumba kubwa, sweetlady, na viherehere wengine wameniambia itabidi nisubiri mpaka miezi sita ndo nisongeshe... Si nitakufa jamani...
We fikiria nili stop hako kamchezo three months before, ukimjumlisha na miezi sita jumla miezi tisa.....mama weee nafa mwaka huu............LOL

Hahahaha Mtambuzi huna ujanja itabidi usubiri tu lol.......hata ukituita viherehere ukweli hauwezi kubadilika!
 
Last edited by a moderator:
mmh, mapenzi hayana formula kihivyo

na kila mtu ana vitu anaweza vumilia mwingine hawezi.

Sigara, big turn Off, serengeti boys over my dead and rotten body, mlevi ohh pulizz

mengine naweza beba strategically.
 
Dah! Mi sifanyi mtoko na mtu hadi nimfahamu vizuri kabisa... Kwa namba 1 na 10 nitakuwa nimeshayajua before.
2,4,6 nitafanya uamuzi wa kuondoka mapema kabla ya muda. 3 nitabadilisha story kabla cjaboreka.
5 nitafurahia uwepo wa marafiki zake maana najua story zitanoga. 7, 8 na 9 baada ya hapo hatoniona wala kunisikia tena.
 
Back
Top Bottom