The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Najua na kuamini kwamba binadamu tumetofautiana kwa kiwango kikubwa lakini sijui hasa wanawake wengi wanapenda sifa zipi awe nazo mume ili waweze kuridhika na pengine kuishi kwa furaha. Najiuliza sana swali hili, pengine dada zangu jamvini mtanisaidia zaidi "from the original..."
Nimewahi kushuhudia dada mmoja, mke wa mtu anakuwa na boyfriend kwa muda mrefu kweli nje ya ndoa yake na inadaiwa kazaa naye ama mtoto au watoto wawili akiwa ndani katika ndoa na mume mpole, very caring (katika mazingira ya kawaida - chumbani sijui..), good provider na ustaarabu mwingi kwa ujumla. Angekuwa na fedha nyingi zaidi nisingeshangaa kumkuta huyu dada anamiliki Gulf Stream.
Tatizo na kinachoshangaza zaidi dada huyo kaachana na huyo boyfriend aliyemzalia mtoto na badala ya kutulia ndani ya ndoa yake sasa anaruka na bwana mwingine tena mume wa shoga yake. Wamejiacha kama hawana ndoa zao vile, mpaka huyo mke wa huyu bwana analalamika hovyo na kuishia kudundwa na mumewe (sijashuhudia hili). Kwa ustaarabu wa yule bwana (Mume Mwema) nilitarajia awe bwana wa mwisho kabisa kutendewa uasi huo na mkewe kwa kuwa anamfaa sana. Cha ajabu anatendewa ndivyo sivyo kuliko mabwana wengine ambao ni "vya-pombe" na sketi - mtu huko katika mabaa na viwanja vingine. Kwa jamaa yangu huyu mambo yanafanywa waziwazi mno!
Kwa mfano wa dada huyu mume angekuwa vipi ndiyo angetulia na kupunguza kujidhalilisha kiasi hicho machoni pa watu?