Mwanamke: Unajua ni kwanini wanaume hupenda kuangalia wanawake hata wawapo na wapenzi wao?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398

Inatokea unapata mtoko na mpenzi mpya na baada ya kubadilishana anuani za mawasiliano zikiwemo zile za mtandaoni unapata tashwishwi ya kuingia katika ukurasa wake wa facebook. Lahaula, huko unakutana na picha kedekede za wanawake warembo hasa na wenye sifa za kugombea mashindano ya ulimbwende.

Unashikwa na udadisi na siku mnapokutana swali lako la kwaza ni kutaka kujua wale ni akina nani. Na yeye bila ya wasiwasi anakujibu kwamba ni marafiki zake tu wa mtandaoni na wala hajawahi kukutana nao zaidi ya kuwasiliana kwa njia hiyo ya mtandaoni.

Lakini kama mjuavyo wanawake walivyo, majibu hayo hayaoneshi kumridhisha, hivyo anaendelea kudadisi zaidi ili kujiridhisha, na si ajabu maswali yakawa mengi kulingana na namna majibu yatakavyokuwa.................

Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa mwanamke kupokea majibu mepesi hasa pale linapotokea jambo analolitilia mashaka, ni lazima atahisi kuna kitu kinaendelea..............

Wakati mwingine inaweza kutokea mwanamke yuko na mpenzi wake wamekaa mahali au wako kwenye mtoko, mara akapita mwanamke, na ghafla akamuona mpenzi wake anageuza shingo na kumkodolea macho, wakati mwingine mwanamke anaweza kupuuza, lakini inaweza kutokea kila anapokatiza mwanamke katika eneo hilo, mwanaume anageuza shingo na kumkodolea macho.................

Kitendo hicho kinaweza kuibua maswali kutoka kwa mwanamke. Na kama mwanaume asipotoa majibu ya kuridhisha kwamba ni kwa nini macho yake yako juu juu kutazama wanawake, kuna uwezekano wa kuzuka tafrani.

Hebu ngoja niwamegee siri, sababu inayotufanya tuwe tunawaangalia wanawake hususan wanawake warembo ni kwa sababu wanaume wanapenda kuangalia wanawake warembo. Wanaume huwa tunapenda kuangalia picha za wanawake warembo, senema zinazoonyesha wanawake warembo, mashindano ya ulimbwende yanayoshirikisha wanawake warembo, yaani tumezaliwa na kukuzwa kwa umri na kimo katika mazingira hayo....

Wanawake, kamwe msidhani kwamba kuwakodolea macho wanawake warembo na labda kutokwa na udenda ndio tunataka kulala nao..... La hasha, tunasafisha kiwi cha macho tu na maisha yanaendelea…………..

Ni vyema jambo hilo mkalichukulia kama kitu cha kawaida. Kama utakuwa na mpenzi ambaye haangalii wanawake warembo wapitao mbele yake. Bila shaka utakuwa una mpenzi au mume mwenye kasoro.... huyo hatakuwa ni mtu wa kawaida.........!

Hatuna mawasiliano nao, wala hatufanyi kitu chochote na wao, zaidi ya kuwaangalia tu na kuwaacha kama walivyo, sasa ya nini mpate jakamoyo na kujipa presha.

Wanaume tunapenda kuangalia wanawake, yaani hilo halina mjadala, inabidi tu mkubaliane na hali halisi kwa hiyo siku nyingine ukimuona mpenzi wako au mumeo anaangalia wanawake warembo wala usijisumbue kugombana naye kwa maswali kwani hali hiyo itamfanya wakati mwingine awe anakandamiza hisia hizo za kuangalia wanawake wengine na kama mjuavyo mtu akikandamiza jambo kwa muda mrefu mwishowe hulipuka na ushawishi wa kwenda mbali zaidi unakuwa ni mkubwa. (kukandamiza maana yake ni kujizuia kwa nguvu zote kufanya jambo au kitu ambacho unatamani sana kukifanya kwa kuhofia kama watu waliokuzunguka watakuonaje, kwa mfano kufanya ngono, kunywa pombe, kuvuta sigara, nk).

Hivyo basi msije tutoboa na vidole vya macho, kwani mwanaume anapowaangalia wanawake warembo huwa anaishia kuangalia kwa macho tu, lakini moyo wake uko kwako...............LOL

 
Hata kama ndo mmeumbwa hivyo kwa nini usimuheshimu mpenzi/mke wako japo kwa huo muda ambao upo nae? Hivi kweli umekaa na mpenzi wako halafu unageuza shingo kumsindikiza mwanamke aliyepita kwa macho?tabia mbaya! Muwe mnawaheshimu mlio nao!
 
Unajua tunataka kuona kaficha nini hapo juu ya skirt, huwa tunawaza kuna kitu tofauti na cha uliye naye na ukiniachia tu lazima nikachungulie mgodi.....
 
Ni vigumu kwa binadamu kukubali ukweli laikini kwa hili la wanaume kuwaangalia wanawake wanapokuwa na wenzi wao halina ubishi. Hata wewe mwanamama ukipita na mumeo halafu wanaume wengine wasikuangalia lazima utakuwa na kasoro
 
Mtambuzi hii ni ngumu sana kueleweka kwa wanawake. Hii inatokana na ukweli kwamba hata wewe huyo uliye naye kabla ya kumtongoza ulianza kwa kumwangalia kwanza, so it's the way towards.........
 
Halafu kinachonikera unakuta jianaume linakuangalia kifuani bila hata aibu

Sasa mnapoacha matiti wazi huku mmeyapaka mafuta yang'ae kabisa mnategema nini?waacheni waangalie!WANAUME ANGALIENI MWAYEGO!
lakini hata sisi tunawaangalia kwa kijicho pembe bila wenyewe kujua kwa hiyo ngoma droo!
 
Macho yanafanya kile moyo unachoelekeza
Ni kweli Mtambuzi ni ngumu sana kukutana na demu mkali as mwanaume halaf usimwangalie..
Kujizuia usiangalie ni kuiumiza nafsi tu..
Sometimes we should let ourselves listen to our heart!
 
Last edited by a moderator:
Sasa mnapoacha matiti wazi huku mmeyapaka mafuta yang'ae kabisa mnategema nini?waacheni waangalie!WANAUME ANGALIENI MWAYEGO!
lakini hata sisi tunawaangalia kwa kijicho pembe bila wenyewe kujua kwa hiyo ngoma droo!

duh maskini! umekosa like yangu kwa sababu ya mchina!
well said either!
 
Kumwangalia demu mwingine mara nyingi inatokea involuntary...yani wadada haswa wazuri wanakuwa kama wanasumaku vile unajishtukia umekodoa tu mimacho..kama ni demu then ukipita kwa ma-meni alafu wakaushe kama vile ajapita mtu,inabidi ujiulize mara sita sita.
 
Huu uzi ushaniletea matatizo..............!
Niliuacha wazi kwa PC yangu na mama Ngina keshauona, nishatwangwa na SMS kali, kabla sijafika home...............
Nitawasimulia yaliyojiri kesho.
 
Hata kama ndo mmeumbwa hivyo kwa nini usimuheshimu mpenzi/mke wako japo kwa huo muda ambao upo nae? Hivi kweli umekaa na mpenzi wako halafu unageuza shingo kumsindikiza mwanamke aliyepita kwa macho?tabia mbaya! Muwe mnawaheshimu mlio nao!

Nyie mnasema nyie... Kuna wakati uko na mamaa demu anapita
ana ushape mpaka wife mwenyewe anageuka anaangalia yaani mnakuta wote mnaangalia alafu we unarudisha shingo lakini unakuta bado wife anaangalia ushepu afu akimaliza anaguna.. Jamani kuna vitu vimeumbwa dunia hii msifanye mchezo
 
Kwakweli lazima tustaajabu kwa alichokiumba Mungu na tusifu na kutukuza kazi za mikono yake hii inatuweka mbali kutenda dhambi ya kutotii amri yake ya USITAMANI MWANAMKE ASIYE MKE WAKO
 
Back
Top Bottom