Mwanamke ni nani?

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,586
Kwangu mimi mwanamke ni kiumbe mzuri anayehitaji uwe na akili kuishi naye, pia aliumbwa na Bwana kwa matumizi ya asili na sio vinginevyo (soma warumi 1:26). Japokuwa kuna wakati huwa tunakoseana lakini bado nawapenda na kuthamini uwepo wao ktk maisha yangu maana bila kusameheana hapana familia wala taifa imara. Je wewe kwako mwanamke ni nini?
 
safi tena ni bora akalegalega mwanamme angalau familia yaweza kusonga ila akilegalega mwanamke familia haiendi popote.
ukirudi nyumbani nyumba safi, chakula kimepikwa vizuri, watoto wameoga na madaftari yamekaguliwa, kilichobaki ni kumpiga mabusu mamsapu tu maana hamna namna.
 
ukirudi nyumbani nyumba safi, chakula kimepikwa vizuri, watoto wameoga na madaftari yamekaguliwa, kilichobaki ni kumpiga mabusu mamsapu tu maana hamna namna.
teh teh kwa kweli kwa mwenendo huo mwanamme utaishi kwa miaka mingi na kwa amani.
 
hongera, tena huwa akipenda anapenda kweli ila kama hakupendi bhasi hakupendi kweli hata umshawishi sana utaishia kudanganywa tu.
kweli kabisa mwanamke akikupenda kakupenda, hata uwe mpiga gambe kama mimi akikupenda kakupenda aisee.
 
Mwanamke ni mzazi,mama,mlezi,mshauri,mwalimu,rafiki,mke na malkia wa nguvu!

Ila huyo mwanamke ukimkoroga maini,ni jambazi,adui ma kiumbe mkatili toka kuumwa hawajawahi tokea!!!na hatotokea kama yy!
duh hatari, akikorogwa anageuka mbogo bhasi wanaume wamesikia.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom