Mwanamke ni lazima apigwe na mume, “lau kidogo”…………..!

Kipipi,

Hakuna anayevumilia kipigo au manyanyaso kwa sababu eti anapenda au anaridhika..

Ukishaingia kwenye hiyo biashara, ndipo unapongundua kwamba ina complications zake.

Naomba tu niishie hapa ila ukweli ni kwamba biashara ya ndoa ni ya ajabu sana!

Babu DC!!

Nakwambia hivi babu DC, hata kuwe na complications za aje au situations zozote.....kichapo kwangu hapana aisee! Hongera zao wenye kuhandle hali kama hiyo ili kutunza ndoa zao, wao waendelee tu na waitwe wake wema.....mie sitaki kabisa hata kuambukizwa chembechembe za namna hiyo!!
 
kipigo kinadumisha ndoa?hii kweli brand new! Cjawahi kuwaona wazazi wangu wakidundana na ndoa yao imedumu miaka yote hii,2sipotoshane jamani

mama isaac Mlugu anaona anachoongea ni sahihi KWA SABABU NI MTU KUTOKA MKOA WA MARA. tehe tehe heee.
 
basi kama ni hao nikiri huyu bwana kitalolo ana matatizo ya akili...

mwanamke anajiheshimu mke wa mtu akifanya upuuzi kama aliofanya mke wa kitalolo mabuti,vifuti,ngumi,vipepsi,vibao ni halali yake....

tena hakika nakuambia....mie shoree wangu yoyote awaye na afanye ujinga huo....lazima awe punching bag....na baadae anakula kibuti.......

hivi wewe mkeo akuambie mbele za mashosti wake nyoooo mwanaume uwe wewe?? usioweza shughuli.....aaah aiseee unategemea nini hapo???? nimpige na kitenge kama msemavyo?


Ha ha ha ha ha,Katika michango yooote naona huu wako Mkuu ni Realistic!! Mwanamke Mnyenyekevu,asiye na Kiburi na Mwenye Hekima hawezi kuviona viganja vya Mume wake isipokuwa wakati vikimpapasa,Kinyume chake Mwanamke ambaye hana hekima katika kauli na Matendo yake lazima atapata Kibano!!

Kwa mfano,huyo mke wa Kalolo,Mimi ningemtandika Fimbo yeye na huyo hawara yake na angeondoka kwangu na vitu vile tu ambavyo amekuja navyo,akienda kulalamika Mahakamani kwamba tugawane Mali nitampa hizo mali lakini hatozifaidi,either atakuwa Mlemavu au nitampoteza kabisa katika Uso wa Dunia!!
Nitamtumia Wazee wa Kazi wamfanyizie!! Huu unaweza ukaonekana USHETANI lakini hawezi kukojolewa na Mwanaume mwingine,ananiletea shahawa za Mwanaume mwingine hadi nyumbani kwangu,hii ni DHARAU na kukosa ADABU Kulikopindukia!!

Yeye akishaamua kuwa na mwanaume mwingine,afanye mambo yake hukohuko,asiniletee nyumbani na asinisumbue kwa kuniletea sheria za wanadamu za kutaka na mali zangu,Nitakuwa mwiba kwake!! Aendelee na Maisha yake na mimi sintombugudhi KAMWE!!

Huyo Bwana Kalolo ana UVUMILIVU ambao mtu hawezi kuwa nao isipokuwa kama ana Yesu ndani yake,tena Yesu yuleyule wa Nazareti maana katika yeye tunayaweza Mambo yote!!

Hata hivyo,Kupiga Wanawake sio Utamaduni Mzuri,Vumilia,tafuta solution zingine Ukishindwa piga chini,Mambo ya Mke na Mume ni Magumu ndiyo maana hata Yesu akuoa wala Paulo etc!!
 
nilikwishajiapiza katika maisha yangu sitakaa niunyanyue mkono wangu kwa mwanamke. na ninakumbuka wakati fulani nikiwa shuleni dada mmoja katika katika kufanya maskhara akanipiga bonge la kofi kwakuwa nilikuwa nikijisemea toka utotoni kuwa sitakaa nimpige mwanamke na kwakuwa nilikuwa nikiamini kuwa mwanamke ni kiumbe dhahifu sana kisichoweza kustahimi japo ukofi kutoka kwangu, nilijikuta nikisikitiswa sana na kitendo cha dada yule kunipiga na hata machozi yalinitoka kwa kumuonea huruma kwamba ikiwa nikiamua kupiga kwahakika ningempi lakini swali nililojiuliza je angeweza kustahimili kipigo hicho?
niliendela na nadhiri yangu ya kutokumpiga mwanammke hadi nilipoingia kwenye ndoa na kila mara mwanamke anaponiudhi uwa namwangalia na kumwona mdogo kama sisimizi na kuwa nimwangalia namwona ni dhaifu haswa ukizingati nimeoa mke mdogo mdogo yaani (portable) huwa akiniudhi sioni mahali pa kumpiga.
ila kuna siku aliniudhi kwa kuninyesha dharau ya hali ya juu kwani nilimpiga na kasuzuki kakawa ndicho cha kubebea wanaume wengine na kurudi nyumbani kwa muda anaotaka na nikimwambia hasiki siku hiyo alikuja boy friend wake mmoja hapo nyumbani na nikiwa naongea na mke wangu akaondoka kwa dharau na kuingia kwenye gari na pembeni kampakia huyo rafiki wake wa kiume na alirudi saa nne ya usiku na hakuwa akiongea na mimi nilijaribu kulala usingi haukuja kwa mawazo, na kesho yake akaondoka asubuhi nilihisi hasira sana na mwili kunitetemeka ndipo niliposema kwahakika leo nitaiondoa nadhiri yangu machoni pa bwana na nitampa kipigo cha mbwa mwizi, na nilisema kuwa ni laizima awe na alama ili kila atazamapo akumbuke kipigo hicho na kuwa mtii. NIlijikuta nikielekea mjini na kununua faru nikarudi nyumbani saa moja jioni mwanamke hajarudi na sijui yuko wapi nilihisi mwili kutetemeka kwa kiwango cha juu na kwa vile mahali tulipokuwa tunakaa tulikuwa wawili tu na majirani wako mbali nilijikuta nikitafakari kipigo atakachopokea huyo mwanamke nakahisi pengine naweza kumuu, nikajikuta nikiinyanyua simu yangu na kumpigia mama yangu mzazi nimpendaye sana na kumwomba anisaidi kumfundisha mke wangu kuwa natabia nzuri kama mama yangu. kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza kuongea na mama yangu maneno mazito sana ambayo hakutegemea kuyasikia kutoka kwangu, na kwavile sauti yangu ilikuwa tofauti kabisa ndipo mama alipotaka nimweleze kulikoni nikamweleza mkasa mzima na kwamba namsubiri na faru na pengine kesho yake watakuwa kwenye msiba wa mke wangu kutokana na kipigo nitakachompa siku ile, sina hakika ila nafikiri mama yangu alimpigia simu na kumsihi mke wangu asirejee nyumbani siku ile kwani hali sio shwari. Asante Mungu kwamba mke wangu alienda kulala kwa wazazi wake. basi hasira zikapoa na tulikuja kukaa kikao cha famili na kumaliza tofauti zetu nasasa tunaishi kwa amani na nimeirejelezea nadhiri yangu mbele za bwana kuwa sitaunyanyua mkono wangu kumpiga mwanamke.
kila nikiingalia ile faru niliyoinunu huwa najiona mjinga sana nimeiifadhi kwa kumbumbuku.''
kitu kingine cha kumshukuru mungu ni kwa jinsi nilivyo na asili ya ugumu ya kuunyanyua mkono wangu kupiga hata ikiwa ni mwanamke au mwanaume. huwa ninatafakari sana na ikiwa ukiniudhi sana huwa najifanyaga mjinga na kuondoka eneo hilo na kwenda kujichanganya namambo mengine na baada ya hasira kuisha naweza kuongea na wewe kama vile hukunikosea. Namshukuru mungu huwa sihifadhi hasira kwa muda mrefu na wala sina kinyongo nikiishaambua kusamehe
Huwa najiuliza siku nikiokoka hakika nitakuwa naishi kama niko paradiso hapa duniani

endeleeni kujifariji mwanamke ni kiumbe dhaifu...... sijui nani kawadanganya?

(a) Mwanamke anaweza kustahimili mazingira magumu kama njaa kwa mda mrefu kuliko mwanaume.
(b) Mwanamke ni katili zaidi kuliko mwanamume.
(c) mwanamke ndiye anayeongoza familia nyingi
(d) Mwanamke huweza kumshika mme wake na akaanza kutenda kwa maelekezo yake

nani dhaifu sasa? mie nakataa, mwanamke siyo dhaifu hata kidogo, ila wanaume ni dhaifu zaidi ila hatutaki kukili ukweli na tunatumia kauli ya mwanamke ni dhaifu kama njia ya kuogopa kutangaza kushindwa
 
labda wanaona sababu kutukanwa hakuna kiungo kinaumia.


Wewe Hus,

Kuna matusi mengine yana uzito ambao ni zaidi hata ya ngumi za mtu kama Tyson...Ila utashangaa watu wanayafumbia macho!!

Binafsi nadhani watu wanatakiwa pia kuwa makini na hizo verbal abuses zilizopitiliza....Utakuta hadi mtu anakonda kama unyasi !!!!

Babu DC!!
 
Leo nimecheka sana..................Sikujua kama bado Wabeijing wana misimamo ya kinafiki namna hii.
lakini nakubaliana na yule aliyesema kwamba hadharani wanawake wanasema hawawezi kukubali vipigo, lakini Gizani wanapokea vipigo kisha wanaficha..................Kisa.... Ni kuogopa kufedheheka!

Kwani hata wale wanaopiga kelele za haki kwa wanawake wakirudi kwa waume zao, kila kitu kinaachwa mlangoni....... Mume ameshika hatamu na mke hafurukuti.
Si kwamba nafagilia lakini kumbukeni kuwa adui wa mwanamke ni mwanmke mwenyewe..........Wakati unafikiria kuondoka kwenye ndoa.....Unawaza jamii itakuelewaje, kwani kwa asilimia kubwa wanawake huvumilia vipigo na manyanyaso kutoka kwa waume zao kwa sababu ndoa zimeshikiliwa na jamii na sio wao wenyewe...........................

Mtambuzi

Mie nasema sikubaliani na adhabu ya kipigo harooo..labda kwa vile ndoa bado bado haina mikiki mingi sana..
Nikihisi nataka kupigwa bora niponyokee hata nje nikae huko
Baada ya muda nikirudi ndani na imani hasira zitakuwa zimepungua .maana nahisi nikijivungia ndani anaweza kuvunja mlango na mauaji yakatokea ...naogopa kutangulia Mtambuzi....
Huwa nawaza siku nikipigwa ngumi moja naweza nikakimbilia mwiko jikoni ama kama kuna stuli karibu itanisaidia
:hand:
eeeh mungu niepushe na hiki kikombe cha kipigo
Amina


mmmh!
 
Hizi ni dharau na kujaza wanawake ujinga. Kuwa akubali kichapo kwa sana kwa kuwa anataka kusimamisha ndoa

Si ndo hapo sasa! Hiyo ndoa inamfaidisha nani ikiwa mke mwenyewe kila siku anaugulia maumivu. Wamekazana tu vumilia, mara ooh muombee mumeo....mbele ya kipigo jamani??? Dah......pole yao
 
Mimi pia wangu anaongea huyoooo. Ataongea anavyoweza kwa kitu kidogo tu masaa kibao haishiwi maneno. Saa Nyingine natoka chumbani nakaa sebuleni basi yeye akiona vile, anaacha mlango wa ndani wazi na kuongeza sauti hadi majirani wanasikia. Na ukimwambia muyamalize ndo unakuwa kama umemwambia aanze upya. Dawa yao ni kumuongezea mke wa pili akianza fyokofyoko awe anajua utakimbilia wapi hapo huwa wanatulia.
 
Mtambuzi

Mie nasema sikubaliani na adhabu ya kipigo harooo..labda kwa vile ndoa bado bado haina mikiki mingi sana..
Nikihisi nataka kupigwa bora niponyokee hata nje nikae huko
Baada ya muda nikirudi ndani na imani hasira zitakuwa zimepungua .maana nahisi nikijivungia ndani anaweza kuvunja mlango na mauaji yakatokea ...naogopa kutangulia Mtambuzi....
Huwa nawaza siku nikipigwa ngumi moja naweza nikakimbilia mwiko jikoni ama kama kuna stuli karibu itanisaidia
:hand:
eeeh mungu niepushe na hiki kikombe cha kipigo
Amina



mmmh!


Endelea na maombi dada ila haya mambo ya ndoa tuyaache kama yalivyo.....!!

Kuna watu hawajawahi hata kuwaza kuinua mkono ila ndoa hazikufikia anniversary ya kwanza wakati wengine wanapeana kichapo toka kwenye uchumba hadi uzeeni!!

Babu DC!!
 
Mimi nilioa nikiwa kijana sana at 26 na wife alikuwa 21, tulikutana chuoni, baada tuu ya kumaliza ni ndoa!. Changamoto za ujana zilipelekea wife kupokea kisago!, that was then!.

Kuna wanawake wanafanya visa ambavyo unajua wazi anatamani kula kichapo!.

Pia kuna kuna wanawake wa maeneo fulani, asipopigwa, anajiona hapendwi!. Hivyo atakufanyia visa ili kukupima wivu, akigundua humuonei wivu, ananyong'onyea, kwake mapenzi ni pamoja na kisago.

Ila pia kuna type ya wanawanawake wana matatizo ya kisaokolijia yanayoitwa "masochisim", wahusika wanaitwa "macho men" "macho women" hawa ni wale mnaokubaliana, mnakwenda mnapokwenda, mnaingia room, unafunga mlango, halafu anakukatalia, mpaka amlazimishe ndipo nguo zinavuliwa ili tuu kuzuia sizichanike, baada ya hapo miguu hufungwa!, mpaka utembeze kisago kama unabaka ndipo unafunguliwa njia!. Kumbe hizo fujo kwa mwenzako ndio anapata gratification!. Ndio maana kuna watu hutaka wapigwe, wafungwe pingu, wateswe, wabake ndipo wafike na ndio maana kuna wengine hung'ata hata kukutoa damu!.

Kwa Wasukuma wa asili, ile ngoma ya chagulaga, ni ubakaji, kuna wanawake wengi wanabakwa na waume zao au wapenzi wao.

Hawa wanawake wa kisasa "easy come easy go", ndio wanaokosa uvumilivu na kupelekea ndoa za siku hizi kuvunjika kirahisi, kosa dogo tuu, mama ana fungasha!. Familia nyingi za kiafrikla za kizamani, mama zetu wamechezea sana vichapo na ndio zimesimama!.

Hata mimi siku hizi tumekuwa watu wazima, sithubutu hata kunyanyulia mkono!.

Paskali
Soma jibu hapo juu

Paskali, maana mitandao mmoja maarufu alituletea habari za kubaka za mtu mashuhuri mno. Jee nikuulize,
hasa kwa warembo weupe kwa kabila lenu ni jadi? Jee kunaweza kuwa na ukweli fulani katika yale yaliyosemwa na maana mitandao yule?

Paskali
 
Back
Top Bottom