Mwanamke Mnene kilo 254

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Brenda Flanagan-Davies mwenye miaka 43 ndie mwanamke mnene kuliko wote nchini Uingereza akiwa na uzito wa kg 254. Mtandao wa The Sun umeripoti.
Zoezi pekee analofanya Bibi Brenda ni kutembea kutoka kitandani mwake hadi choo kiasi cha meta 10 tu. Na muda mwingi, Brenda anashinda chumbani mwake akiwa maejilaza kitandani. Karibu ya kitanda chake kuna friji linalosheheni misosi kama, chokleti, soda, biskuti, pipi nk.

Brenda hajawahi kutoka na kwenda popote nje ya nyumba yake tangu miaka 4 iliyopita. Mahitaji ya Brenda anayapata kwa kununuliwa na watu wanaomuhudumia kwa kumuogesha na kumwandalia chakula na mengineyo. Ama nguo ananunua katika mashirika maalum kupitia mtandaoni.

Pato la Brenda ni Paundi za Uk 300 wiki. Madaktari wameshamuonya BrendaA afuate utaratibu wa kupunguza kula na kula vyakula maalum vinginevyo kifo kinamnyemelea, kwani mwili wake hauna nguvu za kuhimili opereshi ya kupunguza utipwatipwa.

Kwa upande wake bibi Brenda amesema kuwa "Nachukia sana maisha haya, Nijisikia aibu kuwa katika hali hii, natamani kujisaidia lakini sijui nianzie wapi". "Siwezi kuacha kula" amenukuliwa akisikitika.
 
Weka picha!!!!
Na anaendelea kula tu!

r-BRITAINS-FATTEST-WOMAN-large570.jpg


brenda.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom