Mwanamke: Kama unaishi na mwanaume wa aina hii, basi pinga usikubali kuwa mjinga

Hii mada ilikua nzuri. Niliona mzee alikua anampa kichapo sana step mother wetu . Kuna siku yule mama alipigwa vibaya sana akaamua kuondoka kwao . Cha kushangaza baada ya siku 2 akarudi nikaamuuliza kwanini umerudi huyu atakuja kukuua je huoni umeumia sana. Alinijibu nakaa kwa muda nitaondoka. Mama yule hakuondoka mpaka leo lkn niliapa sintakuja kuvumilia kipigo toka kwa mume wangu kwa namna yoyote. Namshukuru Mungu alinipa mtu mwema na mwenye hekima.

Hali hii ukiikemea toka day one basi haiwezi kuendelea kwani nafikiri wanaume wengine hujaribu akiona umepokea kipigo na umekaa kimya basi hurudia tena na tena halafu inakua mazoea lkn dada/mama ukikigomea kipigo toka siku ya kwanza huyo mtu hatorudia kukupiga tena.
 
Wapo wengi tu wanafungishwa virago na si akina Mario. Hayo ya kila mke kuolewa na mume mwenye mali/kipato zaidi ya mke yalikuwa mwaka 47, miaka hii kuna mabinti wengi tu mambo yao kwenye mshiko yako poa sanaaaa.

Nani akishindwa afunge virago? Ni mwanaume yupi atakayekubali kufunga virago aondoke kwenye nyumba baada ya kushindwana na mkewe? Labda Marioo.....
 
Unamzabua na yeye!
Au unavumilia, hoping hatarudia tena; while yeye anakuwa assured that there is nothing u can do hata akikupiga mateke! LOL

ukimzabua na yeye si atakuzabua tena ....mi nachoona hapa hamjui muongeacho

and just for the record ..mwanaume wa kweli na anayekupenda hawezi kukupiga akakuumiza just kukurudisha kwenye mstari kwa pale ulipopitiwa. na ndomana kwenye ule uzi jamaa aliainisha jinsi ya kumpiga mke kwa kumfinya tu mapajani na wala sio mpaka mke atoke damu ila mpaka ngozi iwe nyekundu na kisha baada ya hapo mume huomba msamaha na kumuahidi huto rudia tena na kuanza kutibu majeraha si raha hizo.....na hayo ndio mapenzi
 
Mtambuzi

i met a woman katika maongezi akaniambia ni bora mumewe amcheat kuliko umpiga... baada ya muda akakuta mumewe ana ndogo anaihudumia, akasema ni bora apigwe kuliko kuwa cheated

Both are primitive solutions to our problems (mena and women).... none of them is good, but we do those things involuntarily or willingly

There is no good way yoyote inapokuja kwenye mapenzi ya kuumizana

uhsauri wangu ni kwamba kama dada anatandikwa, ajitahidi kuprevent causes za rabsha, amuache jamaa kabisa au awe na yeye mtaalama wa vichapo ili watandikane, mwanaume yoyote yule hata kama ni mtemi, akipewa za uso vizuri huwa harudi kupigana tena maana anajua matokeo yanaweza kuwa kama ya Manchester United siku hizi

Akina dada chezeni karate na judo maana tumezidi siku hizi... kama sio cheating, basi ni beating, kama sio beating basi ni uyahaya mtupu na ama sio uyahaya wengine wanaishia kuwa mabwabwa....

good men tumebaki hata sita hatufiki:doh::doh::doh::doh::doh::doh::becky::becky::becky::becky:
 
Kongosho huwaga najiambiaga kabisa kwamba sitajiwekea mazingira ya kupigwa kwa maana kwamba sitajibizana nae ili kumpandisha hasira. ila pia sitoruhu mazingira hata ya kumpa nafasi kunyanyua kibao karibu yangu manake ukweli nitairudisha kwa staili ile ile. labda tu cha kwangu kitakuwa hakiumi kama chake.

mmmhh eti kutojiweka mazingira ya kutokupigwa . kuna dada mmoja alileta uzi hapa siku za nyuma kwa kusema kuwa

amejisika raha sana mumewe kampiga yani mpaka na story yenyewe ilikuwa hivi japo kwa ufup ni kwamba mume

alikuwa yupo safarini mkoa jirani na mke hakutarajia mumeo kurudi hiyo siku ,jioni ikafika mke akaona kwakuwa mume

hayupo na siku nyingi hajaenda bar akapanga asipike na ataenda kununua chakula bar ya jirani na kunywa walau bia

moja sasa alipofika bar akakutana na classmate wake ambae walipotezana siku nyingi zilizopita na wala hakuwa mpenzi

wake huko nyuma just classmate basi wakaamua kupata kinywaji pamoja na story mbili tatu mpaka ikafika saa sita

usiku mwanamke kajisahau kabisa kwa story kumbe hukunyuma mume karudi kimya kimya bila kumpa taarifa na kafika

nyumbani mlango umefungwa kapiga simu hazipokelewi na bi dada alikuwa naogopa pokea simu sababu ya kelele za

mziki wa bar na sabab zingine alizozianisha yeye sasa ilipofika hiyo mida ya saa sita ikabidi bi dada amuage yule jamaa

na jamaa akamsindikiza bi dada wakaachana . kufika nyumbani mke akafungua mlango na kuingia ndani mara simu

yake ikaita tena ku cheki ni mumewe basi kwa sauti ya kama mtu aliyetoka kulala akaipokea ile simu mumewe

akamwambia amfungulie mlango kwani amerudi basi mkea akajifanya mtu aliyepitiwa na usingizi kabisa akamfungulia

mlango jamaa akaingia ndani kisha akamuuliza kwanini alikuwa hapokei simu alivyokuwa anampigia ? mkea akajibu

alipitiwa na usingizi jamaa bila kuchelewa akampiga kibao kimoja kisha akamwambia nimekukuta bar na mjinga wako na

kakusindikiza mpaka hapa ...mke kimya kumbe jamaa baada ya kuona hapokelewi simu yake na kuhakikisha hakuna mtu

ndani ikabidi aende kujipumzisha kwenye hiyo bar ya jirani na ndio akamkuta mke na jamaa nakuona mchezo wote ....

analysis
kwanini mume alimpiga mke ?
1) mume anamuamini mke wake ndio maana akampiga kwani anamjua mke wake na anamuamini kabisa na ndio maana alijiridhisha kuwa yule aliyemkuta pale na mkewe si hawala wa mke wake ila tu alipitiwa na story za yule boya sasa ilisiku nyingine asipitiwe tena na awahi kurudi nyumbani hata kama atakutana na shoti basi akamkumbusha . ingekuwa mumeo asiyejua kupiga na wewe usiyepigwa hii ndio ingevunjika kwani mumeo angekuwa na hasira na kinyongo

2) sababu ya pili kumpiga kwa sababu mke alisema uongo sasa ili kumkumbusha uongo hautakiwi kwenye ndoa basi akampiga kidogo

3) sababu ya tatu ni kumweke mume nje ya nyumba yake mpaka saa sita usiku huku akiwa na uchovo na mabegi huku pia mbu wakimng'at eti kisa mke anaongea na rafiki yake wa chuo

4) sababu ya mwisho ni mume alimpiga mke ili kumuonesha kuwa hivi alivyovifanya juu mume alichukia to the maximum kwa hiyo asirudie tena

sasa wewe unataka ufanye hivi vyote kisha twende ndani tuka discuss....akha u discuss ?kwani umesikia bunge hili haya ni maisha ya ndoa na wala sio bunge
vingine havi discusiki vinahitaji action. nakuanzia hapo ile dhana yangu ya kuwa mume asiympiga mkewe basi hampendi yale ni yule mume wa bora liende na asiyekuwa na uchungu na mke

nb story yenyewe ni hii hapa https://www.jamiiforums.com/mahusia...upigwa-makofi-na-mme-wangu-5.html#post7608326
 
mmmh! binafs nawza kuvumilia kila kitu but not kichapo manake pakifika hapa jamani tunatembezeana. uuuwiiiiiiiiii khaaa eeeh! ndipo litakapo timia lile neno mpalestina.

cheza vyovyote na mimi but usiniguse kwa kipondo lol! vingine vyote navumilia ila hili hapana na nilishalisema kabisaa.

hahaha umenifurahisha i promise myself hyooo anaeitwa mume sijui ajenipiga aseee kwanrudi mashami lee.....khaa nkikii??
 
soo..una admitt kuwa "ulivunja ndoa ya baba yako na mama yako"?...

Duuuhhh kama ni kweli basi wee mkareeeeeeee.

niwe niliivunja sikuivunja I dont care, najivunia mama yupo hi mpaka wajukuu amewaona.
 
Demu/ mke anaefanya mambo ya kukera makusudi unamuachaje hivi hivii? Ikiwa utamwambia mtu kitu flani sipendi na akashindwa kuelewa maana yake ana dharau huyo.
Mwanaume + Dharau = Jibu unalo!
 
Alafu mwanaume mpigaji utamjua tu tokea mpo kwenye uchumba!!! Ni mwepesi sana kunyanyua mkono. Watu wanajidanganya kua atabadilika huko mbele... Hizi ndoa zingine, unakikaribisha kifo kwa sherehe kubwa.
 
Demu/ mke anaefanya mambo ya kukera makusudi unamuachaje hivi hivii? Ikiwa utamwambia mtu kitu flani sipendi na akashindwa kuelewa maana yake ana dharau huyo.
Mwanaume + Dharau = Jibu unalo!
Haijalishi kiwango cha maudhi anayokupa!!!
Mwanaume yeyote anaeinua mkono kumpiga mkewe ni ta.hi.ra!
 
119.jpg

Na ukijaribu kunipiga tu, utajua mimi ni mwanamke wa namna gani, hutakuja kunisahau..........!

Uzoefu unaonesha kwamba baadhi ya wanaume au wanawake hutumia kile walichokiona kutoka kwa wazazi wao katika ndoa zao. Tabia za wazazi huakisi sana maisha ya watoto wao hususan katika maisha yao ya ndoa, labda kama watajitambua na kujivua gamba, lakini vinginevyo watakuwa wanatumia kile walichokiona na kujifunza kutoka kwa wazazi wao.
Kwa mfano mwanamke anayeishi na mwanaume mnyanyasaji na mpigani, ni dhahiri kama wana mtoto wa kiume anakuwa na uwezekanao mara saba zaidi kuja kuwa mnyanyasaji kwa mkewe atakapokuwa mkubwa. Na kama ni binti ana uwezekanao mara tatu zaidi kuja kuwa mtu wa kupata vipigo atakapokuwa ameolewa. Hapa wa kulaumiwa ni wazazi, kwa sababu wao ndio wamewafanya wawe hivyo. Kwa kuwa wazazi ndio mashujaa wa watoto wao, huakisi tabia halisi za wazazi wao.

Hebu fikiria una miaka sita na unasikia ukiwa kwenye chumba chako baba yako anapompiga mama yako! Mama yako anapiga mayowe na kulia akiomba msaada! Unamsikia baba yako akimpiga mama yako ngumi na mateke na kumwita majina machafu machafu ambayo kimsingi hutakiwi kuyasikia. Utafanya nini ukiwa ni mtoto na uko katika mazingira kama haya? Ukweli ni kwamba huwezi kuondoka! Na unakuwa huna uchaguzi zaidi yakukubali kuishi na wazazi wako ambao kimsingi aina ya maisha wanayoishi sio kama mke na mume bali mume na mtumwa wake ambaye ni mama yako. Unalazimishwa kuishi hivyo, hutaki hata marafiki zako waje nyumbani kwenu. Mama kila siku ana manundu mwilini kwa vipigo kutoka kwa baba yako. Na si hivyo tu, baba kila siku akirudi nyumbani anaaanza kufoka! Na sasa siri zenu zote ziko nje. Pale mtaani familia yenu imekuwa ni gumzo, huna raha kama watoto wengine. Balaa gani hili!
111.jpg

Mie bado nawalaumu wanawake wanaokubali ujinga huu, ingawa kuna watu wananishambulia humu jamvini, lakini kwa hili siwezi kulinyamazia. Ni ujinga tu ndio unaosababisha wakubali kuishi kwenye ndoa za namna hii. Kama wewe ni binadamu kamili ambaye umezaliwa ukiwa na akili zako timamu, kwa nini ukubali kuishi na mwanaume mfuajaji ?
Kama unataka kuishi na mwanaume wa aina hii, basi pinga usikubali kufanywa gunia la mazoezi. Simama imara ukiwa umeshika kikaango na umwambie, &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Njoo unipige uone. Na siku ukijaribu kunipiga tu, utajua mimi ni mwanamke wa namna gani, hutakuja kusahau.' Au kama huwezi hilo basi zuia upigwaji kwa njia nyingine. Lakini uzoefu unaonesha kwamba, njia iliyo bora kabisa ni kuondoka kwenye uhusiano huo.

Kama uko kwenye ndoa ya mateso na unajikuta huwezi kutoka, umekubali kuwa fuko la mazoezi la mumeo, jiulize ni kwa nini. Anzia kwa wazazi waliokulea na kujiuliza kama wewe siyo mama yako ambaye alikubali kupokea vipigo kwa mumewe huku akiendelea kuvumilia na kuishi katika ndoa hiyo ya mateso. Kama ndivyo, basi kataa kuwa mama yako. Anza safari ya kuwa wewe ambaye huko tayari kuwa mtumwa wa mtu kwa kuhofia kusimama mwenyewe kwa miguu yako. Amua sasa na utamudu, kwani wewe ni binadamu kamili na huhitaji kukamilishwa na mtu mwingine.

Wenyewe wanawake wanakuambia wanakaa tu kwenye manyanyaso kwa ajili ya watoto wao. Na mwanamme akiomba papuchi ama tigo anapewa tena bila hata kinyongo, jamaa akimaliza tu haja yake matusi yanarudi pale pale.
 
Alafu mwanaume mpigaji utamjua tu tokea mpo kwenye uchumba!!! Ni mwepesi sana kunyanyua mkono. Watu wanajidanganya kua atabadilika huko mbele... Hizi ndoa zingine, unakikaribisha kifo kwa sherehe kubwa.
Karne hii Mwanamke kupigwa na kuendelea kukubali vipigo kutoka kwa mwanaume anatakiwa kupimwa akili huenda ana kasoro kwenye ubongo. Kumbuka kuna taasisi zisizo za kiserikali za kutetea unyanyasaji wa kijinsia hapa nchini kuanzia TAWLA, WILAC, TGNP, TAMWA pamoja na tume ya haki za binadamu halafu unakubali kipigo.
 
Wanaendekeza mapenzi ya kijinga!!!
 
Alafu mwanaume mpigaji utamjua tu tokea mpo kwenye uchumba!!! Ni mwepesi sana kunyanyua mkono. Watu wanajidanganya kua atabadilika huko mbele... Hizi ndoa zingine, unakikaribisha kifo kwa sherehe kubwa.
Paprika, hata kuwa spanked hutaki?
 
119.jpg

Na ukijaribu kunipiga tu, utajua mimi ni mwanamke wa namna gani, hutakuja kunisahau..........!

Uzoefu unaonesha kwamba baadhi ya wanaume au wanawake hutumia kile walichokiona kutoka kwa wazazi wao katika ndoa zao. Tabia za wazazi huakisi sana maisha ya watoto wao hususan katika maisha yao ya ndoa, labda kama watajitambua na kujivua gamba, lakini vinginevyo watakuwa wanatumia kile walichokiona na kujifunza kutoka kwa wazazi wao.
Kwa mfano mwanamke anayeishi na mwanaume mnyanyasaji na mpigani, ni dhahiri kama wana mtoto wa kiume anakuwa na uwezekanao mara saba zaidi kuja kuwa mnyanyasaji kwa mkewe atakapokuwa mkubwa. Na kama ni binti ana uwezekanao mara tatu zaidi kuja kuwa mtu wa kupata vipigo atakapokuwa ameolewa. Hapa wa kulaumiwa ni wazazi, kwa sababu wao ndio wamewafanya wawe hivyo. Kwa kuwa wazazi ndio mashujaa wa watoto wao, huakisi tabia halisi za wazazi wao.

Hebu fikiria una miaka sita na unasikia ukiwa kwenye chumba chako baba yako anapompiga mama yako! Mama yako anapiga mayowe na kulia akiomba msaada! Unamsikia baba yako akimpiga mama yako ngumi na mateke na kumwita majina machafu machafu ambayo kimsingi hutakiwi kuyasikia. Utafanya nini ukiwa ni mtoto na uko katika mazingira kama haya? Ukweli ni kwamba huwezi kuondoka! Na unakuwa huna uchaguzi zaidi yakukubali kuishi na wazazi wako ambao kimsingi aina ya maisha wanayoishi sio kama mke na mume bali mume na mtumwa wake ambaye ni mama yako. Unalazimishwa kuishi hivyo, hutaki hata marafiki zako waje nyumbani kwenu. Mama kila siku ana manundu mwilini kwa vipigo kutoka kwa baba yako. Na si hivyo tu, baba kila siku akirudi nyumbani anaaanza kufoka! Na sasa siri zenu zote ziko nje. Pale mtaani familia yenu imekuwa ni gumzo, huna raha kama watoto wengine. Balaa gani hili!
111.jpg

Mie bado nawalaumu wanawake wanaokubali ujinga huu, ingawa kuna watu wananishambulia humu jamvini, lakini kwa hili siwezi kulinyamazia. Ni ujinga tu ndio unaosababisha wakubali kuishi kwenye ndoa za namna hii. Kama wewe ni binadamu kamili ambaye umezaliwa ukiwa na akili zako timamu, kwa nini ukubali kuishi na mwanaume mfuajaji ? Kama unataka kuishi na mwanaume wa aina hii, basi pinga usikubali kufanywa gunia la mazoezi. Simama imara ukiwa umeshika kikaango na umwambie, &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Njoo unipige uone. Na siku ukijaribu kunipiga tu, utajua mimi ni mwanamke wa namna gani, hutakuja kusahau.' Au kama huwezi hilo basi zuia upigwaji kwa njia nyingine. Lakini uzoefu unaonesha kwamba, njia iliyo bora kabisa ni kuondoka kwenye uhusiano huo.

Kama uko kwenye ndoa ya mateso na unajikuta huwezi kutoka, umekubali kuwa fuko la mazoezi la mumeo, jiulize ni kwa nini. Anzia kwa wazazi waliokulea na kujiuliza kama wewe siyo mama yako ambaye alikubali kupokea vipigo kwa mumewe huku akiendelea kuvumilia na kuishi katika ndoa hiyo ya mateso. Kama ndivyo, basi kataa kuwa mama yako. Anza safari ya kuwa wewe ambaye huko tayari kuwa mtumwa wa mtu kwa kuhofia kusimama mwenyewe kwa miguu yako. Amua sasa na utamudu, kwani wewe ni binadamu kamili na huhitaji kukamilishwa na mtu mwingine.
Una mume wewe!? Au ndo guberi la mtaani
 
Back
Top Bottom