Mwanamke: Je, unatafuta mchumba? Fuata kanuni hii hakika utapata mchumba mwenye tabia uzitakazo

Mi nishasoma The Secret na Movie yake pia nikaiangalia. Nikafanya ka experiment kidogo kakawa, but sikuipa much thought afterward. For me i dont know what it is yet lakini naona kama inakinzana na mafundisho yangu ya dini hata kama formula ni ile ile ya kuamini na utapewa. I wonder in my humble kinda way pale tukipata kuijua na kuitumia vyema kutakuwa na limit kweli? Si itakuwa uwanja wa fujo? Na kwa wale wamuaminio Mungu si ni sawa na kumvua Mungu uwezoe maana hapa naona hakuna mpaka au nijiulize na kujijibu kuwa Mungu (The Universe according to The Secret) yupo kwa ajili ya ku serve our every need tu. Msaada Mtambuzi
Thank you
 
Last edited by a moderator:
Mi nishasoma The Secret na Movie yake pia nikaiangalia. Nikafanya ka experiment kidogo kakawa, but sikuipa much thought afterward. For me i dont know what it is yet lakini naona kama inakinzana na mafundisho yangu ya dini hata kama formula ni ile ile ya kuamini na utapewa. I wonder in my humble kinda way pale tukipata kuijua na kuitumia vyema kutakuwa na limit kweli? Si itakuwa uwanja wa fujo? Na kwa wale wamuaminio Mungu si ni sawa na kumvua Mungu uwezoe maana hapa naona hakuna mpaka au nijiulize na kujijibu kuwa Mungu (The Universe according to The Secret) yupo kwa ajili ya ku serve our every need tu. Msaada Mtambuzi
Thank you
Elizabeth Dominic,

Ukweli ni kwamba tumechaguliwa kila kitu tulicho nacho katika maisha tunayoishi leo, tumechaguliwa dini za kuabudu, tumechaguliwa taaluma za kusomea, tumechaguliwa aina ya maisha tuanayoishi, tumekuwa sio sisi bali tumekuwa wazazi wetu ndugu zetu au jamii. Utakuta baba anataka uwe yeye, mama nae anataka uwe yeye, shangazi, mjomba, shekh, mchungaji, jirani, rafiki na kila mtu aliyekuzunguka anataka uwe yeye. Sasa wewe ukiwa wao utakuwa na miili mingapi?

Sisemi tusiheshimu maoni ya wazazi wetu, la hasha, bali namaanisha kwamba yapo baadhi ya maamuzi tunapaswa kuamua wenyewe aina ya maisha tunayotaka kuishi. Kwa sababu kila mtu yupo hapa duniani kwa lengo maalum. Tembea dunia yote hii hutakuta mtu yeyote anayefanana na wewe kwa kila kitu, labda sana sana, utasikia "Huyu anafanana na fulani" kwa maana ya kwamba kuna baadhi ya maeneo ameshabihiana na mtu fulani lakini huyo mtu sio wewe.

Kwa hiyo ile kuwa wewe, ni jambo la kujivunia, wewe ni mtu kamili na una umaalum wako, huhitaji kukamilishwa na mtu mwingine. Kimsingi kanuni ya kufikiri vizuri inahitaji mazoezi ya kutosha kwa sababu tumelelewa na kufundishwa kufikiri vibaya, kwa hiyo mawazo yetu yamekandamizwa sana kiasi kwamba hatukuwa na uhuru wa kufikiri tofauti na wazazi wetu.

Kama maisha yako yalitawaliwa na nguvu hasi nyingi, na labda umeshawahi kuwafanyia watu ubaya, kudhulumu au kuwaumiza watu wengine kihisia huko nyuma kutokana na kufikiri kwako vibaya, basi utakuwa umepanda nguvu hasi nyingi ambazo zitakuwa zimekuzunguka. Kwa kawaida ukipanda nguvu hasi unavuna nguvu hasi, kwani huwezi kupanda mahindi ukavuna mtama, tunavuna kile tulichopanda.

Kwa kuwa ile nguvu hasi inakuwa inakuzunguka, ndio sababu maisha yetu yanakuwa, magumu. Kama mtu umeishi na nguvu hasi kwa muda mrefu, ukiamua kuanza kufikiri vizuri usidhani kuwa ile nguvu hasi uliyopanda kabla hujajitambua itakuacha, ni lazima itaendelea kukuzunguka, kwa hiyo wakati mwingine ukiwa unafikiri vizuri na kujenga uzingativu, nguvu hiyo inaweza ikaja ghafla na kukusomba na hivyo kukutoa kwenye kufikiri kwako vizuri.

Usipokuwa makini, wa kuzipokea changamoto hizo basi hutapata matokeo mazuri, kwa sababu kufikiri kwako vizuri kunategemea na imani uliyonayo juu ya kile unachofikiri na kuamini, kama imani yako ina mashaka, basi na kufikiri kwako kutakuwa hakuna maana. Kinachotakiwa ni kupokea hizo changamoto, kwa sababu tulizipanda wenyewe kutokana kwamba tulikuwa hatujajitambua.........
 
Last edited by a moderator:
Mfumo wa kufikiri upo mmoja ila umegawanyika katika sehemu mbili:

( i )Mfumo wa kufikiri vibaya

hebu tutajie mambo au matukio uliyokuwa unayafikiria siku mbili au tatu zilizopita. Bila shaka yote ni mabaya na yenye kuumiza. Ni mfumo ambao mtu anawaza au kufikiri mambo ambayo yanamuumiza yeye au mtu mwingine. Katika mfumo huu, mtu anazijaza fikra zake na picha (taswira) zenye matarajio na matukio ya kuumiza, maanguko, wasiwasi, hofu, hasira, kukata tamaa, visasi, majuto, kinyongo, chuki, fitina, kujishusha, kujikosoa n.k.

Mfumo huu ndiyo unaoongoza maisha ya mwanadamu. Anafikiri vibaya kwa sababu anaongozwa na mwili. Ndiyo maana majuto na hofu haviishi. Amefundishwa na kuzoeshwa kupokea, kutafsiri na kusema au kuona kirahisi zaidi yale yaliyo mabaya tu. Ni bahati sana kumkuta anafikria mambo mazuri kwa muda mrefu wa siku. Anapenda kutazama upande mbaya wa tukio au binadamu mwingine. Mfano: mtu anaweza kufanya yaliyo sahihi kumi. Ikitokea akakosea moja, kwa mujibu wa mfumo wetu wa kufikri, hili moja baya ndiyo litatamalaki na kupewa nguvu. Yale kumi yatafutwa haraka sana kwenye kumbukumbu.

Kwa kutokujua sisi ni nani, matokeo yake miili hii badala ya kuimiliki, yenyewe ndiyo hutumiliki na kuwa mali yake. Kumbuka miili hii haitumii akili yetu, inatumia akili tuliyopewa. Baada ya kufanya yale yanayotokana na kufikiri vibaya (kwa matakwa ya mwili), ndipo sisi hujitokeza nyuma ya miili hiyo na kuanza kujuta na kulaumu. Lakini baada ya muda, miili hututhibiti tena na kuturudisha kwenye mazoea yetu na hivyo kurejea kwenye mateso ya maisha. Kwa mfano: unapoachwa na mume au mke unaumia sana. Kinachokuumiza siyo kuachwa, kinachokuumiza ni ile tafsiri uliyofundishwa kwamba kuachwa ni kubaya. Tukio siyo tatizo, tatizo ni tafsiri yako. Kila tatizo (changamoto) unayoipata, fahamu kwamba ufumbuzi wake unao, kama huna, haliwezi kukutokea, na kama utalikataa, ujue unatafuta tatizo jingine jipya na lazima utaumia tu. Ukweli ni kwamba, furaha, amani na utulivu haviwezi kustawi katika mfumo huu wa kufikiri vibaya.

( ii ) Mfumo wa kufikiri vizuri:

ni ule mfumo ambao mtu anawaza au kufikiri mambo ambayo hayamuumizi yeye wala mtu mwingine. Ni kuzijaza fikra zetu na masuala, matukio, matarajio na picha/taswira zenye kutupa moyo, matumaini na faraja. Tunapaswa kuishi kwa wakati na mahali tulipo tu, sasa hivi, hapa ulipo. Hakuna kitu kinachoitwa mambo mengi ( bize), timiza kila jambo kwa wakati wake. Mfumo huu ni mgeni kwetu au hatuufahamu.

Huna uwezo wa kuzuia mawazo yasiingie kwenye mfumo wako wa kufikiri. Mawazo yote mabaya kwa mazuri yataingia kwenye mfumo wako wa kufikiri ( mfano: mawazo ya kuiba, kusaidia, kuzini, kufukuzwa kazi, kudhulumiwa, kudhulumu, kupigana, kusali/kuswali, kujiua, kupata kazi, kufanikiwa n.k.). Swali kubwa la kujiuliza ni hili: Mawazo hayo yanapoingia kwenye mfumo wako wa kufikiri, wewe unatoa nafasi na muda kwa mawazo yapi?

Kwa kawaida, huwa tunatoa nafasi na muda kwa mawazo mabaya (yale ambayo hatuyataki, yale yanayotuumiza, yale yanayowaumiza watu wengine). Kwa kutoa nafasiI na muda kwa mawazo hayo, tunayavuta yaje kwetu, na hivyo yanatutokea kweli. Lakini pia, usitoe nafasi na muda kwa kukataa jambo usilolitaka. Mfano, sitaki kuolewa na askari. Ukweli ni kwamba, utaolewa na askari. Kwa nini usitoe nafasi na muda kwa mtu unayetaka akuoe?

Huna budi kubadili mfumo wako wa kufikiri. Toa nafasi na muda kwa yale tu unayoyataka, kwa yale tu yanayokupa nafuu, kwa yale tu ambayo hayakuumizi na kwa yale tu ambayo hayamuumizi mtu mwingine. Kumbuka kila jambo lina pande mbili, upande mzuri na upande mbaya. Pande zote hizi mbili ziko sawa. Mfano, bila utajiri kusingekuwa na umaskini, bila kupoteza kazi kusingekuwa na kupata kazi, bila kuzaliwa kusingekuwa na kufa. Hakuna jambo hata moja hapa duniani ambalo lina upande mmoja tu. Kama lipo, binadamu halijui. Hivyo, hakuna jambo baya wala zuri ila wewe unasemaje!!!

Katika kila jambo au tukio, kinachoanza ni kufikiri, tunapofikiri tunapata hisia ambazo zinatupelekea kutenda jambo fulani (mawazo – hisia – kitendo). Baada ya kutenda jambo hilo tunakuwa sisi, sisi akina nani? (Sisi wapole, sisi wakorofi, sisi wakatili, sisi waungwana, sisi wagomvi n.k.). kila wakati, hakikisha unachofikiri, unachowaza, unachosema au unachotenda hakikuumizi wewe au mtu mwingine. kumbuka, maumbile hayajui samahani, hasira au kulewa, yanachojua ni kile ulichotenda. Jitahidi kuwa taa kila unapokuwa ila hakikisha miili yako iko sawa. Kuna uhusiano mkubwa kati ya mwili wa akili, wa hisia na huu unaoonekana. (Mada hii nitaizungumzia baadae kwajinsi ninavyoendelea kuandika makala juu ya maarifa haya) Linaanza wazo au fikra kwenye mwili wa akili, wazo hili linazaa hisia fulani. Mwili unaoonekana unajibu kwa kutoa vichocheo ili kuulinda mwili. Kwa kuwa vichocheo hivi hutolewa wakati wa dharula tu, hivyo kuendelea kuchokozeka kihisia kutokana na kufikiri vibaya, huudhuru/kuumiza mwili huu unaoonekana na hivyo kusababisha magonjwa kama vidonda vya tumbo na shinikizo la damu.

Jiulize, kutokana na kufikiri kwako, maisha yako ni kero kwako kwa kiasi gani? Lakini pia ni kero kwa wengine kwa kiasi gani? Huoni kwamba kufikiri kwako ni muhimu sana, huoni kwamba ndiyo njia muhimu ya kukupa amani, furaha na ridhiko katika maisha yako? Ukiweza kuratibu mwili wako wa akili, ni rahisi zaidi kuratibu miili mingine. Ukiamka huna furaha, jiulize ni mwili gani unakunyima furaha. Kufikiri vizuri ndiyo hatua ya kwanza ya kuelekea kupata furaha ya kweli. Ili uipate furaha ni lazima usafiri pia, na ukiwa njiani utaipata, na ukiipata inapoteza maana (kinakuwa kitu cha kawaida). Furaha unayo ndani, usiitafutie nje. Kumbuka tumekuja duniani kutafuta furaha kwa kufanya jambo tunalolipenda zaidi (lengo).

Ili umudu kuutumia mwili wako wa akili vizuri, unapaswa:

(I) Kujua kwamba, unafikiri. lakini siyo kufikiri tu, bali kufikiri vizuri. kufikiri vizuri maana yake ni kuruhusu fikra zenye kukupa furaha na kuwapa wengine furaha, kuingia kwenye mfumo wako mkuu wa kufikiri.

(II) Kujua kwamba, mazingira na watu wengine hawapaswi kukupangia ufikirie kitu gani, bali wewe ndiye mwamuzi wa unachotaka kufikiri.

(III) Kujua kwamba, unapaswa kufikiria kuhusu yale unayotaka, na siyo usiyoyataka. Kama jambo hulitaki, unalitafutia nini?

(IV) Jua kwamba, kuna mambo ambayo yamewekwa kichwani mwako kupitia mawazo yako ya kina. Yalianza kuwekwa tangu ukiwa tumboni mwa mama yako, mengine yaliwekwa wakati wa makuzi yako, ambayo ndiyo leo unayaita akili yako. Kama yanakukera au kuwakera wengine, jua kwamba hayakufai.
 
Hivi nilikuwa wapi mpaka huu uzi ukanipita?
Shukrani kwa Da AshaDii kwa kutukusanyia hizi Theads zilizowahi kubamba na leo hii mie mtoka mbali nimepata fursa ya kujifunza
 
Last edited by a moderator:
'The Secret' is a good book.I happen to watch its movie too.So fantastic!!
 
ubarikiwe,kumbe naweza kupata ninayemtaka!

Charminglady

Kumbe hadi July 2012 ulikuwa hujampata unayemtaka?

Kutoka post yako ya mambo ya ndoa jana uliniambia nimechelea, nadhani mambo ya Mtambuzi yamefanya kazi na kipindi cha

Julay - Nov 2012 umeshampata unayemtaka, hogera!
 
charminglady wala haihitaji kwenda kwa KARUMANZILA, nguvu ya mvuto inaweza kuvuta kitu chochote ukitakacho, iwe ni mume, mke, nyumba, gari, utajiri, watoto, yaani kila kitu. Kinachotakiwa ni kuwa na urazini, (awareness) kujua kila kinachoingia na kutoka akilini mwako (Kuratibu mawazo yako na kuepuka kuwazza vibaya- negatives), vitendo (Action) matendo yako ni ya namna gani, jamii iliyokuzunguka inakonaje, mwema, muadilifu, mkorofi, mwenye vurugu kichwani nk, Kulenga (Focus) katika kutumia nguvu hiyo ya mvuto umelenga kitu gani, mume mkorofi au muadilifu...? Kama ukimudu kutumia kanuni hiyo hakika utaishi maisha uyatakayo na si jamii itakavyo................................................

Mzee Mtambuzi.... Nashukuru sana kwa hii post yako! Napenda kutoa ushuhuda wa NGUVU YA MVUTO. Ni kweli hii nguvu inafanya kazi. Na nimeshapata tokeo moja la nguvu ya mvuto. Ngoja niendelee tena huenda kukawa na matokeo zaidi......
 
Last edited by a moderator:
Npenda sna vitabu vya namna hiyo big upo bro icho cha the secret sijabahatika kukiona nitajitahidi kukitafuta ila pia ukiwa na muda naamini tutaona na review ya the power of your subconscious mind, success through positive thinking...!
 
Mi nishasoma The Secret na Movie yake pia nikaiangalia. Nikafanya ka experiment kidogo kakawa, but sikuipa much thought afterward. For me i dont know what it is yet lakini naona kama inakinzana na mafundisho yangu ya dini hata kama formula ni ile ile ya kuamini na utapewa. I wonder in my humble kinda way pale tukipata kuijua na kuitumia vyema kutakuwa na limit kweli? Si itakuwa uwanja wa fujo? Na kwa wale wamuaminio Mungu si ni sawa na kumvua Mungu uwezoe maana hapa naona hakuna mpaka au nijiulize na kujijibu kuwa Mungu (The Universe according to The Secret) yupo kwa ajili ya ku serve our every need tu. Msaada Mtambuzi
Thank you

Binafsi pia naona kama inakinzana kidogo na imani yangu ya dini kuwa MUNGU ndio mtoaji, hata hiyo universe imeumbwa na MUNGU. I thnk a gud concept is the power of positive thnking
 
Last edited by a moderator:
Lakini kunabaadhi ya vitabu vinakupa hata mistari biblia kama uthibitisho wa wacho kiandika na hata Yesu mwenyewe alisema ukiwa na imani kama chembe ya harabani unaweza kuuamuru mlima ung'oke na ukajitose baharini kwa hiyo kilichopo ni sisi hutuwezi kutumia kile kilicho ndani yetu maana tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na kuna mahali biblia inasema mtakolo lifunga duniani na mbinguni limefungwa na likifunguliwa duniani na mbinguni limefunguliwa ina maana nasi tumepewa mamlaka ya kufungua na kufunga....me binafsi sioni kama inapingana na imani ya dini.
 
Hata me natafuta ila me ninavyo kama viwili cha power of ur subconcious mind na power of positive thinking kama utahitaji nitumie mail yako
 


black-woman-waiting.jpg
JJJJ

Kuna kitu kinaitwa nguvu ya mvuto, lakini pia huenda mmeshawahi kusikia au kusoma kitabu kinachoitwa “The Secret.” Ni kitabu kizuri sana kinachoeleza kwa kirefu na kwa lugha nyepesi inayoeleweka jinsi nguvu hii ya mvuto inavyofanya kazi. Katika kitabu cha The Secret mwandishi Rhonda Byrne anasema kwamba mawazo yetu ni kama sumaku. Kwa kawaida sisi wanadamu tumezungukwa na nguvu ambazo hatuzioni lakini zipo kwa hiyo Kwa jinsi tunavyofikiri hayo mawazo yanakuwa na nguvu ambazo zinavuta kila kitu tunachowaza, kiwe kizuri au kibaya, ni lazima kitarudi kilipotoka, ambapo sipengine bali kwako wewe mwenyewe.

Rhonda anazidi kubainisha utendaji wa mawazo yetu kwa kutoa mfano wa ufanyaji kazi wa Luninga (TV). Kama wote tunavyofahamu kuwa ili kituo cha kurusha matangazo ya Luninga kifanye kazi kunakuwa na minara inayosafirisha mawimbi na kuyageuza katika mfumo wa picha na hivyo kutuwezesha kuona matangazo ya luninga tukiwa majumbani kwetu. Wengi wetu hatufahamu mitambo hiyo inafanya kazi namna gani, lakini tunafahamu kwamba kila chaneli ina mawimbi yake ambapo kila tukichagua chaneli fulani tunapata picha katika luninga zetu. Tunachagua mawimbi kwa kubadilisha chaneli na ndipo tunapopata picha za matangazo kutoka katika chaneli hiyo. Kama tunataka kuona picha na matangazo tofauti katika luninga zetu tunabadilisha chaneli kwa kutafuta mawimbi ya chaneli nyingine.
AR.jpg

Sisi kama wanaadamu tuko sawa na mnara wa kurusha matangazo ya luninga na tuna nguvu kuliko minara ya kurusha matangazo iliyowahi kuwepo hapa duniani. Mawimbi yetu ndiyo yanayoratibu maisha yetu na ndiyo yanayoifanya dunia iwe kama livyo leo, kwani tunatengeneza mawimbi kutokana na namna tunavyowaza. Ile picha tunayopata au tunayoiona kupitia mawazo yetu, sio sawa na ile tunayoiona katika luninga zetu sebuleni kwetu, bali ni picha ya maisha yetu! Mawazo yetu yanatengeneza mawimbi na yanavuta kila tunachokiwaza na kuwa ndio maisha yetu halisi.

Iwapo tunataka kubadili chochote katika maisha yetu, basi inatulazimu tubadili chaneli na mawimbi kwa kubadili namna yetu ya kufikiri. Mwandishi huyo anaendelea kusema, kinachosabisha watu wengi wasipate kile wanachokitaka maishani ni kwa sababu wanafikiria zaidi kuhusu kile wasichokitaka badala ya kile wanachokitaka. Hebu tujaribu kuchunguza mawazo yetu na kauli zetu, tutagundua siri kubwa. Kwani nguvu ya mawazo ipo na inafanya kazi. Ugonjwa mkubwa sana unaowakabili wanadamu hapa duniani karne kwa karne ni ugonjwa wa “sitaki” au “sipendi,” anabainisha mama huyo. “Watu wameendelea kuacha ugonjwa huu uendelee kutawala katika mawazo yao, vitendo vyao na kauli zao, wakiendelea kuzingatia yale wasiyoyataka au wasiyoyapenda.” Anamalizia kusema mwandishi huyo.

Ugonjwa huo ndio unaowatesa baadhi ya wanawake wanaotafuta wapenzi. Mfano halisi ni kauli kama, “mimi sipendi wanaume wafupi,” au “mimi sipendi kuolewa na mwanaume mnyanyasaji….” na kauli nyingine zinazofanana na hizo. Ukweli ni kwamba kitakacho watokea wanawake wenye kutoa kauli kama hizo ni kuishia kuolewa na wanaume wa aina hiyo….. kinachofanyiwa kazi na mawazo yetu ya kina (Unconscious Mind) ni kile tunachokitamka, iwe ndicho tunachokitaka au tusichokitaka, mawazo yetu ya kina hayajui neno sipendi au sitaki, hukuletea kile ulichokitamka na kukijaza katika akili yako.
black-successful-woman-thinking.jpg

Kuna wanawake wengi ambao wameolewa au wamewahi kujenga mahusiano na wanaume ambao waliwahi kutamka hadharani kwamba kamwe hawatoweza kujenga mahusiano nao au kuolewa nao. Hayo ni matokeo ya kauli zao ambazo walizitamka bila kujua madhara yake. Kwa hiyo basi kwa kutumia kanuni hiyo ya mvuto kama alivyosema mwandishi Rhonda Byrne mnatakiwa kuanza kuratibu mawazo yenu na kauli zenu kwa kutamka aina ya wanaume ambao mngependa kujenga mahusiano nao au kuolewa nao na haiishii hapo ni vyema mkajiweka katika mazingira ambayo yatawavuta kuelekea mahali ambapo mtakutana na aina ya wapenzi muwatakao. Huwezi tu kukaa nyumbani kwako au kutembelea eneo moja hilo hilo kila siku halafu utarajie kukutana na aina ya mpenzi umtakaye itakuwa ngumu, labda uwe na bahati sana.

, ACHA KUPOTOSHA KUPITIA STORY , NDIYO MANA UATKUTA WATU WANAACHA KUJISHUGHULISHA WANASOMA VITABU ILI KUPATA MAJIBU, ETI THINK BIG, SJUI NINI HAAA !, Hayo mambo hutegemea sana mambo makuu matano. 1) personality ya mtu, 2) Socialization ya mtu 3) level and interaction capacity, 4) types of social network. 5) socio- economic status.
 
Mi nishasoma The Secret na Movie yake pia nikaiangalia. Nikafanya ka experiment kidogo kakawa, but sikuipa much thought afterward. For me i dont know what it is yet lakini naona kama inakinzana na mafundisho yangu ya dini hata kama formula ni ile ile ya kuamini na utapewa. I wonder in my humble kinda way pale tukipata kuijua na kuitumia vyema kutakuwa na limit kweli? Si itakuwa uwanja wa fujo? Na kwa wale wamuaminio Mungu si ni sawa na kumvua Mungu uwezoe maana hapa naona hakuna mpaka au nijiulize na kujijibu kuwa Mungu (The Universe according to The Secret) yupo kwa ajili ya ku serve our every need tu. Msaada Mtambuzi
Thank you

Upo sahihi ukikiamini kitabu hiki ni kama unamtoa Mungu pembeni.Niliwahi kukisoma ilifika sehemu niliacha maana kinakupa nguvu sana unaweza kuitumia vibaya personally nimekitumia hata kwenye case ambazo unaona kabisa ni makosa
Ni biblia na Quran naamini ndio best books na utapata kila utakacho huko shida tu vitabu hivyo vinahitaji ujue kufumbua mafumbo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom