Mwanamke Je, bado una hisia za kumpenda mpenzi mliyeachana?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 16, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi JF Gold Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,275
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 48
  [​IMG]
  Kuondokana na hisia za mapenzi dhidi ya mpenzi uliyetokea kumpenda sana lakini mkaachana katika mazingira ambayo hukuyatarajia, si jambo rahisi na hasa kama wewe ndiye uliyeachwa. Unaweza kujiambia kwamba amekosea sana kukuacha na kamwe hatoweza kumpata mwanamke atakayempenda kama ulivyompenda wewe. Lakini kiukweli ndani ya moyo wako unampenda na kitendo cha kukuacha bado kinakuumiza na kukutesa. Inawezekana pia ukawa unatamani sana akurudie kwa sababu ulimpenda sana na unahisi upweke moyoni. Kwa mwanamke aliyeachwa, kuwaza hivyo ni jambo la kawaida kabisa, labda kama hukutokea kumpenda mwanaume huyo. Lakini kama miezi na miaka inapita na bado unaendelea kuwa na mawazo ya aina hiyo, basi hilo litakuwa ni tatizo, na hapa chini nitajaribu kueleza namna ya kuondokana na mawazo ya aina hiyo na kuendelea na maisha, kwani kuachwa na mpenzi sio mwisho wa dunia.
  [​IMG]
  1.Unamuwaza muda wote

  Hili ni jambo la kawaida, lakini duh, kama unajikuta unamuwaza mpenzi aliyekuacha muda wote na kujikuta unashindwa kufanya mambo yako ya msingi kwa ustawi wa maisha yako, basi hilo ni tatizo ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi. Ingawa waswahili husema “lisilo machoni, halipo moyoni,” lakini mimi nasema sio kila lisilo machoni halipo moyoni, kwa swala la mapenzi nadhani iko hivyo. Ukweli ni kwamba hujui yuko wapi, anafanya nini au yuko na nani na hapo ndipo utakapojikuta ukitafuta picha mlizopiga mkiwa pamoja wakati wa kilele cha mapenzi yenu, na wakati mwingine unaweza kusikia wimbo fulani ambao aliupenda sana ukakukumbusha tukio lililowakuta mkiwa pamoja ambalo linahusiana na wimbo huo. Kwa kifupi ni kwamba, ni jambo la kawaida sana kumkumbuka mpenzi mliyeachana mara kwa mara baada ya kuachana. Lakini kama mawazo hayo yanaonekana kukuumiza na kukupotezea muda basi jua kwamba, jambo hilo linaweza kukuletea matatizo makubwa sana kiafya.

  Namna gani utaondokana na tatizo hili: Muda ni nyenzo muhimu sana katika kuponya. Kama unashindwa kupata suluhu ya namna ya kuondokana na mawazo ya huyo mpenzi mliyeachana naye, basi jipe muda, kwani kwa kujipa muda zaidi unajipa nafasi ya kuponya majeraha ambayo yanaonekana kukutesa. Kwa jinsi muda unavyochukua nafasi ndivyo unavyomudu kusahau na ndio maana waswahili husema yaliyopita si ndwele tugange yajayo
  [​IMG]
  2.Unaogopa kumkubali mwanaume mwingine…

  Mojawapo ya dalili za kuonyesha kwamba bado unamkumbuka mpenzi wako uliyeachana naye ni kitendo cha kuogopa kuwa na mtoko na mwanaume mwingine. Unachofanya na labda hukijui ni kulinganisha wanaume wanaokuomba mtoko na huyo mpenzi wako, na mara nyingi kinachotokea ni kwamba kila mwanaume unayekutana naye anakuwa na tofauti kubwa na mpenzi uliyeacha naye na hapo ndipo unapojikuta ukishindwa kukubali kutoka naye. Jambo usilolijua ni kwamba sifa za huyo mpenzi wako uliyeachana naye unaziweka juu sana kiasi kwamba kila mwanaume unayekutana naye unashindwa kumpa nafasi kwani unajaribu kumfanya huyo mpenzi wako mliyeachana naye kama vile ni mtu asiye na kasoro kabisa jambo ambalo si kweli.

  Namna ya kuondokana na tatizo hilo: Usilazimishe. Kama huko tayari kutoka na mwanaume mwingine, basi jipe muda kwani ukilazimisha, hutakuwa unamtendea haki huyo mpenzi mpya kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kugombana mapema mno kutokana na kujaribu kwako kutaka kumbadilisha afanane na mpenzi mliyeachana naye. Na kama ikitokea uhusiano wenu ukavunjika mapema, itakuumiza zaidi. Hata hivyo naomba kutahadharisha kwamba kuwa na mtoko na mwanaume haina maana ya kuingia katika mahusiano. Wakati mwingie kuwa na mtoko na mwanaume na kujirusha katika klabu mbalimbali za starehe inasaidia sana kuharakisha kukuondoa katika maumivu ya kuachana na mpenzi wako wa zamani.
  [​IMG]
  3. Unaumia sana baada ya kumuona akiwa na mpenzi mwingine….

  Inaumiza sana baada ya kugundua kwamba mpenzi wako kapata mpenzi mwingine nakuendela na maisha muda mfupi tu baada ya kuachana kwenu. Yaani wakati wewe bado unauguza vidonda vya kuachana na mpenzi wako, yeye zamaaani keshakusahau na kusonga mbele na maisha huku akiwa na mpenzi mpya. Hii inauma sana na ni sawa na kukupiga kofi la usoni.Iwapo umeachana na mpenzi wako halafu inatokea unamkuta akiwa na mpenzi mwingine na hali hiyo ikawa haikushtui wala kukukera basi jua kwamba, jambo hilo limeshapita na umemudu kuondokana nalo. Lakini kama ukikutana na mpenzi mliyeachana akiwa na mwanamke mwingine na jambo hilo likakuumiza kihisia na kuhisi wivu basi ujue kwamba, bado unampenda mpenzi huyo na bado hujamudu kumuondoa mawazoni mwako.

  Namna ya kuondokana na tatizo hilo: Endelea na maisha na huhitaji kujiumiza kwa kumuwaza sana, haitakusasidia kumrudisha. Ni kweli kwamba, kitendo cha kumuona akiwa na mwanamke mwingine kinakera na kinaumiza hisia, lakini kumbuka kwamba huna jinsi, maji yameshamwagika. Jaribu kuutumia muda wako mwingi na marafiki au familia yako na jichanganye na marafiki wenye upendo ambao watakufariji na kukutoa katika simanzi ya kujeruhiwa kihisia.
  [​IMG]
  4. Bado unatembelea maeneo mliyokuwa mkitoka pamoja…

  Kama unajikuta bado unatembelea katika maeneo mliyokuwa mkitoka pamoja wakati wa kilele cha mapenzi yenu, inaweza ikawa ni kwenye Mghahawa, ukumbi senema, au klabu ya usiku, basi inawezekana bila kujijua unajikuta ukipenda kutembelea katika maeneo hayo ukitarajia kuonana naye. Lakini inawezekana ukawa unatembelea maeneo hayo ukiwa na dhamira ya kuonana naye. Unaweza kujipamba hasa na lebasi za ulimbwende na mavazi ya thamani na kwenda katika maeneo hayo kwa lengo la kutaka akuone jinsi ulivyo mzuri na ulivyopendeza ili akurudie. Kama unajikuta ukifanya hivyo, basi jua kwamba hujaondokana na jakamoyo la kuachwa na kama akikuona asipoonyesha kujali wala kuvutiwa na wewe, utaumia zaidi.

  Namna ya kuondokana na tatizo hilo: Acha ujinga mwanamke. Fanya kinyume chake na badilisha maeneo ya kutembelea na punguza mitoko kwa kadiri uwezavyo kama unayo dhamira hasa ya kumuondoa katika mawazo yako. Iwapo marafiki zako unaotoka nao wanasisitiza kwenda katika maeneo ambayo mlikuwa mkitoka na huyo mpenzi wako na unahisi unaweza kukutana naye, kutokana na yeye kupenda sana kutembelea maeneo hayo, basi ni vyema usitishe huo mtoko.
  [​IMG]
  5. Unafanya vibweka katika mitandao ya kijamii......

  Hii mara nyingi hufanywa na mabinti wa siku hizi wanaotumia mitandao ya kijamii kama Facebook, twitter nk. Mabinti wa siku hizi hutumia sana mitandao ya kijamii katika kuwasiliana na kuweka picha za matukio yanayowahusu. Iwapo inatokea unatumia mbinu mbalimbali za kuweka picha zako katika mitandao ya kijamii ambazo zinaamsha hisia za mapenzi kwa nia ya kumvuta mpenzi wako ili akurudie, unaweza kujisikia vibaya na labda kuumia kihisia kama itatokea hataguswa na picha hizo.

  Namna ya kuondokana na tatizo hilo: Usiwe mtoto mdogo. Kumbuka kwamba kuendelea kumkumbuka mpenzi mliyechana ni jambo lenye kuumiza sana. Ukweli ni kwamba itakuwa ni ujinga kufanya mbinu hizo za kitoto kutumia mitandao ya kijamii kutaka kumvuta mpenzi mliyeachana, kwani kitendo hicho kitakufanya azidi kukudharau na kukuponda. Jaribu kwa juhudi kubwa kutoyapa uzito mawazo yoyote yatakayokukumbusha mapenzi yenu na mpenzi mliyeachana naye. Kwani kuendelea kuyapa uzito mawazo hayo, ndio sababu ya wewe kusumbuka sana kwa mbinu mbalimbali kutaka mrudiane. Iwapo utafanikiwa kuyazika mawazo yote kuhusu huyo mpenzi mliyeachana, hakika utamudu kusonga mbele kwa ustawi wa maisha yako……………….
  [​IMG]
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 26,894
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 48
  Katika mambo ambayo yanatesa hisia za wanawake ni hili,mimi binafsi kama mwanaume nikikutana na mwanamke wa aina hii,ili kumsaidia nitakuwa rafiki yake na sio kutaka kuwa mpenzi.Kuwa rafiki kuna maana ya kumsaidia na kumpa kampani ya kumsaidia kujua kuwa maisha bado yana maana.Ni jambo gumu sana kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mtu wa aina hii!
   
 3. felinda

  felinda JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  msg delivered,,,,,,,,,,,,,i will work on it!
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,168
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 48
  mmmm, asante!
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 32,869
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 113
  Kweli Mtambuzi umetoa msaada mkubwa!
   
 6. mito

  mito JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 6,494
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 83
  Ila kuachwa jamani mmh ..... kusikie tu kwa jirani!
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,846
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 38
  Kibuti kibaya mkuu....maana kichaa chake hakina dawa mirembe.
   
 8. N

  Neylu JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,637
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  Duh... Mi hata kuielezea hii kitu inanishinda.. Hayo machungu yake jamani hayaelezeki..! Kutokana na mazingira tuliyoachania na huyo bwana kwa kweli haijatokea hata siku moja nikatamani nimrudie maana niliumia sanaaa na nikahisi hata ningejipendekeza tena kwake ningeambulia maumivu plus plus.!
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi JF Gold Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,275
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 48
  Pole binti, naamini yaliyopita si ndwele sasa ganga yajayo..............................
   
 10. N

  Neylu JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,637
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  Asante sana Baba Ngina... Aaah.. Saivi niko na life nyingine kabisa sina hata muda nae huyo..!
   
 11. Fhorbity

  Fhorbity Member

  #11
  Apr 30, 2013
  Joined: Apr 12, 2013
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  da namimi imetokea kama hyo nimeachwa na mpenzi nilo mpenda sana yani sijui hata nifanye nini
   
 12. P

  PreetG Senior Member

  #12
  Apr 30, 2013
  Joined: Apr 23, 2013
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilijifunza kusamahe, kusahau na kumove on na maisha yangu!
   
 13. babby

  babby Member

  #13
  Apr 30, 2013
  Joined: Apr 23, 2013
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nampenda sana!! sijui kama ntaweza kumsahau..R.I.P ma luv
   
 14. amu

  amu JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,925
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 48
  Mtambuzi ahsante
  halafu naomba muulize huyu Mentor ananitaka? aseme tu maana kila nikiingia naona kanimention na kuniunganisha na wanaume za watu humu ndani watu, watu wanandoa zao humu na mahawara kila kona anataka alete vita vya dunia? Mentor naomba useme tu manake niko single, am available kabla sijapokea proposal za wengine
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. amu

  amu JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,925
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 48
  halafu kwa nini nyie wanaume mnamtenda mtu akishamove on na maisha yake kakusahau unarudi mikono nyuma magoti umepiga kuomba msamaha???/
   
 16. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2013
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 14,037
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 63
  mbona hii kama ngekewa..too good to be true.

  Yes Raiza nakupenda, nakutaka, nakuhitajiiiii
  Moyo wangu wakuwaza vile uko mbali nami....

  I want you, I love you then I need youuuuu
  My heart is thinking of you though you are far away from me...

  Je veux que vous, Je t'aime, puis J'ai besoin de vous
  mon coeur pense à toi si tu es loin de moi.

  Kaka BAK nisaidie kumwekea link hapo.

  ...anxiously waiting.:pray2:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. amu

  amu JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,925
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 48
  subiri nimalize ku:mvutaji::mvutaji::mvutaji: nitakurudia
   
 18. B

  Baraka mungure Senior Member

  #18
  Apr 30, 2013
  Joined: Apr 10, 2013
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapenz ndo hayo! Katika mapenz msipokuwa na neno moja tu "Nisamehe" hayo mpenz huwa hayafiki mbali epuken maneno ya watu. Niushaur tu mwenyewe cjaingi ktk mapenz.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2013
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 43,970
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mentor suuzika roho yako
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2013
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 14,037
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 63
  Cc: mbebs Raiza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 21. S

  Septemba11 JF-Expert Member

  #21
  May 1, 2013
  Joined: Jan 18, 2013
  Messages: 262
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Somo zuri sna mkuu!
   
 22. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #22
  May 1, 2013
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 12,819
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 48
  Mapenzi yataka uvumilivu.
   
 23. Lady doctor

  Lady doctor JF-Expert Member

  #23
  May 1, 2013
  Joined: Apr 13, 2013
  Messages: 8,768
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Somo nzuri sana, linatufaa sana nasisi wapewa vibuti watarajiwa he hehe..
   
 24. INGENJA

  INGENJA JF-Expert Member

  #24
  Mar 10, 2014
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 1,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 38

  Nadhani hili haliwahusu wanawake tuu,hata wanaume kwaupande mwingine linatugusa..staki kuamini kama kweli wanawake ndo wanaoteswa zaidi na mapenzi kuliko wanaume,hii kitu inaweza kuwa the same lakini kwakuwa wanaume hujitia viburi basi huweza kuyaficha baadhi ya maumivu yao kwa nje walau kwanyakati tuu..

  Kwamfano; mwanume anapo ingia kwenye mahusioano mapya muda mfupi baada ya kuachana na mwenza wa zamani hii maranyingi huchagizwa na unguli tuliojitia vichwani kuwa tunauwezo wakushawishi na kumpata yoyote hata akiondoka huyu tena tukijia huenda akawa mrembo zidi ya huyu,lakini kwa uwelewa wangu hii yote nikama malipizi au kujipepetua mbele ya mpenzi wazamani ili akuone bado upo,lakini dhahiri shahiri kuna maumivu na mateso ndani ya huo moyo.

  Nadhani hii ni kutoka na asili ya mwanaume iliokatika uumbaji zaidi kuwa mwanaume nimwepesi wa kuyakubali na kuyakabili matatizo yake kwa wakati wowote ya napomkumba..

  Nihayo tuu mdau ntafurahi kuzipokea changamoto katika hii comment
   
 25. Bantu lady

  Bantu lady JF-Expert Member

  #25
  Mar 10, 2014
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 2,788
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Asante Mtambuzi, kwa maelezo mazuri.
  Kuachana kunauma mmmmh!!!!!
   
 26. Mr.genius

  Mr.genius JF-Expert Member

  #26
  Mar 11, 2014
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 18
  Duuu mkuu Mentor umetisha mzaz yaan kwa vochal hizo hatoki mtu hapo!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016

Share This Page