Iselamagazi
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 5,918
- 6,007
Kumbe wakati mwingine unaweza ukamsababisha mwenzi wako akakucheat!Sikia hii,.Mke ni mhasibu wa shirika la umeme tanzania Tanesco,mkoa wa Tabora(sio jina sahihi).Mumemi mwajiriwa serikalini,mume huyu amekua bize sana kiasi kwamba kumpata nyumbuni ni bahati labda usiku kuanzia saa 6 usiku.Kwa maelezo ya mkewe ni kwamba mumewe akifika huwa amechoka sana na wakati mwingine hali chakula ambacho mkewe hujitahidi kukipika hata kama nae huwa bize kiasi gani,amejiwekea utaratibu chakula cha usiku lazima apike yeye.Siku ya tukio mumewe alikua amesafiri kwa muda mwezi na nusu kikazi Dar,siku aliyotakiwa kurudi alimpigia mkewe simu kuwa atapitia Shinyanga kwenye semina itakayochukua siku mbili,lakini alipofika Shinyanga akapewa taarifa kuwa semina imeahirishwa,ikabidi ageuze kurudi Tabora,alipofika Nzega akakumbuka hajamjulisha mkewe dharula iliyojitokeza,akaamua kumpigia mkewe simu,lakini ikawa haipatikani,alifanya hivyo mara kadhaa bila mafanikio,akaamua aende tu,kabla ya kufika nyumbani akamkuta mkewe akifanya ngono na kijana ambae anaishi jirani na pale.Ulitokea mtafaruku watu wenye busara wakalizima zogo lile.Yule bwana akasema hamuitaji mkewe,ila wakashauriwa waende kanisani kutatua mzozo kwani walikua ni watu wazima!Kweli walienda ndipo mkewe yule bwana alipofunguka na kudai mumewe amekua hampi haki ya ndoa na kama akimpa ni mara moja kwa wiki mbili na hata hiyo mara moja siyo ya kuridhisha,alipoulizwa mumewe alikubali lakini akadai ni ubize kazini ndo chanzo!Bahati nzuri padri aliwaelesha makosa yao wakaombana msamaha yakaisha.Sasa huyu mwanamke ana makosa?Inawezekana alikosea kufanyia home lakini chanzo cha tatizo ni mumewe!So kucheat kwingine kuna mashiko!
Confronted with gossip! Watu wa Tabora tunawajua.