Mwanamke auawa kikatili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,115
Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30 ambaye hakutambuliwa jina lake, ameuawa kikatili na kisha kukatwa sehemu zake za siri na watu wasiojulikana.

Mwili wa mwanamke huyo umegunduliwa asubuhi ya Februari 16, mwaka huu, katika kitongoji cha Magema, kijiji cha Nyamarembo, kilometa kama sita kutoka makao makuu ya wilaya ya Geita ukiwa umewekwa chini ya mti mkubwa ukiwa bila nguo.

Mwili huo uligunduliwa na mwanamke aliyekuwa katika matembezi yake na kisha kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kuibua hofu kubwa katika mji wa Geita na vitongoji vyake, huku wengi wakilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Alexi Evaristi, amesema kuwa baada ya kugunduliwa kwa mwili huo walitoa taarifa polisi ambao walifika katika eneo hilo pamoja na daktari na baada ya uchunguzi mwili huo ulizikwa jirani na eneo ulipookotwa kutokana na kutotambuliwa.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi, akiwemo Twikalehe Bwire ambaye ni kiongozi wa shina namba 4 lilipotokea tukio hilo, walielekeza shutuma zao kwa waganga wa kienyeji ambao wameibuka kwa wingi katika maeneo hayo licha ya serkali kufuta leseni zao.

Kwa upande wake, Kamanda wa Ulinzi wa Jadi katika kitongoji hicho, Sung'ho Gamaya, pamoja na kulihusisha tukio hilo na imani za ushirikina, alidai kuwa maiti hiyo ilihamishiwa eneo hilo baada ya mtu huyo kuuawa sehemu nyingine tofauti.

Alisema katika eneo ulipokutwa mwili huo hapakuwepo na dalili zozote za kuwepo kwa pukurushani, hali inayowafanya waamini huenda mwili huo ulipelekwa eneo hilo baada ya kuuawa na kunyofolewa sehemu ya siri.

Tukio hili limekuja huku kukiwa na ongezeo la waganga wa jadi wanaodaiwa kuendesha huduma hiyo kwa kuhamahama ikiwemo kufikia katika nyuma za wageni na kuzungunguka mitatani na vijijijini kutafuta wateja.

Afisa Utamaduni Wilaya ya Geita, Mufungo Pharesi, alipotakiwa kuzungumzia kuwepo utitiri wa waganga wa jadi wilayani humo wakiwemo wanaodaiwa kutoka nje ya nchi, alisema hatambui kuwepo kwa waganga hao kwani vibali vyote vilishafutwa.



CHANZO: NIPASHE

 
poleni wana-Geita kwa msiba huo.Hata hivyo mtu anafariki hata ndugu na jamaa kushindwa kumtambua?,au hakuaga nyumbani?.
 
Back
Top Bottom