Mwanamke anayewatesa majirani kwa Kelele za Ngono atiwa Mbaroni tena

Mar 6, 2010
74
0
Mwanamke Anayewatesa Majirani Kwa Kelele za Ngono Atiwa Mbaroni Tena

Tuesday, March 23, 2010 1:52 AM

Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye alishawahi kufikishwa mahakamani kutokana na makelele yake ya kimahaba anayoyatoa wakati akifanya mapenzi na mumewe ametiwa tena mbaroni kwa mara nyingine baada ya kuwasumbua tena majirani zake kwa kelele zake za ngono.Caroline Cartwright alifikishwa mahakamani wiki nane zilizopita kwa kuvunja amri ya mahakama ya kutowasumbua tena majirani zake kwa kelele zake za ngono anapofanya mapenzi na mumewe, Steve.

Caroline mwenye umri wa miaka 49 alihukumiwa kifungo cha nje wakati huo na kuamuriwa aache kupiga kelele wakati wa tendo la ndoa na mumewe.

Lakini wiki iliyopita Caroline alitiwa tena mbaroni kwa kuwasumbua majirani zake na kelele za ngono kwenye majira ya saa nne asubuhi ya siku ya jumapili.

"Ilikuwa ni dakika 10 tu sio masaa mawili kama kawaida yetu, iweje majirani wametusikia wakati kitanda tulikiamshia chumba cha chini na sio chumbani", alilalamika Caroline.

Mwaka jana Caroline kutokana na kosa kama hili alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 12 na kuamuriwa asitoe kelele tena wakati akifanya mapenzi kwenye maeneo yoyote ya nchini Uingereza na Wales.

Mahakama ilisikilizishwa sauti anazotoa bi Caroline Cartwright wakati akifanya mapenzi na mumewe Steve Cartwright na kuungana na madai ya majirani wa mtaa wake ambao walisema kuwa kelele zake huwakosesha usingizi kwani ni sawa na kelele za mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali sana wakati akijeruhiwa au kutolewa roho.

Ilidaiwa pia kuwa hata jirani yake mmoja ambaye ni nusu kiziwi hukosoka usingizi kelele hizo zinapoanza.

"Sauti anazotoa Caroline na miungurumo ya mumewe Steve si za asili ni kama vile wote wawili wapo kwenye maumivu makali sana", mahakama iliambiwa katika kesi yake ya awali.

Caroline atafikishwa tena mahakamani mei 13.

ILIKOTOKEA: Mwanamke Anayewatesa Majirani Kwa Kelele za Ngono Ashindwa Kesi - JamiiForums
 
Tusaidieni hizo sheria zije na China. Hawa jamaa ovyo sana kwani wake zao wanalia sana usiku. Utasikia kelele kila kona hasa usiku wa kuanzia saa 6.
 
Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye alikuwa akiwatesa majirani kwa sauti zake kali za kimahaba wakati akijamiiana na mumewe ameshindwa kesi ya rufaa kupinga kupigwa marufuku baada ya mahakama kusema sauti anazotoa si za kawaida ni kama sauti za mtu aliye kwenye maumivu makali sana ya kujeruhiwa au kuuliwa.

Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye alipigwa marufuku na mahakama kuwasumbua majirani zake kwa kelele zake kali za kimahaba anazotoa kila anapofanya mapenzi na mumewe, ameshindwa kesi yake ya rufaa aliyofungua kupinga hukumu hiyo.

Mahakama ilisikilizishwa sauti anazotoa bi Caroline Cartwright wakati akifanya mapenzi na mumewe Steve Cartwright na kuungana na madai ya majirani wa mtaa wake ambao walisema kuwa kelele zake huwakosesha usingizi kwani ni sawa na za kelele za mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali sana wakati akijeruhiwa au kutolewa roho.

Mahakama ilisikilizishwa dakika 10 za kaseti ya sauti iliyorekodiwa wakati bi Caroline na mumewe wakifanya mapenzi usiku na kuukosesha usingizi mtaa mzima.

Hata jirani yake mmoja ambaye ni nusu kiziwi hukosoka usingizi kelele hizo zinapoanza.

"Sauti anazotoa Caroline na miungurumo ya mumewe Steve si za asili ni kama vile wote wawili wapo kwenye maumivu makali sana", mahakama ya mjini Newcastle iliambiwa.

Majirani, wapita njia mpaka mfanyakazi wa posta walitoa malalamiko yao kuhusiana na kelele hizo.

Caroline na mumewe walipigwa marufuku na mahakama kupiga makelele au kuongea kwa sauti kubwa zinazotoka nje ya nyumba yao lakini Caroline Cartwright, mwenye umri wa miaka 48, alikata rufaa kwa misingi ya haki za binadamu baada ya kupandishwa tena kizimbani kwa kuivunja amri ya mahakama ya kutowasumbua majirani zake kwa kelele zake za kimahaba.

Akitoa hukumu jana jumanne, jaji wa kesi hiyo alisisitiza hukumu iliyotolewa mwanzo iendelee na Caroline ataendelea kupigwa marufuku kupiga kelele zake za kimahaba.

Caroline Cartwright aliiambia mahakama kuwa anashindwa kujizuia kutoa sauti anazotoa.

"Nimejaribu kujizuia sana nimeshindwa, nimejaribu hadi kuweka mto usoni kwangu kupunguza kelele bila mafanikio", alisema.

Hata hivyo jaji alitupilia mbali utetezi huo.

"Hatuna shaka kuwa kelele unazotoa zinaweza kusikika kwenye nyumba za jirani, mtaa wako na mitaa ya jirani", alisema jaji huyo.

Jaji huyo aliendelea kusema kuwa kelele hizo zinasababisha kero kwa majirani kwakuwa huendelea kwa masaa kadhaa.

"Hali hii inasababisha kero kubwa kwakuwa inatokea karibia kila usiku", alisema jaji huyo.

Mahakama iliambiwa kuwa kelele hizo huanza majira ya saa sita usiku na huendelea kwa masaa kadhaa wakati mwingine mpaka asubuhi.

Jirani yake wa mlango unaotizamana bi Rachel O'Connor aliiambia mahakama "Kelele wanazozitoa si za kawaida, siwezi kuzielezea, sijawahi kusikia kitu chenye mfano wake".

"Huwa naweka sauti ya TV yangu hadi mwisho chumbani kwangu lakini sauti zao huizidi sauti ya TV yangu na huwa nashindwa kusikia chochote toka kwenye TV", bi O'Connor aliiambia mahakama.

Mwanzoni mwa mwaka huu bi Caroline Cartwright alipewa onyo la miaka minne na mahakama kutowasumbua watu kwa kelele zake kokote kule nchini Uingereza.

Lakini alipandishwa kizimbani wiki chache baade baada ya kukiuka mara tatu maagizo aliyopewa na mahakama ndani ya siku kumi tangia alipoonywa.
 

Attachments

  • 903513.jpg
    903513.jpg
    23.1 KB · Views: 69
Back
Top Bottom