mwanamke ambaye hajaolewa vs mwanaume ambaye hajaoa.

Oh Lizzy dearest.... Ndoa haina adabu kama ilivo Mapenzi hayana adabu.... Believe me. Mie ni moja wapo napenda saana ndoa, napenda wanandoa, napenda institution ya ndoa.... Na bana am telling you haina formulae... Siku zinavozidi kuenda ndio mtihani zaidi waongezeka... Wanaume ambao ni wanaume kweli wa kuoa idadi imeshuka, Wanawake ambao ni wanawake kweli potential wives ndo inapotea kabisa (mabinti wanashindwa kutofautisha haki sawa na wanaume na majukumu yake ndani ya ndoa; yaani kuchanganya mambo kuenda mbele)

Kwa mantik hio, unayoongea ni ya msingi... And to God I wish it was simple and possible... BUT i know kazi ipo. Labda with extra effort kama ulivo suggest iwezekane... But kazi ipo... Na katika institutiona ya ndoa walau akina mama tunajitahidi saana kuheshimu ndoa zetu, mtihani unabaki kwa hawa watoto wakubwa hawa.... Dah! Nashindwa niseme nini...

Ndo unajikuta tu you as a wife unaipaka tu rangi ndoa ambayo kumbe ni ndoano... Sometimes hata huelewi kwanini. But Mungu mkubwa kuna wengine hatimae zinarudi katika mstari... One thing i know for sure ni kua kama wenye matatizo na ndoa zao woote waamue kua waachie ngazi - katika mia zitabaki literally hata saba tu!

Unajua kwanini nimesema sifa zitolewe pale zinapostahili tu dearest???Kwasababu hizo sifa bure ni moja wapo ya vigezo kwa watu kuingia kwenye ndoa. Unakuta mtu anaolewa/oa tu ili aheshimike mbele ya jamii na sio kwasababu anampenda sana mwenzake au hata kutaka kumuoa/olewa nae. Hivyo hiyo heshima ilipaswa iwe earned....ili watu wajue kwamba kuingia tu kwenye ndoa hakutoshi kukufanya uonekane unafaa sana mbele ya jamii bali matendo yako ndani ya ndoa ndio yatakayoamua hivyo.

Binafsi sishauri walioingia watoke ila nasisitiza waliopo nje wasiingie tu ili mradi.

Hahahah..alafu we unawatetea kina mama ehhh??
Siku hizi si wababa..si wamama.. wote wamekua waharibifu aisee!!!
 
DoubleR,AshaDii na Lizzy,habari za jioni.
Nina mengi ya kukwambieni kuhusu mada hii lakini sitaki.
goodnight.
Just know kwamba mengi mliyosema katu sikubaliani nayo,more importantly ni la kusema eti 'wasio na ndoa wanatamani wawe nazo' balls ! Ninachojua mimi na ni kwa uhakika wa asilimia 100 wanandoa wengi (hasa wanaume) wanatamani wangeturn back the time na waendelee kuwa ma bachelor,mnabisha? Mengine sisemi.
 
Hio paragraph in blue ndo nimekupata vema sasa.... Kwamba hizo sifa za kupaka rangi zinafanya wengi waingie mkenge, ambalo kwa kweli kwa kiasi kikubwa saana ni kweli.

Sasa wee Lizzy nitaacha kujitetea tena na hali mi pia ni mmama?? lol... ila bana tuende mbele turudi nyuma ni kweli kabisa kua woote wamekua waharibifu but wababa wamezidi bana!! Afadhali kiduchu sie akina mama.... (naomba usibishe... kwa hisani ya watu wa Marekani)
 
B' mie nitaongea na wewe kesho... Saizi uko via mobile, ni wazi kabisa upo counter ya juu....lol... Na mtu wa counter ya juu anakua sio mwenzio kabisa ki mjadala.
 
Bishanga yapi sasa usiyokubaliana nayo???

Hilo la walio nje wanazitamani hata mimi sikubaliani nalo kwa kiasi kikubwa ila wapo watu wanaozitamani sana tu.

Hehehheeh..ngoja niache hilo la wamama kama lilivyo!!!
 
Hivi katika jamii nani ana set standards za hicho kinaitwa 'maadili'?
Who are we to judge other peoples life styles?
Pilipili usiyokula yakuwashia nini?
Mtu yuko kwake na wanae wanakula,wanavaa ,wanasoma,kwenye bembea anawapeka,always she/he is there for them,sisi wengine hizi kelele ni za nini?
Watoto wangapi wanalelewa katika so called perfect arrangement ya baba na mama under one roof na unakuta baba wiki haoni watoto ni kuondoka alfajiri kurudi usiku mama mlevi,baba na mama wanapigana mbele ya watoto na matusi kwa kwenda mbele, etc.
Wana mmu jamani live and let live,tuache kuwa tunahukumu maisha ya watu,afterall kitanda usicholalia...

Unanidai like kwa hii point! Hiyo counter ya juu safi sanaaa!
 
mhhhhhhhh! ngoja nisome tu hii kitu kwani nikiingilia ni kama ntakuwa nauondoa utamu. Shukeni mavituuuuuuuuuuz watu tudese mamaaa Asad na Lizzzzzy. shukeni mambo ila hakuna hasira mie ni refa wenu, mpo hapo!
 
Mwanamke ambae Hajaolewa at age 28+ bila sababu za msingi.
  • Anaonekana kama alikua wakujirahisi hasa kama ana zaidi ya mtoto mmoja baba tofauti.
  • Anaonekana kama alikua anachagua saana wachumba mpaka kashangaa tu umri umeenda.
  • Anaonekana ana kasoro hasa mwilini (hata awe mzuri vipi) hasa maeneo husika.
  • Anaonekana kama vile sio wife material, tena usiombe ni msomi ambae ni independent.
  • Akiwa na watoto wa baba mmoja anakua defined kama nyumba ndogo...
  • Ukweli ni kwamba pamoja na kusema heshima ipo, heshima sio genuine tofauti na rika hilo mwenye mume ama aliewahi olewa.
Mwanaume kama hajaoa 35+ bila sababu za msingi...
  • Anaonekana hapendi majukumu ya kulea familia - hasa kama ana watoto.
  • Asipoonekana na wanawake mara kwa mara huonekana *******... ama kua na matatizo fulani, saa ingine hata kuzushiwa shoga...
  • Anoanekana ni player, tena mara nyingi na vibinti vidogo... (jamaa wa namna hii hupoteza hata marafiki) maana wanajua tabia zake, hawamtaki karibu na dada/wake/watoto zao..
  • Anaonekana si kamilifu mbele ya wanaume wenzake hata kama anabadilisha wanawake kama nguo...
Take NOTE: Nimeongelea wale ambao kabisa hawajawahi Oa/Olewa. ALAFU Tusidanganyane Jamani, Ndoa ina Heshima yake kubwa saana katika Jamii na macho ya Jamii.. Ni moja ya taasisi ambayo inamfanya mtu aheshimike, hata hivo wale ambao hawakubaliani na maneno yangu... sio lazima.[/QUOTE

Umenena dada! nakuletea kadi unichangie fasta kabla sijagonga 40! lol
 
Binafsi nina mtazamo wa kivyangu,sioni sababu ya kuwashaangaa hawa ambao wamezaa na kuamua kuishi peke yao bila ndoa iwe mwanamke au mwanaume,coz naamin kbs sio wote kati yao walikuwa wameyapanga maisha yao yaishie hivyo kila mmoja ana situation iliyomkuta na kujikuta yuko hivyo,wengine labda alikuwa na mtu wakashindwana njian na kuamua kuishi kivyake,mwingine kafikiria na kuona ndoa haina umuhimu kwake kutokana na sababu zake binafsi na kuamua kuzaa wanae na maisha yakaendelea,wapo wengi tu hawana hizo ndoa na ni watu wakubwa na wanaheshimika na jamii na wana maisha mzuri na wanalea watoto wao na wapo wenye hizo ndoa ni aibu tupu kila kukicha na wala hazina hata chembe ya maadili kiasi kwamba wanataman maisha yao ya single!
Yani ktk hili cha msingi jamii ielewe kila mtu ana haki ya kishii apendavyo ili mradi havunji sheria ya nchi wala hajamsumbua mtu kwa style yake ya maisha,kwan sio kweli kwamba wote wanao ishi bila ndoa hawana maadili.
 
B' mie nitaongea na wewe kesho... Saizi uko via mobile, ni wazi kabisa upo counter ya juu....lol... Na mtu wa counter ya juu anakua sio mwenzio kabisa ki mjadala.

haya,henken zishantoka kichwani,tuendelee na mada, na ninasisitizia msimamo wangu ule ule kwamba'waliomo wanatamani kutoka'.
 
Bishanga yapi sasa usiyokubaliana nayo???

Hilo la walio nje wanazitamani hata mimi sikubaliani nalo kwa kiasi kikubwa ila wapo watu wanaozitamani sana tu.

Hehehheeh..ngoja niache hilo la wamama kama lilivyo!!!
wanazitamani ndio,wakishaonja joto la jiwe(hasa wanaume) ndo wanaanza kutafuta mlango wa kutokea na hawauoni maana washaaza,ndo unasikia mke anamwambia mume...'halo mi nilijua kuolewa tu na sio kuachwa...'
 
Mwanamke ambae Hajaolewa at age 28+ bila sababu za msingi.
  • Anaonekana kama alikua wakujirahisi hasa kama ana zaidi ya mtoto mmoja baba tofauti.
  • Anaonekana kama alikua anachagua saana wachumba mpaka kashangaa tu umri umeenda.
  • Anaonekana ana kasoro hasa mwilini (hata awe mzuri vipi) hasa maeneo husika.
  • Anaonekana kama vile sio wife material, tena usiombe ni msomi ambae ni independent.
  • Akiwa na watoto wa baba mmoja anakua defined kama nyumba ndogo...
  • Ukweli ni kwamba pamoja na kusema heshima ipo, heshima sio genuine tofauti na rika hilo mwenye mume ama aliewahi olewa.
Mwanaume kama hajaoa 35+ bila sababu za msingi...
  • Anaonekana hapendi majukumu ya kulea familia - hasa kama ana watoto.
  • Asipoonekana na wanawake mara kwa mara huonekana *******... ama kua na matatizo fulani, saa ingine hata kuzushiwa shoga...
  • Anoanekana ni player, tena mara nyingi na vibinti vidogo... (jamaa wa namna hii hupoteza hata marafiki) maana wanajua tabia zake, hawamtaki karibu na dada/wake/watoto zao..
  • Anaonekana si kamilifu mbele ya wanaume wenzake hata kama anabadilisha wanawake kama nguo...
Take NOTE: Nimeongelea wale ambao kabisa hawajawahi Oa/Olewa. ALAFU Tusidanganyane Jamani, Ndoa ina Heshima yake kubwa saana katika Jamii na macho ya Jamii.. Ni moja ya taasisi ambayo inamfanya mtu aheshimike, hata hivo wale ambao hawakubaliani na maneno yangu... sio lazima.[/QUOTE

Umenena dada! nakuletea kadi unichangie fasta kabla sijagonga 40! lol
40........ndoa.......mmmmmhhhh!!!!!!!
 
DoubleR,AshaDii na Lizzy,habari za jioni.
Nina mengi ya kukwambieni kuhusu mada hii lakini sitaki.
goodnight.
Just know kwamba mengi mliyosema katu sikubaliani nayo,more importantly ni la kusema eti 'wasio na ndoa wanatamani wawe nazo' balls ! Ninachojua mimi na ni kwa uhakika wa asilimia 100 wanandoa wengi (hasa wanaume) wanatamani wangeturn back the time na waendelee kuwa ma bachelor,mnabisha? Mengine sisemi.

HAHAHAHAAAAi! sina uhakika kama umefanya research au unatumia kale ka msemo "waliomo nje wanatamani kuingia ndani ya ndoa na walioko ndani wanatamani kutoka nje ya ndoa''
 
Mwanamke ambae Hajaolewa at age 28+ bila sababu za msingi.
  • Anaonekana kama alikua wakujirahisi hasa kama ana zaidi ya mtoto mmoja baba tofauti.
  • Anaonekana kama alikua anachagua saana wachumba mpaka kashangaa tu umri umeenda.
  • Anaonekana ana kasoro hasa mwilini (hata awe mzuri vipi) hasa maeneo husika.
  • Anaonekana kama vile sio wife material, tena usiombe ni msomi ambae ni independent.
  • Akiwa na watoto wa baba mmoja anakua defined kama nyumba ndogo...
  • Ukweli ni kwamba pamoja na kusema heshima ipo, heshima sio genuine tofauti na rika hilo mwenye mume ama aliewahi olewa.
Mwanaume kama hajaoa 35+ bila sababu za msingi...
  • Anaonekana hapendi majukumu ya kulea familia - hasa kama ana watoto.
  • Asipoonekana na wanawake mara kwa mara huonekana *******... ama kua na matatizo fulani, saa ingine hata kuzushiwa shoga...
  • Anoanekana ni player, tena mara nyingi na vibinti vidogo... (jamaa wa namna hii hupoteza hata marafiki) maana wanajua tabia zake, hawamtaki karibu na dada/wake/watoto zao..
  • Anaonekana si kamilifu mbele ya wanaume wenzake hata kama anabadilisha wanawake kama nguo...
Take NOTE: Nimeongelea wale ambao kabisa hawajawahi Oa/Olewa. ALAFU Tusidanganyane Jamani, Ndoa ina Heshima yake kubwa saana katika Jamii na macho ya Jamii.. Ni moja ya taasisi ambayo inamfanya mtu aheshimike, hata hivo wale ambao hawakubaliani na maneno yangu... sio lazima.

lol! Ashadii upo makini katika hii fani. nashukuru sana kwa kunidadavulia hili swala.
 
Nani aliekudanganya kwamba ni lazima ndoa ili wawili waweze kuishi pamoja???
Wapo watu wengi tu hawajaona rasmi ila wanaishi pamoja na wanalea watoto wao kama wanao. Na wapo watu waliopo kwenye ndoa zinazotambulika ila kiukweli kule ndani ni kama vile hawapo....na watoto wanabaki kua jukumu la mzazi mmoja wakati wote wawili wanajulikana kua ni wanandoa.

Napenda definition ya ndoa ya sheria za ndoa, si lazima harusi, si lazima mahari, si lazima vyeti. Mkikaa pamoja tu kama mke na mume zaidi ya miezi kadhaa hiyo ni ndoa. Hao pia wameooana ingawaje hawana vyeti.
 
DoubleR,AshaDii na Lizzy,habari za jioni.
Nina mengi ya kukwambieni kuhusu mada hii lakini sitaki.
goodnight.
Just know kwamba mengi mliyosema katu sikubaliani nayo,more importantly ni la kusema eti 'wasio na ndoa wanatamani wawe nazo' balls ! Ninachojua mimi na ni kwa uhakika wa asilimia 100 wanandoa wengi (hasa wanaume) wanatamani wangeturn back the time na waendelee kuwa ma bachelor,mnabisha? Mengine sisemi.[/QUOTE

Nakubaliana na unachosema, ila yote ni kweli. Waliomo wanatamani kutoka illa wengi wanabaki, ambao hawamo wanatamani kuwa nazo. Ni kama tumefungwa na mtazamo fulani hivi. Ukitoka inaonekana kwamba yamekushinda na wanawake kwenye jamii yetu wanatafsiriwa vibaya zaidi. Ni uvumilivu unaozitunza ndoa.
 
nahisi wote but wanawake wanachukuliwa na jamii kuwa hawana maadili
 
Swali la msingi...kuoa ni maadili?...

hapo chacha me naona me naona enzi za mwalimu ilikuwa ni maadili nowdays afadhaili aliyesingle wengi wenye ndoa ndo wanamatukio ya kushangaza so ndoa sio maadili ka upande wangu ni matukio tu ya kawaida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom