Mwanamke aachi ana achwa je ni kwel?

MUREFU

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,331
349
Hv ninasikia mwanaume ndo anaeacha na haachwi kwan hata mwanamke akimwacha mwanaume anasema ameachwa na co kuacha akiwa anawaelezea wenzie je ni kwel?
 
huwa wanajipa matumaini kuwa nimemwacha yule,kumbe limeachwa lenyewe niliona kwa babangu mzazi,alivyokuwa anajifariji huku sisi tunamcheka maana kibuti kibaya
 
Aliyeolewa ndiye anaeachwa kwa hali yoyote...bottomline ni nani anayekuwa ameolewa!
Kama mnakuwa mlioana, then mnaachana!

................Nachukia sana kuachana wanandoa!
 
jaman mbona 2naona waz na ukwel co lazma wawe wanandoa hata wakawaida yan m2 na demu wake au mpenz wake
 
Hv ninasikia mwanaume ndo anaeacha na haachwi kwan hata mwanamke akimwacha mwanaume anasema ameachwa na co kuacha akiwa anawaelezea wenzie je ni kwel?

Mwanamke kiIslam anaweza kuacha ikiwa mwananmme hatimizi masharti. kwani ndoa kiIslam ni mkataba wa pande mbili (AKDI).

Kuachana kiIslam, haijalishi ni nani aliyemuacha mwenziwe, ni TALAKA. Kuachana ni kuachana na hakupendezi. Vyote utavosema baada ya hapo inabaki kuwa TALAKA na inawahusu watu wawili, iwe ameachwa, ameacha au wameachana inaishia ni Talaka.

Sijui kwa kiKatoliki kama imo kuacha, kuachwa, kuachana?
 
hlo nalo neno zomba ila hii ni tetez mm cjui kinacho endelea ila nilikuwa ninajua hlo 2 la kuachana peke yake
 
huwa wanajipa matumaini kuwa nimemwacha yule,kumbe limeachwa lenyewe niliona kwa babangu mzazi,alivyokuwa anajifariji huku sisi tunamcheka maana kibuti kibaya

shosti umenichekesha sana. Badala ya kumfariji baba yenu mnamcheka! Watoto wabaya nyie,
 
Mie natumiaga gear ya kumpata demu mwingine, demu wangu aliniacha so akiona huruma tuuuuu kaisha...
 
huwa wanajipa matumaini kuwa nimemwacha yule,kumbe limeachwa lenyewe niliona kwa babangu mzazi,alivyokuwa anajifariji huku sisi tunamcheka maana kibuti kibaya

dada shosti msimcheke baba yenu ila jifunzeni madhara ya kuvunjika ndoa na mlinde zenu zisivunjike wapendwa. kuhusu nani anaacha na nani anachwa, nadhani haya ni maneno ya kiswahili rahisi na yapaswa kimaanisha maana yake halisi. aliyeanzisha hatua za kumuacha mwenzake ndiye ndiye aliyeacha na mwenziye aliyekuwa bado anamhitaji ila kashindwa kumshawishi abaki, huyo ndiye aliyeachwa. hapo hakuna cha mwanamke wala mwanaume. pia kuna wakati wanakubaliana kuwa waachane. hapo ndipo tunasema wameachana.

mantiki kuwa mwanamke ndiyee anayeachwa imejengwa zaidi na mazoea ya kijamii na ukweli kuwa ndoa nyingi zinazovunjika unakuta baba ndiye aliyemfukuza mwanamke nyumbani. hili laweza kuchangiwa na mfumo dume katika jamii na uungwana na uvumulivu wa wakina mama kwa ajili ya kulinda ndoa zao. yaani mwanamke huvumilia kwa muda mrefu zaidi kuliko mwanaume na huvendelea kuvumilia hata pale ambapo kuna sababu za wazi za kumuacha mumewe na kuondoka.

binafsi najisikia heshima kuwa majority wanawake ndio huwa tunaachwa, hii inadhihirisha kuwa tu waaminifu na wavumilivu. ee Mungu tuongezee imani na uvumilivu. amen
 
shosti umenichekesha sana. Badala ya kumfariji baba yenu mnamcheka! Watoto wabaya nyie,

halafu sio kumcheka tu,tunawaeleza alowaongopea hadithi nzima ilivyokuwa ikawa kama snema,yeye anaongopa sisi tunasawazisha pata picha
 
dada shosti msimcheke baba yenu ila jifunzeni madhara ya kuvunjika ndoa na mlinde zenu zisivunjike wapendwa. kuhusu nani anaacha na nani anachwa, nadhani haya ni maneno ya kiswahili rahisi na yapaswa kimaanisha maana yake halisi. aliyeanzisha hatua za kumuacha mwenzake ndiye ndiye aliyeacha na mwenziye aliyekuwa bado anamhitaji ila kashindwa kumshawishi abaki, huyo ndiye aliyeachwa. hapo hakuna cha mwanamke wala mwanaume. pia kuna wakati wanakubaliana kuwa waachane. hapo ndipo tunasema wameachana.

mantiki kuwa mwanamke ndiyee anayeachwa imejengwa zaidi na mazoea ya kijamii na ukweli kuwa ndoa nyingi zinazovunjika unakuta baba ndiye aliyemfukuza mwanamke nyumbani. hili laweza kuchangiwa na mfumo dume katika jamii na uungwana na uvumulivu wa wakina mama kwa ajili ya kulinda ndoa zao. yaani mwanamke huvumilia kwa muda mrefu zaidi kuliko mwanaume na huvendelea kuvumilia hata pale ambapo kuna sababu za wazi za kumuacha mumewe na kuondoka. binafsi najisikia heshima kuwa majoroty wanawake ndio huwa tunaachwa, hii inadhihirisha kuwa tu waaminifu na wavumilivu. ee Mungu tuongezee imani na uvumilivu. amen
Ushawahi kufika mahali ukasema hapana,sasa ndipo ilipofikia kwa upane wetu,na usijilazimishe kuwa kwenye ndoa ambayo ni ndoano,kwangu mimi hakuna tofauti ya kuwa na ndoa ama kutokuwa nayo,na hamna atakaenibadilisha kwa hilo
 
yote maisha tu dadangu, ubarikiwe lakini
 
Wanawake tunaacha,katika mahusiano yule anayefanya uamuzi wa kumuacha mwenzie ndiye anayeacha na anayepokea uamuzi au hata asipopokea ndo aliyeachwa. Binafsi sijisikii heshima kuwa majority ya wanawake ndo tunaachwa eti kwa sababu si ni wavumilivu na waaminifu.......hakuna aliyeumbwa kuvumilia shida na kuwa mwaminifu kwa asiye mwaminifu na kuvumilia shida anazopewa.....Hakuna thawabu kwenye hili,Mungu anataka tufurahi,tuwe wavumilivu kwa kiasi.Uvumulivu wetu unachukuliwa kama kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi na kutokuwa na nguvu katika mahusiano,ndo maana watu hawabadiliki kwa kuwa eti si ni wavumilivu!
 
Ushawahi kufika mahali ukasema hapana,sasa ndipo ilipofikia kwa upane wetu,na usijilazimishe kuwa kwenye ndoa ambayo ni ndoano,kwangu mimi hakuna tofauti ya kuwa na ndoa ama kutokuwa nayo,na hamna atakaenibadilisha kwa hilo

Mh...!!! Sawa mama.......:crying::A S-confused1:
 
duh! Sasa ndo nafunguka kimawazo mana nilikuwa cjaelewa vzur kumbe hil nalo ni tatzo eeh
 
Kuachwa kunauma sana hasa kama bado unakuwa unampenda mwenzi wako,mimi yamenikuta mwaka jana na mpaka sasa bado nina machungu ya kuachana na mwenzi wangu ila sijawaambia watu kama nimeacha au kuachwa bali tumeachana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom