MwanaKJJ IJumaa: Kwanini Ni Vigumu Kuamini "Udikteta" Wakisema CHADEMA?

Wananchi wanataka maendeleo baaasi. Hayo madudu mengine ni yenu wanasiasa.

Ref Libya na Gaddafi ishu ya true democracy na udikteta wake kwa mujibu wa vibaraka.
Nice try but your answer is irrelevant cuz' sijauliza 7+9=? but 7x9=? Refresh first your memory on "how to do multiplication" in modular arithmetic before you come back with a relevant answer!
 
Niletee na Sheria ya Jeshi la polisi kuhusu kuandamana na kufanya mikutano inasemaje? tuanzie hapo kwanza ukishelewa sheria ya Jeshi la polisi ndio tutaongea

Sheria ya jeshi la polisi iko ya katiba? Jeshi linalofanya kazi kwa kusikiliza viongozi wanaoweka maslahi ya chama chao mbele unaweza kufanya sheria yako iwe na nguvu kuliko katiba ambayo ndio sheria mama? Tafadhali ndugu kila mtu anafahamu jeshi letu la polisi linavyofanya kazi na jinsi linavyotumika vibaya na watawala kwa kuendekeza itikadi za kisiasa.

Nitakupa mfano mdogo kabisa uone udhaifu wa jeshi la polisi. Mwezi uliopita ccm ilifanya mkutano wake kumpata mwenyekiti wake mpya, wote tuliona jinsi jeshi la polisi lilivyohakikisha ulinzi unaimarishwa. Hivi majuzi Cuf nao wakafanya mkutano wake wa kumpata mwenyekiti mpya, nadhani uliona zile fujo zilizotokea mpaka leo hii mwenyekiti hajapatikana. Sasa uwe mkweli, je kama alivyokwenda Prof. Lipumba kwenye mkutano ule na maelezo yake tena akiwa na kundi la watu na hatimaye fujo kutokea, polisi haohao wangeweza kumuachia Lowassa aingie kwenye ule mkutano wa ccm kisa kaitwa na wanachama wanaomkubali ndani ya ccm kwenye ule mkutano wao mkuu? Sasa katika mazingira hayo unaweza kuweka sheria ya polisi juu ya katiba inasemaje?
 
Mzee Mwanakijiji yupo sahihi kabisa....kama utaweka mahaba ya vyama pembeni na kuzama kwenge hoja zake........ndipo utaweza kuuona uzito wa hoja....lakiini kama ukijenga taswira ya chuki kwenye moyo wako huwezi kuona...

Ni wazi kuwa wengi wa watu wapo kwenye mafuriko wakiwa wamesombwa na kauli za wanasiasa.....watu ambao wapo tayari kuandamana pengine bila hata kujua japo aya moja ya katiba anayoaminishwa kuwa inavunjwa......huyu ni kama mbuzi anayepelekwa kwenye machinjio huku akifurahia......
Pia kuna kundi la watu waliotumia akili zao katika kutafakari kwa kina na kuona mantiki ya yeye kuandamana baada ya kuona kuww ni wazi kuna vifungu vya katiba ambapo ndio sheria mama...vimevunjwa au vimekiukwa......na huyu atakwenda kuandamana kwa nguvu zote na kwa uzalendo wote.....kwa kuwa anajua anachokipigania......
 
akilizakuambiwa.png
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna msemo wa Kiswahili kwamba Aliyeumwa na nyoka, akiona unyasi anashtuka; msemo huo unafanana maudhui yake na ule wa Kiingereza kuwa Once beaten, twice shy. Misemo yote hii miwili inatukumbusha tu kuwa mtu yeyote aliyefikwa na jambo baya; na hasa jambo ambalo hakulitegemea kabisa basi anakuwa mwoga hasa mazingira yale yale yanapotokea tena kwani anaweza kuhisi jambo lile lile baya linaweza kumtokea tena.

Hili linanikumbusha mojawapo ya michango mikubwa ya Rais Kikwete katika mijadala ya kisiasa na lugha nchini ni pale alipoelezea wakati fulani jambo ambalo lilikuwa kama kichekesho lakini hadi leo limekolea ndani ya hoja za lugha zetu. Ni pale alipowahi kuhutubia huko nyuma na kuwaasa Watanzania kuwa wawe waangalifu kama alivyokuwa Mbayuwayu ambaye alipewa ushauri na ndege Gong’ota na ushauri ule kama angeusikiliza ungekuwa mwisho wake. Kwamba, Mbayuwayu alimuuliza huyo ndege jinsi gani anaweza kutoboa miti kwa midomo yake. Gong’ota akamwambia kuwa inabidi aruke kwa kasi halafu agonge mdomo wake kwenye jiwe mara mbili ndio utakuwa na uwezo wa kutoboa miti. Mbayuwayu akakubali na akaenda kuchukua kasi alipokaribia lile jiwe akajiuliza nini kitamkuta akigonga jiwe; akaona ule ulikuwa ushauri mbaya na hivyo akajisemea “akili za kuambiwa changanya na za kwako”.

Swali langu la leo lina lengo la kujenga hoja tu kwamba huku tunakokwenda kuna watu wanaweza kabisa kutuambia kuwa jinsi ya kutoboa miti ni lazima tugonge midomo yetu kwenye mawe; na wapo ambao kati yetu wako tayari kuanza kuruka kasi na wamejipanga kura kasi kwenda kugonga jiwe ili wawe na uwezo wa kutoboa miti. Swali ni je watachanganya na za kwao?

Kuna watu ambao wanampinga Magufuli na ambao wanaamini kabisa kuwa Magufuli anaunda utawala wa kidikteta na wengine wanatumia hata neno “ufashisti”. Wapo ambao wanasema hivi wakiwa wanaongozwa na misimamo ya ndani kabisa (conviction) na hawafanyi hivi kwa sababu ya siasa. Yawezekana wengi wa hawa ni watu ambao kweli wanasema kwa sababu wanaamini katika wanachokisema. Hawa sina tatizo nao kwani wanaongozwa na imani na misimamo yao.

Kwa wale ambao hawachoki kusoma hoja ndefu UNAWEZA KUSOMA HAPA.
1Uko sahihi sana mzee wangu,tatizo pesa za Lowassa Zimeradicalise vijana wasiojitambua.mpaka Wanatia simanzi................
 
Sheria ya jeshi la polisi iko ya katiba? Jeshi linalofanya kazi kwa kusikiliza viongozi wanaoweka maslahi ya chama chao mbele unaweza kufanya sheria yako iwe na nguvu kuliko katiba ambayo ndio sheria mama? Tafadhali ndugu kila mtu anafahamu jeshi letu la polisi linavyofanya kazi na jinsi linavyotumika vibaya na watawala kwa kuendekeza itikadi za kisiasa.

Nitakupa mfano mdogo kabisa uone udhaifu wa jeshi la polisi. Mwezi uliopita ccm ilifanya mkutano wake kumpata mwenyekiti wake mpya, wote tuliona jinsi jeshi la polisi lilivyohakikisha ulinzi unaimarishwa. Hivi majuzi Cuf nao wakafanya mkutano wake wa kumpata mwenyekiti mpya, nadhani uliona zile fujo zilizotokea mpaka leo hii mwenyekiti hajapatikana. Sasa uwe mkweli, je kama alivyokwenda Prof. Lipumba kwenye mkutano ule na maelezo yake tena akiwa na kundi la watu na hatimaye fujo kutokea, polisi haohao wangeweza kumuachia Lowassa aingie kwenye ule mkutano wa ccm kisa kaitwa na wanachama wanaomkubali ndani ya ccm kwenye ule mkutano wao mkuu? Sasa katika mazingira hayo unaweza kuweka sheria ya polisi juu ya katiba inasemaje?
We umeniletea sheria ya vyama vya siasa na mimi nimekuletea sheria ya Jeshi la polisi, kwa hiyo kama unataka tuongwee sheria zinasemaje sawa, ila ukitaka tuongee sheria zinatekelezwaje hapo ni Jambo lingine kabisa
 
43. (1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.

Sawa lakini si kwa Tamko la Raisi kuipiga marufuku
 
Sawa lakini si kwa Tamko la Raisi kuipiga marufuku
Ukiangalia kwa upana hata kama Rais asinge sema hadharani ni kua OCD hatoi kibali bila kuomba ruhusa kwa RPC, na RPC hatoi maamuzi bila Kumjulisha IGP... na IGP kwa hiyo msimamo wa polisi utakua ni ule ule tu
 
asante kaka

kwa tunamfahamu MKJJ

amekuwa akisimamia anachikiamini, hilo tu

hili linawapa shida sana n.y.um.b.u ambao muda wowote wako tayari kussema ' ndio' kwa lolote lile

I wish Mbowe, angepigana kusema anataka kuonana na rais, ni KUB for God's sake unless aseme magufuli alimnyima kabisa kukaa naye

hii kuamua pembeni na kuwaaambia watu waende barabarani, ni risk kwa yeye mwenyewe pia......incase turnout ikiwa zero/poor inamharibia yeye

Mbowe angeonana na rais kabla ya chochote

angenyimwa, angeshtaki kwa wananchi kuwa ...'nimejaribu kuonana nae na kakataa''

Mbowe is a nigga

Yaani mtu avunje katiba na sheria ya vyama vya siasa, Halafu reaction iwe ni yeye kukakaa Ikulu, watu wamuombe kuonana naye.

Unataka wapate hisani yake katika ile iliyo haki yao kikatiba na kisheria?.

By the way, kuandamana na kufanya mikutano bado ni haki ya Chadema na vyama vingine, kwa hiyo wanachotaka kufanya Chadema tarehe mosi September bado ni haki yao kikatiba!
 
Kama kweli ujinga na umasikini wa wananchi ndiyo unaofanya watu waendelee kuipigia kura ccm,basi inawezekana kabisa hata upinzani hutumia njia hiyohiyo ya ujinga na umasikini wa watanzania kuwapelekesha na kuaminisha chochote.
 
Mzee Mwanakijiji, Usipende sana kitu wala kuchukia kitu sana kwani hali hiyo inaweza kukupelekea ushindwe kuwa " Free minded!".

Pia wakati mwingine ni bora ukatulia na kusikiliza wanachosema wengine kuliko kusema wewe, kwani unaposema kwa kawaida unakuwa unarudia jambo ambalo tayari unalijua ndani ya akili yako (liwe sahihi au la!) lakini unapotulia na kusikiliza au kusoma wengine, unakuwa umejitwalia fursa ya kujifunza na kujipa nafasi ya kupata taarifa mpya.
Kuntu
 
Ukiangalia kwa upana hata kama Rais asinge sema hadharani ni kua OCD hatoi kibali bila kuomba ruhusa kwa RPC, na RPC hatoi maamuzi bila Kumjulisha IGP... na IGP kwa hiyo msimamo wa polisi utakua ni ule ule tu

Mikutano inaweza kukatazwa kwa ground za Usalama , Na kukatazwa kwenyewe inabidi utoe room ya kufanyika siku nyingine iliyo salama. Siyo kuipiga marufuku once and for all.
Huwezi kuipiga mikutano marufuku kwa sababu za Kisiasa kwamba " Kila aliyeshinda katika jimbo lake afanye mikutano katika jimbo hilo", kufanya hivyo ni kuitafsiri sheria unavyotaka wewe
 
Kweli kuna watu wao wanajiona kama wanajua sana kufikiria zaidi ya wengine, hivi si nyie ndo mlikuwa mnamponda sana mzee wangu JK kuwa hana maamuzi magumu hawashughulikii mafisadi nk, mkaenda mbali zaidi na kusema kwa nchi ilipofikia inahitaji dikteta ndo aongoze, ss dikteta mliyemtaka si ndo huyu ss tena mnamkataaa hahaha kwel Mbowe kachukua akilin zenu hata za ziada hajawaachia, baada ya kupambana ipatikane katiba mpya mnaleta mada zisizo na maana hapa, huyu Tundu eti mwanasheria wakati sheria imemshinda akamkimbilia Tulia si angepambana nae kwa vifungo kuliko kumkimbia, hiv hajasoma katika ya tanzaniaikoje ama, imeruhusi maandamano lkn mwisho ikamalizia endapo kutakuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani basi Jeshi la polisi ......... malizien wenyewe.
 
We umeniletea sheria ya vyama vya siasa na mimi nimekuletea sheria ya Jeshi la polisi, kwa hiyo kama unataka tuongwee sheria zinasemaje sawa, ila ukitaka tuongee sheria zinatekelezwaje hapo ni Jambo lingine kabisa

utekelezaji uko wazi, tekeleza sheria inavyosema na.sio waziri aliyeshiba itakadi anavyotaka. shida iliyoko hapa ni weledi wa wale waliopoewa mamlaka, ndio sheria hizo zinatekelezwa kwa double standard.
 
Nice try but your answer is irrelevant cuz' sijauliza 7+9=? but 7x9=? Refresh first your memory on "how to do multiplication" in modular arithmetic before you come back with a relevant answer!
Hapa kazi tuuu.. Vibaraka uwa hamkosekani
 
Maneno, na ushauri kuntu huu! . Mwenye masikio na asikie! .

Pasco

Hua nakaa na kujiuliza MMK, akisha andika habari kama hili hua anaanza kucheka, kulog out Jamiiforum, kukaa tu anapitia michongo za wengine au anajiona kua kuna watu anawakomoa huku Tanzania?

Make ata yule mzee wangu ambaye aliishia shule ya msingi awezi kua na mawazo ya chini kiasi hiki.
 
Hajasema kua katiba na sheria za nchi hazikiukwi.....alichosema kwa nini tuamini kile wanachokisema CDM, maana baadae wanaweza kuja kutugeuka.... Walituaminisha Lowasa Fisadi kwa maneno yao na watu wakaamini? nini kinasababisha wewe usiamini kua baadae watageuka hiki wanachokisema?

If that's a case; yeye kwa mawazo yake anaonaje? make nchi hii siyo ya CHADEMA bali ya waTanzania wote.
 
Mwanasheria wewe unasemaje? Utaandamana?
Mimi sio mwasheria bali nilitoa tuu tongotongo pale UDSM kwenye kitivo cha sheria.

Kusomea sheria ni jambo moja, kutoa tongotongo ni jambo jingine na kuwa mwanasheria ni jambo jingine kabisa. Sio kila aliyesomea sheria ni mwanasheria! .

Kuhusu maandamano, mimi nitaandamana na naendelea kutoa wito, tujitokeze kwa wingi.

Pasco
 
Back
Top Bottom