Mwanakijiji yuko wapi kuhusu tiba ya babu wa Loliondo?

kina Mahita, Hosea,Laizer na watu wakubwa kibao wameshapiga hii dawa . Wewe bado unaifananisha na DECI? Hivi ngoja nikuulize swali ina maana kama unafikiri ni changa la macho madhara yake yatakuwa ni nini? Kutapeliwa hio tsh 500? Au..

Tatizo sio shillingi mia tano. Tatizo ni kuwapa watu matumaini kuwa wamepona magonjwa yaliyobobea kama ukimwi na kisukari, itafanya wenye magonjwa hayo kutofuatilia taratibu za tiba zao, na kuanza kuishi kama zamani, Wagonjwa kisukari wataanza kubugia makande, ugali,wali na mbalagha na wagonjwa ukimwi wataacha kutumia salama, na dawa zao za kawaida.
 
Kuna breakdown ya hiyo 500tsh. Mzee hachukui yote. Tsh200. ni kwa wachimba dawa, 200 nyingine hutoa zaka ( tithe) kanisani na 100 ni yake yeye.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom