Mwanakijiji na Uislamu wa TAA/TANU mpaka CCM

@MUHADHIRI huu ni upotoshaji. MCT hawajataja Tanzania Daima. Walisema vyombo vya habari kwa ujumla. Wanasema kumekuwapo na headlines za kijumla jumla, mfano wakristo wafanya jambo fulani.... Au waislamu wakataa kitu fulani...... Wakati anayekataa ni mtu mmoja au watu wa chache au madhehebu fulani. Pia wamesema vyombo vya habari vihakikishe mtoa habari kwa niaba ya taasisi ya dini awe mwenye mamlaka ya kuisemea sila kila kujiibukia na kunukuliwa kuwa dini fulani inasema jambo fulani.
 
There are currently 51 users browsing this thread. (15 members and 36 guests)

Peasant,VISIONEER,Tumaini Jipya,Ame,chetuntu,Mohammed Shossi,Ngekewa,Prof Kasambanda,Mzee wa Rula,GWeLa 2003,Mr.Mak,Masanga,

Jamaa kaona amechemsha kaamua kukaa kimya kwenye thread yake mwenyewe!!

Sijakaa kimya na wala hakuna wa kuninyamazisha kwani wewe ukiona wingu unajua mvua inanyesha? mtu anaweza kuwa online lakini akawa hayupo kwenye laptop (away) kwahiyo siku nyingine ukiona hivyo ujue huyo mtu hayupo kwani nilipo post hii thread wengi walikuwa na mishughuliko yao mie bahati mbaya nimetenga muda wa mambo ya JF na FB na muda wa familia yangu siwezi kukaa 24 hours kwenye JF I have life to live bro.
 
Hapa tz ukiona jambo linafuatiliwa ujue kuna msukumo wa ziada.Kwa mtu aliyesoma andiko la M/kijiji kuanzia kichwa cha habari hakuandika kama hitimisho!aliandika kwa mtindo wa swali huku akitoa sura ya vyama vyote viwili;chadema na ccm.lilikuwa ni jukumu la msomaji kusoma makala:kama mmojawapo wa waliosoma taswira inanijia ni kwamba hatuwezi kuhitimisha kwamba kuna udini/ukabila kwenye vyama hivyo.NA HII INAJIDHIHIRISHA KUTOKANA NA UTENDAJI WAKE,VISHEN NK.
 
Poleni CCM kwa kuruhusu na kudhani uislamu ndo mtaji wa ushindi. Mmepandikiza mbegu mbaya hadi mmefika mahala mnapandikiza wagombea mbalimbali katika uongozi wa elimu ya juu kwa imani yakumiliki vyou. Jengeni vyenu na kimoja mlipewa na rais mkristo kile cha Morogoro hamjifunzi uungwana wa wenzenu? Chuo kimoja kule dodoma kimetoa funzo kwa mawazo yenu yakuona kila kitu chenu na uislamu ni dini bora kuliko za wenzenu nakuwa mmkiguswa mnakasirika
 
Hata kama angewataja wote kama unavyotaka wewe iwe bado, haiondoi ukweli kwamba waislamu wengi walishiriki kuianzisha TAA/TANU/CCM lakini hawakuanza harakati zao kwa malengo ya kidini bali kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika, na hawakuwabagua watu wasio wa dini yao, hadi wakakubali kumpisha kijana mkristu Nyerere kuchukua uenyekiti wa TANU. Enzi hizo hakukuwa na ubaguzi kama leo mnavyowaita wenzenu kafiri, kwakuwa waislamu wa enzi zile walikuwa watu safi hawakuwa wanafiki.

Ili makala inoge ni katika kuweka ulinganifu (differences and similarities) wa pande mbili, au tatizo lako hukutaka hoja inoge?? Kama hoja ya mwanakijiji isingenoga bilashaka usingepata elimu kama ulivyoipata.

Na isingebadilisha ukweli kuwa hao Waislam hawakuwa waroho wa madaraka walimwachia Mwalim Nyerere na hapo ndipo tungejiuliza maswali mengi moja kubwa ni kuwa je Mbowe yupo tayari kumwachia Zitto Kabwe uenyekiti? kwanini Zitto anapigwa vita eti kwa kuwa tu anautaka uenyekiti? tungeenda mbali na kukumbuka yaliyojiri kwenye uchaguzi wa uenyekiti alipokuwa aking'atuka Makani sote tunakumbuka ni nani na nani waligombea nafasi ya uenyekiti na matokeo yake tunayajua.
 
. Tumbiri. Kuna kusoma na kuelewa. Jamaa amemsoma vizuri tuu tatizo ni kuelewa. Uelewa wa MS humu jamvini si unaeleweka fika!.

Mimi mwenye uelewa mdogo huwa najiuliza iweje chama kiwe na wabunge wanaotoka koo moja huku wengine wakiwa wamepita kwa nafasi za upendeleo? utakuta baba mkwe, mkwe na mtoto wote ni wabunge na mkwe ndie aliechaguliwa lakini mtoto na mkwe wamepita kwenye nafasi za upendeleo. Hili wenye uelewa mdogo kama wangu watashindwa kulielewa.
 
Na isingebadilisha ukweli kuwa hao Waislam hawakuwa waroho wa madaraka walimwachia Mwalim Nyerere na hapo ndipo tungejiuliza maswali mengi moja kubwa ni kuwa je Mbowe yupo tayari kumwachia Zitto Kabwe uenyekiti? kwanini Zitto anapigwa vita eti kwa kuwa tu anautaka uenyekiti? tungeenda mbali na kukumbuka yaliyojiri kwenye uchaguzi wa uenyekiti alipokuwa aking'atuka Makani sote tunakumbuka ni nani na nani waligombea nafasi ya uenyekiti na matokeo yake tunayajua.

justify statement yako kuwa zitto anautaka uenyekiti ...... vinginevyo mada zako zipo kwa mtindo wa speculations
 
Mimi mwenye uelewa mdogo huwa najiuliza iweje chama kiwe na wabunge wanaotoka koo moja huku wengine wakiwa wamepita kwa nafasi za upendeleo? utakuta baba mkwe, mkwe na mtoto wote ni wabunge na mkwe ndie aliechaguliwa lakini mtoto na mkwe wamepita kwenye nafasi za upendeleo. Hili wenye uelewa mdogo kama wangu watashindwa kulielewa.
tutajie kwa majina hao unaowazungumzia i.e wabunge wachagga wenye uhusiano uliosema.
 
Na isingebadilisha ukweli kuwa hao Waislam hawakuwa waroho wa madaraka walimwachia Mwalim Nyerere na hapo ndipo tungejiuliza maswali mengi moja kubwa ni kuwa je Mbowe yupo tayari kumwachia Zitto Kabwe uenyekiti? kwanini Zitto anapigwa vita eti kwa kuwa tu anautaka uenyekiti? tungeenda mbali na kukumbuka yaliyojiri kwenye uchaguzi wa uenyekiti alipokuwa aking'atuka Makani sote tunakumbuka ni nani na nani waligombea nafasi ya uenyekiti na matokeo yake tunayajua.

Haiwezekani upewe uenyekiti kisa Uislam.
Mbowe was/is much better kwa uenyekiti than Zitto.
Wakati wa Zitto kuwa chair utakuja but not now.
 
Mimi mwenye uelewa mdogo huwa najiuliza iweje chama kiwe na wabunge wanaotoka koo moja huku wengine wakiwa wamepita kwa nafasi za upendeleo? utakuta baba mkwe, mkwe na mtoto wote ni wabunge na mkwe ndie aliechaguliwa lakini mtoto na mkwe wamepita kwenye nafasi za upendeleo. Hili wenye uelewa mdogo kama wangu watashindwa kulielewa.

mkuu ... i think you are running out of your conscious

upo hapa kumjibu Mwanakijiji au upo hapa kuipa mipasho CDM....!
 
Hivi UDINI au UKABILA ni majina tu au KAULI zinazoambatana na vitendo? Wazee wanaotajwa kwenye thread hii hawakuwahi kujadili wala kuulizana DINI wala KABILA zao kwenye vikao na harakati zao za kudai uhuru wa NCHI hii. Haya ya UDINI yamekuja baada ya baadhi kuanza kufilisika kisiasa na wengine kuanguka sana kiuchumi na wakawa wanaangalia ni namna gani wataitafuna nchi yetu baada ya uhuru. Wakakuta Mwalimu ana msimamo mkali kwa kauli na vitendo juu ya rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za Watanganyika wakati huo.
Hata ukichunguza kwa sasa udini na ukabila unaoongelewa umekaa kimaslahi zaidi. Siasa imekuwa ni uwekezaji wa nguvu. Viongozi hawatafutwi kama wale wazee walivyomtafuta Mwalimu. Kila mtu sasa hivi anadhani anaweza kuwa kiongozi ili mradi ataweza kuchuma yeye na kundi lake. Nimeona juzi JK anazindua chuo cha viongozi. Ikumbukwe tu kwamba uongozi ni KIPAJI kwanza.
 
Sijaona tofauti ya kile alichoandika mzee mwanakijiji na hii ya shossi!! hizi propaganda za udini na ukabila zinazoenezwa na wale waliopewa jukumu la kutuongoza na badala yake wakaendekeza matumbo yao hazitatusaidia kitu. udini na ukabila ni upuuzi wa wanasiasa wachache walioshindwa kua waadilifu katika ofisi za uma!

Tujadili kwa nini bado sisi ni maskini wa kutupwa pamoja na rasilimali lukuki tulizojaliwa na mola...
 
Kwanza mtu mwenye miaka chini ya 40 kama huyu mtoa mada kwa mazingira ya Tanzania huwezi kutoa Historia, hapa unapiga porojo na longo longo tu, ngoja nitafute thread za maana, hapa naona uharo tu.
 
Na isingebadilisha ukweli kuwa hao Waislam hawakuwa waroho wa madaraka walimwachia Mwalim Nyerere na hapo ndipo tungejiuliza maswali mengi moja kubwa ni kuwa je Mbowe yupo tayari kumwachia Zitto Kabwe uenyekiti? kwanini Zitto anapigwa vita eti kwa kuwa tu anautaka uenyekiti? tungeenda mbali na kukumbuka yaliyojiri kwenye uchaguzi wa uenyekiti alipokuwa aking'atuka Makani sote tunakumbuka ni nani na nani waligombea nafasi ya uenyekiti na matokeo yake tunayajua.
Zitto apewe uenyekiti kwa sababu ya Uislamu wake? Kwa nini baadhi ya watu wanazifanya DINI sawa na mama zao? Kwangu mimi dini ni sawa na mke tu. Naweza kuiacha, kuibadili nikawa dini nyingine, naiasi kila siku.
 
Kama wewe si mwalimu basi una moyo kweli wa kufundisha.

Hivi Mwanakijiji, huoni kwamba umefika wakati sasa tuachane na hii thread maana mwenye akili ameelewa vizuri ni nini makala yako imemaanisha, usipoteze mda kuendelea kujibizana na watu waliogoma kuelewa, hii yaweza kuwa ni njama ya kutaka kuhujumu mda wako ili utumie mda mwingi kujibizana nao ilihali unatakiwa kufikiria mambo mengine muhimu katika kuelimisha jamii. Nawapongeza sana wachaga wangekuwa na mioyo kama Mohammed Shossi nadhani kungetokea malumbano makali sana na Nape.
 
Soma Upya article mama ya Mwanakijiji utajiona ulivyo Ngumbaru! Unashindwa elewa vitu vyepesi vigumu je?

Heshima yako mkuu,

Ni kweli nashindwa kuelewa magumu kama
1. Kwanini hakuelezea undugu uliopo CDM ushahidi upo na tunajua ya kwamba kuna watu wamepewa viti maalumu mkwe na mtoto wa mmoja wa waasisi wa chama. Hili kwangu ni gumu ni kweli sitalielewa hasa ukizingatia kulikuwa na vikao vya kufanya mchakato wa viti maalum vilifanya kazi yake vizuri lakini baadae chama kwa utashi wa viongozi wakaamua kumtea mwanaume awachague wanawake wa kuwawakilisha wanawake wenzao kupitia viti maalum. Ndugu yetu Kitila Mkumbo ndie aliekuwa consultant akawalima waliokuwa wamependekezwa na baraza la wanawake akiwemo aliekuwa mwenyekiti wake mama Musori na kurudisha sura zile zile za miaka yote.

2. CDM ni chama kinachopendwa na vijana ambao kwa takwimu ndio wapiga kura wengi kwahiyo nakushauri usome hii link utajua vitu gani Mwanakijiji ameshindwa kuvionyesha kwenye makala yake ambayo watu wanakuwa na mashaka na chama hizi kasoro ndogo na za makusudi zikirekebishwa basi hakuna chama cha upinzani kitakachokuwa na mvuto kukishinda CDM
Vijana tunakiamini chama cha demokrasia na maendeleo,kwa namna kinavyosimama na kuibua na kuhoji mambo muhimu sana katika jamii yetu.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/132237-waraka-kwa-mbowe-na-zitto.html

Hata wazazi wetu wanaamini chadema ndio kimbilio letu, licha ya wao kutuonya kuhusu kujitokeza mbele sana kwenye harakati za siasa, wakihofia usalama wetu.

Ila sasa viongozi wetu mnapoonekana kuvutana kwa ajiri ya tamaa za madaraka na ruzuku, ni aibu sana na ipo siku vijana wengi watafuatilia kiundani mambo ya chama chetu na ikiwa watabaini ukweli ulio tofauti na hisia zao, basi wataingia msituni kwani hawataamini mabadiliko kupitia chama cha siasa.

Ikiwa CHADEMA hakitabadilika kimtazamo, kisera na ki-organisation, hakuna mafanikio, nawaomba sana Mbowe, Slaa na Zitto kubalini kukaa na kushauriana.

I dnt understant wht the deal with uwenyekiti, tafadhali sana vijana vyuoni sasa wameanza kuhoji undani wa ugomvi wa Mbowe na Zitto kila wanapo onana.

Na ni kwa nini wanaonekana kutosikilizana hata kwa jambo la maana, tunajitahidi kujibu maswali magumu sana kutoka kwa vijana wasiojua CHADEMA, ila tunafanikiwa kuwatuliza na kuwapa moyo, ila wakati mwingine unajibu mtu na unaona haimwingii akilini.

Please msituumize kabisaaa.

2.
 
Zitto apewe uenyekiti kwa sababu ya Uislamu wake? Kwa nini baadhi ya watu wanazifanya DINI sawa na mama zao? Kwangu mimi dini ni sawa na mke tu. Naweza kuiacha, kuibadili nikawa dini nyingine, naiasi kila siku.

Kwahiyo hizi chokochoko dhidi yake kwa kuwa amesema anautaka uenyekiti na pengine kugombea urais ni kwasababu ya dini yake? is he in a wrong ship?
 
Kwanza mtu mwenye miaka chini ya 40 kama huyu mtoa mada kwa mazingira ya Tanzania huwezi kutoa Historia, hapa unapiga porojo na longo longo tu, ngoja nitafute thread za maana, hapa naona uharo tu.

Una maana baada ya miaka mia na hamsini kukiwa hakuna hata mtu mmoja aliezaliwa kabla ya uhuru watu hawatasoma na kujua historia ya nchi yao? Hivi wamarekani waliopata uhuru kwa miaka zaidi ya mia mbili hawasomi historia kwa kuwa wanaowafundisha ni chini ya miaka mia mbili? duh kweli kazi ipo!
 
Back
Top Bottom