Mwanakijiji na Uislamu wa TAA/TANU mpaka CCM

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,301
Nitaomba radhi kwa kuanzisha thread mpya ili niweze kupata fursa ya kujibu hoja za ndugu yangu Mimi Mwanakijiji au kama anavyojiita sauti ya kijijini inayoelezea iliyoandikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu? K

Napende niwaeleze wale wote walioshabikia historia ya TANU kuwa wamelishwa "tango pori" na mheshimiwa sana Mwanakijiji japo sijaelewa amefanya kwa makusudi au kwa kutokufahamu kwakuwa tunae humu jamvini ni imani yangu atatueleza na kututanabaisha mapenzi yake juu ya vyama alivyovizungumzia, ila ningependa kumshauri awe mzalendo zaidi na apendelee kuwaelimisha watu kwa historia ya ukweli japo kwa kiwango cha asilimia 80 kama si mia kwa mia.

Pengine ni vyema tuangalie mtiririko wa kupigania uhuru wa nchi hii ili tuone mchango wa Mwanakijiji juu ya hoja yake na tupate kumuenzi kwa kutupa elimu na historia adhimu tusioijua:

1929: TAA yaundwa ikiwa na wajumbe wafuatao:

1. Kleist Sykes, 2. Mzee bin Sudi, 3. Ibrahim Hamis, 4. Zibe Kidasi, 5. Ali Said Mpima, 6. Suleiman Majisu, 7. Raikes Kusi, 8. Rawson Watts, 9. Cecil Matola.

1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kujenga mawasiliano na chama cha Kenya African Union (KAU).

1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la TAA; likiwa na wajumbe wafuatao:

1. Abdulwahid Sykes (Secretary)
2. Sheikh Hassan bin Amir
3. Hamza Kibwana Mwapachu.
4. Said Chaurembo
5. Dk. Kyaruzi.
6. John Rupia.
7. Stephen Mhando

1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika Arusha. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, Dossa Aziz na Stephen Mhando.

1952: Abdulwahid alichaguliwa kuwa Rais wa TAA.

1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika.

Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid.

Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano.

1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU.

Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Mohammed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate na Mwinjuma Mwinyikambi. Wengine walikuwa Rajab Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidar Mwinyimvua na Idd Faiz Mafongo. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia na Mashado Ramadhani Plantan.

Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa.

1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, ,

Abubakar Ilanga na Saadan Abdu Kandoro. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia.

Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine.

Napenda kumfahamisha ndugu yangu Mwanakijiji kuwa pia ndani ya TAA na TANU kulikuwa na kina
Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi, Dr Luciano Tsere, Dome Budohi, Zuberi Mtemvu, Ali Mwinyi Tambwe, Tatu bint Mzee, Mwinyijuma Mwinyikambi, Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo

Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi Titi Mohamed kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25.

Ndugu yangu Mwanakijiji,

Kwa watu makini makala yako ni moja ya utumiaji kalamu kupotosha jamii makala yako imebaka historia ya kweli ya TAA/TANU na sasa CCM kama nilivyoeleza mwanzo pengine mapenzi ya chama kimoja wapo ndio mapenzi hayo yamekusukuma kuinanga historia ya kweli.

Ni matumaini yangu ipo siku utaungana na Joseph Mihagwa utajitolea kuuvunjaa mwiko wa kuuzungumzia muungano
inavyostahili.

Shukrani sana na nakutakia siku njema wewe na jamaa wote wa JF.

Mohammed Shossi.

Kwa kuhitimisha napenda kujibu hoja ya Mwanakijiji pale alipo sema

Tatizo ni kuwa Shossi hataki kuvuka ambapo mantiki inamtaka avuke. Anauona ukweli lakini hataki kuuitikia japo unapiga kelele uitikwe. Chadema hakijawahi kuwa Chama cha Wachagga - iwe katika uanzilishi wake, uongozi wake, sera zake au hata katika kukubalika kwake. HILO SOTE TUNAJUA. Wanaosema ni cha Kichagga ni kwa sababu ya majina tu ya "Baadhi" ya viongozi wake. Hata tukikubali kwa ajili ya hoja kuwa uamuzi wa kiongozi mmoja ulifanywa kwa sababu ya kabila - kitu ambacho hakuna mtu amewahi kukithibitisha zaidi ya kutuambau "wanajua" haiwezekani hilo lifanye chama kizima kuwa cha kabila la watu hao wawili kwani ukikubali uwezekano huo inabidi ukubali pia kuwa kama kiongozi mmoja wa CCM ambaye ni Mndengereko akimuajiri mndengereko mwenzake basi CCM imekuwa ni ya Wandengereko! Ataliikataa hilo kwa CCM lakini atalikubali kwa Chadema.

Akiwa ni mtu anayependa ukweli ingempasa akubali na kukiri kuwa Chadema siyo chama cha kikabila kwa sababu hakuna ushahidi wowote wa ukabila ambao umewahi kuwekwa wazi au kuoneshwa kuwa unatengenezwa na Katiba, Sera au Viongozi. Kwa sababu kama upo aidha hao waliouona ni watu wazembe na waoga ambao walitakiwa kuripoti kwa Msajili ili uchunguze ufanyike kwani kunavunja Sheria ya Vyama vya Siasa. Kama kuna kiongozi yeyote wa Chadema ambaye amewahi kukataliwa kwa sababu ya kabila lake au dini yake alipaswa kusiimama na kwenda kutoa ushahidi au hata kufungua kesi kwani hili ni suala la haki yake kama raia. Zaidi ya kulalamika pembeni hakuna ushahidi wowote. NONE. Kama viongozi au watu hao wapo ambao wanajua kuwa kuna mambo Chadema inafanya kwa misingi ya ukabila au dini na watu hao wamenyamaza kimya basi ni watu waoga na wasiofaa kupewa hata uenyekiti wa nyumba zao.

So far Shossi amefanya kazi nzuri sana ya kutuonesha kuwa hakuna ukabila ndani ya Chadema na kuwa CCM siyo chama cha Waislamu. Hata hivyo nina uhakika atakubali hilo la pili na kukataa la kwanza.

Namsauri asome maandiko ya Ernesto Cheka ili aweze kuyajibu kwa hoja na kuweza kuwaondoa watu fikra kuwa CDM ni chama cha kikabila kwani watu Kama Cheka wanaweza kuwafanya watu waamini kutokana na mazingira yalivyo ndani ya chama. Hii itaijenga cdm na sio kuona kama ni uasi kuzungumzia yale yote yanayosemwa kwa ubaya kwa chama.

The Moment Of Truth:The Complete Text.(What Every Tanzanian Should Read)

by Ernesto Sheka

Ndoto na chuki zaja hadharani sasa;

Baada ya miaka takribani 26,Julai 1992 mfumo wa vyama vingi ukaanza.The same year Mtei akaanzisha Chadema na mpaka ninapoandika hili,in practical terms yeye ni mwenyekiti wa Chadema,kwake yeye ile ni fimbo maalumu ya kumchapa Mwalimu Nyerere siku akifanikiwa japo kila mara anakosea mahesabu huku jamii ikizidi kuamka na kujua historia ya taifa na kuchambua mambo hatua kwa hatua.Uzee wake umekuwa wa mashaka na wasiwasi.Ni dhahiri kuwa masterplan ya kuanza kwa Chadema ilianza kuandikwa Nairobi na baadaye Washington huku ikiuwaza ubepari na Ikulu kabla hata ya usajili.Lilian Mbowe ni mtoto wa kike wa Edwin Mtei ambaye aliolewa na Mbowe.Ni daktari ambaye kama nilivyosema awali anajishughulisha na kuendesha club ya usiku katikati ya jiji la Dar es salaam mtaa wa Mkwepu.Nyumba zao hutumika kukusanya vijana na wengi wana upofu na historia ya Chadema,wanaogundua huondoka mara moja.(Mtafuteni David Kafulila atawahadithia sehemu hii).
Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Edwin Mtei namnukuu akisema,"we can't give this position to a man from nowhere" akimaanisha Zitto Kabwe,Zitto alitaka kuondoka ila alibaki kwa sababu zake.Tafakari hiyo kauli ya Mtei.Who's a man from nowhere and who's a man from somewhere??Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?To revenge and take back his dignity and self interests.Ni ndoto yake ya ujanani na anaomba Watz tumsaidie aitimize.
Imefanikiwa kiasi gani?
Hali ni ngumu,ukabila bado umekuwa tatizo.Kifo cha Wangwe,maneno kuhusu viti maalumu,uwepo wa Deus Mallya aliyevuruga mpango wa kufunika sakata la kula pound za waingereza kama ruzuku kwa chama na baadaye kufoji risiti .(John Mnyika alikuwa kinara wa shughuli hii ya kuchakachua risiti).Wangwe's head had a price but Deus Mallya made a noise and Chadema let him went down and come up alone(sifa kubwa ya majasusi unapoharibu mpango wa kazi na ukapata tatizo).Ninapoandika hili,Deus Mallya ni mpiga picha na designer rasmi wa Chadema huku mifupa na damu ya Chacha Zakayo Wangwe ikilala udongoni kule Tarime.

Na haitakuwa mbaya pia maswala kama haya hapa chini yakatolewa ufumbuzi.

Vijana tunakiamini chama cha demokrasia na maendeleo,kwa namna kinavyosimama na kuibua na kuhoji mambo muhimu sana katika jamii yetu.

Hata wazazi wetu wanaamini chadema ndio kimbilio letu, licha ya wao kutuonya kuhusu kujitokeza mbele sana kwenye harakati za siasa, wakihofia usalama wetu.

Ila sasa viongozi wetu mnapoonekana kuvutana kwa ajiri ya tamaa za madaraka na ruzuku, ni aibu sana na ipo siku vijana wengi watafuatilia kiundani mambo ya chama chetu na ikiwa watabaini ukweli ulio tofauti na hisia zao, basi wataingia msituni kwani hawataamini mabadiliko kupitia chama cha siasa.

Ikiwa CHADEMA hakitabadilika kimtazamo, kisera na ki-organisation, hakuna mafanikio, nawaomba sana Mbowe, Slaa na Zitto kubalini kukaa na kushauriana.

I dnt understant wht the deal with uwenyekiti, tafadhali sana vijana vyuoni sasa wameanza kuhoji undani wa ugomvi wa Mbowe na Zitto kila wanapo onana.

Na ni kwa nini wanaonekana kutosikilizana hata kwa jambo la maana, tunajitahidi kujibu maswali magumu sana kutoka kwa vijana wasiojua CHADEMA, ila tunafanikiwa kuwatuliza na kuwapa moyo, ila wakati mwingine unajibu mtu na unaona haimwingii akilini.

Please msituumize kabisaaa.

1.M.M Mwanakijiji amefanya kile ambacho viongozi wa CDM wamekataa kukihubiri.
Hoja ya Mwanakijiji ina ukweli mkubwa na itashika kasi sana kwa kuwa CCM (serikali ) ilmekuwa ikiizushia CDM udini na ukabila.
Aliwahi kuonya Askofu Leizer kuwa with time Wakristo watajiuliza if CDM is Christians, CCM belong to whom-if not Muslims
Hapa ndipo tunapoelekea na Mwanakijiji ametoa mazingira yanayoweza kuwaaminisha wakristo in case
CCM ilitumia udhaifu wa viongozi wa Kiislam kueneza uongo ikidhani hamna maisha baada ya uchaguzi.

2.kama ulivyokiri misikiti,magazeti na redio za kiislam zilitumika kwa nini serikali kwa wakati ule haikukemia vyombo hivi
mfano gazeti la Al nuur liliandika Dr.Slaa azikataa kura za wanawake wa kiislam

3.Halikuwepo tatizo la udini kwenye chaguzi/siasa lilianza tu pale JK mwenyewe alipoanza kuhubiri jambo lisilokuwepo.Manzese Tiptop kwenye muhadhara mkubwa wa kila siku wakaanza kuwahimiza waislam wasimpe Lipumba kura 2010 kwa maana kufanya hivyo kutaweka rehani ushindi wa mwislamu wmenzao JK baada yake waipigie CCM

Ndug Mohammed Shossi:
1.ikiwa idadi ya wakristo ndani ya CDM imefanya kizushiwe christianity kwa nini idadi ya waislam isitumike kukuita CCM chama cha kiislam?
2.ikiwa MWANZILISHI MCHAGAA mkristo kwa nini CCM PWANI ISIWE UISLAM?

Hapa naona CCM haikujua ipo jumba la vioo ikarusha mawe muda mrefu,CDM waligoma kujibu ila Mwanakijiji kaanzisha backfires.
 
Mkuu Shossi asante kwa historia hapo juu ila pia nina haya ya kusema:

1. Wewe unazungumzia TANU Mwanakijiji anazungumzia CCM. Wewe umezungumzia muundo wa TANU ulivyo kuwa yeye anazungumzia muundo wa CCM sasa. Kuna tofauti kubwa hapo.

2. Mwanakijiji hajasema moja kwa moja kwamba CCM ni chama cha Waislamu ila kama umesoma vizuri amesema kama ukikiita Chadema chama cha Wachaga basi kwa kutumia logic hiyo hiyo lazima ukiite CCM chama cha Waislamu na vice versa ila hiyo ni batili kama mtu haukioni Chadema kama chama cha kikabila na CCM cha kidini. SIjui umenielewa hapo mkuu?

Ni hayo tu kwa sasa. Akija atajieleza mwenyewe zaidi.
 
Nitaomba radhi kwa kuanzisha thread mpya ili niweze kupata fursa ya kujibu hoja za ndugu yangu Mimi Mwanakijiji au kama anavyojiita sauti ya kijijini inayoelezea iliyoandikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu? K

Napende niwaeleze wale wote walioshabikia historia ya TANU kuwa wamelishwa "tango pori" na mheshimiwa sana Mwanakijiji japo sijaelewa amefanya kwa makusudi au kwa kutokufahamu kwakuwa tunae humu jamvini ni imani yangu atatueleza na kututanabaisha mapenzi yake juu ya vyama alivyovizungumzia, ila ningependa kumshauri awe mzalendo zaidi na apendelee kuwaelimisha watu kwa historia ya ukweli japo kwa kiwango cha asilimia 80 kama si mia kwa mia.

Pengine ni vyema tuangalie mtiririko wa kupigania uhuru wa nchi hii ili tuone mchango wa Mwanakijiji juu ya hoja yake na tupate kumuenzi kwa kutupa elimu na historia adhimu tusioijua:

1929: TAA yaundwa ikiwa na wajumbe wafuatao:

1. Kleist Sykes, 2. Mzee bin Sudi, 3. Ibrahim Hamis, 4. Zibe Kidasi, 5. Ali Said Mpima, 6. Suleiman Majisu, 7. Raikes Kusi, 8. Rawson Watts, 9. Cecil Matola.

1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kujenga mawasiliano na chama cha Kenya African Union (KAU).

1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la TAA; likiwa na wajumbe wafuatao:

1. Abdulwahid Sykes (Secretary)
2. Sheikh Hassan bin Amir
3. Hamza Kibwana Mwapachu.
4. Said Chaurembo
5. Dk. Kyaruzi.
6. John Rupia.
7. Stephen Mhando

1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika Arusha. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, Dossa Aziz na Stephen Mhando.

1952: Abdulwahid alichaguliwa kuwa Rais wa TAA.

1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika.

Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid.

Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano.

1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU.

Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Mohammed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate na Mwinjuma Mwinyikambi. Wengine walikuwa Rajab Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidar Mwinyimvua na Idd Faiz Mafongo. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia na Mashado Ramadhani Plantan.

Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa.

1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, ,

Abubakar Ilanga na Saadan Abdu Kandoro. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia.

Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine.

Napenda kumfahamisha ndugu yangu Mwanakijiji kuwa pia ndani ya TAA na TANU kulikuwa na kina Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi, Dr Luciano Tsere, Dome Budohi, Zuberi Mtemvu, Ali Mwinyi Tambwe, Tatu bint Mzee, Mwinyijuma Mwinyikambi, Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo

Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi Titi Mohamed kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25.

Ndugu yangu kwa Mwanakijiji.

Kwa watu makini makala yako ni moja ya utumiaji kalamu kupotosha jamii makala yako imebaka historia ya kweli ya TAA/TANU na sasa CCM kama nilivyoeleza mwanzo pengine mapenzi ya chama kimoja wapo ndio mapenzi hayo yamekusukuma kuinanga historia ya kweli.

Ni matumaini yangu ipo siku utaungana na Joseph Mihagwa utajitolea kuuvunjaa mwiko wa kuuzungumzia muungano inavyostahili.

Shukrani sana na nakutakia siku njema wewe na jamaa wote wa JF.

Mohammed Shossi.

Maelezo yako hayapishani na maelezo ya M. M. Mwanakijiji. Mwanakijiji aliamua kwa makusudi kabisa kutowaingiza wajumbe watatu wa mwisho (kwenye red) kujenga hoja yake ambayo inawasilishwa na watu wanaopenda kuangalia mambo nusu nusu. Naomba kunukuu sehemu ya andiko lake:

"Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga"

Ikiwa watu hawawaoni viongozi wengine waanzilishi wa CHADEMA kama Bob Makani, Jacob Nkomola, na Mzee Brown Ng'wilulupi (ambao si wachaga) kwa sababu ya uchache wao; basi pia iwe ni halali kutowaona wakristu wachache waanzilishi ndani ya TANU na hivyo hivyo kwa CCM.

Kwa yako maelezo mkuu Mohammed Shosi; sioni alipopotoka M. M. Mwanakijiji.
 
Nilikuwa namheshimu sana huyo Mwanakijiji lakini kwa makala yake hiyo amepoteza kabisa heshima yake kwangu.
Kumbe yeye ni tool ileile inayoutumiwa na kundi moja la watanzania kuwakandamiza wengine!.
Tangu lini CCM ikafungamana na Waislamu? Waislamu wamenyanyaswa sana na kukandamizwa na hicho cha wakishirikiana na kanisa.
Kumbuka MOU nyingi zilisainiwa na makubaliano mengi yakunufaisha kanisa yalifikiwa na chama hicho kwa manufaa ya wakristo wa watanzania.
Kuwafungamanisha waislamu na CCM ni sawa na kuwatukana waziwazi!

Nakubali kwa siku za karibuni waislamu wameonyesha kama kuunga mkono serikali ya Kikwete. Ieleweke vema hapa waislamu hawaungi mkono CCM bali wanamtetea Rais ambaye anasakamwa kwa sababu ya dini yake.
Kwakuwa wakristo waliamua kumsakama Kikwete kwa kutumia Chadema, by default Waislamu watakuwa upande wa pili!.
N.B Kwanini Mwanakiji hakulaumu swala la UKRISTO ndani ya Chadema badala yake kakimbilia uchaga! Pia udini haupimwi kwa majina ya viongozi! bali ni dhamira za Chama!
Chadema ni tool ya kanisa hilo halina ubishi hata muandike makala ndefu kiasi gani!
 
Mkuu Shossi asante kwa historia hapo juu ila pia nina haya ya kusema:

1. Wewe unazungumzia TANU Mwanakijiji anazungumzia CCM. Wewe umezungumzia muundo wa TANU ulivyo kuwa yeye anazungumzia muundo wa CCM sasa. Kuna tofauti kubwa hapo.

2. Mwanakijiji hajasema moja kwa moja kwamba CCM ni chama cha Waislamu ila kama umesoma vizuri amesema kama ukikiita Chadema chama cha Wachaga basi kwa kutumia logic hiyo hiyo lazima ukiite CCM chama cha Waislamu na vice versa ila hiyo ni batili kama mtu haukioni Chadema kama chama cha kikabila na CCM cha kidini. SIjui umenielewa hapo mkuu?

Ni hayo tu kwa sasa. Akija atajieleza mwenyewe zaidi.

Ukweli unawauuma sana hawa wa CCM!
 
Hakuna udini unaokera kama kuangalia jina la mtu tu na kufikia tamati juu ya imani yake (dini yake!) na mbaya zaidi wakati mwingine 'kutoa hukumu'.
 
Chama Cha Mapinduzi kilipoasisiwa (wakati huo kikiitwa TANU na ASP) viongozi wake wengi walikuwa ni Waislamu. Hili siyo siri. Kwa upande wa TANU viongozi waanzilishi wake kabla hata Mwalimu Nyerere hajahamia Jijini Dar na kuanza shughuli za kisiasa rasmi walikuwa ni Waislamu maarufu wa Jiji la Dar ambao majina yao yalikuwa yakijulikana wakati huo.

Miongoni mwao tunaowakumbuka leo hii ni familia ya Sykes (maarufu kati yao akiwa ni Abdulwahid Sykes na kaka zake Ali na Abbas), masheikh maarufu wa Jiji la Dar es Salaam kama kina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Chaurembo na mzungumzaji maarufu, Sheikh Suleiman Takadir.

Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga.

Ni Waislamu hata hivyo waliokuwa na nguvu zaidi ndani ya TANU kutokana na nafasi zao na uwezo wao wa kifedha katika Jiji la Dar. Walitumia mali na nafasi zao kuweza kukijenga chama na wengine walitoa hata nyumba zao kwa ajili ya matumizi ya TANU.

Kitabu cha Mohammed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika kinaelezea kwa kina jinsi Waislamu walivyokuwa na nafasi ya pekee katika kuanzishwa kwa TANU kiasi kwamba sehemu mojawapo Said anatangaza pasipo shaka wala kujiuma meno kuwa “Kimsingi Chama cha TANU kilikuwa ni chama cha Waislamu”.

Lakini siyo kutokana na uasisi wake tu ndio maana TANU ilikuwa ni chama cha Waislamu bali pia eneo lake ambapo kilikuwa na nguvu sana. Kama CHADEMA kuwa na nguvu kwa muda mrefu mikoa ya Kaskazini kutokana na kukubalika zaidi maeneo hayo TANU nayo ilikuwa na nguvu sana katika maeneo ya Pwani na maeneo ambayo yalikuwa na Waislamu wengi kama Tabora, Tanga na Dar yenyewe.

Hivyo, kilikuwa ni chama cha Waislamu siyo kutokana na uasisi wake tu bali pia kutokana na maeneo yake ambayo kilikuwa kimekubalika zaidi kwani hata katika maeneo hayo mengine ni viongozi wengi wa Kiislamu waliokuwa wakijitokeza kukiunga mkono.

Kabla hatujaenda mbali labda tujikumbushe kilichoandikwa na mkjj kule kwenye ile thread nyingine
 
Nimesoma thread yako mara mbili kutafuta tofauti ya ulichokiandika na article ya Mwanakijiji. Sijaona tofauti katika maudhui na ujumbe.

Tofauti ni style ya presentation. Whilst wewe umetumia hisia za kishabiki zaidi (fanatism), Mwanakijiji ame-present objectively and in a balanced manner.
 
Nilikuwa namheshimu sana huyo Mwanakijiji lakini kwa makala yake hiyo amepoteza kabisa heshima yake kwangu.
Kumbe yeye ni tool ileile inayoutumiwa na kundi moja la watanzania kuwakandamiza wengine!.
Tangu lini CCM ikafungamana na Waislamu? Waislamu wamenyanyaswa sana na kukandamizwa na hicho cha wakishirikiana na kanisa.
Kumbuka MOU nyingi zilisainiwa na makubaliano mengi yakunufaisha kanisa yalifikiwa na chama hicho kwa manufaa ya wakristo wa watanzania.
Kuwafungamanisha waislamu na CCM ni sawa na kuwatukana waziwazi!

Nakubali kwa siku za karibuni waislamu wameonyesha kama kuunga mkono serikali ya Kikwete. Ieleweke vema hapa waislamu hawaungi mkono CCM bali wanamtetea Rais ambaye anasakamwa kwa sababu ya dini yake.
Kwakuwa wakristo waliamua kumsakama Kikwete kwa kutumia Chadema, by default Waislamu watakuwa upande wa pili!.
N.B Kwanini Mwanakiji hakulaumu swala la UKRISTO ndani ya Chadema badala yake kakimbilia uchaga! Pia udini haupimwi kwa majina ya viongozi! bali ni dhamira za Chama!
Chadema ni tool ya kanisa hilo halina ubishi hata muandike makala ndefu kiasi gani!

Kwa hiyo heshima yako umempa MS?
 
Magamba haoo....wamelipuliwa sasa wanahaha!
 
Attachments

  • Asilia Jazz Band2.rar
    1.7 MB · Views: 53
Mkuu Shossi asante kwa historia hapo juu ila pia nina haya ya kusema:

1. Wewe unazungumzia TANU Mwanakijiji anazungumzia CCM. Wewe umezungumzia muundo wa TANU ulivyo kuwa yeye anazungumzia muundo wa CCM sasa. Kuna tofauti kubwa hapo.

2. Mwanakijiji hajasema moja kwa moja kwamba CCM ni chama cha Waislamu ila kama umesoma vizuri amesema kama ukikiita Chadema chama cha Wachaga basi kwa kutumia logic hiyo hiyo lazima ukiite CCM chama cha Waislamu na vice versa ila hiyo ni batili kama mtu haukioni Chadema kama chama cha kikabila na CCM cha kidini. SIjui umenielewa hapo mkuu?

Ni hayo tu kwa sasa. Akija atajieleza mwenyewe zaidi.

Tatizo Mwanakijiji alipoa amua kuelezea historia ya TANU kwa kusudi alimua ku omit kwa kusudi role ya Wakristo na akatoa impression kuwa historia ya CCM ilianza na TANU ili hali mambo yalianza na TAA
 
Wangapi wanajua historia ya madaktari watano – Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere na mchango wao katika kusukuma mbele harakati za TAA kati ya 1948 – 1950?

Mohammed Shossi.

I dare to say, kuna watu hata kama walikwenda shule haijawasaidia sana, makala aliyoitoa MMK, ilijaribu kuainisha, kulinganisha na baadae kuweka bayana yale ambayo watu wataanza kujiuliza, kama CDM inadaiwa kuwa ya wachaga na wakristo kwa hoja tu eti kwasababu waanzilishi ni Christians na watu kutoka kilimanjaro, the same persons wanaweza kujiuliza swali hilo hilo juu ya vyama vingine, kama CCM, CUF NCCR-Mageuzi etc. Hapa kipi ambacho hakieleweki...kwanini watu tunapenda kufikiri ndani ya box na si nje? Unapokuwa na watu wa jinsi au aina ya MALARIA SUGU.....Ambao siku zote ukifuatilia post zao wanaongea upuuzi tu, na hakuna unachoweza kuambulia matokeo yake yatakuwa haya. Kila kinachojadilia au kuhojia kinapokuna na neno " Islam" ni negativity mwanzo-Mwisho.

Angalizo: Funguke viumbe mliopumbazika kwa ujinga wa watala wenu. Mnashindwa kujadili kwanini maisha yamekuwa magumu, nini source ya hayo yote tunaangalia upuuzi wa nanma hii..."damn". Jengeni hoja zitakazo mkomboa mtanzania na si habari ya wewe islam wewe christian, yatatufikisha wapi haya.
Wewe the so called Malaria Sugu, unatibu hospital ile ile ambayo haina madaktari, unapeleka watoto wako shule zile zile ambazo hazina vifaa na miundo mbinu nyingine, wewe huyo huyo unatoka kijiji kile kile kama changu ambako hakuna maji wala umeme achilia mbali huduma za afya, nani anapaswa kuyafanya haya, nani anapaswa kuhoji haya. Tubadirike Watanzania, tufunguke macho yetu, achaneni na viongozi wa dini au siasa wanao hubiri ujinga huu.
 
......mimi siyo mod lakini ninaamini wametumia busara ya kuondoa duplications kwani ulichoandika weye na kile cha Mwanakijiji hakuna tofauti kubwa za msingi in terms of the facts presented.

tofauti pekee ni kuwa wewe umetumia hamaki ya ushabiki (fanatism) zaidi. basi.

hata miye ningekuwa mod ningeiondoa kuokoa the much needed cyber resources!
 
Kiongozi tatizo thread yako imekuja kiutetezi.

Title yako inasema : "Mwanakijiji na Uislam wa TAA/TANU mpaka CCM" kwa nini haikuwa "Mwanakijiji na Uchaga wa Chadema"??

Makala ya Mwanakijiji haikumaanisha CCM ni ya waislaam alichokifanya ni kuuambia Umma wa Tanzania kuwa iwapo tunakubali kikundi cha watu (CCM) kutuambia wale ni wachaga (CDM) au wale ni waislam siasa kali (CUF) basi tutumie fomula hiyo hiyo kuitazama CCM ili tuweze kuhukumu kwamba "ile ni ya waislam au ya wazanaki".

Hakuna haja ya kutoa povu kwa jambo lisilokuwepo, hoja ya MMM inawaonya watanzania wasiendekeze ubaguzi. Kama mnataka mjadala basi uwe juu ya fomula ilotumika kusema hawa ni wachaga/wakatolik/wakristo na hawa ni waislam/wa mwambao.

Hivi maelezo kama haya chini yana ugwadu wowote???

"Hivyo tunaweza kuona kwa urahisi kabisa kuwa tuhuma za Uchagga wa CHADEMA zinatokana na mambo makubwa matatu: uasisi wake, uongozi wake na nafasi za wanachama wake maarufu wanatoka maeneo gani ya nchi. Tukumbuke kuwa kinachoangaliwa katika “ukabila” huu ni kile kinachoonekana ni “wingi” au idadi ya Wachagga ndani ya CHADEMA na nafasi zao kubwa za kisiasa. "

"Kitabu cha Mohammed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika kinaelezea kwa kina jinsi Waislamu walivyokuwa na nafasi ya pekee katika kuanzishwa kwa TANU kiasi kwamba sehemu mojawapo Said anatangaza pasipo shaka wala kujiuma meno kuwa “Kimsingi Chama cha TANU kilikuwa ni chama cha Waislamu”.

"Kuwaendekeza hawa ni kuliandaa taifa kwa majanga kwani chuki dhidi ya Wachagga ambayo imepandikizwa kwa muda mrefu katika jamii fulani ya watu inazidi kukua na sasa kuna ushahidi imepitishwa kwenda kizazi cha pili. Tunakumbuka sisi wengine kuwa chuki hii ilikuwepo wakati wa Mwalimu hadi tume ya Mang’enya ikaundwa kufuatilia na sasa hivi wameibuka watu wengine ambao wanalindwa na watawala walioko madarakani kwa ajili ya kujipatia manufaa ya kisiasa wakiendeleza chuki dhidi ya Wachagga."
 
Back
Top Bottom