Mwanakijiji apendekeza mabadiliko ya Mfumo wa Uongozi CHADEMA

All I would say is IF IT'S NOT BROKEN DON'T TRY TO FIX IT.Kama mfumo wa sasa umeweza kuifikisha Chadema hapa ilipo sasa,kwanini tuanze mifumo mingine ya majaribio?What if it's not going to work?Practically,katika mazingira tuliyonayo na ukweli kwamba Chadema bado ni chama kichanga,jaribio la kutenganisha uongozi linaweza kupelekea kusambaratisha chama hicho.

Ubunge si jukumu linaloweza kumnyima mwanasiasa fursa ya kukitumikia chama chake na wananchi kwa uadilifu iwapo anajua majukumu na priority zake.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Duh itabidi niisome vizuri tena ilivyochapishwa kwa sababu kwa kadiri ninavyojua sikuwaomba watu wajiuzulu uongozi CHADEMA! Mawazo yangu juu ya hili siyo mageni, nilishayainisha kwenye "Kutoka Hapa Mpaka Kule" na kuelezea jinsi vitani huwezi kupeleka majemedari wote mstari wa mbele halafu hao hao ndio wawe mstari wa nyuma kupanga yanayotokea mstari wa mbele. Nakumbuka nilitoa mfano kuwa Pentagon haipeleki majemedari wake wote Iraq au Afghanistan. Na kimsini hakuna jeshi linaloweza kufanya hivyo.

Hata CCM haifanyi hivyo, Kinana, Msekwa, Makamba, Malecela na wengine hawaiingii Bungeni.. Ni utilization of resources. Chadema sasa hivi ina watu wengi sana kiasi kwamba concentration of power inahitaji kuangaliwa upya kama kweli ushindi ndio dhamira. Fikiria:

Mwenyeki wa Chama => Ni Mbunge wa Hai => Kiongozi wa Kambi ya Upinzani => Waziri Kivuli (PM) => Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama => n.k n.k

Naweza kutolea mifano wengine. Chadema inaelekea miaka 20 ya kuwepo kwake siyo chama kichanga tena kama wengine wanavyoamini na wakati umefika kianze kuonesha ukomavu na kubadili hata muundo wake usifanane na wa CCM sasa hivi karibu vyama vyote nchini vina mfumo wa kisoshalisti wa kiongozi ulioingizwa na kujengwa na CCM. Labda ndio mfumo pekee tunaoujua.

Wengine wanasema ati mabadiliko hayo siyo sasa hadi 2015. Niwahakikishie pasipo kutumia nguvu kubwa ya kubashiri. Kama Chadema itaenda kwenye uchaguzi mkuu katika mtindo huu ambapo 90 percent ya viongozi wake wa chama ni wagombea basi CCM hawatoitaji kufanya kazi kubwa kustrain the party machinery kama walivyofanya uchaguzi uliopita na kama nilivyoonesha mapema wakati ule vile vile. It is all political mechanization..

Sijasema wajiuzulu (kama walivyofanya CCM) bali chama kiangalie mfumo na muundo wake kwanza ili wainstitute mabadiliko ambayo yatasababisha wabunge wasiwe viongozi watendaji wa chama. Haliitaji kufanyika kesho lakini halipaswi kusubiri miaka miwili kabla ya uchaguzi. Ninaamini linahitaji kutokea sometimes mwaka huu.

While I quite agree with most of ideas in this concept bado naona kwa CHADEMA ku institute hii concept ni mapema mno kwani bado ni chama kichanga. Uchanga wake si kwa miaka iliyoishi lakini kwenye Ideology yake na wanachama wake. Hakuna common conceptualization amongst members wa CHADEMA ambao bado hawajaijua vizuri what are the core values and where do they stand when it comes to conceptualization/Ideology. Viongozi waliopo ndiyo haswa visionery wa CHADEMA and they need to be in all areas to make sure chama hakiwi sabotaged na newly recruited members ambao bado hatujui ni opportunist ama they are dedicated to the party. Hatari ni kuwa hawa executive wasipokuwa na some of the authoritarian powers at one point things might go out of hands and easily defeated by their opponents. So kama ilivyo kwa katiba ya nchi ambayo Nyerere alijipa madaraka makubwa kwani this was very relevant wakati huo ambapo most of the people could be easly used kama hata apply a kind of dictatorship for the sake of kujenga nchi. Lakini hii yeye kama founder aliamini kuwa anafanya for a good faith lakini matokeo yake tumeona aliposhindwa kui dismantle mapema pale alipo ona sasa balance of power ina hitajika ili kuwe na acounterbilities.

So what you are proposing ni very relevant kwa CCM ambayo Ideology yao inajulikana japo hata wao wamekuwa of the moment derailed from it. Lakini kuna members wana stake kwenye chama so betrayals ni nonelikely kuliko ilivyo kwenye CHADEMA ambapo Slaa; Mbowe and wazee wa chama wame invest kiasi cha kutosha kwamba ku betray is like self denial na hivyo you will expect them doing all the time to the favour of the party in whatever the case. Hii kwenye system building tunaiita public procurement stage; maana hapa unapojenga system huangalii push and pull mechanisms ili kuwe na balancing of the two opposing or indirectly propotional forces na hivyo ni muhimu kuipa nguvu moja ambayo inaweza kulemewa na mara nyingi ni hii push. So the pushing agents for this case are the founders wa chama.
 
All I would say is IF IT'S NOT BROKEN DON'T TRY TO FIX IT.Kama mfumo wa sasa umeweza kuifikisha Chadema hapa ilipo sasa

Mlalahoi, unapresume kuwa hapa ilipofikishwa ni bora zaidi. Hoja yangu ni kuwa mabadiliko ya mfumo kama yangefanyika mapema zaidi yangeweza kuifikisha Chadema mbali zaidi kuliko illipo sasa. Binafsi ninaamini kuwa mfumo uliopo sasa uliigharimu sana Chadema kura za wabunge na usimamizi kuelekea uchaguzi mkuu na hivyo kama ungekuwa umebadilishwa mapema labda wangepata zaidi ya viti 100 vya kuchaguliwa siyo 23!

So, the system is broken si kwa maana ya kuwa haujafanya vizuri bali kwa maana ya kwamba haujafanya vizuri ambavyo ingewezekana. Kwa mfano, gari ambalo limetoka upepo kwenye matairi linaweza kwenda lakini halitokwenda vizuri kama ambavyo lingekuwa na matairi. Sasa kusema gari limeweza kutufikisha maili 20 kwa dakika kumi wakati kama lingekuwa na upepo lingeweza kutufikisha kwa dakika tano hatuwezi kusema tusijaze upepo kwa sababu "mbona tumefika"?

,kwanini tuanze mifumo mingine ya majaribio?What if it's not going to work?Practically,katika mazingira tuliyonayo na ukweli kwamba Chadema bado ni chama kichanga,jaribio la kutenganisha uongozi linaweza kupelekea kusambaratisha chama hicho.

Tukiendelea kuamini kuwa Chadema ni chama kichanga tutaendelea kukilisha kwa kijiko na kubeba mgongoni hadi wakati unafika kinatuambia "mama kaa chini ninyonye". Chadema siyo chama kichanga tena. Kimeshirika chaguzi kuu nne, kina wabunge kuanzia 1995 na hivyo dhana ya "uchanga" haipo tena.

Ubunge si jukumu linaloweza kumnyima mwanasiasa fursa ya kukitumikia chama chake na wananchi kwa uadilifu iwapo anajua majukumu na priority zake.

Jiulize hivi: Wakati Kikao cha Bunge kinaendelea Dodoma:

Mwenyekiti yuko Dodoma
Makamu yuko Dodoma
Naibu yuko Dodoma
vwajumbe karibu wote wa Kamati Kuu wanakuwa Dodoma.

Hii ina maana maofisa wote wa chama wanalazimika kuwa Dodoma. Sasa wenzetu CCM wana akili.. guess makao makuu ya CCM yako wapi? DODOMA! Ndio maana CCM wanaweza kupanga vikao vya kamati kuu, halmashauri kuu huko huko Dodoma. Kwa Chadema makao makuu yako Dar inabidi maofisa wa chama wawe wanafuatilia mambo Dodoma ili kuwa na wabunge ambao ni viongozi wa chama.

Hilo ni tatizo moja

Tatizo la pili ni kuwa inapokuja kwenye kusimamia nidhamu ya Chama Makao Makuu na Bungeni watu wale wale ndio wenye kusimamia mambo yale yale. Matokeo yake kwa mfano bungeni, Mwenyekiti wa Chama ndiye kiongozi Mkuu wa Upinzani na hivyo anakuwa na kofia mbili za kutumia - anaweza kutumia Uenyekiti wake kuleta nidhamu au kutumia uongozi wa KRU. Je, wabunge wa chama chake wanapoona kuwa mambo hayaendi vizuri kule Bungeni waende kumwambia nani? - well.. mwenyekiti! Tatizo jingine ni kuwa Naibu Katibu Mkuu naye ni Mbunge na wakati huo huo ni kiongozi mkuu msaidizi wa upinzani!

Well ni mfumo mbovu tu. Is unnecessary concentration of power and duties in the handful number of individuals. Nitakupa mfano mzuri. Hivi unajua kwanini viongozi wa Republican au Democrats Makao Makuu siyo Wawakilishi au Maseneta huko Marekani?
 
Hili wazo zuri sana. Kama wengine walivyosema, liwe lengo la muda mrefu. CCM ndio inatakiwa iwatenganishe watendaji wa serikali na wa chama
 
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ktk gazeti la mwanahalisi wiki hii- ilikuwa ni makala nzuri sana. Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM inayojivua gamba. Anashauri kuwa viongozi wa Chadema ambao ni wabunge na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao. Yaani kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA.
Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake.
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.

Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.

Duh! Dr Slaa aliuliza kwanza tofauti ya malipo ya bungeni na yale yatokanayo na ruzuku! Bungeni kuna ulaji.
 
Mlalahoi, unapresume kuwa hapa ilipofikishwa ni bora zaidi. Hoja yangu ni kuwa mabadiliko ya mfumo kama yangefanyika mapema zaidi yangeweza kuifikisha Chadema mbali zaidi kuliko illipo sasa. Binafsi ninaamini kuwa mfumo uliopo sasa uliigharimu sana Chadema kura za wabunge na usimamizi kuelekea uchaguzi mkuu na hivyo kama ungekuwa umebadilishwa mapema labda wangepata zaidi ya viti 100 vya kuchaguliwa siyo 23!

So, the system is broken si kwa maana ya kuwa haujafanya vizuri bali kwa maana ya kwamba haujafanya vizuri ambavyo ingewezekana. Kwa mfano, gari ambalo limetoka upepo kwenye matairi linaweza kwenda lakini halitokwenda vizuri kama ambavyo lingekuwa na matairi. Sasa kusema gari limeweza kutufikisha maili 20 kwa dakika kumi wakati kama lingekuwa na upepo lingeweza kutufikisha kwa dakika tano hatuwezi kusema tusijaze upepo kwa sababu "mbona tumefika"?

Tukiendelea kuamini kuwa Chadema ni chama kichanga tutaendelea kukilisha kwa kijiko na kubeba mgongoni hadi wakati unafika kinatuambia "mama kaa chini ninyonye". Chadema siyo chama kichanga tena. Kimeshirika chaguzi kuu nne, kina wabunge kuanzia 1995 na hivyo dhana ya "uchanga" haipo tena.

Jiulize hivi: Wakati Kikao cha Bunge kinaendelea Dodoma:

Mwenyekiti yuko Dodoma
Makamu yuko Dodoma
Naibu yuko Dodoma
vwajumbe karibu wote wa Kamati Kuu wanakuwa Dodoma.

Hii ina maana maofisa wote wa chama wanalazimika kuwa Dodoma. Sasa wenzetu CCM wana akili.. guess makao makuu ya CCM yako wapi? DODOMA! Ndio maana CCM wanaweza kupanga vikao vya kamati kuu, halmashauri kuu huko huko Dodoma. Kwa Chadema makao makuu yako Dar inabidi maofisa wa chama wawe wanafuatilia mambo Dodoma ili kuwa na wabunge ambao ni viongozi wa chama.

Hilo ni tatizo moja

Tatizo la pili ni kuwa inapokuja kwenye kusimamia nidhamu ya Chama Makao Makuu na Bungeni watu wale wale ndio wenye kusimamia mambo yale yale. Matokeo yake kwa mfano bungeni, Mwenyekiti wa Chama ndiye kiongozi Mkuu wa Upinzani na hivyo anakuwa na kofia mbili za kutumia - anaweza kutumia Uenyekiti wake kuleta nidhamu au kutumia uongozi wa KRU. Je, wabunge wa chama chake wanapoona kuwa mambo hayaendi vizuri kule Bungeni waende kumwambia nani? - well.. mwenyekiti! Tatizo jingine ni kuwa Naibu Katibu Mkuu naye ni Mbunge na wakati huo huo ni kiongozi mkuu msaidizi wa upinzani!

Well ni mfumo mbovu tu. Is unnecessary concentration of power and duties in the handful number of individuals. Nitakupa mfano mzuri. Hivi unajua kwanini viongozi wa Republican au Democrats Makao Makuu siyo Wawakilishi au Maseneta huko Marekani?

UK PIA sivyo, Kameroon siyo wala Obama siyo Mwenyekiti wa chama chake! sijui wala siungi Mkona hoja ila nimeipenda sana; Pia kuna nyingine naipenda sana ipo Kenya kama huwezi kushinda Ubunge huwezi kuwa Raisi au!? .
 
UK na US mfumo ambao unakubalika ni kuwa chama kinapomtoa Rais/Waziri Mkuu basi ndiyo anakuwa "Kiongozi Mkuu wa Chama" yaani anakuwa hata juu ya Mwenyekiti wa Chama kwa muda wote anashikilia nafasi hizo. Hata hivyo haingilia mambo ya utendaji ni kiongozi kwa maana ya kupush ajenda ya chama chake katika muda wake wa uongozi.
 
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ktk gazeti la mwanahalisi wiki hii- ilikuwa ni makala nzuri sana. Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM inayojivua gamba. Anashauri kuwa viongozi wa Chadema ambao ni wabunge na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao. Yaani kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA.
Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake.
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.

Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.

siku zote nitaunga hoja zenye maana mkono kama hii, ila simtu: ni kweli CDM uchaguzi uliyopita SLAA alipambana mwenyewe kwa kiasi kikubwa kwani timu ambayo alikuwa nayo niwachache sana waliyo kuwa wanaweza kumuongezea SLAA kura , wengi wao walikuwa ni wapigakelele tu, ila walikuwa hawana ushawishi kwa wananchi, mtu ambaye alikuwa akimpatia slaa kura kwenye msafara ule kutoka kwenye makundi ya vijana ni yule kijana wa tarime kama sikosei anaitwa john eche,

kiukweli mawazo haya niyakuyafanyia kazi kwelikweli kwakuwa watanzania wanamatumaini makubwa sana na CDM ilikufanikiwa lazima sasa wapatikane watendaji ambao hawajabanwa na shughuli zingine kazi zao ziwe ni siasa tu.
kwa mfano: nitashangaa sana kwa mbunge yeyote yule wa chadema kwasasa atakaye gombea nafasi yeyote ile ya vijana BAVICHA taifa kiukweli watakuwa hawajatenda haki , kama kamati kuu ya chama hicho itakaa na kupitisha jina la mbunge yeyote yule. tunategemea watachukua wengi fomu ila warudi wachache.

kwani vijana wa CDM watakuwa ndiyo engneer ya chama na tumaini jipya kwa vijana na taifa lao
 
hii ni mipango ya muda mrefu kwakweli maana inabidi kujua source ya fund kwa CHADEMA na bajeti zao mapato na matumizi then kinachobaki unajua kumhudumia mwenyekiti na sekretariet yake inahitaji gharama kubwa sana itabidi CHADEMA wajipange kwanza kwa hilo!

I do agree with u kwani CDM kwa sasa lazima wawe na vitega uchumi ambavyo vitasaidia wanachama wengine ambao sio wabunge kuwa na madaraka ktk chama na kuwapunguzia mzigo wabunge. Na pia kuwapa fursa wanachama kushiriki kikamilifu katika uongozi na kuondoa biaseness interms of good governance.
 
I dont think if the new proposed system will work out. Kumbuka hao viongozi wa ccm ambao hawaingii bungeni wengi wao wamewahi kuwa wabunge na wengine kushika nyazfa mbalimbali serikalini. Kwa kifupi ni watu ambao wanajulikana machoni mwa watu. Chadema bado hakijawa na makada wengi wa aina hiyo ambao wanaweza kushikilia nafasi za uongozi nadhan mfumo wa uongozi uliopo unapaswa kuendelea hadi chama kitakapokuwa kimejijenga vya kutosha.
 
Yes,

Nakubaliana na wewe hapo juu. Hebu imagine CDM imechukua nchi 2015, nani atasema ah mimi sataki cheo chochote serikalini yaani mtu aukatae uwaziri eti abaki kuwa kiongozi wa chama, hayupo. Wote wataingia serikalini na atakosekana mtendaji wa chama, hadi utakapofanyika uchaguzi, lioneni hilo.

Sina uhakika ni nani aliyejibu pale juu kwamba "Wazo baya, hatuwezi kuiga popote, oh tuna utaratibu wetu na kwamba hawezi ku-resign popote". Huyu anaonekana ni kati ya wabunge tulionao na kwa vyovyote ni kati ya viongozi wa chama. Sawa ni mawazo yake. Lakini akumbuke chama ni mali ya wana chama, na haya mawazo yanayotolewa hayawezi tu kupuuzwa, ni lazima tuwe more focused.

Anasema hatuwezi kuiga< Nani kasema kwamba kuiga mambo mazuri ni kosa. Iga mambo mazuri, usiige uozo ndiyo principle. Naomba wazo la Mwanakijiji lisipuuzwe, tusije sema tungejua!!.
 
naamini chadema kama taasisi wanafahamu kipindi hiki muhimu cha kufanya mabadiliko hivyo nisahihi kufanyia kazi maoni ya mwanakijiji.
 
Back
Top Bottom