Mwanakijiji apendekeza mabadiliko ya Mfumo wa Uongozi CHADEMA

hoja yako ni nzuri,lakini si mwafaka kwa kipindi hiki. Acha wabunge wawe pia viongozi wa chama hadi CDM itakapokomboa nchi ndipo mgawanyo wa ki madaraka (CHAMA + SERIAKALI) utakapojipambanua
Upo sawa kaka
 
Ni mpango mzuri sana lakini...
Kwa misimamo ya KITANZANIA...
UBINAFSI, CHUKI NA CHOYO...
UFISADI NA UCHU WA MADARAKA...
ushauri huo unaweza kuwa ndilo kaburi rasmi la CHADEMA na VYAMA vingine VILIVYOKO NCHI HII!!
 
Ubunge ndio unawapa mshahara hivyo kuwa na nguvu ya kupigana zaidi. Jiulize kwa nini Maalim Seif aliolewa na ccm kirahisi hivyo bila hata kulipiwa mahari na tena akafika mahali akaanza kampeni kwamba uchaguzi usifanyike Zanzibar ili apate kula kidogo (hakuamini kwamba angekuja kupewa cheo cha mama wa nyumbani ikulu)
Teh teh teh baba umeuaaaaa!!!!'
 
mwaka 2006, nilipoanza kusoma post za Mmkjj hakika hapo ndipo nilipoanza kuzinduka, nikaanza kujiamini, uchungu na asila vikaongezeka.
 
ni wazo zuri sio siri. Ila muda wake bado, isubiriwe 2015 chadema iwe chama tawala...ndio hili swala litungiwe mwongozo kwenye chama.

aluta continua
 
Its too early to do that,kwa sasa napendekeza utaratibu ubaki kama ulivyo,
Ukiona tim pinzani inahangaika kubadili wachezaji ni dalili ya kuzidiwa ki mchezo na sisi tukithubutu kubadili tu itakula kwetu mbaya

Lakini mbona nikiangalia CCM bado haina safu yoyote ya mashambulizi hata iumize watu akili labda kwa tahadhari tuangalie namna ya kuzichunga pasi .
 
Nadhani ni busara kupata muongozo rasmi toka kwa wenyewe CDM, kwamba hili wazo wamelichukulia vipi.
Ila ni wazo lenye mashiko sana.
Ila natamani niwasikie kwanza wenyewe CDM wanalizungumziaje hili wazo
 
PHP:
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ktk gazeti la mwanahalisi wiki hii-  ilikuwa ni makala nzuri sana. Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo  ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM  inayojivua gamba. Anashauri kuwa  viongozi wa Chadema ambao ni wabunge  na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM  inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata  system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao. Yaani  kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha  uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa  Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao  ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA. 
Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana  na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake. 
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.
 
Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya  kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa  mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge  hawalipwi kabisa.
Hoja hii ina mashiko......Chadema nao wajivue gamba la kujirundikia madaraka mtu mmoja na kuonyesha kwa vitendo wanaelewa maana halisi ya mgawanyo wa madaraka wa mihimili mitatu ya dola ambayo ni moja ya hoja ya kudai katiba mpya......................a speck in CCM eye is intolerable but a cobweb in Chadema'eye is tolerable.........it does not click at all.................
 
hoja yako hatakuwa na maana kwani kazi kubwa ya chama cha siasa ni kjiandaa ili kuchukuwa uongozi. kuwa kiongozi wa chama cha siasa kazi kubwa inayofanywa ni kuwajengea viongozi wa chama husika uwezo ili wao waweze kuchukua hatamu. hivyo sioni kama wazo lako linaumuhimu kwani muda mwingi utatumika kufanya chguzi badala ya kufanya maendeleo. ushauri wangu namuomba mwanakijiji ajiulize ni kwanini kunavyama vya siasa na usumbufu utaojitokeza kwani naamini kiuongozi kuwa mwakilishi wa watu hapohapo unajukumu ndani ya chama hebu fikiria vizuri before hujaandika
 
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ktk gazeti la mwanahalisi wiki hii- ilikuwa ni makala nzuri sana. Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM inayojivua gamba. Anashauri kuwa viongozi wa Chadema ambao ni wabunge na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao. Yaani kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA.
Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake.
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.

Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.


Mi nilidhani wapo bungeni kutetea wananchi kama wanavyohubiri! Kumbe ni kwa ajili ya mishahara tuu?
No wonder CDM leaders hate Tanzania So Much!
 
Mwanakijiji kichwa! Endelea kuwashauri ili wajipange vyema. A typical great thinker
 
Mimi nimuunge mkono Mkjj kuwa wazo ni zuri ila linapaswa kutekelezwa kwa umakini mkubwa kama CDM wataliafiki. Kwa mtazamo wangu stress iwekwe kwenye Secretariet maana hicho ndio chombo muhimu kwa chama kiutendaji. Ukizingatia sasa hv kuwa CDM bado ni chama kinachokua ila ni maarufu kuliko CCM.

Ipo kazi kubwa ya kujenga misingi na kujitangaza zaidi kwa wananchi ili kuweza kukabiliana na nguvu iliyobakia ya CCM huko rural areas. Sasa Dr. Slaa anatakiwa kuwa na timu madhubuti ambayo moja ya kazi kubwa ni kujua namna ya kutafuta resources za kufanya hiyo kazi ya uenezi. Ila kwa mfumo wa sasa wa wajumbe wa secretariet kuwa wabunge inawanyima fursa ya kufanya shughuli nyingi za chama. Mimi naamini CDM ina mtaji mkubwa tu wa watendaji hodari hata kama kina Zitto na Mnyika wakipumzishwa kwenye secretariet.

Kwa nafasi ya Mwenyekiti mimi sioni haja kufanyiwa kufanyiwa mabadiliko kutokana na Mwenyekiti kushiriki zaidi kwenye vikao vya maamuzi kuliko uwajibikaji wa kila siku kwenye chama. Tena kama CDM wanataka kufanya vyemawasikurupuke ila inapaswa kutekeleza haya katika kikao kijacho cha uchaguzi ndani ya chama na sio kutimuana kama CCM huko dodoma wasije kuyumba na kupoteza mwelekeo ili kutoa fursa kwa viongozi wanaoshika nafasi mbalimbali kupima sasa kuwa kipi wanakimudu zaidi.

Naomba kuwasilisha.
 
Duh itabidi niisome vizuri tena ilivyochapishwa kwa sababu kwa kadiri ninavyojua sikuwaomba watu wajiuzulu uongozi CHADEMA! Mawazo yangu juu ya hili siyo mageni, nilishayainisha kwenye "Kutoka Hapa Mpaka Kule" na kuelezea jinsi vitani huwezi kupeleka majemedari wote mstari wa mbele halafu hao hao ndio wawe mstari wa nyuma kupanga yanayotokea mstari wa mbele. Nakumbuka nilitoa mfano kuwa Pentagon haipeleki majemedari wake wote Iraq au Afghanistan. Na kimsini hakuna jeshi linaloweza kufanya hivyo.

Hata CCM haifanyi hivyo, Kinana, Msekwa, Makamba, Malecela na wengine hawaiingii Bungeni.. Ni utilization of resources. Chadema sasa hivi ina watu wengi sana kiasi kwamba concentration of power inahitaji kuangaliwa upya kama kweli ushindi ndio dhamira. Fikiria:

Mwenyeki wa Chama => Ni Mbunge wa Hai => Kiongozi wa Kambi ya Upinzani => Waziri Kivuli (PM) => Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama => n.k n.k

Naweza kutolea mifano wengine. Chadema inaelekea miaka 20 ya kuwepo kwake siyo chama kichanga tena kama wengine wanavyoamini na wakati umefika kianze kuonesha ukomavu na kubadili hata muundo wake usifanane na wa CCM sasa hivi karibu vyama vyote nchini vina mfumo wa kisoshalisti wa kiongozi ulioingizwa na kujengwa na CCM. Labda ndio mfumo pekee tunaoujua.

Wengine wanasema ati mabadiliko hayo siyo sasa hadi 2015. Niwahakikishie pasipo kutumia nguvu kubwa ya kubashiri. Kama Chadema itaenda kwenye uchaguzi mkuu katika mtindo huu ambapo 90 percent ya viongozi wake wa chama ni wagombea basi CCM hawatoitaji kufanya kazi kubwa kustrain the party machinery kama walivyofanya uchaguzi uliopita na kama nilivyoonesha mapema wakati ule vile vile. It is all political mechanization..

Sijasema wajiuzulu (kama walivyofanya CCM) bali chama kiangalie mfumo na muundo wake kwanza ili wainstitute mabadiliko ambayo yatasababisha wabunge wasiwe viongozi watendaji wa chama. Haliitaji kufanyika kesho lakini halipaswi kusubiri miaka miwili kabla ya uchaguzi. Ninaamini linahitaji kutokea sometimes mwaka huu.
 
Kwa ujumla uwezo wa kujikimu ni muhimu ili mtu aendeleze mapambano. Ndiyo maana naunga mkono, kwa sasa, kuvaa kofia mbili

Lakini Chadema waanze kupunguza over dependence kwa wabunge wao. Kuna majimbo chama kiliimarishwa bila kuwepo wabunge. Wananchi wanajitolea, hasa sasa wanapenda Chadema. Viongozi wa chama waratibu nguvu za wananchi kuimarisha chama vijijini.

Wabunge hawana muda wa kutosha. Vikao vya bunge vikiisha kazi za kamati zinaanza. Ama watashindwa kufanya kazi za bunge vizuri au kazi ya kuimarisha chama. Tumeona hata maandamano husitishwa kila vikao vya bunge vikianza

Pia lazima kuwe na kundi linalotunga sera na kutoa miongozo na discipline kwa wabunge wao. Namna hii hata hisia za wabunge wa Chadema kununuliwa zitapungua
 
Ni mawazo mazuri lakini yanahitaji tafiti za kisayansi kuonaadhari zinazojweza kujiitokeza kwa mtu kuwa mbunge na kiongozi wa kingozi wa chama. vinginevyo sioni kama kuna shida mtu kuwa na kofia mbili. na si lazima kuiga mfumo wa wamarekani mana siasa za marekani ni tofauti na TZ.
 
Mawazo ya MKKJ ni mazuri lakini kwa mazingira yetu Africa sidhani kama yanawezekana. Lakini kwenye hiyo article, je alijaribu kulinganisha UK na USA systems? Maana ya Uk ni kama hii ya Kibongo!!
 
Twende taratibu.Ingawa sijaisoma hiyo habari lakin sishauri kuwa iwe hivyo.Hawa njaa itawakaba na halafu watkuja kutekwa nyara kirahisi na ccm.Kumbuka njaa si mchezo,bora wabakie huko then vijisent vyao viwasaidie visiwe kikwazo kwa majukumu yao.Mfumo huo wa marekani ni kwamba chama kina pesa ya kuwalipa hao viongozi,wala hawahitaji kukimbilia serikalini kupata fadhila.
 
Back
Top Bottom