Mwanakijiji amshitua Pinda

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameshtushwa na swali lililomtaka kutoa maelezo ya kwa nini Serikali inahofu kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyobariki mgombea binafsi.

Swali hilo liliulizwa jana na mkazi wa kijiji cha Ibushi, Joseph Mazwazwa, mara baada ya Pinda kukagua bwawa linalotumika kwa shughuli mbalimbali za binadamu, wanyama na kilimo.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu ni kwa nini Serikali inahofia kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ingawa Mahakama Kuu ilishabariki kuwapo kwa mfumo huo katika uchaguzi?," aliuliza.

Waziri Mkuu alimjibu kwa kusema, ni kweli Mahakama Kuu ilibariki mgombea binafsi baada ya kesi ya suala hilo kuwasilishwa mahakamani hapo.

Alisema hata hivyo suala hilo linaleta utatanishi kutokana na tafsiri ya kikatiba, kwa kuwa Katiba inasema mgombea katika nafasi za kisiasa, kama diwani, Mbunge na Rais, ni lazima atokane na chama cha siasa kilichosajiliwa.

Alisema, hatua hiyo ndiyo inayoleta utata kwa Serikali kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi.

"Ni sababu hizi hasa ndizo ambazo zimetufanya kupinga uamuzi huu wa Mahakama. Hata hivyo wenzetu bado wanataka mfumo huu uwepo na ndiyo maana wamekata rufaa katika chombo cha juu ambacho ni Mahakama ya Rufaa ili mfumo huu uruhusiwe.

"Hata hivyo kesi hii kwa ngazi ya Mahakama ya Rufaa bado haijatolewa uamuzi, kwa hiyo ni vigumu kueleza. Mahakama ya Rufaa ikibariki uamuzi huu basi hatutakuwa na la kufanya itabidi tukubaliane na matokeo katika suala hili," alisema Waziri Mkuu.

Kesi ya kutaka Mahakama kukubaliana na kuwapo kwa mfumo wa mgombea binafsi, ilifunguliwa katika Mahakama Kuu na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na Mahakama hiyo iliamuru mfumo huo kuanza kutumika, lakini Serikali ilikataa kutekeleza amri hiyo ya Mahakama.

Hata hivyo katika siku za karibuni wanaharakati wamekuwa wakishinikiza Serikali ikubali mfumo huo kwani tayari kuna uamuzi wa Mahakama wa kuuruhusu, hata kama Mahakama ya Rufaa itakuwa bado haijatoa uamuzi kwa suala hilo.
 
1. Wanavijiji wa Tanzania tunawa-underestimate sana, mimi nilivyosoma kichwa cha thread nikafikiri huyu ni "Mwanakijiji" wetu hapa JF, kumbe kuna watu wana rep huko.

2. Jibu la Pinda ni unafiki mtupu. Kama Mahakama ndicho chombo cha ku-interpret sheria, kwa nini serikali kuu ina hijack hiyo role?

Bottom line, tunahitaji mabadiliko ya katiba na kufanya overhaul.
 
Ni sababu hizi hasa ndizo ambazo zimetufanya kupinga uamuzi huu wa Mahakama. Hata hivyo wenzetu bado wanataka mfumo huu uwepo na ndiyo maana wamekata rufaa katika chombo cha juu ambacho ni Mahakama ya Rufaa ili mfumo huu uruhusiwe.

“Hata hivyo kesi hii kwa ngazi ya Mahakama ya Rufaa bado haijatolewa uamuzi, kwa hiyo ni vigumu kueleza. Mahakama ya Rufaa ikibariki uamuzi huu basi hatutakuwa na la kufanya itabidi tukubaliane na matokeo katika suala hili

huyu mtu ana matatizo!

kwanza, ni serikali iliyokata rufaa, pili Mahakama Kuu imeshabariki uamuzi huo kwa kutoa angalizo. Hivi wakati kina Nguza wamekata rufaa walikuwa nje wanasubiri hukumu yao badala ya kuendelea kutekeleza hukumu ya awali? Hivi kukata rufaa kunasababisha automatic stay ya hukumu ya awali?
 
NOP ndio wanasema nchi ni ya kwao sisi wengine tulie tu.
 
huyu mtu ana matatizo!

kwanza, ni serikali iliyokata rufaa, pili Mahakama Kuu imeshabariki uamuzi huo kwa kutoa angalizo. Hivi wakati kina Nguza wamekata rufaa walikuwa nje wanasubiri hukumu yao badala ya kuendelea kutekeleza hukumu ya awali? Hivi kukata rufaa kunasababisha automatic stay ya hukumu ya awali?

Nilivosoma heading kwa haraka nilidhani ni wewe mkuu kumbw we kijiji chako kiko mjini teh teh
 
huyu mtu ana matatizo!

kwanza, ni serikali iliyokata rufaa, pili Mahakama Kuu imeshabariki uamuzi huo kwa kutoa angalizo. Hivi wakati kina Nguza wamekata rufaa walikuwa nje wanasubiri hukumu yao badala ya kuendelea kutekeleza hukumu ya awali? Hivi kukata rufaa kunasababisha automatic stay ya hukumu ya awali?

Nilivosoma heading kwa haraka nilidhani ni wewe mkuu kumbe we kijiji chako kiko mjini teh teh
 
1. Wanavijiji wa Tanzania tunawa-underestimate sana, mimi nilivyosoma kichwa cha thread nikafikiri huyu ni "Mwanakijiji" wetu hapa JF, kumbe kuna watu wana rep huko.

2. Jibu la Pinda ni unafiki mtupu. Kama Mahakama ndicho chombo cha ku-interpret sheria, kwa nini serikali kuu ina hijack hiyo role?

Bottom line, tunahitaji mabadiliko ya katiba na kufanya overhaul.

Kuna watu hawafanyi kazi zao vyema wakishindwa kwenye uchaguzi, wanakimbilia kusema vijijini watu hawajaamka! ona sasa !
 
Watabana weeee mwishowe wataachiz. Ngoja nijiandae kugombea mie
 
that is the story behind the name.. tumedharauliwa kiasi cha kutosha; tumepuuzwa kiasi cha kutosha; na tumenyanyaswa kiasi cha kutosha. Ni unyonge wetu uliotufanya tudharauliwe, tupuuzwe na tunyanyaswe! sasa tunataka haki yetu! Haki yetu ya kuweza kuwahoji watawala wetu na kuwapinga, haki yetu ya kukataa majibu ya uongo na haki yetu kutoa mapendekezo ya kile kinachopaswa kufanyika.

Hongera mwanakijiji mwenzangu.. inanikumbusha yule mtoto wa mwanakijiji mwingine aliyewahi kumuuliza swali Waziri Mkuu mwingine!!
 
that is the story behind the name.. tumedharauliwa kiasi cha kutosha; tumepuuzwa kiasi cha kutosha; na tumenyanyaswa kiasi cha kutosha. Ni unyonge wetu uliotufanya tudharauliwe, tupuuzwe na tunyanyaswe! sasa tunataka haki yetu! Haki yetu ya kuweza kuwahoji watawala wetu na kuwapinga, haki yetu ya kukataa majibu ya uongo na haki yetu kutoa mapendekezo ya kile kinachopaswa kufanyika.

Mbona unapunguza makali ya hiyo nukuu uliyoimwakikagile kutoka kwenye Azimio la Arusha? Sasa "tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na wala tusipuuzwe tena." Hiki ndicho tunachotaka sio hizo nyimbo za Nothing Going On (NGOs) za 'Haki' bila utayari wa kuleta mapinduzi ya Haki! Haki haitolewi kwenye sinia la fedha kwa vigelegele!
 
nadhani kusema right to liberty, life and pursuit of happiness huitaji kutaja source.. AR is a document that Tanzanians should freely quote from it with pride! It is theirs!
 
Kiu na hamu ya mabadiliko chanya inasambaa Tanzania kwa kasi, Tanzania ya leo sio ya mwaka 2005, uelewa wa watu wetu unazidi kuwa mkubwa, ipo elimu ya uraia inawafikia, hamu ya kutaka kushiriki siasa kuvitendo inawaingia.

Hamu yakutaka kuona Mustakabali wa taifa hili ukienda vyema unawaingia.

Tunatarajia mageuzi makubwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Unaweza kudhani miaka kumi toka sasa ni mingi, la hasha. Ipo Tanzania yenye NEEMA TELE mbele yetu.
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameshtushwa na swali lililomtaka kutoa maelezo ya kwa nini Serikali inahofu kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyobariki mgombea binafsi.

Swali hilo liliulizwa jana na mkazi wa kijiji cha Ibushi, Joseph Mazwazwa, mara baada ya Pinda kukagua bwawa linalotumika kwa shughuli mbalimbali za binadamu, wanyama na kilimo.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu ni kwa nini Serikali inahofia kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ingawa Mahakama Kuu ilishabariki kuwapo kwa mfumo huo katika uchaguzi?,” aliuliza.

Waziri Mkuu alimjibu kwa kusema, ni kweli Mahakama Kuu ilibariki mgombea binafsi baada ya kesi ya suala hilo kuwasilishwa mahakamani hapo.

Alisema hata hivyo suala hilo linaleta utatanishi kutokana na tafsiri ya kikatiba, kwa kuwa Katiba inasema mgombea katika nafasi za kisiasa, kama diwani, Mbunge na Rais, ni lazima atokane na chama cha siasa kilichosajiliwa.

Alisema, hatua hiyo ndiyo inayoleta utata kwa Serikali kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi.

“Ni sababu hizi hasa ndizo ambazo zimetufanya kupinga uamuzi huu wa Mahakama. Hata hivyo wenzetu bado wanataka mfumo huu uwepo na ndiyo maana wamekata rufaa katika chombo cha juu ambacho ni Mahakama ya Rufaa ili mfumo huu uruhusiwe.

“Hata hivyo kesi hii kwa ngazi ya Mahakama ya Rufaa bado haijatolewa uamuzi, kwa hiyo ni vigumu kueleza. Mahakama ya Rufaa ikibariki uamuzi huu basi hatutakuwa na la kufanya itabidi tukubaliane na matokeo katika suala hili,” alisema Waziri Mkuu.

Kesi ya kutaka Mahakama kukubaliana na kuwapo kwa mfumo wa mgombea binafsi, ilifunguliwa katika Mahakama Kuu na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na Mahakama hiyo iliamuru mfumo huo kuanza kutumika, lakini Serikali ilikataa kutekeleza amri hiyo ya Mahakama.

Hata hivyo katika siku za karibuni wanaharakati wamekuwa wakishinikiza Serikali ikubali mfumo huo kwani tayari kuna uamuzi wa Mahakama wa kuuruhusu, hata kama Mahakama ya Rufaa itakuwa bado haijatoa uamuzi kwa suala hilo.
 
Wanakijiji wana natural logic, ukienda kichwakichwa wanakureduce to absurdity. Likini serikali ya CCM inaogopa nini kuruhusu hili jambo hata baada ya sheria kuruhusu?
 
Hata mimi nilidhani ni Mzee MKJJ!

Walizoea wanasiasa waTZ kuwa wanakijiji wapo tu kuimba nyimbo za kuwapokea na kubaki kushangaa huku wakipigwa jua na kusikiliza hotuba zisizokua na mwisho!

Sasa hivi na uhuru na wingi wa vyombo vya habari angalau habari zinafika huko, na wanakijiji si kwamba ni wajinga, mara nyingi ni kutokua na taarifa.

Tuombe Mungu hii trend iendelee,labda ndio jambo litakalookoa nchi yetu
 
Hilo ni funzo kwa serikali ya JK . Kwamba hata uchaguzi ujao wananchi wengi wa kawaida kabisa watakuwa namaswali yafuatayo?
A. Ni vipi serikali ilipata kigugumizi kuwawajibisha watuhumiwa wa Richmond?
B.Una vigezo vipi ili kutushawishi ili tukupe kura?
c. serikali inasemaje kuhusu mwanasheria mkuu Jonson Mwanyika aliyestaafu kwa kumaliza muda wake wa utumishi wa umma wakati alitakiwa kuwajibishwa kutokana na zabuni tata ya Richmond? Sina uhakika kama wagombea kwa tiketi ya CCM wameandaa majibu hayo. Niwashauri kuwa hakutakuwa na maswali mengine tofauti ukiacha yale yalizoeleka na yenye majibu rahisi, kama sababu za ufinyu wa bajeti ila tutajitahidi bajeti hii. Hayo ni majibu ya tangu uhuru mpaka hadi 2005. Wanasahau kuwa sasa wanavijiji ni form six,form four,na wengi wakitokea shule za kata, au malufu kama yeboyebo. Wengi waliokuwa wanasomea chini ya miembe yaani wateja wa CCM wameisha kuwa wazee sana au wamekwisha kufa na au hawawezi kupiga kura tena. Wapiga kura wa leo chumvi wakipewa wanapokea kura chadema. nawashauli warudishe mkanda nyuma wakumbuke uchaguzi mdogo wa busanda Geita, Bihalamuro mjini. Majibu anayo Mzee makamba. JK timiza wajibu wako uinusulu CCM. Usanii ulishapitwa na wakati kwa vile watanzania wengi nao walishajifunza usanii. Jifunze kutoka hata nchi jirani .Maisha tunayoyapitia wote walisha yapitia. hakuna aliyesalia nisisi pekee tunasubiliwa .Suruhu ni kuwabananisha Mafisadi. Halafu kura huhitaji kurudia kama ulivyokuwa unajieleza kistadi mwaka 2005. Yale hatuhitaji kuyasikia tena kwa vile majibu yake tunayo. Oh ,niongeze miaka hii iliyo baki nisawazishe. Make nawe ni mahili kinywani tena huende ukampigia debe jamaa yako Uliyeshindwa kumshughulikia .
 
Back
Top Bottom