Mwanajeshi Mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mwanajeshi Mbaroni kwa tuhuma za mauaji


JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wawili akiwemo mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)
kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya Mwamuzi Masawe ambaye awali aliripotiwa kuuawa na
wananchi wenye hasira kali.
Awali taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi ilieleza kuwa kijana huyo aliuawa na wananchi wenye hasira kali wakati akiwa kwenye jaribio la
wizi katika duka la Bw. Raymond Miraku (60) katika kijiji cha Kitandu
wilayani humo.
Akielezea tukio hilo kwa kupewa maelekezo na Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Yusuph Ilembo Mkuu wa Upelelezi
mkoani humu (RCO) Obadia Jornas alisema baada ya kutoa taarifa
ya awali kwa vyombo vya habari walitaarifiwa kuwa kijana huyo
hakuuawa na wananchi wenye hasira kali hali ambayo iliwalazimu
kufika tena eneo la tukio na kufanya upelelezi ambapo waliwashikilia
watu hao kwa ajili ya upelelezi zaidi wa tukio hilo.
Aliwataja watu hao wanaoshikiliwa kuwa ni Bw. Patrick Michael
(56) ambaye ni mwanajeshi mstaafu na ndiye Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kirima Juu Kibosho wilayani Moshi pamoja na Bw. Raymond Miraku
mfanyabiashara ambaye ndiye ilidaiwa kuwa duka lake lilivunjwa.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa kijana huyo aliuawa
nyumbani kwake katika kijiji cha Kirima Juu na Mwenyekiti wa kijiji
ambaye anashikiliwa na Polisi na baadaye kupelekwa katika duka la
Bw. Raymond huku akiwa hajitambui.
Akitoa maelezo ya tukio hilo mke wa marehemu Bi. Joyce Priscus
alisema kuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho alifika nyumbani kwake
akiwa na vijana watatu siku ya tukio saa mbili usiku ambapo alisukuma
mlango na kumkuta mwanamke huyo akimnyonyesha mtoto na
kumuulizia mme wake ambapo alijibu kuwa amelala.
Bi. Priscus ambaye ni mzazi wa mtoto wa siku 12 alisema baada ya
kutoa majibu hayo kwa mwenyekiti huyo alimfuata mumewe alipokuwa
amelala na kumkamata mguu ambapo alianza kumshambulia kwa
mapanga bila kutoa maelezo yoyote kwa mkewe.
“Baada ya kuona hivyo mimi nilianza kulia na kuuliza kwanini
unamkatakata mume wangu kwa mapanga nilisukumwa chini na
baadaye kutolewa nje na vijana aliokuwa nao huku mwenyekiti
akiendelea kumshambulia mume wangu”alieleza
Januari 12 jeshi la polisi lilitoa taarifa kuwa mnamo Januari 11 saa
mbili usiku katika kijiji cha Kitandu Kibosho wananchi wenye hasira
walimuua jambazi sugu aliyejulikana kwa jina la Mwamuzi Sipendi (24)
baada ya kukutwa akiiba katika duka la Bw. Raymond Miraku.

 
Hawa wastaafu tunaweenzi vipi............au tunawatelekeza tu.........na mwishowe inabidi wajifunze ufisadi kama njia ya kumudu ugumu wa maisha..................................
 
Hawa wastaafu tunaweenzi vipi............au tunawatelekeza tu.........na mwishowe inabidi wajifunze ufisadi kama njia ya kumudu ugumu wa maisha..................................

Maisha magumu si tiketi ya uhalifu. Zaidi ya 90% ya watanzania ni wana maisha magumu kuliko huyo mwanajeshi ambaye naamini anapata pensheni yake japo kidogo kila baada ya muda fulani. Kama ni suala la maisha magumu nadhani ihiyo 90% ya watanzania wote wangekuwa wahalifu. Ni tamaa tu ndo imempeleka huko katika kufanya uhalifu
 
Back
Top Bottom