MwanaHalisi, Tz.Daima, Dira,Raia Mwema, Mwananchi yafungwa mdomo kuhusu Manji

Huyo jamaa aombe tu na kutambika kwa bibi zake Zimwi la Magamba liendelee kutushikilia Watanzania make tukifunguka yumo katika orodha ya manyonyaji tutakayoyashugulikia halaka iwezeklanavyo.
<br />
<br />
Nakubaliana na wewe, lakini tatizo hili suala si tena la kisiasa na tukiweka siasa inakua malumbano kati ya Chadema na CCM, na hapo tutapoteza muelekeo na wana CCM humu watashindwa kuchangia. Ni vyema tuwe waangalifu na michango yetu iwe na nia ya kusaidia wahalifu wachukuliwe hatua na kama alivyosema Tina tusicheze ngoma ya mafisadi kwamba wamepeleka fedha CCM ili wapate kinga. Kama walichangia CCM kama wengi mulivyochangia ni kwa utashi wao na chama chao lakini si wizi. Kuna vibaka wengi wako jela kwa kuiba simu, fedha katika SACOS lakini wana kadi za CCM na wamewahi kuchangia vijisenti vyao (si vya Chenge) na hivyo hawawezi kutolewa jela kwa sababu eti waliwahi kuchangia CCM na kumsaidia Mwenyekiti wa Mtaa ama Diwani wao kushinda. Wako jela na hawana kinga, kwann sasa kinga iwe kwa wengine? Kwanini kina Rajabu Maranda na Farijala wamehukumiwa? Kwanini kina Johnson Lukaza wana kesi? Kwanini Jeetu Patel ana kesi? Hawa nao tunajua wamechangia CCM sana, tusibweteke Watanzania wenzangu, tupambane haki itendeke na serikali ijue huu ukimya wake ni bomu la saa (time bomb) ambalo likilipuka kuzima kwake ni gharama kubwa sana. Watu wanaona na kujua kwamba sheria zinawabagua!!!
 
Hakuna cha ugomvi binafsi, maana naona hapa hata wenye magazeti husika wanachekelea:

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977

Uhuru wa
Maoni Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.
 
Back
Top Bottom