MwanaHalisi, Tz.Daima, Dira,Raia Mwema, Mwananchi yafungwa mdomo kuhusu Manji

Mimi naamini yote ni ushahidi tu kuwa tuna one of the most incompetent, irresponsible and incapable DPP in Eliezer Feleshi. Kama huyu jamaa angeamua japo kwa siku moja kufanya kazi yake kweli kweli hawa kina Manji wasingefanya wanayofanya. Ni kana kwamba nchi haina law enforcement agents.
 
Mimi naamini yote ni ushahidi tu kuwa tuna one of the most incompetent, irresponsible and incapable DPP in Eliezer Feleshi. Kama huyu jamaa angeamua japo kwa siku moja kufanya kazi yake kweli kweli hawa kina Manji wasingefanya wanayofanya. Ni kana kwamba nchi haina law enforcement agents.

Kwa mwendo huu tusije shangaa siku jamabazi likaenda mahakamani kuomba mahakama itoe zuio la polisi, mashshushu, mgambo or any law enforcement agents kuwa katika radius ya mita 500 kutoka nyumbani kwake.
 
Baada ya kufanikiwa kupata uamuzi wa mahakama ya Temeke kuzuia Mwanahalisi lisimuandike na kubenea kukabidhi nyaraka zote kumhusu, Manji sasa amepata uamuzi wa mahakama ya kinondoni kuzuia raia mwema lisimuandike na kuzuia raia mwema na marafiki zake kutoandika wala kutoweka ktk mitandao habari zozote kuhusu Kagoda na Manji. Pia imefahamika kwamba ameshafanikiwa toka Julai 2001 kupata hukumu Mahakama ya kinondoni kuzuia magazeti yanayotolewa na Mwananchi Communication ya Mwananchi na Citizen kumuandika kuhusu jambo lolote bila kibali chake.

Pia kesho anataka mahakama ya kinondoni izuie Tanzania Daima lisimuandike. Tayari Manji amekwama kumzuia Mengi, Msemakweli na wengine kumuandika ama kumsema. Manji amefungua kesi mbili tofauti zinazofanana mahakama kuu na zote anataka kuzuia uhuru wa habari kwa kutaka mitandao yote izuiwe kumuandika na itoe habari zake zote haraka iwezekanavyo na wote wenye uhusiano na aliowashitaki kisiasa, kijamii na kibiashara kuzuiwa nao kumsema kwa njia yoyote. Hii ni historia mpya katika uhuru wa habari japo wapo wanaoshangilia na kuneemeka kwa UJINGA huu

Katk kesi zOte hizo, manji anawakilishwa na mawakali Nasir Rantansi anbaye ndiye aliyesimamia mkataba kati ya Manji na Kagoda na Law Associates ambao wamo ktk kampuni pacha na Kagoda ya Afritainer (docs ziko JF). Tumerogwa!!!
 
Hii issue ni hot, kwa hiyo ni lazima watumie kila mbinu inyowezekana ili kuituliza. Ngoja tusikilizie.
 
Mimi naamini yote ni ushahidi tu kuwa tuna one of the most incompetent, irresponsible and incapable DPP in Eliezer Feleshi. Kama huyu jamaa angeamua japo kwa siku moja kufanya kazi yake kweli kweli hawa kina Manji wasingefanya wanayofanya. Ni kana kwamba nchi haina law enforcement agents.

Huyu ni mtumishi wao, na kazi yake ni kuwalinda, ni kama Hosea na wengineo. Chakusikitisha sasa wanashika na mahakama baada ya kufaulu sehemu zingine zote.

Tuchukue hatua, tupiganie uhuru
 
Leo Tanzania Daima nao wamezuiwa rasmi na mahakama kumuandika Manji na gazeti la Dira nalo limeshitakiwa katika mahakama ya Kisarawe na kuzuiwa kumuandika pia huyo "bosi" wa wengi wa jamaa zetu!! Hii inatisha, MwanaHalisi (Kesi 4), Mwananchi na The Citizen, Tanzania Daima, Raia Mwema na sasa Dira, wote wamezuiwa.
 
Mdosi dume huyo, anajiamini sana. safari hii lazima wamlipe nyingi tu.
<br />
<br />
That's reflect something to our modern society. Biashara huria siku hizi, kuna ndama, madume na majike ya ng'ombe na madume na majike husaidiana kutengeneza ndama na maziwa yake.
 
Njia anayoifuata siyo mbaya, a-make sure tu kuwa huo ni uamuzi sahihi; na njia hiyo itakomfikisha asianze kurudi nyuma kwa maana atakosa pa kutokea! Hongera manji, funga midomo wote (JF utaiwezea wapi?)
 
Waache kupoteza muda wa mahakama. Kwa muda mrefu tumekuwa tunalalamika mlundikano wa kesi mahakamani, kumbe tunalundika uupuzi tu
 
nadhani imefika wakati wa jamii kuandamana ili kuishinikiza serikali kuwafuta uraia mafisadi wote....au kuwatafutia kisiwa na kuwaweka huko kama jera yao
 
Leo Tanzania Daima nao wamezuiwa rasmi na mahakama kumuandika Manji na gazeti la Dira nalo limeshitakiwa katika mahakama ya Kisarawe na kuzuiwa kumuandika pia huyo "bosi" wa wengi wa jamaa zetu!! Hii inatisha, MwanaHalisi (Kesi 4), Mwananchi na The Citizen, Tanzania Daima, Raia Mwema na sasa Dira, wote wamezuiwa.

Kwa hali kama hii ni wazi kwamba sasa mahakama nazo zimeanza kuingizwa mfukoni mwa mafisadi taratiiiibu.

Bado mahakama kuu na mahakama ya rufaa kama wakiingia mfukoni kwa manji basi nchi yote kwa ujumla wake itakuwa mateka. Bunge lilishaingizwa mfukoni siku nyingi likitanguliwa na serikali na sasa mahakama.
 
Sheria zingine hazina maana, inawezekanaje kuwakataza watanzania wasikujadili kwa uovu ama mazuri uliofanya? Mahakama itupilie mbali mashtaka ya kishenzi ya aina hii. Watu wanahaki ya kujadili lolote, iwe kwenye magazeti, radio, television, mitandaoni, mikutanoni nk. Uhuru huo Mungu alimpa kila binadamu. Gaddafi aliwazuia watu kuzungumza mwishowe wamemkimbiza. Huyu Manchi ni nani katika nchi hii? -fokolofu member wa kagoda!
 
Afanyayo Manji niliyatabiri majuzi Mwita25 akaniaona kichaa kumbe mimi ni zaidi ya akili zake .Leo kafanya yale yale .
 
Ina maana nikitaja jina la manji tu na mimi naunganishwa kwenye kesi??? Duu kweli ukiwa na hela bongo unaishi kama uko peponi.
 
Manji sasa ana mpango wa kutumia mahakama na polisi kuwakamata na kuhakikisha waandishi kadhaa wanafungwa na kwa kuanzia ameshatengeneza mashitaka ya jinai (criminal charge) dhidi ya Kubenea ambaye anaweza kwenda jela Jumatatu kwa maombi ya Manji. Charge sheet imeshaandaliwa ikidai kwamba Kubenea amesema uongo na shahidi mkuu wa kesi hiyo ni Dk. Gideon Mohamed Safari Shoo, ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya G&S na pia Printech ambapo Kubenea anachapa magazeti. G&S ilianzishwa na Shoo na Salva Rweyemamu wa Ikulu na itakumbukwa ilipewa kazi ya kupigia debe mitambo ya Richmond. Kubenea amegoma kwenda Tanga kwenye kikao cha wahariri na NSSF ambacho Dk Shoo chini ya G&S ndio waandaaji. Shoo anatajwa sasa kufanya kazi bega kwa bega na Manji. Huu ni mwanzo wa mwisho, kila ndege ataonekana rangi yake halisi, na wale waliopotea watarudi kundini na waliovamia kundi la ndege waadilifu watajipembua pole pole na tutajua mbivu na mbichi
 
Yafungwa mdomo?!
<br />
<br />
"Kufungwa mdomo" haina maana ya "mdomo", ni sawa na kusema Slaa "awasha moto" Jangwani, haina maana ameunguza ama amechoma moto Jangwani. Kila neno linasomeka kwa maana yake ya ujumla hasa katika matumizi ya vichwa vya habari kuwasilisha maana ya habari nzima. Kama nia ni ufafanuzi inatosheleza ila kama nia ni kubeza nadhani hutaelewa.
 
Back
Top Bottom