MwanaHalisi: Serikali hali ngumu - yaagiza kusitisha ajira na kutopandisha vyeo kuelekea 2012

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wadau;


Serikali yetu inayoongozwa na magamba sasa imedhihirika rasmi kwamba imefilisika. Mwanahalisi leo imeandika kwamba serikali iko hoi kifedha na imetoa nakala ya barua kutoka menejiment ya utumishi wa Umma ambayo ni taasisi chini ya Ofisi ya rais kwenda kwa makatibu Wakuu wote ikiwaagiza kwamba kutokana na ufinyu wa mapato ya serikali, ajira mpya zipunguzwe kwa asilimia 50. Upandishwaji vyeo nao upunguzwe kwa asilimia hiyo hiyo.

CCM KAZI KWISHA!!! WAMESHINDWA KABISA KUSIMAMIA NCHI!
 
Na bado! Ndo maana wanakazania Kafulila asamehwe bcoz hawana hela za by-elections?
Na jee iwapo serikali ya magamba itakazania kuona akina Lema na wabunge wengine wa CDM wenye kesi za uchaguzi wakishindwa kesi hizo?
 
Ni kweli Taasisis zote za serikali, Wizara na Halmashauri zimeshaagizwa kupunguza bajeti ya Mishahara by January 2012 wapeleke bajeti mpya isiyojumuisha ajira mpya na kupanda vyeo.
 
weka habari ndugu, wengine tuko jimboni kwa Tundu Lissu, magazeti huku 'mbado'.
 
Serikali kufirisika sipendi kabisa kuamini kauli hiyo: Ni namna tu kwa walioko juu waweze kuchukua chao mapema kwani 2015 imekaribika: iweje serikali ifirisike wakati wataalamu wa kupiga usingizi MJENGONI wanajiongezea posho!!!!!!!, Raisi ajaye anakazi kubwa ya kuziba mapengo kwani atakuta Hazina haina kitu kabisa.
 
Sisi tunapiga kazi kwa wazungu mpaka saa hizi tumeisha tia kibindoni maelfu ya shilingi. sijui tutafika mwaka mpya na pesa?
 
Mficha mauti, ugonjwa humuumbua!

Zitto alisema siku nyingi tu kuwa hamna kitu mule, kipara akabisha. Sasa mambo hadharani, tukae mkao wa kukimbia. Ukimbizi wa kiuchumi utakuwa mpya kwa watakaotupokea. Mi nilifikiri wangekata bajeti ya Land Cruiser V8, badala yake wanakata ajira mpya, mweh!

Waongeze bajeti ya FFU manake mwakani tutaandamana mfano wake hakuna
 
nchi zote zinazoendelea bajeti yake kama 3/4 yote ina enda kwenye matumizi ya utawala..
 
na kwa wale wenye kawaida ya kusherehekea sikukuu, nwapeni pole kwani mishahara hakuna na mwezi utapita hivhivi
 
Masikini JK. Kama ni kweli angalia cha kufanya.

AM sure rais ajaye atakua makini hali hii (kama ni kweli) isitokee.
 
Alichokikimbilia mule jumba jeupe ndio atakijua sasa!!!!historia haitamsahau huyu mjomba!!aibu kubwa sana anaturudisha enzi zile za ankal yake nae nchi ilienda mrama kama sasa!!
 
Nasubiri FF atuletee zile figure zake za uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi chini ya uongozi wa JK!!
 
Serikali ipunguze matumizi kwa kufuta wizara ambazo hazina maana wala tija kwa taifa.
1. Wassira na Wizara yake ya uhusiano (haina tija kabisa)
2. Utawala bora (tayari tuna wizara ya katiba na sheria)
3. Uwezekezaji (tunayo wizara ya viwanda na biashara)
4. Wizara inayosimamia ajira - ifutwe kabisa hakuna kitu pale. Ajira gani wakati vijana wanauza viberiti ubungo mataa tena kwa kufukuzana na city?
 
Back
Top Bottom