Mwanahalisi linakufa kifo cha kawaida Makamanda mpo wapi kulisaidia

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF.
Kila siku zinavyokwenda hali ni mbaya kwa gazeti letu pendwa la Mwanahalisi. Kutokana na udhaifu wa kiutendaji wa gazeti hilo sasa hivi limekuwa gazeti pekee linalobakia kwenye vibanda vya kuuzia magazeti.

Imefikia wakati gazeti la Mwanahalisi linauzwa kwa kilo maeneo ya kariakoo baada ya kukosa soko.

Makamanda jaribuni kulinunua kwa wingi kila Jumatano kuliokoa gazeti letu pendwa kulipa fadhila zaidi yapo tutalipoteza gazeti letu pendwa.
 
si kweli..magazeti yanayo uzwa kwa kilo ni yale yaliokwisha muda wake..sasa mtu anunue nagazeti yaleo leo kwakilo anaenda kugawa barabarani kama mwendawazim ama?? umetia chumvi sana

si kweli..magazeti yanayo uzwa kwa kilo ni yale yaliokwisha muda wake..sasa mtu anunue nagazeti yaleo leo kwakilo anaenda kugawa barabarani kama mwendawazim ama?? umetia chumvi sana

Kaka sijakuambia hivyo kama unavyosema nina maanisha kuwa baada ya kukosa wateja linapitwa na wkt linauzwa kwa kilo kwa bei rahisi tofauti na kipindi cha nyuma siku ya Jumatano ikifika saa 5 asubuhi huwezi kulipata gazeti pendwa la Mwanahalisi.
 
si kweli huku songea mda mwingine yanakua machache mbaka 2nauziwa sh.1000
 
Niliacha kusoma Mwanahalisi kitambo! Nilipogundua halina uzalendo bali ni propaganda tool ya NORTHERN ALLIANCE!
 
Siyo kweli kabisa, bado linaongoza likifuatiwa na Raia Mwema, Dira, Jamhuri na Rai
 
Toleo la jana la Mwanahalisi ni zuri tu, lina nakala kibao na limewakumbuka hadi jamaa zetu wa mabwepande...

Sema tu linakosa kabisa matangazo ya biashara, ambayo ndio moja ya vipato vikubwa vya magazeti. Kama nchi hii ingekuwa fair lingekuwa linaongoza kwa matangazo, we utashangaa hata Uhuru na Mzalendo kuna matangazo lakini Mwanahalisi hakuna wakati magazeti ya chama wanasoma akina Nape peke yao
 
Hili gazeti mwanzoni wakati watu hawajalijua vizuri walilishabikia sana baada muda watu wameligundua ni gazeti linaloeneza propaganda za kisiasa kuchafua weatu fulani na kutukuza watu fulani baada hapo limepoteza umaarufu kwa sababu hoja zake si za busara ni za kejeli na matusi hakuna uzalendo ata kidogo katika kuwakilisha hoja zake kwa sasa halina hoja za msingi limebaki kudandaia dandia hoja zisizo na mashiko na kuzipa kipaumbele,muda si mrefu linakufa kibudu!
 
Back
Top Bottom