Mwanahalisi leo latoboa ile ya ndani kabisa ya EPA!

Hivi Salome Mbatia alikufa kifo cha kawaida au?...na yule dereva aliyesababisha ajaali ile alishaonekana?
 
Kazi ipo, but km aliyajua yoote haya why now????????? Mungu tusaidie watanzania tufunguke na kuujua ukweli!!!na wote tuseme AMINA
 
Hivi Salome Mbatia alikufa kifo cha kawaida au?...na yule dereva aliyesababisha ajaali ile alishaonekana?

Wafiwa machungu yalishaisha sasa wewe unataka kuwakumbushia? Wewe unaamini kuna Mungu? Kwani hujui nani mwenye uwezo wa kutoa pumzi ya uhai?
 
thats exactly my point.. ndio maana sikuhizi kwa kweli sihangaiki kufichua ufisadi zaidi kwa sababu tumeshapigwa ganzi.. sasa hivi ni kujipanga kuushughulikia tu.. Tangu Loliondo hadi leo bado tupo hapo hapo.. kashfa kashfa kashfa..

Mkuu,mbona Malaria ipo tangu zamani hizooo lakini vita dhidi ya ugonjwa huo,including elimu kwa umma,inaendelea?Na ukimwi nao ni hivyo hivyo.Kuufichua ufisadi pia ni sehemu ya kuushughulikia.Wengi wetu tunaafikiana nawe kuwa kwa hakika inaweza kukatisha tamaa lakini tusikate tamaa.

By the way, ufisadi uliowekwa hadharani hususan kwenye mainstream media unaweza kutumika kwenye mahakama (hapo zitakapokuwa huru)...
 
Nimeipata nyingine hii kutoka Mwanahalisi la leo Ukurasa wa 11 -- makala iliyoandikwa na Saed Kubenea inayozungumzia matamshi ya Kinana. Hii inazidi ku-prove alichokisema Marandi Jumamosi ni kweli kabisa na kwamba safari hii CCM wameminywa sehemu mbaya sana. Paragraphs husika:



………."hata ndani ya Kamati ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi iliyoundwa na chama chake kutafuta suluhu ya migogoro ndani ya Bunge na katika Chama, suala la CCM kujinufaisha na fedha za EPA liliibuka.

Mjadala ulipopamba moto, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (utawala Bora), Sophia Simba alijitokeza na kukaripia wanaotuhumu. Akiongea kwa sauti iliyojaa mipasho, waziri Simba alimtuhumu Anne Kilango Malecela kuwa ni miongoni walionufaika na fedha za EPA.

Alisema Kilango alinufaika na fedha hizo kupitia kwa mfanyabiashara Jeetu Patel aliyekuwa anafadhili kampeni za mume wake, John Samuel Malecela. Kauli ya Simba ilitokana na hoja kadhaa zilizokuwa zinajengwa na baadhi ya Wabunge akiwamo Kilango, kwamba serikali imeshindwa kushughulikia ufisadi wa EPA kwa sababu baadhi ya fedha zilizoibwa zilinufaisha chama hicho.

Wabunge hao waliokuwa wamepachikwa jina la "Makamanda wa Ufisadi" walilenga mabilioni ya fedha yaliyokwapuliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited. Kampuni ya Kagoda ilichota zaidi ya Sh 40 bilioni kupitia BoT.

(Sophia Simba) alisema. "Mimi ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri. Hata Takukukuru iko chini yangu. Idara ya usalama wa taifa iko pale kwangu. Mlango wangu uko karibu na lango la rais. Nafahamu kilichotendeka."

Aliongeza, "Nafahamu kwamba baadhi ya fedha za EPA ambazo leo Kilango anatuhumu zimetunufaisha baadhi yetu, zilinufaisha hata kampeni ya mumewe."

Hakuna hata mahali popote ambapo CCM ilikana madai ya Simba.

Pamoja na kwamba Kinana alikuwa mjumbe katika kamati ya Mwinyi, na kwamba yeye na katibu mkuu wake, Yusuph Makamba walihudhuria mkutano uliomtuhumu Kilango, lakini hawakujitokeza kukana kauli ya Simba.

Hii ni kwa sababu, Kinana alijua kuwa yeye na Simba katika kujua siri za sereikali, wako tofauti. Mwenzake ni waziri anayehitajika kila wakati katika kazi za kuendesha serikali, yeye (Kinana) huwa anatafutwa wakati wa kampeni tu.

Aidha, Kinana anajua kuwa tofauti na waziri Simba anayehudhuria vikao vya baraza la mawaziri, anayeshiriki mipango ya uendeshaji wa serikali, yeye (Kinana) hulazimika kusubiri ripoti ifikishwe kwenye vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC). Isipotolewa basi!

Pili, tofauti na Sophia Simba, Kinana hana ubavu wa kusoma mafaili ya watuhumiwa wa ufisadi wanaochunguzwa na Takukuru. Hivyo basi, hawezi kujua nani ameiba nini, wapi na kwa kushirikiana na nani?

Hawezi kujua kwa ufasaha kwamba Jeetu Patel alisema nini katika kiapo chake mbele ya Kamati ya Rais ambayo mtendaji mkuu wa Takukuru, Edward Hoseah alikuwa mjumbe.

Hafahamu kwa undani kwa nini Jeetu amegoma kurejesha fedha zilizokwapuliwa na nini ameegemea………………………..












 
Mwanakijiji tuhuma za ufisadi zimekuwa nyingi sana. Kwasasa watu wanataka concrete evidences ambazo hata ukienda kufungua kesi unakuwa na uhakika wa kushinda.
Sasa ushahidi wa aina hii raia wa kawaida hawaujui, ingawa wanafahamu kuwa fedha zimeibwa.

Unapokuja na story kama hii ya Mwanahalisi, unakuwa umewapata wananchi new insight kuhusu kilichotokea. Kwa jinsi hiyo unafanya wananchi wakuamini zaidi, kitu ambacho kitaongeza kura za wapinzani kwa kiasi kikubwa.

No wonder CCM hawana amani. Coz watu wana-relate maisha magumu na wizi, jibu wanalopata ni kura kwa upinzani.

Tutaona na kusikia mengi zaidi ya haya.
 
Nilisha sema CCM hawatumii akili yao tu!

Kitakacho amua matokeao ya Kinyaganyoro cha urais kwa musimu huu ni EPA

Watachezaje huo mchezo ...we wait and see!!
 
Hivi mkijua zaidi inawasaidia nini zaidi? ni kitu gai mkisikia kitawashtusha?
Mzee MKJJ kujua zaidi inatusaidia sana. Inakuwa kama kujaza upepo wa tairi la baiskeli kwa pump ya mkono, inabidi ufanye strokes nyingi kwa kurudia rudia hadi tairi litakapojaa. Hizi habari ni kama strokes za pump hiyo na karibu tairi linajaa na safari itaanza.
Mimi ninaomba mendelee kutujuza zaidi na mwisho tutajaza upepo na kuamka, na huenda upepo umekwisha jaa na safari itaanza tarehe 31 Oct ..
Sungura
 
ni kweli watu wanalalamika njombe kaskazini

yule mgombea wa ccm hana elimu na inasemekana ni jambazi mkubwa

ila amejificha chini ya mwavuli wa ccm
 
Kazi ya Timu Nzima ya MwanaHALISI ni ya kutukuka na MUNGU azidi kuwatia moyo na kuwalinda kwa Faida ya Nchi Yetu na Watu wake.
 
thats exactly my point.. ndio maana sikuhizi kwa kweli sihangaiki kufichua ufisadi zaidi kwa sababu tumeshapigwa ganzi.. sasa hivi ni kujipanga kuushughulikia tu.. Tangu Loliondo hadi leo bado tupo hapo hapo.. kashfa kashfa kashfa..

People need facts. Mimi sijawahi kusikia mahali prosecutor anasema hatutaki ushahidi mwingine. Yuo bring all your facts and nail the accused. that is the nature of the game. Sasa wewe unapobania facts na kudai zipo za kutosha...sijui una maana gani! Nadhani hiyo ni a very sad philosophy!
 
thats exactly my point.. ndio maana sikuhizi kwa kweli sihangaiki kufichua ufisadi zaidi kwa sababu tumeshapigwa ganzi.. sasa hivi ni kujipanga kuushughulikia tu.. Tangu Loliondo hadi leo bado tupo hapo hapo.. kashfa kashfa kashfa..

What is the Plan ya kushugulikia Mwanakijiji?

  • Riot ?
  • Kuandamana ?
  • Kugoma ?
  • Kuwa na massive grassroot movement?
In fact kitu ambacho CHADEMA wanafanya sasa cha "Movement For Change" M4C ni sawa na ile kitu iliyomuweka Obama madarakani www.moveon.org. Sijui kama CHADEMA wanajua.

The only problem CHADEMA wameanza very late na si wengi wanajua M4C. Pia ilitakiwa NGO ndiyo ziisimamie.
 
Wana-JF,

Gazeti la Mwanahalisi la leo ni moto wa kuotea mbali. Ndani ya stori yao kuu ya leo kuna habari kuhusu yale aliyoyatamka Marando katika Viwanja vya Jangwani siku ya Jumamosi hadi TBC wakamkata. Leo gazeti hilo limeweka bayana kwamba Marando alikuwa anauhakika asilimia 100 kilw alichokisema -- jinsi CCM ilivyofanya hujuma kubwa ya kihistoria kwa Watanzania pale viongozi wake wakuu walipokula njama kuibia BoT mabilioni kupitia akaunti ya EPA.

Mwanahalisi limeweka bayana, tena kwa undani kabisha na kwa ushahidi usiopingika kwamba aliyosenma Marando hayakuwa matusi au kejeli yoyote, bali ni ukweli kabisa kwamba CVCM ilituma watu kuchota mahela hayo kwa ajili ya kufanyia kampeni zilizoimwingiza JK mwaka 2005.

Wana-JF ntajaribu kupata soft copy na kuiweka hapa muda si mrefu, ikishindikana nitajaribu kui-key story na hasa zile ibara husika. It's damaging to CCM. It really is!!!!!!

ubarikiwe na ufanikiwe kwa hilo...!!
 
mada zako unazoletaga hapa we unazani huwa zinatusaidia nini?
This is very good answer to the gentleman yeye anadharau makala za wenzake anafikiri za kwake huwa zinatusaidia sana wakati tunajua nyimbo ni zile zile tofauti ni choirmaster tu, haa haa haaaa big up Edson.
 
Back
Top Bottom