MwanaHALISI lambana Rostam kortini

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
GAzeti la MwanaHALISI limefungua kesi ya madai namba 83 ya mwaka 2009 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakiitaka mahakama imwamuru Rostam Aziz kuomba radhi na kufuta kauli yake kwamba gazeti hilo, linatumiwa na wapinzani wake kumchafua.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam, RA alidai kuwa gazeti la MwanaHALISI ni miongoni mwa magazeti yanayofadhiliwa na Mengi ili kumchafua yeye na swahiba wake mkuu Edward Lowassa.

Katika hati ya kiapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers inayochapisha gazeti hilo, Saed Kubenea, amekanusha madai hayo akisema gazeti lake limekuwa na msimamo wa kuandika ukweli, hata kabla ya RA na Mengi kuingia katika mgogoro.

Ametoa mfano wa makala mbalimbali na habari mbalimbali ikiwemo hatua ya Karamagi kusaini mkataba wa Buzwagi wakiwa na Lowassa na Rostam nchini Uingereza.

Kwa msingi huo anasema kauli ya RA imedhalilisha gazeti lao na limeivunjia hadhi mbele ya jamii na hivyo wanaiomba mahakama imwamrishe RA kufuta kauli yake na kuomba radhi pamoja na kulipa fidia ya Sh bilioni tano.

Kesi imeanza kutajwa jana na inaanza kusikilizwa Agosti 28, mwaka huu kwa Jaji Shangwa.

MwanaHALISI linatetewa na wakili mashuhuri Mabere Marando na Rostam anatetewa na Fungamtama.

Ikumbuke kwamba MwanaHALISI tayari imemzuia RA kutekeleza hukumu aliyoipata kwa njia ya panya katika kesi yake dhidi ya gazeti hilo na kwamba kesi ya RA inaendelea kusiklizwa na mahakama ya Rufaa baada ya MwanaHALISI kusikiliza rufaa yake ikipiga kesi hiyo kusilikizwa upande mmoja.
 
HAya sasa kumekucha, MwanaHALISI wameibuka. Rostam hapendi kupingwa pingwa sasa hili sijui itakuaje!!!??? Kwa Mtaji huo sijui kama Kubenea atapona kweli? aangalie yasije kutokea ya tindikali tena!!!!!
 
Nguvu ya umma iko nyuma ya mwanahalisi so the Iranian guy he knows.Wao wapambane huko na si kuuana .
 
haya ngoja mahakama iamue.
hata hivyo mwanahalisi iwe makini kwamba kesi hii
inaweza endelea mpaka 2010 na ikatumika kuwabana kumwaga cheche zao 2010.
 
Mtu anisaidie, kwani mwanahalisi ingeamua kukaa kimya aingeathirika kivipi, maanda dawa ya hawa jamaa ni kuwapiga mawe ya mbali, hii ya sasa ina hatari zaidi kwa mwanahalisi!

Au changa la macho? maana RA na Jk lao moja, mwanahalisi nalo ni la .....

kazi kweli kweli
 
Nguvu ya umma iko nyuma ya mwanahalisi so the Iranian guy he knows.Wao wapambane huko na si kuuana .

Isipokuwa mafisadi na wapambe wao. Dira yangu yasema hawatashinda, na hivi sasa wameanza ku-retreat. Uongo hauwezi kushinda kamwe, Ukweli, kama vile jua na mwezi, utafichika kwa muda tu lakini hatimaye hujitokeza. Alisema hayo Confucius -- mwanasalfasa wa Kichina katika karne ya 6 kabla ya ujio wa Kristo!
 
Back
Top Bottom