MwanaHalisi laivua nguo Tume ya Uchaguzi

Hivi ni kweli NEC inabandika orodha ya majina katika vituo ikijua fika kwamba orodha hiyo ni fake? Jamani CDM, hebu changamkieni hili haraka sana. Naam, naamini kabisa usemi kwamba Siku za mwizi ni arobaini. Na hizo sasa ndiyo zimefika.

NEC - you just cant fool all the people all the time, hata kama ni Wadanganyika!
 
WENYE KADI MBILI KWENYE DAFTARI
mboje.jpg
pimbi.jpg
jisena.jpg
Hawa wako katika kituo kimoja na wameorodheshwa kuwa na kadi mbili. Inawezekana walipoteza kadi wakapewa zingine. Tume ilitakiwa ifute kadi zao za zamani katika daftari. Haikufanya hivyo kwa makusudi kabisa ili kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura ccm waweze kupenyeza kura feki bila kushtukiwa. Hii kazi ilifanywa 2010 na Usalama wa Taifa wakishirikiana na mafisi kutoka india waliokodishwa na Kikwete jr. Hii ni mbinu mojawapo waliotumia, zilikuwepo nyingi. Mfano wale walioripotiwa wamekufa nao walirudishwa kwenye daftari. Sasa hivi wamechanganyikiwa hawajui nani amekufa na nani yuko hai. Igunga watu wengi walifika kituoni na kuambiwa wameshafariki hivyo hawawezi kupiga kura. Tume inajitahidi kulisafissha lakini kazi ni kubwa na kuna mvurugano wa kufa mtu. Daftari halifai hata kidogo kutumiwa katika chaguzi kwani lina madudu mengi sana.
 
WENYE KADI MBILI KWENYE DAFTARI
View attachment 39027
View attachment 39028
View attachment 39029
Hawa wako katika kituo kimoja na wameorodheshwa kuwa na kadi mbili. Inawezekana walipoteza kadi wakapewa zingine. Tume ilitakiwa ifute kadi zao za zamani katika daftari. Haikufanya hivyo kwa makusudi kabisa ili kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura ccm waweze kupenyeza kura feki bila kushtukiwa. Hii kazi ilifanywa 2010 na Usalama wa Taifa wakishirikiana na mafisi kutoka india waliokodishwa na Kikwete jr. Hii ni mbinu mojawapo waliotumia, zilikuwepo nyingi. Mfano wale walioripotiwa wamekufa nao walirudishwa kwenye daftari. Sasa hivi wamechanganyikiwa hawajui nani amekufa na nani yuko hai. Igunga watu wengi walifika kituoni na kuambiwa wameshafariki hivyo hawawezi kupiga kura. Tume inajitahidi kulisafissha lakini kazi ni kubwa na kuna mvurugano wa kufa mtu. Daftari halifai hata kidogo kutumiwa katika chaguzi kwani lina madudu mengi sana.

Nakumbuka kama miaka 3 au 4 hivi iliyopita, CUF waligundua maelfu ya shahada za wapiga kura zilizokuwa zimechomwa moto na baadhi kuungua nusu nusu katika eneo la nyuma ya jengo la Govt Press, Nerere Road.

NEC walisema hizo shahada zilikuwa za watu waliokufa ambazo zilirudishwa NEC. Swali, walizirudisha vipi na hali wao wamekufa? Inatia shaka sana!

CUF walilipeleka suala hili Bungeni lakini baada ya kubanwa sana kuhusu maelezo ya kuridhisha kuhusu shahada hizo Pinda aliwajibu kwamba waende mahakamani.

Nadhani sasa hivi ni wakati muafaka wa kwenda mahakamani. Kitu kinachoweza kuwaokoa NEC ni kukiri kosa kuhusu Igunga na watamke kufuta matokeo ya uchaguzi ule. Vinginevyo ni uhuni tu wanaoufanya.

Nadhani sasa
 
Kwanini huo ushahidi usitumike mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi na watu waliozuliwa kifo na kukosa kupiga kura wapo?

Nadhani CDM wameanza kazi nzuri na wasikubali kukomea hapo wafungue kesi mahakamani kupinga hayo matokeo na wana Igunga na watanzania wachangie fedha za kesi kama kweli wapo serious na mabadiliko ya kuingowa CCM na udhalimu wake hapa Tanzania
 
Kwa ujumla daftari zima la wapigakura ni uozo mtupu, halifai na iwapo hilo hilo ndilo litakalotumika mwaka 2015, basi upinzani ni lazima waende mahakamani kulipinga. Halifai.

Hata CCM wenyewe ambao ndiyo walengwa katika kunufaika ni lazima wawe na wasiwasi kwamba linaweza kuwageukia hata wao wenyewe hasa kutokana na kubadilika kwa ufuasi wa vyama ambao CCM wenyewe wanauona. Na ndiyo maana NEC imekuwa ikijaza kwa wingi majina kwenye daftari ili kuweka 'watu' wanaoweza kuwatumia eti bila kujulikana!

Wamelichafua kiasi kwamba haliwezi kutakasika, hadi lipatikane daftari jipya.
 
kweli hapa inabidi ifanyike kazi nzito ya kuwaadabisha hawa jamaa wa tume ya Magamba.Wanauza haki za watu mchana kweupe
 
Nadhani cha kwanza ambacho CDM inatakiwa ikifanye ni kufanya press conference haraka sana kwa kuitaka NEC itoe tamko kuhusu hili, Waipe NEC Wiki mbili kuwaeleza umma iwapo ni kweli walichakachua daftari, na kama kweli waseme kwa nini walifanya hivyo. Vinginevyo mahakamani.

Imefika mahala NEC na CCM yao watambue kwamba baskeli si chombo cha usafiri, bali ni kuchosha tu miguu.
 
Kwa kitendo hiki cha NEC kuchakachua hadharani; TUNAOMBA CHADEMA WATOE TAMKO-Haiwezekani tukachezewa hivi kwa kodi zetu!
 
Kwa wenzetu waliondelea hasa huko nchi za Magharibi (baadhi) NEC nzima ingejiuzuu mara moja kutoana na kuibuliwa kwa kashfa hii.
 
aiwezekani idadi ya waliojiandikisha zaidi ya 171,000 na wapige kula 52,000 hapa kuna namna hinafanywa na wajanja.
 
Back
Top Bottom