Mwanahalisi kumtusi na kumkejeli Rais, je ni haki?

Yaani mods mnaona raisi anatukanwa wazi wazi halafu mnaacha hii sredi iendelee??
Hebu fanyeni kazi!!
 
MTUKUFU RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE SI KIGEUGEU NI MTU MWENYE MISIMAMO THABITI NI MKWERRE MWENYE KUSIMAMIA HAKI NA USAWA NI MPENDA AMANI NA ANAWAPENDA WANYONGE, AHADI ZAKE NI ZA KWELI ANAKUFA NJAA KWAAJILI YA KUTAFUTA CHAKULA CHA WATANZANIA ANGANI, kubenea ilitakiwa aaandike hivyo kwa raisi huyu jamani, ukiandika tofauti ya hapo umemtukana!
 
Kama unataka kutuambia kusema ukweli ndiyo maana ya matusi, basi kweli ametukanwa. Lakini kama kusema ukweli inamaanisha kuzungumza jambo la kweli linalojitokeza, basi sioni hoja yako kuwa na mantiki. Ukigeugeu wa Rais JK unaonekana kwenye sura nyingi za uongozi wake...hata suala la kupunguza na kuongeza bei ya mafuta ya taa ni ukigeugeu...mwanzoni ni baraza la mawaziri lililoridhia kupandishwa bei kwa mafuta ya taa...nani mwenyekiti wa baraza la mawaziri? JK! Kamati kuu inakaa na kusema bei ya mafuta ishushwe, mh.JK anasema sawa! Siyo ukigeugeu ni nini huo?
Juzi alisema barabara ya lami itapitishwa Serengeti watu wakapiga makofi, leo anaenda bondeni anasema yeye ni mwanamazingira nambari moja kwa hiyo hataweza kuruhusu barabara ipitie Serengeti..huo siyo ukigeugeu?

We regret having a multifaced President who will never be trusted by whatever he promises. He is a chameleon type and a liar!
Kwa kuunga hoja hivi sasa niko mbioni kutoa wimbo wa Kigeugeu
 
Hiyo itakuwa ni KEJELI
MTUKUFU RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE SI KIGEUGEU NI MTU MWENYE MISIMAMO THABITI NI MKWERRE MWENYE KUSIMAMIA HAKI NA USAWA NI MPENDA AMANI NA ANAWAPENDA WANYONGE, AHADI ZAKE NI ZA KWELI ANAKUFA NJAA KWAAJILI YA KUTAFUTA CHAKULA CHA WATANZANIA ANGANI, kubenea ilitakiwa aaandike hivyo kwa raisi huyu jamani, ukiandika tofauti ya hapo umemtukana!
<br />
<br />
 
" KIKWETE KIGEUGEU"

Mwandishi Saed Kubenea

Sheria ya nchi iko wazi kwa mtu yeyote kumtusi Rais Mtikila alifunguliwa mashitaka kwa kumtusi Rais
Kwa maneno haya Mwandishi Saed kubenea anapeleka taarifa kwa watanzania kuwa nchi ina Rais kigeugeu
Je nchi inaweza kuongozwa na Rais kigeugeu?

Huu ni uandishi wa namna gani? hili gazeti inabidi lichukuliwe hatua za kusheria na mwandishi huyu afikishwe mahakamani

Gezeti limepoteza muelekeo limeanza kuwa na mambo ya kidaku daku

Mtikila ni rais wa wapi(taasisi gani)?
 
Yaani mods mnaona raisi anatukanwa wazi wazi halafu mnaacha hii sredi iendelee??
Hebu fanyeni kazi!!
Kama Don King vile alivyojipendekeza kwenye msiba wa baba wa bondia wa wa upande wa mpinzani wake aliyekuwa anamtaka ajiunge na kambi yake
 
haya tutaandika kuwa Rais wetu ni kijana tena mwenye mvuto.....hapo ndio tumemsifia eeeh
 
Serikali hiii legelege ya kikwete ni matokeo ya kikwete mwenyewe kuwa kigeugeu.................
Nchi haina rais...ina mtalii
 
endeleeni kumshambulia huyu ndugu lakini naaamin kama tutakuwa hai tutakuja kukugundua JAMAA ALIKUWA RAIS.........sasa hivi tumekuwa na ushabiki tu na uhalisia umewekwa pembeni...
MINGU IBARIKI TANZANIA

Mungu aibariki Tanzania Mara ngapi?
 
Wewe ndo huelewi Kiswahili. Tusi liko wapi hapo?

KIGEUGEU ni mtu asiye na msimamo (Inconstant), mtu anayebadilikabadilika. Pia inaweza kutumika kumaanisha mwongo (deceitful). Kama unasema jambo fulani leo, na kesho ukalikana maana yake ni mwongo, kigeugeu.

Sasa wewe tueleze matusi yako wapi? mtu akiambiwa ni mwongo au kigeugeu ni tusi.[/QUOTE]
Mkuu hiyo rangi ukweli unauma, lkn mtu mzima joto linampata abadan!!
labda angetumia neno sporadic??? ie rainbow state-leadership !!!!!!!
 
" KIKWETE KIGEUGEU"

Mwandishi Saed Kubenea

Sheria ya nchi iko wazi kwa mtu yeyote kumtusi Rais ,Mtikila alifunguliwa mashitaka kwa kumtusi Rais
Kwa maneno haya Mwandishi Saed kubenea anapeleka taarifa kwa watanzania kuwa nchi ina Rais kigeugeu
Je nchi inaweza kuongozwa na Rais kigeugeu?

Huu ni uandishi wa namna gani? hili gazeti inabidi lichukuliwe hatua za kusheria na mwandishi huyu afikishwe mahakamani

Gezeti limepoteza muelekeo limeanza kuwa na mambo ya kidaku daku

Wewe ndiye unayepaswa kufikishwa mahakamani kwa uzushi na uchochezii. Kwani mtu kuitwa KIGEUGEU ni tusi? Ebo! Wewe vipi?
 
Back
Top Bottom