Mwanahalisi imeandika kweli kuhusu hii ya Kikwete na Mkapa? Tuijadili

Kiti

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
359
234
"Mwanahalisi toleo namba 249".......Kiongozi huyo wa nchi (Kikwete), mtoa taarifa anasema, ana simu tatu za mkononi ambazo anatembea nazo kila anakopita; jambo linalomfanya kupokea umbea kutoka kwa wasaidizi na maswahiba wake.
“Hata Mkapa (rais mstaafu Benjamin Mkapa) alikuwa na simu ya mkononi. Lakini simu ya Mkapa ilikuwa ya kupiga tu. Ilikuwa huwezi kumpata Mkapa kwenye simu yake ya mkononi, hadi yeye akupigie,” anaeleza kigogo mmoja wa ikulu ambaye alikuwa karibu na Mkapa.
Anasema, “Hata mawaziri wake walikuwa hawawezi kuongea naye kupitia simu yake ya mkononi. Simu ya Mkapa ilikuwa kwa mawasiliano ya watu wasiozidi sita wakiwamo watoto wake wawili na mkewe.”
Anasema hadi sasa, Mkapa anamiliki simu ya mkononi, lakini huwezi kumpata hadi yeye akupigie. Ile ni simu ya yeye kukupigia, si wewe kumpigia. Ni tofauti na Kikwete. Huyu bwana amegawa namba yake ya simu kwa watu ambao wengine wanaitumia kumpelekea umbeya,” anaeleza.
Anasema simu ya Rais Kikwete inapokea ujumbe wa kila mmoja na kuna wakati yeye hujibu ujumbe aliotumiwa usiku wa manane. Anahoji, “Sasa katika mazingira hayo, rais anapata wapi muda wa kupumzika na kusoma nyaraka?”
Gazeti hili liliwahi kuchapisha ujumbe wa simu uliodaiwa kutoka kwa Rais Kikwete kwenda kwa aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum, Amina Chifupa aliyekuwa ameomba ushauri wa kisiasa kwa rais Kikwete.Amina aliusambaza ujumbe uliotoka kwa rais kwa watu mbalimbali akiwamo Zitto Kabwe na Emmanuel Nchimbi.
 
Waambie hao mwanahalisi na wewe kama unamtazamo huo, dunia imebadilika. JK ni kiongozo anayekwenda na muda (Yupo fb, twitter, youtube n.k.), na kwa taarifa yako JK ni kiongozi anayejaribu kwenda na vijana, ni muwazi ila sema timu yake ndiyo imejaa waoga na wala rushwa na ni mabingwa wa kumdanganya. Lakini angekuwa na timu nzuri basi nadhani angeweza kuwa rais bora zaidi ktk JMT.
 
Ni kweli , hata mm nimeshuhuidia mwanamke mmoja akionyesha msg toka kwa JK . Wakuda na washambemnga wote wana nmaba zake na huwajibu msg. Kwa mfano Msg moja ilisema " Mtafute msaidizi wangu Bwana.......nitamwachia maelekezo". Hili jina nimeihifadhi lakini yupo kweli.

If you look at the woman who could converse with presida you get shocked. Rais wa ajabu kabisa tuliokwisha kuwa nae. Loh
 
Napita waungwana, napita. Mie ninazo simu mbili, sijajua kama ni kosa bado. NAPITA.
 
jakaya kikwete lazima aende na wakati na ndivyo anavyofanya.mwanahalisi hawamtakii mema kwani jk kuwasiliana mara kwa mara na wapiga kura wake ni dhambi?.acheni unafiki
 
Mimi hapo sioni tatizo lolote. Raisi na haki ya mawasiliano kama watu wengine
 
Tatizo ni nini hapo?

We hauni tatizo?
Kikwete anatakiwa kutulia na kufanya kazi aliyopewa na watanzania
kwa ufanisi, time is money, sasa kama anapata muda wa kuchat chat
wakati wowote unategemea ni wakati gani anaconcentrate nakutimiza
wajibu wake.

aache kuchat kwa sms asome na kuandika vitu vya msingi
vyenye kuboresha maisha au kuondoa kero za wenye nchi.

Ameishakuwa Rais tayari anasumbuka na kutafuta popularity
kwa faida ya nani? au nyie ndio mnaofaidika na weaknesses zake?
 
mie ninaline 6 za simu kwenye simu tatu za kichina zenye line mbili kila moja. sina makuu, sasa iweje hapo. yeye anazo 2 au tatu. mie sita
 
mie ninaline 6 za simu kwenye simu tatu za kichina zenye line mbili kila moja. sina makuu, sasa iweje hapo. yeye anazo 2 au tatu. mie sita



Mkuru anachati na kuzidi kutoa ahadi za papo kwa papo,wakati hata ambazo ziko kwenye ilani hajatekeleza.Huu si uungwana hata kidogo!!
 
Mimi hapo sioni tatizo lolote. Raisi na haki ya mawasiliano kama watu wengine

Ni haki yake kama mtu yoyote yule,zama za Rais kuvisha utukufu uliopitiliza ni kumkufuru Mungu.Kwa hili JK anastahiki pongezi kwa kuwa anakwenda na ulimwengu unavyokwenda.Tena ingebidi apewe blackberry ili afike kwenye majukwaa kama haya.Kwa kuwa alishakuwa ni Rais wa zama za ulimwengu wa sasa hayo ya Rais asimilki simu kwa kuwa anapelekewa majungu hayo yamepitwa na wakati.Acha simu yake itumike mpaka huko chini nayo ni sehemu nzuri ya kuwa karibu na umma.

Ndio maana za kwa usasa alionao hafuatilii wala hana hofu na mitandao yenye mlengo wa kujenga,amabyo wafuasi wake wasiojua zama na nayakati wamebaki kuwa wanapiga kelele kuomba achukue hatua.
 
Acheni chuki nyie mnaoshindwa kufikir,leo hii hata Mkapa nae anaonekana dhahabu!? Aloyafanya ndo yanaangamiza taifa,umeme wa IPTL,kauza migodi ya dhahabu na kufukia watu hai Bulanhulu,Tanzanite na AFGEM mmesahau? Leo mnajadili kuwa alikuwa na handset moja tena had akupigie.hilo lilisaidia nini Taifa? Au asipatikane kuhojiwa alipokuwa anauwa watu.mikono yake imejaa damu ya wazanzibar,wasukuma wanaapolo na Mwembechai.achen kujadili upuuzi,tusaidie Taifa kwa kujadili mambo ya msingi,km ajira zinachukuliwa na wakenya,elimu isikidhi ubora na ushindan wa dunia ya leo,ukosefu wa wasomi wa masomo ya sayansi,wimbi la watoto wa mitaani.kupanda kwa gharama za maisha na c wingi au upokeaji wa cm za Rais.huu utakuwa ni ujuha.
 
obama_1118825a.jpg


Bill Clinton sent only two e-mail messages as president and has yet to pick up the habit. George W. Bush ceased using e-mail in January 2001 but has said he's looking forward to e-mailing "my buddies" after leaving Washington, D.C.

 
Back
Top Bottom