Elections 2010 Mwanahalisi: CCM wajipanga kumzuia Dr Slaa

Naanza kupata wasiwasi mkubwa zaidi! Kwa asilia ya mataifa ya kiafrika, pale wanapozidiwa nguvu na upinzani, hujeukia mapinduzi (sio mapinduzi kama yalivyoasisiwa na Mwl Nyerere)- CHADEMA mlindeni huyu mzee, watamtoa roho! Yaani huwezi ukaelewa- kwa nini isiwe ni kupokezana na madaraka, ni nini kinachowafanya CCM waone kama akipata huyu basi ni mwisho wao!

Nina imani kubwa kama CCM ingekuwa walau kwa kipindi kimoja chama cha upinzani, Tanzania ingenyooka sana. CCM ni dume inapokuwa upinzani, CHADEMA ingewabidi tu wafanye kila jema na kwa mstari ili tu wasiondolewe madarakani kabla ya muda wao. Hii inaleta hali murua katika uongozi bora. Kwa sasa hivi tulikuwa na upinzani mzege mzege(sijui ndio kiswahili).
 
Njilembera,
Mbona sababu ni rahisi sana? CCM wanaogopa wakiondolewa mamlakani wengi wao wataishia lupango. Madudu waliyoyafanya ni mengi sana kuanzia enzi za Mzee Ruksa, fisadi Mkapa na sasa msanii huyo. Watatafuta kila njia kuzuia mabadiliko ya kweli yasitokee.
 
Dr. Slaa yuko makini kuliko kiongozi yeyote CCM.
Slaa si mtu wa kukurupuka, naamini kama angekuwa ni mtu wa kukurupuka sasa hivi angekuwa Segerea kwenye sakata ya kutaja majina vigogo wanaoitafuna hii nchi. Subirini mtaona umakini wake zaidi pale atakapokuwa anapakua santuri zile mpya 20 hivi karibuni wakati wa kampeni.

Wanapoteza muda na fedha, ingekuwa jambo la maana kama wangewatafutia hao vijana kazi za kufanya kuhimili ugumu wa maisha.

Penye red: Fedha? Siyo fedha zitokazo mifukoni mwao, ni fedha zetu wenyewe wanazotuibia.
 
Waungwana wanamapinduzi mliopo huko nyumbani nawaomba mjaribu kuscan na kutuwekea habari kama hizi.Baadhi yetu tunaweza kuzitumia huku tulipo JUST IN CASE....
 
Njilembera,
Mbona sababu ni rahisi sana? CCM wanaogopa wakiondolewa mamlakani wengi wao wataishia lupango. Madudu waliyoyafanya ni mengi sana kuanzia enzi za Mzee Ruksa, fisadi Mkapa na sasa msanii huyo. Watatafuta kila njia kuzuia mabadiliko ya kweli yasitokee.

Mhhh....Hili halitatokea Tanzania, no matter who become President. Sana sana watatakiwa kurudisha mali walizoiba iwapo itathibitika mahakamani. Hatuna viongozi wenye hulka ya aina hii katika duru hili la siasa!!
 
CHADEMA hajiamini ndio maana kila siku mnazusha uongo. Leteni ushahidi wa habari hizo sio mambo ya "inasemekana, nasikia, kuna tetesi n.k"

CHADEMA kama inataka kuchukua nchi kama watu wengi wanavyotaka, inabidi iwe makini nashutuma zao. sio kila mwananchi ni mfuata upepo kuna wananchi makini sana ambao hafuati uzushi na tetesi.
Hii inaitwa Media politics hata Obama aliitumia, Chadema inaungwa mkono na magazeti hayazidi matatu lakini yanavyozichanga karata zake hutadhani upande mwingine unaungwa mkono na lukuki ya magazeti.
 
Ni wazi kwamba CCM watajaribu kutumia technicalities kumzuia Dr Slaa. Wanajua fika hawawezi kumshinda kwa hoja. Yeye ana hoja kubwa ya kupiga vita ufisadi. CCM wakisema watapiga vita ufisadi hakuna mtu atawaamini. Wameulelea miaka yote hii.

Hofu yangu ni kwamba CCM itatumia vibaya mahakama kumzuia Slaa. In vibaraka sehemu mbalimbali. Kitu kitakachotuepusha na mbinu chafu ni kujitokeza kwa Watanzania wengi kumuunga mkono Dr. Slaa. CCM haitataka vurugu. Slaa akiwa na wafuasi wengi mbinu chafu zitaogopwa.
 
Ni wazi kwamba CCM watajaribu kutumia technicalities kumzuia Dr Slaa. Wanajua fika hawawezi kumshinda kwa hoja. Yeye ana hoja kubwa ya kupiga vita ufisadi. CCM wakisema watapiga vita ufisadi hakuna mtu atawaamini. Wameulelea miaka yote hii.

Hofu yangu ni kwamba CCM itatumia vibaya mahakama kumzuia Slaa. In vibaraka sehemu mbalimbali. Kitu kitakachotuepusha na mbinu chafu ni kujitokeza kwa Watanzania wengi kumuunga mkono Dr. Slaa. CCM haitataka vurugu. Slaa akiwa na wafuasi wengi mbinu chafu zitaogopwa.

Na ofcourse there is a bigger problem more than that, ok say Slaa amezuiwa CCM kampeni zao watafanyia wapi? Hii inaweza kuwa chanzo cha vurugu kubwa kama ilivyowahi kutokea nchi nyingine za Africa. Na kwa sababu for years sera za CCM zimekuwa zikizalisha the group with the name " We have nothing to loose" Shughuli yake lazima itakuwa pevu.
 
CCM wajipanga kumzuia Dr Slaa

• Waandaa mamluki kumdhamini
• Waomba msaada wa vyama vidogo

Na Saed Kubenea

Mkakati umesukwa na viongozi ndani ya CCM ili kuzima safari ya Dk Wilbrod Slaa kwenda Ikulu, Mwanahalizi limeelezwa.

Taarifa zinasema, kwa kushirikiana na vyama vidogo vya upinzani, CCM imesuka njama za kumkwamisha Dk Slaa katika hatua ya kurejesha fomu za kuwania urais.

"Kama hatukufanikiwa kumkosesha wadhamini halali, basi tutakwenda mahakamani….lakini hapiti," kimeeleza chanzo cha gazeti hili kikimkariri mmoja wa viongozi waliopewa jukumu la kumzamisha Dr Slaa.

Mwanahalisi lina taarifa kamili juu ya njama hizo zinazodaiwa kuhusisha baadhi ya viongozi wa CCM, serikali na vyama vya upinzani.

Dk Slaa aliibuka wiki tatu zilizopita, pale alipotangazwa na Chadema kuwa mgombea urais kwa tiketi hiyo.

Kuingia kwa Dk Slaa ulingoni kulibadili upepo wa kisiasa nchini, na kuleta kiwewe ndani ya CCM na hata kufanya viongozi wastaafu wa chama hicho kutamka hadharani kuwa "Slaa ni makini…. Hashikiki."

Hatua ya kwanza ya mkakati wa kumwangamiza Dk Slaa kisiasa inahusisha kumchomekea "wadhamini feki" katika fomu zake za kutaka kuwania urais.

Hatua hii inahusisha maandalizi ya genge la vijana ambao uraia wao una utata. Hawa watapelekwa mikoa mbali mbali nchini ili watie saini fomu zake za udhamini.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, wadhamini hao "feki" watafika kwa maofisa wa Chadema wanaoendesha zoezi la kuandikisha wadhamini wakiwa na vitambulisho vyao vya kupiga kura, kwa lengo la kutimiza jukumu walilopewa.

"Vijana hao wakimaliza kujiandikisha, wataripoti kwa maofisa wa chama xhao (CCM) ambao watarekodi kadi zao. Kwa kutumia kadi hizo za wasio Watanzania, Dk Slaa atawekewa pingamizi," ameeleza mtoa habari.

"Nakukuhakikishiua, Chadema wasipokuwa makini, Dk Slaa hawezi kuwa mgombea urais. Tayari vijana wametumwa mikoani kutimiza azma ya kumkwamisham" ameeleza kiongozi mmoja wa CCM ambaye hakutaka kutajwa.

Sheria ya uchaguzi inamtaka kila mgombea wa urais awe na wadhamini 200 kutoka mikoa 10 nchini, ikiwamo miwili ya Visiwani.

Kwa taarifa za juzi Jumatatu, jukumu la kumwekea pingamizi Dk Slaa litakabidhiwa kwa "wagombea urais wa vyama pinzani." Haijafahamika ni kina nani watapewa jukumu hilo.

Wadau, stori kamili katika front page ya Mwanahalisi ya leo. Mwenye soft copy yake atuwekee hapa.









Hiyo red hapo juu: zoezi ili ni la kijinga na bila kufikiri na linanipa faraja kwani wadhamini hao 'feki' wamo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura; sasa ni makosa ya nani kama si National Electoral Commission (NEC)? Na ni kigezo kizuri sana cha mdhamini kuwa mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari la wapiga kura! Chadema hili likitokea basi uchaguzi usimamishwe kwa amri ya mahakama pamoja na gharama zote za maandalizi ili kutoa muda kwa NEC kushirikiana na uhamiaji kuhakiki daftari la wapiga kura. Pili CCM ndio wanafuga majitu sio raia ndani ya nchi yetu na ndio maana wimbi la ujambazi ni kubwa.

Kama ujinga huu utafanikiwa, nafikiri it is a hight time now to use our forests and streets to fight for our freedom!!
 
Hizo ndizo siasa lakini kwa watu makini hakuna wa kumzuia Dr. Slaa kugombea. nafikiri kwa vyama vingine vifurahi ili at least mwaka huu tupate upinzani kidogo kwa wale wanaotaka ushindi wa kishindo. Inabidi watu waache demokrasia ifanye kazi yake.
 
Watu wakijani kwa mawazo mafupi bado tu mnasubiri mkono udondoke, wenzenu leo wameanza kampeni nyie bado mnamawazo ya kizamani ya ushindi mezani, nendeni mkafanye kampeni si kusubiri mwingine awekewe pingamizi. NEC imeshawapitisha wagombea na wameshaanza rasmi kampeni kama hamjui hilo basi endeleeni kuota.
 
Back
Top Bottom