Mwanahalisi bila ya KUBENEA linawezekana?

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Nimekuwa mpenzi mkubwa wa gazeti la Mwanahalisi.
Lkn nimeshtuka muda wa miezi hii michache kuona gazeti hili limekosa mvuto kwa wasomaji
Habari nyingi za front page sasa zinaonekana zimekosa mwelekeo
Matoleo 5 mfululizo limekuwa likinukuu Mikutano ya Chadema kama ndio source yake.Leo hii limenukuu magazeti mengine kama ndio source yake
ule uchunguzi wa Kina kama ulivyokuwa unafanywa na Kubenea sasa unaoenekana umepotea.
inaonekana waandishi wanakaa juu ya viti na kuwangalia mitaaandao inasemaje.
kwa mfano Chini ya Kubenea miezi 3 iliopita. Gazeti liliripoti Uteuzi wa Mh warioba ndie Mwenyekiti ktk Kamati ya Katiba
Liliripoti Uteuzi wa Mkuu wa Chombo kimoja cha Usalama nchini. ndio liliripoti Email za Maalim Seif na Pia ndio liliripoti mawasiliano ya Mh zitto

Tunaambiwa kubenea yupo Masomoni Ulaya.
JEE ENDAPO KUBENEA ATAKUWA NJE YA MWANAHALISI. GAZETI HILI LITADUMU NA LITAKUWA CHACHU YA MAGEUZI NCHINI AU LITAKUWA RAI?
 
Back
Top Bottom