Mwanafunzi Wangu Amenitoa Machozi

Aug 2, 2012
9
15
Wengi mnafahamu SHULE ZIMEFUNGWA ILA DARASA LA SABA NA LA NNE BADO WANAENDELEA NA MASOMO WAKIJIANDAA NA MITHANI YA TAIFA. L eo nilipoingia darasa la saba kufundisha nimekuta watoto wanamjadala mkubwa. kwakuwa kelele zilikua nyingi nikalazimika kujua kuna nini. Watoto wote walicheka kisha ikawa hivi:
Mimi: Mbona mnapiga kelele hamna kazi ya kufanya?
Wanafunzi: kicheko
Mtoto: Hamis si useme tu?
Zaituni: msiposema nawasema
Mimi: Zaitini niambie mama yangu!
Mtoto mwingine: Eti ni kweli mshahara wenu ni mdogo sana kuliko hata......(anataja kazi)
Mimi: Nitawaambia siku zijazo. Tuendelee na somo la leo. (NAPOTEZEA). Kisha naandika ubaoni mada dogo ya leo. METHALI NA NAHAU. (nikaligeukia darasa na ona watoto bado wanacheka). Haya Hamis tumbie methali yoyote uliyoweza kupata kwenye habari tuliyosoma jana.
Hamis: Fimbo ya wanyonge ni umoja wao
Mimi: Vizuri! Sasa nani anaweza kuifafanua methali hii.
Hamis: Mfano mwalimu ninyi si mnalipwa kidogo mkiwa na umoja mtalipwa nyingi na nyinyi kama wengine.
Watoto: kicheko
Mimi: Naanzisha wimbo na watoto wanaitikia huku wakicheka (napotezea ila naumia naamua kuandika maswali ubaoni ) fanyeni maswali haya kisha monitor utaniletea kwenye dawati langu.

Kilichoniuma si ukweli kuwa tunaloipwa kidogo ni ile hali ya kuona hata watoto tunaowafundisha nao wanaidharau kazi hii kiasi hiki!
 
very sad.zaman teacher alikuwa anaheshimika sana siku izi naona walimu mmeshindwa kuwa wamoja na kuwa na sauti moja
 
very sad.zaman teacher alikuwa anaheshimika sana siku izi naona walimu mmeshindwa kuwa wamoja na kuwa na sauti moja
tatizo la siku hizi unachanganya waalimu competent, wa upe,na wa voda faster,wa corruption sasa hapo ndipo umoja unapokosekana.
 
Poleni walimu. Ila matatizo haya huwa mnajitakia wenyewe, yaani nyie kila mwaka wa uchaguzi hamkomi kutumiwa katika kampeni halafu mnaachwa huku mkiamini mambo yatabadilika. Tokea 1995, 2000,2005 and 2010, hamchoki tu!
Mko wengi na mna ushawishi katika jamii kama mkitumia nafasi zenu vizuri.
Kumbukeni, mliyempigia kura mara mbili ameshawaambia hayo madai yenu hayawezekani kabisaaaaaa!
Amkeni bana!
 
Mbona walimu kazi mnayo dawa yake wauzieni kachori darasani
 
Kusema kwamba watoto wanaidharau inaweza kuwa si sawa kwa sababu mfano uliouonyesha unaweza kutafsiriwa kwamba watoto wanaonyesha kukerwa na hili na kuonyesha mshikamano nanyi kiasi hata kufanya reference kwenye methali.

Mambo ya zama za uwazi, enzi zetu hata kujua mwalimu analipwa mshahara gani utaanzia wapi?
 
Duh! Pole sana mwalimu.

Kwa yaliyojiri hapo inaonesha kuwa sasa ni muda muafaka walimu mtafakari na kisha mchukue hatua kwenye uchaguzi ujao. Binafsi mimi huwa nawa-hold ninyi responsible kwa kusaidia/kuipitisha/kuibeba ccm aidha kwa kura halali au kura haramu.

Mkithibutu na kuacha kuibeba ccm hasa kwa njia chafu na rushwa ukombozi wenu utakuwa mikononi mwenu.
 
Hadithi nzima niya kuchonga kwa kuangalia uhalisia wa mazingira ya mwalimu na mwanafunzi wawapo shuleni hasa mwalimu anapokuwa anaingia darasani . Japo ukweli ni kwamba walimu hawalipwi vizuri.
 
Hadithi nzima niya kuchonga kwa kuangalia uhalisia wa mazingira ya mwalimu na mwanafunzi wawapo shuleni hasa mwalimu anapokuwa anaingia darasani . Japo ukweli ni kwamba walimu hawalipwi vizuri.
umeichonga wewe? Nenda kwa banda huko.
 
Wengi mnafahamu SHULE ZIMEFUNGWA ILA DARASA LA SABA NA LA NNE BADO WANAENDELEA NA MASOMO WAKIJIANDAA NA MITHANI YA TAIFA. L eo nilipoingia darasa la saba kufundisha nimekuta watoto wanamjadala mkubwa. kwakuwa kelele zilikua nyingi nikalazimika kujua kuna nini. Watoto wote walicheka kisha ikawa hivi:
Mimi: Mbona mnapiga kelele hamna kazi ya kufanya?
Wanafunzi: kicheko
Mtoto: Hamis si useme tu?
Zaituni: msiposema nawasema
Mimi: Zaitini niambie mama yangu!
Mtoto mwingine: Eti ni kweli mshahara wenu ni mdogo sana kuliko hata......(anataja kazi)
Mimi: Nitawaambia siku zijazo. Tuendelee na somo la leo. (NAPOTEZEA). Kisha naandika ubaoni mada dogo ya leo. METHALI NA NAHAU. (nikaligeukia darasa na ona watoto bado wanacheka). Haya Hamis tumbie methali yoyote uliyoweza kupata kwenye habari tuliyosoma jana.
Hamis: Fimbo ya wanyonge ni umoja wao
Mimi: Vizuri! Sasa nani anaweza kuifafanua methali hii.
Hamis: Mfano mwalimu ninyi si mnalipwa kidogo mkiwa na umoja mtalipwa nyingi na nyinyi kama wengine.
Watoto: kicheko
Mimi: Naanzisha wimbo na watoto wanaitikia huku wakicheka (napotezea ila naumia naamua kuandika maswali ubaoni ) fanyeni maswali haya kisha monitor utaniletea kwenye dawati langu.

Kilichoniuma si ukweli kuwa tunaloipwa kidogo ni ile hali ya kuona hata watoto tunaowafundisha nao wanaidharau kazi hii kiasi hiki!

Mbona umetoa maswali(zoezi) wakati umefundisha methali moja tu?
 
Nyie si ndio baadhi yenu ni vinara wa kuisaidia CiCiMizi kuiba kura? Mshahara wa dhambi ni mauti. Mpaka mtakapojua kuwa CiCiMizi anawatumia kutenda dhambi, ndipo Mungu atasikia kilio chenu. Walimu wengi, hasa wa kike, ni wasaliti wa watanzania. Tatizo ni kuwa walimu wengi wa kike wameolewa na wenye nazo (mfano mzuri ni Teacher Salma na Mama Maria Nyerere).
 
tatizo lenu waalimu nyie ndo mnaowafundisha watoto kila kitu, kunawa uso, kuchana nywele, kuoga, yaani mengi mengi mengi. kubwa zaidi hata namna ya kufikiri. SASA CHA KUSHANGAZA ETI WATOTO HAOHAO MLIOWAFUTA TONGOTONGO LEO WANARUDI WANAWADANGANYA KWA CHUMVI NA TISHETI ZA NJANO NA NYIE MNAKUBALI. WENGINE MPAKA SIKU HIZI NASIKIA WANAWATANDIKA HATA BAKORA. hivi waalimu hamuoni kama hii ni aibu ya maisha????? kwa uwezo na wingi wenu, mkiamua, ni kusema tu, kwamba TUNAIBADILISHA HII SERIKALI ILI TUPATE MWAJIRI MPYA ANAYEJARI MASLAHI YETU. hakuna hata haja kulumbana na mwanafunzi wako uliyemfuta tongotongo halafu eti yeye ndio amekuwa na akili mpaka anakuambia eti
''AKILI ZA MBAYUWAYU'' hamuoni kama anawadhalilisha huyu dhaifu??? jamani walimu, mtaamka lini kutoka usingiziniiiiiiii??????
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom