Mwanafunzi wa Udaktari Aua Watu Wawili Ili Ajifunze Wanavyokata Roho

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
2597018.jpg

Thursday, July 23, 2009 3:27 AM
Mwanafunzi mmoja wa udaktari nchini Urusi amewaua wazee wawili kwa shoka ili ajifunze jinsi watu wanavyokata roho kwaajili ya masomo yake ya udaktari. Mwanafunzi huyo aliyetajwa kwa jina la Tatyana mwenye umri wa miaka 24, aliwaua wazee wawili kwa shoka ili aone jinsi watu wanavyokata roho.

Polisi wa Urusi walisema kwamba Tatyana amekiri kufanya mauaji hayo.

Mtu wa kwanza kumuua alikuwa ni jirani yake bibi Olga Stepushenko aliyekuwa na umri wa miaka 85. "Nilichukua shoka na nilimpiga nalo kichwani mara kadhaa" alisema Tatyana.

"Wakati alipodondoka chini, nilikaa pembeni yake na kusubiria mpaka alipofariki, niliangalia jinsi alivyokuwa akikata roho".

Siku nne baadae Tatyana alimuua jirani wa bibi huyo, bibi Zoya Karpova aliyekuwa na umri wa miaka 87 kwa kumkata kata na shoka mara nane.

Tatyana aliiacha maiti ya bibi huyo kwenye nyumba yake na kuondoka na alirudi baada ya wiki mbili kuangalia na kurekodi jinsi maiti hiyo ilivyokuwa ikioza.

"Nilitaka nipate vielelezo zaidi kuhusiana na kifo ili nivitumie kwenye masomo yangu" alisema Tatyana na kuongeza "Nilitaka nione jinsi minyoo itakavyoifanya maiti ya Zoya ioze".

Tatyana aliambatanisha vielelezo vya utafiti wake huo kwenye taasisi moja kubwa ya udaktari nchini humo.

Mwanafunzi huyo anayetoka mji wa Novosibirsk alikuwa akikaribia kuhitimu masomo yake kama daktari maalumu wa upasuaji lakini alikamatwa kabla hajamalizia utafiti wake aliokuwa akiufanya.

"Wakati tulipoona watu wawili wameuliwa katika staili inayofanana, tulijua kuwa muuaji tunayemtafuta atakuwa akili zake haziko sawa" alisema afisa wa polisi.

Majirani walisema kuwa Tatyana alikuwa akiwatembelea bibi hao mara kwa mara kabla ya kuwaua. Nyumba yake iliposachiwa, shoka alilokuwa akilitumia katika mauaji yake lilipatikana likiwa lina damu damu.

Polisi wanachunguza kama kuna watu zaidi waliouliwa na Tatyana. Tatyana anakabiliwa na miaka 20 jela.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2597018&&Cat=2
 
huyo jamaa lazima atakuwa ana kasoro tu coz hata masomo ya udaktari huwa utafiti wake haufanywi hivyo kwa kuua raia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom