Mwanafunzi akamatwa na vitambulisho vya jeshi vyenye sahihi ya rais

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Mwanafunzi akamatwa na vitambulisho vya jeshi vyenye sahihi ya rais
Na Mashaka Kibaya, Manyara


MWANAFUNZI wa kidato cha nne, Alex Marongo, 30, anashikiliwa na polisi kwa kupatikana na vitambulisho vitatu vinavyomuonesha akiwa amevaa kombati za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huku vikiwa vimeghushiwa sahihi za waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.



Marongo alikamatwa na polisi kwa ushirikino wa raia wema na alipopekuliwa aligundulika kuwa alimaliza elimu yake katika Shule ya Sekondari Imboru tarehe Oktoba 27, 2008, lakini vitambulisho alivyokutwa navyo vimegongwa mihuri ya JWTZ kambi ya Ruvu.



Inadaiwa kuwa Marongo amekuwa akijitangaza kama ofisa wa serikali mwenye cheo cha kapteni X. Baada ya taarifa za raia wema wa wilaya ya Mbulu, mtuhumiwa alitiwa nguvuni na makachero wa jeshi la polisi waliokuwa doria.



Uchunguzi wa polisi umebaini kwamba vitambulisho ambavyo alikuwa akivitumia mwanafunzi huyo vimeandikwa kwamba haruhusiwi kugharimia matibabu wala gharama za malazi kwenye nyumba za wageni kwa vile ni mlinzi wa nchi hadi 2016.


Mwanafunzi huyo alikamatwa juzi maeneo ya Ujenzi, Mbulu mkoani Manyara wakati Ispekta Joseph Ng’eve, akiwa doria na wenzake, walipoelezwa kuwa kuna mtu anajitangaza askari wa JWTZ na ndipo walipoamua kumfuatilia na kumkamata.



SSP Josephat Mwingira, akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Manyara, alisema mtuhumiwa baada ya kutiwa nguvuni na kuhojiwa alikiri kutengeneza mwenyewe vitambulisho hivyo na kusema alimaliza shule hivi karibuni.



Alisema mtuhumiwa aliwafahamisha polisi kwamba alimaliza kidato cha nne mwaka 2002 katika Shule ya Sekondari ya Endasaki wilayani Hanang’ na akawa anafanya shughuli za ualimu kwa kujitolea huko Endasaki na baadaye akarudia kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Imboru.



“Huyu bwana tunayemshikilia amekutwa na vitambulisho vitatu vyenye sahihi za Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amekutwa na kofia ya mtumba na shati lenye cheo cha kapteni X,” alisema



Taarifa ya polisi kwa Mwananchi inaeleza kwamba uchunguzi zaidi unaendelea juu ya tukio hilo la mwanafunzi huyo kuhusika na ujambazi na kwamba lengo ni kubaini kama mtuhumiwa alipata huduma kwa kutumia vitamblisho hivyo sehemu nyingin
 
Back
Top Bottom