Mwanafunzi afariki St Augustino University Mwanza kwa kukanyagwa na wenzie

carmel

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,837
262
Kuna taarifa kutoka chanzo kwa mtu wangu wa karibu aliyepo chuoni hapo kwamba mwanafunzi wa kike amefariki jana baada ya kukanyagwa na wenzie kwa kile kilichoelezwa ni kukimbilia kuwahi seat wakati wa kufanya mitihani.
Kinachonisikitisha ni kwamba, hawa ni wanafunzi watu wazima na wengine wana waume/wake na watoto lakini hawajastaarabika hadi kufikia kumuua mwenzao katika purukushani za kuwahi viti. Tena ni wanafunzi wanaotarajia kumwaliza chuo mwaka huu sio hata first year kwamba utasema bado wanao usekondari ndani yao, na inasemekana ni wanaosomea ualimu..what a shame.
Na pia nashangaa sana kwamba hata ST Augustino wana matatizo ya kutokuwa na seat za kutosha kwa ajili ya wanafunzi wao? is it fair?, mbona ada inalipwa kubwa na chuo kina wafadhili? mi nilidhani haya mambo ya kusoma mmesimama au nje ya madirisha yao tu udsm. Mbona hatuna ustaarabu kwenye elimu jamani.
Mwisho natoa pole kwa familia ya huyo marehemu na Mungu aiweke pema roho yake. Amen.
 
Watanzania tumezidi upole, mtu unalipia huduma harafu unauziwa huduma duni kuliko ulicholipia na unakubali bila malalamiko au hata malalamiko kidogo tu. Mke wangu anasoma CBE na yeye analalamika tatizo hilohilo kwamba akichelewa kufika chuoni hawezi kupata kiti, hawa wanafunzi hawajawahi hata kugoma kushinikiza chuo kuweka miundombinu inayoendana na wanafunzi waliodahiliwa, na hiki ndicho kilele cha uzembe na upole huu!
Tunawachagua wanasiasa kwa ahadi kedekede na wala wasipozitimiza hatuwawajibishi ipasavyo.... SHAME on you fellow Tanzanian for being so feeble!
 
Jamani fedha zote anachukua Rostam Aziz sasa hivyo viti watanunua kwa kutumia Mawe!!!
Poleni sana siyo lazima msome Tanzania karibuni sana upande mwingine wa dunia mje kusoma kwa starehe na raha!!!
 
RIP mwanafunzi. Hayo ni matokeo ya kuwahi siti za nyuma ili wadese/watumie vinyoka/ kutazamia au kutengeneza loop za kucheat. Ndo elimu yetu ya Tanzania ambayo serikali yetu imekuwa ikitengeneza.
 
I also thought the same
 
Jamani fedha zote anachukua Rostam Aziz sasa hivyo viti watanunua kwa kutumia Mawe!!!
Poleni sana siyo lazima msome Tanzania karibuni sana upande mwingine wa dunia mje kusoma kwa starehe na raha!!!

kila ujinga mnaofanya mnamsingizia Rostam! si kosa lako ndivyo mlivyofundishwa!
 
Jamani fedha zote anachukua Rostam Aziz sasa hivyo viti watanunua kwa kutumia Mawe!!!
Poleni sana siyo lazima msome Tanzania karibuni sana upande mwingine wa dunia mje kusoma kwa starehe na raha!!!

we kama umebahatika kusoma nje ya tz shukuru maana kuna watu wanakesha kutafuta scholarship hawapati na hali halisi ni kwamba wazazi hawana uwezo wa kuwapeleka kusoma huko.
 
Jamani fedha zote anachukua Rostam Aziz sasa hivyo viti watanunua kwa kutumia Mawe!!!
Poleni sana siyo lazima msome Tanzania karibuni sana upande mwingine wa dunia mje kusoma kwa starehe na raha!!!

St Augustion na rostam wapi na wapi? kile si chuo cha wakatoliki? au nako rostam kashaingia lol
 
Watanzania tumezidi upole, mtu unalipia huduma harafu unauziwa huduma duni kuliko ulicholipia na unakubali bila malalamiko au hata malalamiko kidogo tu. Mke wangu anasoma CBE na yeye analalamika tatizo hilohilo kwamba akichelewa kufika chuoni hawezi kupata kiti, hawa wanafunzi hawajawahi hata kugoma kushinikiza chuo kuweka miundombinu inayoendana na wanafunzi waliodahiliwa, na hiki ndicho kilele cha uzembe na upole huu!
Tunawachagua wanasiasa kwa ahadi kedekede na wala wasipozitimiza hatuwawajibishi ipasavyo.... SHAME on you fellow Tanzanian for being so feeble!

Ila sio siri upole wetu unatucost. imagine hata kama ni mkopo wa bodi utakuja kulipa na kumbe hata kiti darasani kupata ni shida, mi nakumbuka udsm tulikuwa na vipindi kadhaa ambavyo vina wanafunzi wengi hadi watu wanasimama dirishani what a shame, wasomi wa aina gani tunaowatengeneza namna hii, kutakuwa na critibal thinking namna hii kweli?
 
tukio hilo linasikitisha sana. Pamoja na hayo napenda kumsahihisha aliyeweka thread hii hapa jamvini. Mosi, mwanafunzi ni mwanafunzi bila kujali ana umri gani au yuko mwaka wa ngapi. Mara nyingi mtu akishakua mwanafunzi anaweka umri wake pembeni.

Pili, suala la uhaba wa vyumba vya kusomea sio la SAUTI peke yake bali ni janga la kitaifa, Nenda UDSM, SUA, MZUMBE na hata UDOM utakuta tatizo lilelile. Wanafunzi wanabanana darasani hadi wengine wanasimama madirishani. Nenda UDSM uone wanafunzi wanavyopigana vikumbo kupanda shuttle kuelekea chuoni hadi wengine wanapitia madirishani. Pia nenda UDOM uone wanafunzi wanavyobanana hadi mwalimu anakosa mahali pa kusimama.

Tatu, kauli ya kwamba SAUTI wanatoza ada kubwa lakini wanashindwa kuudumia wanafunzi ni UONGO na UZUSHI uliopindukia. Ukweli ni kwamba SAUTI ni chuo pekee cha binafsi kinachotoza ada ndogo zaidi. Zaidi ya hapo **** baadhi ya kozi ambazo vyuo vya umma vinatoza ada ya juu kuliko ile inayotozwa na SAUTI.

Kuhusu suala la SAUTI kua na wafadhili sioni tatizo lolote kwa kua serikali haichangii chochote kwenye vyuo vya binafsi kwa maana hiyo wafadhili hao kwao ndio wanabeba nafasi ya serikali.

Mwisho kama ni kweli tukio hilo limetokea basi naamini itakua ni bahati mbaya na hivyo natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kwa msiba huo uliotokea.

Nawasilisha.
 
Jamani mmenitisha kweli nina dada yangu kule imebidi baada ya kusoma tu nikampigia simu fasta.
Alichoniambia ni kweli huyo dada amekufa lakini si kwa kukanyagana kama ilivyopostiwa hapa. nikuwa alikuwa na matatizo ya moyo na toka asubuhi alikua analalamika kujisikia vibaya lakini akasema atapiga pepa hivyo hivyo.
wakati wa kuingia kweli kulikuwa na kuwahi nafasi lakini si kiasi cha kukanyagana na alipo ingia chumba cha mtihani wakati pepa zinagawiwa akazidi kujisikia vibaya zaidi akatolewa nje akatafutiwa usafiri, bahati mbaya akafia njiani.
hii ni kwa mujubu wa class mate wake yaani dada yangu
 
Kama ni hivyo basi watu wanaoweka post humu wasikurupuke bila kua na uhakika na kile wanachokiandika. Ni bora ukatafuta zaidi ya chanzo kimoja upate uhakika zaidi kuliko kukurupuka na kuwashutumu wanafunzi kwa kitu ambacho hawajakifanya. Vinginevyo ni bora ukaandika kwamba hiyo ni tetesi.
 
mkubwa hujajua kuwa tatizo sio seat bali wanachuo wana msemo wao kuwa position itself has got some marks.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom