Mwanadamu na matumizi ya uwezo wake!!!!

Sitaki kuamini kuwa na wale wanaojisaidia pembeni wakati wanaliona tundu la choo lipo, kuwa nao wametumia 10% ya uwezo wao kufikiri

u neva knw bro........ since we all at 10% may be goin further inaeza ikaleta tabia za kituko zaidi kuliko hao uliowataja hapo kwny red...... considering da fact from our applauded scientists of all tym, wote walikua wana weird behaviours...
 
Nadhani tukitumia nusu ya uwezo wetu wa kufikiri dunia haitakuwa sehemu nzuri ya kuishi. Na wengi watakuwa vichaa kwa kufikiri sana.
 
yesu ni Mtume kwa wana wa israel tatizo letu binadam hatupendi kusoma tukamjua Mungu,badilika ndugu yangu!
 
Soma kitabu THE VOICE OF KNOWLEDGE by don Miguel Ruiz unaweza kujua kwanini tunatumia tu 10%
 
Mungu amesema, "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake mwenyewe. Ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:26 Mungu alisema na tufanye mtu kwa mfano wetu". Hivyo tumeumbwa kwa mfano wa Mungu katika kila kitu including uwezo wa akili. Ila kwa vile tumekataa Kweli ambayo ni Neno la Mungu basi hatuwezi kutumia asilimia kubwa ya uwezo aliotupa Mungu. Angalia wanaoishi maisha matakatifu wana uwezo wa kufanya makubwa sana kwa kutegemea Nguvu za Mungu. Tukibadilika mbona tuna uwezo wa kufanya makubwa!!!
Inaonekana binadamu ana uwezo mkubwa sana lakini bado hajautumia.Niliwahi kusoma utafiti mmoja na ikagundulika kwenye utafiti ule kuwa mwanadamu anatumia uwezo wake wa akili au kufikiri kwa asilimia 10 tu!Yaani pamoja na vituko vyote hatujaweza hata kutumia asilimia 50!Kumbe inawezekana ikawa sababu ya upofu wetu wa kujijua na kujua kuhusu nguvu zinazotuzunguka kama Mungu n.k,au ndo maana tunaamini katika hizo nguvu,yaani huenda hazipo na tunashindwa kujua hazipo kwa sababu hatufikiri vyema!
 
Yesu sio mtume, ni mwana wa Mungu alie hai. Ni Mungu mwana, ambae ni Neno la Mungu. Kasome Yohana 1: 1 inasema "Hapo mwanzo palikuwapo Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu". Soma mpaka mstari wa tatu. Kama hutalielewa hili neno omba mtu anaejua akutafsirie, kwani tatizo la watu wengi wanasoma neno la Mungu bila kulielewa. Kuelewa neno la Mungu unahitaji akili za kiroho, hivyo ni budi kusali kwanza Mungu akufunulie maandiko ndipo usome. Usisome neno la Mungu bila kusali kwanza.
yesu ni Mtume kwa wana wa israel tatizo letu binadam hatupendi kusoma tukamjua Mungu,badilika ndugu yangu!
 
kama unaijua bible vizuri hiyo Yohana 1:1 haikusemwa na yesu kristo wala hazikunasibishwa naye na mtunzi wa injili kulingana na Yohana.hivyo mistari hiyo si hoja kuonyesha uungu wa Yesu,hasa unapozingatia shaka walizonazo wanazuoni wakristo kuhusu Injili ya nne.Wanazuoni wa Biblia waliotunga THE FIVE GOSPELS( Injili Tano ) wamesema " Sura mbili zilizochorwa na Yohana na waandishi wa Injili tatu nyingine SYNOPTIC GOSPELS, yaan injili ya Mathayo, Marko na Luka) haziwez kuwa zote kwa pamoja ni sahihi kihistoria" MANENO YALIONASIBISHWA NA YESU KATIKA INJILI YA NNE NI KAZI YA MWINJILISTI KWA SEHEMU KUBWA.
Pia neno la kiyunan kwa Mungu liilotumika ktk ibara naye "neno alikuwa kwa mungu' ni aina ya wazi hotheos inayomaanisha "Mungu". Hata hivyo ktk ibara ya pili "naye neno alikuwa mungu" neno la kiyunan lililotumika si aina hiyo ya dhahiri tontheos, linalomaanisha "mungu" kwa hiyo Yohana1:1 kwa usawa zaid inatakiwa itafsriwe. Hapo mwanzo kulikuwa na Neno naye Neno alikuawa kwa Mungu .Hivyo ikiwa neno alikuwa kwa Mungu kwa maana yake halisi itamanisha ipo miungu miwili.Hata hivyo ktk lugha ya bible neno "mungu" linatumika kuashiria mamlaka na nguvu.Mfano, Paulo alimuita shetani "mungu" ktk 2 wakorintho 4:4 "Hao hawaamini sababu yule mungu wa ulimwengu amezitia giza akili zao...."Musa pia ameitwa mungu ktk kutoka 7:1 "Mungu akamuambia Musa tazama mimi nakufanya kama mungu kwa farao, nae ndugu yako aaron atakuwa nabii wako" tuwasiliane ndugu yangu pengine mimi siijui vizuri biblia basi nifafanulie vizuri ili niijue ipi haki ipi batili. Let us discus bcause DISCUSSION IS AN EXCHANGE OF INTELLIGENCE AND ARGUMENT IS AN EXCHANGE OF IGNORANCE! achu2488@yahoo.com
 
Sitaki kuamini kuwa na wale wanaojisaidia pembeni wakati wanaliona tundu la choo lipo, kuwa nao wametumia 10% ya uwezo wao kufikiri

Naungana na we' mkuu............ maana kuna watu duhh!! ................ hata hiyo 5% sidhani!
 
manchoso,acha usanii wa dr Zakir Naik bana.Achana na mawazo ya watu angalia maandiko.Mjadala uliouanzisha japokua unatutoa kwenye mada nitakusaidia kidogo:Uungu wa Yesu umeanzia agano la kale,lakini nitakupa mistari michache kutoka agano jipya.Pia namna Yesu alivyoitwa Mungu ni tofauti na Musa na baadhi ya mifano uliyotoa,hilo tuliache.Kwenye ufu 1:8 kuna kauli ina sema,"Mimi ni alfa na omega asema Bwana Mungu,aliyeko na aliyekuwako na atakaekuja,Mwenyezi".Kama unataka kumjua huyo aliyesemwa hapo ni nani,jiulize ni nani alisema atakuja?Pia ufu 21:7,Yesu anasema,"Yeye ashindae atayarithi haya,nami nitakua Mungu kwake nae atakua mwanangu".Unadhani Musa au kuna mtume yoyote unaemjua wewe aliyewahi kutoa kauli hii?Thubutu!!!Pia ufu 22:16 anasema,"Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia mambo hayo katika makanisa.Mimi niliye shina na mzao wa Daudi,ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi".Hivi unadhani ni mwanadamu gani anaweza kusema "nimemtuma malaika WANGU"?Sote tunajua malaika ni wa Mungu kwa sababu amewaumba,tangu Adam mpaka leo hakuna mwanadamu alidai ana malaika,Yesu hakuwa mwanadamu bali Mungu,na yeye ndie aliyewaumba malaika na vyote Yoh 1:3.Asingesema hayo kama angekuwa mwanadamu!
 
Last edited by a moderator:
Dini ni tamaduni tu ya jamii fulani pahala fulani.
Tatizo tuna penda na tumekubali ku adapt tamaduni za wenxetu walio endelea mf. Waarabu na wamisionary.

Mtoto kuwa mkristo, mpagan au muislamu ni kurithi tu toka kwa wazazi wake na ndo maana tunaendelea kurithi tu cjui mpaka lini? Kwa nn hatuluendelea kurithi za babu zetu?

China, urus kuna baadhi ya maeneo hakuna kanisa wala mskiti inakuwaje hapo?

Jiulize swali moja hili:
Kipindi tunakua tumekua tukiambiwa Jerusalemu ni mji wa maajabu, wenye lulu,blah blah blah na tukajengeka kuwa kila mtu anataMani kufka maana kwa uwezo wetu hakuna liye amin kuwa anaweza kufika kirahsi.

Lakin leo inakuchukua saaana siku mbili kufika Jerusalem...hahaha

Babu zetu hawakua wanajua au kufikiri kuwa mawasiliano yanaweza kua kama hv leo kwa maana hiyo huo ndo ulikua ukomo wa uwezo wao wa kufikiri na hiyo ndo maana ya Mungu yaani ni mwisho wa uwezo wako wa kufikir.

Jiulize ni kwa nini the same book ( BIBLE/QURAN) but pple never understand it...why?
 
u neva knw bro........ since we all at 10% may be goin further inaeza ikaleta tabia za kituko zaidi kuliko hao uliowataja hapo kwny red...... considering da fact from our applauded scientists of all tym, wote walikua wana weird behaviours...

Wengine wanadai kwamba ukifikiri na kutumia akili zaidi ya hiyo 10% unaingia katika hali ya insanity.
 
akohi,ni kweli dini ni utamaduni lakini imani ni kitu kingine kabisa.Uwezo wetu wa kufikiri una matatizo ndo maana sayansi imeshindwa kuthibitisha au kukanusha uwepo wa Mungu,kushindwa huko ni dalili tosha ya kushindwa kwetu kuitumia akili yetu vile inatakiwa na sayansi ni matokeo ya kufikiri kwa mwanadamu,kama kufikiri huko kuna matatizo lazima na sayansi nayo itakua na matatizo pia.China na Urusi nako pia kuna dini,usidanganywe kuwa hakuna dini.Pia usiulinganishe Ukristo na Uislam,hizi ni imani mbili tofauti na hata anaeabudiwa na Ukristo siye anaeabudiwa na Uislam,hivyo sababu za kutokuelewa vitabu vya imani hizo ni tofauti pia!
 
Last edited by a moderator:
Wengine wanadai kwamba ukifikiri na kutumia akili zaidi ya hiyo 10% unaingia katika hali ya insanity.

Sio kweli,uoga wa kuitumia akili yetu ipasavyo ndo insanity!
 
Eiyer.
Swali langu ni kwanini watu dunia nzima tumetofautiana kuielewa Biblia?

Take your time and think!
 
akohi,sababu zinatofautiana kutoka mtu mmoja kwenda mwingine.Kuna wengine wameathiriwa na mapokeo ya kimafundisho,yaani anaposoma maandiko anayatafsiri kwa mujibu wa namna alivyofundishwa kuitafsiri biblia,wengine uwezo mdogo wa kufikiri n.k.Lakini yote katika yote tunarudi palepale kwenye namna ya kuutumia uwezo wa akili yetu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom