Elections 2010 mwanachama wa ccm akamatwa akiiba mtihani wa shule za msingi

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Walimu mbaroni wizi wa mitihani ya darasa la saba




Waandishi Wetu
WALIMU wakuu na wasimamizi wa mitihani, wanashikiliwa na polisi na kuhojiwa kwa tuhuma za wizi wa mitihani ya darasa la saba iliyomalizika juzi nchini kote.

Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa walimu na wasimamizi hao, ambao jumla yao ni 14 walikamatwa kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Ruvuma na Mwanza.

Kutoka Ruvuma habari zimeeleza kwamba walimu wakuu wawili, wasimamizi watatu na walimu wengine wanne wa kawaida walikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi huo wa mitihani.

Alisema wote wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakitoa majibu ya mtihani wa taifa Kiswahili na Hesabu kwa wanafunzi waliokuwa wakifanya mithini hiyo ya kumaliza elimu ya msingi.

Inadaiwa kuwa walimu hao walikamatwa jana majira ya saa tano asubuhi kwa nyakati na baada ya kupekuliwa simu zao za mkononi walikutwa na majibu ya mitihani ya hiyo iliyofanyika Septemba 6,mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kizungumza na gazeti hili jana, Kamuhanda alidai kuwa walimu na wasimamizi hao walishirikiana kutoa majibu hayo kwa wanafunzi wa shule za msingi za Ruvuma na Kipera.

Akielezea tukio hilo, kamanda Kamuhanda alidai kuwa baada ya kufungua mitihani hiyo, wasimamizi hao walibaki na baadhi yao na kuifanya kisha kutuma majibu kwa walimu wakuu wa shule hizo.

"Walimu hao waliandika majibu kwenye makaratasi na kupeleka ****** kisha wanafunzi walikuwa wakiaga kuwa wanaenda ****** na kwenda kuchukua majibu," alidai Kamanda huyo wa polisi.

"Tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusiana na kuwepo kwa taarifa za udanganyifu wa mtihani, tukaweka mtego na kufanikiwa walimu na wasimamizi hao. Hadi sasa tunawashikilia na watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi," alidai Kamanda Kamuhanda.

Wakati hayo yakitoa mkoani Ruvuma, walimu wengine watano wamekamatwa na kuhojiwa mkoani Mwanza baada ya kukutwa na karatasi za majibu ya mtihani wa Kiingereza.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Sirro alidai mbele ya waandishi wa habari jana kwamba, tukio hilo limetokea wilayani Sengerema.

Alidai kwamba, walimu hao walikutwa wamejifungia chumbani wakijibu mtihani huyo wa Kiingereza baada ya kulipwa Sh1,329,500.

Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, walimu hao wa Shule ya Msingi Nyamzumla iliyopo wilayani Sengerema kata ya Kagunga tarafa ya Nyachenche mkoani Mwanza, walikamatwa Septemba saba mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi wakiwa wamejifungia nyumbani kwa mkuu wao wa shule na kujibu maswali hayo.

Alidai kuwa polisi waliwakamata walimu hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kwamba, kuna walimu wamejifungia ndani wakijibu mtihani huo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wa 30 kushinda.

Kamanda Sirro alidai kwamba, baada ya polisi kufika kwenye nyumba hiyo walimkuta mwalimu mkuu mmoja akiwa na karatasi 50 za maswali ya mtihani huo pamoja na karatasi za majibu.

"Mwalimu huyo mkuu pia tulimkuta akiwa na karatasi ndogo 65 ambazo zilikuwa hazijaandikwa kitu, lakini zinaonekana zilikusudiwa kuandikia majibu maswali hayo kwa ajili ya wanafunzi, alikuwa na kalamu tatu za wino wa Bluu na kalamu nyekundi moja. Pia alikuwa na fedha taslimu Sh 350,000," alidai kamanda Sirro.

Kamanda huyo alidai kuwa baada ya upekuzi wa kina, polisi ilibaini kuwa mwalimu huyo alikuwa na karatasi tatu za majina ya wanafunzi ambao idadi yao inafikia 30.

"Kati yake majina 13 ya mkondo A, 11 ya mkondo B na majina 6 ya mkondo C. Yote yakiwa ya wanafunzi ambao walikuwa wanashiriki mtihani huo wa darasa la saba katika shule yake," alidai Kamanda Sirro.

Kamanda huyo wa polisi aliwataka walimu wengine waliokamatwa kwa tuhuma hizo kuwa ni Hamza Othman (25) alisema kuwa amekutwa na karatasi tatu za majibu na maswali pamoja na fedha Sh979,500 akiwa amezificha katika mifuko mbalimbali ya suluari tatu alizokuwa amevaa.

Alisema mwalimu huyo pia alikutwa na kadi ya uanachama wa CCM yenye namba za usajili AE 448569.

"Walimu wengine ambao tuliweza kuwakamata nyumbani humo hawakukutwa na karatasi zozote wala fedha lakini walikuwa wamejifungia ndani humo," alidai.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu shtaka la kula njama na kuiba mitihani hiyo baada ya upelelezi kukamilika.

Wakati huohuo, jijini Dar es Salaam mwanafunzi wa darasa la saba aliyemaliza mitihani yake juzi Mahona Sukambi (14), amefariki dunia baada ya kuzama baharini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanafunzi huyo alizama juzi alipokuwa akiogelea na wenzake kusherehekea kuhitimu elimu ya msingi.

Kamanda Missime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8:00 mchana ufukweni kwa Bahari ya Hindi, eneo la Kidete Kigamboni wilaya ya Temeke.

Imeandaliwa na Joyce Joliga, Songea; Frederick Katulanda, Mwanza na Tumsifu Sanga/
source MWANANCHI.CO.TZ
 
"mwanachama wa ccm akamatwa akiiba mtihani wa shule za msingi."

Huu ni uandikaji mpya!

Tunaomba wawe wanatuandikia kila mwizi na chama chake cha siasa! That would be fantastic!
 
Back
Top Bottom