Mwana jf, tukikupa urais wa tanzania 2015 utatufanyia mambo gani ili tusikuite dhaifu?..

Mimi kwa makusudi ningeimarisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi kwa kuongeza uwakilishi bungeni wa angalau chama tawala 55% na upinzani 45%. Lengo likiwa ni kuimarisha majadiliano bungeni. Pili, kila mwisho wa mwezi ningekuwa na tabia ya kukutana na viongozi wa upinzani ili niwashirikishe na kupokea maoni yao yahusuyo utekelezaji wa mipango ya kitaifa ya maendeleo ya nchi.
 
ningehakikisha kila nyumba ipo connected na TBL au serengeti breweries....ili projection za makusanyo zijulikane mapema kabla ya kipindi cha bajeti
 
kila kukicha asilimia kubwa ya thread zinazoanzishwa hapa ni za kutoridhishwa na utawala uliopo. Sasa mie nimekaa nimefikiri na kujiuliza hivi wewe mlalamikaji kama mimi (mimi pia hulalamikia utawala kwa mambo tofauti) ungekuwa rais ungefanya nini.
Mie binafsi ningeanza na mambo yafuatayo
mkuu wa polisi ningetafuta dizaini ya mahita.
Muungano ningeuvunjilia mbali na wazanzibari wote ningewapa siku saba wawe wamerudi kwao na ningetuma meli na ndege kuwarudisha ndugu zangu bara kutoka zanzibar.
Waziri mkuu wangu angetoka chama cha upinzani ili kuwe na maamuzi ya kukosoana siyo mambo ya ndiyo mzee.
Hukumu ya kifo kwa mafisadi.
Ningeanzisha ile kitu ya tajirika na mrema , yaani ukifichua mabovu ikajulikana ni kweli basi una milioni tano. Hii ingefanya wengi waogope kuiba na ujambazi ungepungua sana hata mafisadi wasingeweza kwa sababu kila mtanzania angekuwa polisi.
Nitahakikisha kila kiongozi aliyepita mali zake zinachunguzwa hii ikiwa na familia yake kwa ujumla na ikionekana ni mali ya uma au rushwa basi anafilisiwa na kufikishwa kizimbani kama mbarak.
Bandari ya mtwara ingekuwa free port kama dubai.
Mapato ya mafuta na gesi ningeyapeleka kwenye sekta za afya, elimu na kilimo which means elimu bure kwa wote, afya bure kwa wote na msaada wa bure kwa wakulima wadogo, kuwe na mtrekta ya serikali kila kijiji kuwalimia bure wasiojiweza.
Wanzafunzi wanakopeshwa wakifika vyuoni ili wajiandae na maisha yao halafu watalipa wakati wanafanya kazi.
W azee wote ningewatunza bure.
Ukianzisha kikundi kama uamsho unakuwa umejitangazia kifo nitahakikisha unapotezwa kikolimba

haya ni mawazo yangu binafsi wewe je????
ntahakikisha nazalisha umeme wa kumwaga kiasi kwamba unit moja inunuliwe kwa shilingi moja ya kitanzania!! Umeme ndo siri ya maendeleo , hayo mengine ni kujazilishia tu.
 
Nitahakikisha nafanya yafuatayo;
1. Nitaangalia upya uhusiano wetu na Marekani na Uingereza.
2. Nitaangalia na upya Mikataba yote ya Madini (Hapa nitakuwa Dikteta kidogo... Naweza kutumia ubabe kulazimisha kuanzia kipindi hicho walipe 45% kwa serikali badala ya haka wanachotoa sasa)
3. Nitatengeneza vipaumbele hivi;
(i) Upatikanaji wa Nishati ya Umeme - Makaa ya mawe Liganga na Mchuchuchuma (Nitauza 50% ya magari ya serikali na kufuta nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kupata fedha za kutekeleza mradi huu)
(ii) Nitafufua viwanda vitatu kwa awamu ya kwanza - Tanganyika Packers, UFI, na Kiwanda cha Baiskeli. (Nitafilisi mali za mafisadi wote kutekeleza mpango huu)
(iii) Nitaninia ndege 2 kubwa kwa ajili ya Shirika la ndege ATCL (Nitauza ndege ya Serikali na fedha nyingine za kuongezea nitatoa kwenye ile Account zinakorudishwa fedha za EPA)
4. Majukumu mengine ya Serikali yataendeshwa kwa kodi zinazokusanywa za kawaida, Baraza langu la Mawaziri litakuwa na mawaziri 16 tu (Pamoja na manaibu). Nafasi ya AG nitamteua Mhe.Mabere Marando na nafasi ya Takukuru itabadilishwa namna ya kumpata. Nafasi ya Jaji mkuu pia itaangaliwa upya namna ya Kupatikana kwake.

Orodha ya utekelezaji ni ndefu... Kwa leo inatosha muhimu nipeni kiti niwaonyeshe kwa Vitendo!.
 
mimi ningeanza na nape,nyonga uyu mtu alafu nyonga wote waliokua viongozi msimu wote wa JK,alafu ningemaliza na vasco mwenyewe ningemtundika msalabani akiwa hai juu yake nikaweka bango la dhaifu akabaki kuwa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo vijue kwamba tulishawahi kutawaliwa na kilaza
 
Kwa post hii nimegundua kuwa Baadhi ya Wana JF ama ni 'waoga kubuni namna ya kuitoa Tanzania hapa ilipo', ama ni 'Wavivu kuandia mawazo yao' au ni 'Wachoyo wa Idea'..
 
Ili 'nisiitwe dhaifu' ntatumia mbinu walizotumia watangulizi wa Jakaya,kuminya uhuru wa kujieleza hasa wa vyobo vya habari!
 
1. Ningeanza kwa kupiga marufuku siasa.. that means, no wasanii, no jumba la sanaa. Siasa imekuwa ni engo ya kuhalalisha ujinga na kupigia kura mambo ambayo yalitakiwa yafanyiwe tathmini ya kitaalamu based on reason. Transparency inaweza kuchukua nafasi ya domo-crazy, japo si mbaya kukawa na kamati za kuratibu mawazo ya wananchi ktk continuous basis na kupelekwa ktk decisio-making bodies.

2. Pili, ningewekeza ktk uendelezaji rasilimali ili ziiendeleze nchi, badala ya mfumo wa sasa kuwaachia wageni wachote maji masafi kwenye kisima chetu na kutuachia kikiwa kimekauka na kubakia matope. Serikali isiyokua na pesa ni serikali-suruwali, na katu haitoweza kuhudumia na kukidhi matarajio ya wananchi wake. Ukishakua na pesa, mambo mengi yataeza kuwa afforded na sekta karibu zote zitakuwa boosted kwa wakati mmoja.

3. Tatu, ningeimarisha ujuzi na elimu kwa wote. Watu wasio na ujuzi na maarifa ni mzigo mkubwa na aghalabu kupata maendeleo endelevu kwa kukosa kuona fursa zilizopo mbele yao. Kuchochea ujuzi na maarifa ndio siri ya ufanisi, creativity na individualism.

4. Muundo wa watawala utategemea merits(vyeo vya kuteuana marufuku maana ndio kitovu cha uzembe na kutowajibika), na mambo nyeti kama commitment za pesa, mikataba au rasilimali zitafanywa kwa uwazi na kisayansi.

5. All whistleblowers will be recognized kama mashujaa wa taifa.
 
Kaka umenifurahisha sana , kama ukiamua hata kugombea udiwani naomba unijulishe ni jim,bo gani nitakuja kukusaidia kampeni yako. Akili kama zako ndio tunazohitaji katika nji hii
 
Kaka umenifurahisha sana , kama ukiamua hata kugombea udiwani naomba unijulishe ni jim,bo gani nitakuja kukusaidia kampeni yako. Akili kama zako ndio tunazohitaji katika nji hii
Sasa huoni nikigombea nitakua nimejipinga hapo dondoo #1...?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom