Elections 2010 Mwana CCM Mwenzangu Usikipigie kura chama chetu kama...

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Mwana CCM Mwenzangu usikipigie kura chama Chetu na JK kwa ujumla kama hutapata Majibu ya maswali yafuatayo kabla ya tarehe 30 October 2010.
a) Kagoda ni nani na nani aliasisi wizi wa pesa pale BOT? Kwa nini mpaka sasa hajafikiswa
katika vyombo vya usalama?
b) Richmond ni nani? Na kwa nini hajakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria?
c) Nani alihusika na kusign mkataba wa kununua RADA ya taifa? kwa nini hajakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria?
d) Nini hasa chanzo za umasikini wa watanzania? Madini kibao, Mali asili usiseme, Utalii wa
kumwaga, sasa nini tatizo hapa?
e) Kwa nini Chama hakijachukua hatua kupitia mikataba yote ya madini na mali asili
zingine, kwani mikataba hii imeonekana na uwalakini mwingi tu?
f) Kwa nini Chama chetu kimeshindwa ku address suala la KILIMO? kwani tangu enzi za TANU na ASP tulisema KILIMO ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu?

g) Je unaridhika kwamba kauli mbiu ya KILIMO KWANZA kimekidhi haja kwa wananchi kuelekea mapinduzi ya kilimo cha kisasa?

h) Je Priorities ya Chama chetu katika uongozi wa nchi hii ni zipi? kama siyo ELIMU, AFYA na MAKAZI BORA basi usikichague chama chetu.

i) Je unaridhika na matumizi ya fedha zetu za umma? serikali yetu inatumia ipasavyo? Je bajeti ya serikali kila mwaka inamfikia mlengwa au inaishia huko huko juu kwa wenyewe?

j) Je Sera ya ardhi ya Chama chetu inakidhi kumlinda mwananchi wake? umeona wafugaji wanavyohangaika, wananchi walio karibu na migodi wanavyo nyanyaswa - Jibu ni kura yako

k) Je Chama chetu kina Sera nzuri juu ya walemavu kwa ujumla, wazee (Senior citizens) watoto na kina mama wajawazito? au ndiyo hizo Bajaji 400 kila mkoa kwa wajawazito?

Na mengine mengi tu, nduguyangu usifuate ushabiki utaumia, chagua KIONGOZI wa kukusaidia, nchi hii ni yako na wala si ya kikundi cha watu furani - usije ukajuta miaka mingine mitano ijayo - CHANGUA KIONGOZI BORA

Tunahitaji
a) Kurudisha uzalendo na heshima ya taifa letu
b) Misingi ya Utawala bora wa kisheria
c) Mali asili zote zirudi mikononi mwa wananchi wenyewe
d) Kufufua Viwanda na uzalishaji wa ndani
e) Kufufua mashirika ya Umaa yaliyokufa kama ATC, RELI, BANDARI na mengine mengi tu.

CHAGUA DR. SLAA..
 
Kwa kweli mtu atakayempigia kura Kikwete anayesema Lowasa ni msafi alisingiziwa, Mramba ana kesi ndo tu atashinda, Chenge ni msafi, Rostam Azizi (jangili mkuu wa uchumi wetu) ni msafi n.k sitamwelewa kabisa.
 
acha wewe mbona kama unatuponda cc tulishakunywa maji ya bendera hatukubali kumuuuliza mheshumiwa maswali magumu hayo!
 
kikwete anazunguka kuaga wananchi na nadhani 31.10.2010 ni kumtoa ikulu kabisa bila shida yoyote. Afungashe mapema, salma aache kuzunguka apaki kila kilicho chake
 
Back
Top Bottom