Mwamtafuta Mchungaji? Ni Mimi...

........Siogopi wala sijiumiumi nitawaambia ukweli, nyinyi ndio chimbuko la Matatizo ya Tanzania na Kikwazo cha Maendeleo ya Taifa letu..........
.....Kabla hamjaharibu sana, jiulizeni ni kitu gani mnachfanya ambacho kimemfanya Mchungaji aanze kuwaongelea tena!

SAFI,

Wakati wa kupigania Uhuru wa nchi za kusini mwa afriaca nadhani kulikuwa na wazalendo na wawajibikaji kwa manufaaa ya taifa letu, na baaada ya awamu ya kwanza kutoweka kwisha habari yao sijui waliingiliwa na mdudu gani?

Nadhani kuna madudu humo ndani "TISS" na kulindana kwa maovu yao ili yasije toka nje, Nchi hii jamani sio ya wote ni ya watu wachache mkae mkijua hilo.

Pili na uhakika ndani ya TISS kuna mparaganyiko mkubwa sana na hakuna mawasiliano mazuri kuna walio nunuliwa na hilo kundi la watu wachache na kuliongoza taifa na wale wasio nunulika na hawana nguvu wao wamo tu wame piga kimya huku wakiomba dua kwa Mungu mambo yalipuke na ndio watatuambia ni fulani na fulani waliokuwa mstari wa mbele kulipeleka taifa jinsi watakavyo.

Juzi nilikuwa na check USA White House Organization Chat yao duuuuuh security i mean swala la usalama kwao ni kitu cha msingi na kina kipaumbele kwa mfano taasisi kama DOJ inashirikiana vyema na DOD na DHS sasa hapa kwetu duuuh sijui hata kama izo taasisi zipo? na kama zipo basi ni za kisiri sana na zafanya kazi kwa matakwa ya kundi fulani la watu wachache.

tatu mkitaka nchi isonge mbele hapa ni lile wazo la Majimbo na ndipo hapo mtaona uongozi bora na uwajibikaji na ufanisi wa hizi taaasisi wawakirishi kutoka majimboni wakikutana kwa vikao maalumu watu hawatotaka mchezo bwana watakuwa wametumwa toka majimboni mwao na viongozi wengi watakuwa responsible kwa majimbo yao kwani wanajua wakichemsha tu there out.

Kwa uongozi huu wa ujumla kuwa waziri na watumishi wengine mwafanya kazi kwa pamoja ni kukanganyana tu hapa
 
Nimekuwa napokea subliminal messages kwa muda mrefu, makombora kwa muda mrefu watu wakihoji huyu Mchungaji ni nani, anajua nini, anapata wapi habari zake, lengo lake ni nini, anakaa wapi, anamipango gani ya baadaye kugombea na mengine mengi.

Basi nawarahisishia msiendelee kupasuka mishipa na kukosa usingizi, iwe ni nyie Mafisadi na Vibaraka wao, UWT, Vyama vya Siasa au wengine wachangiaji humu jukwaani.

Mimi ni Raia, Mzalendo, Mwananchi wa Tanzania. Nawasilisha nafasi ya Mtanzania aliyeko Kasulu, Mpanda, Geita, Micheweni, Mbinga, Mafia, Arusha Mjini, London, Washington, Dubai, Pretoria na sehemu nyingine nyingi.

Kama mwakilishi wa Wananchi hawa, nafanya kazi yangu kwa mapenzi ya nchi yangu, ni wajibu wangu, ni kiapo changu kulitumikia Taifa langu, kwa manufaa ya Taifa na Wananchi wake.

Mwaniogopea nini, wakati mimi ni mtu wa kawaida tuu?

Ni mwiba katika ngozi zenu, nondo inayokomaza zege la Taifa, Kungwi kwa chipukizi kama Jmushi, Swahiba kwa wazee kama Kibunango.

Makao yangu ni mtaani, kijiweni, magazetini, sehemu ambako mwananchi anakaa, mahali ambako mwananchi hulia kilio cha Uzazi, kwenye Rubisi, Chipsi Dume, Msokoto, Slipuwei, hata kwenye vikao vyenu vya Siri!

Sasa najiuliza mwanitafuta kwa shauri gani ikiwa in Raia wa Kawaida? NImefanya nini kilichozua shauku lenu kujua Mchungaji ni nani?

Upevu na Upeo wa mawazo asili na msingi wake ni Kifimbo, kisha machungu ya maisha na kuwa mkweli kwa nafsi yakafuatia. Wepesi wa kuunganisha nukta kwa kutazama kile kile tunachotazama wote, ni Baraka za Mungu, sina Dataz wala kianzio cha Dataz kama Mzee mwenzangu Kamanda Mkuu.

Je mwataka niwafundishe kazi haswa nyie wa Umoja wa Waangalizi? Niwafundisheni kipi ambacho hamkujifunza Malindi, Kurasini, Monduli au Ngerengere?

Nyinyi mmesomea fani, kwa jasho la Taifa, wengine ni vipawa tuu, na baraka za Mola ndio maana maoni na uchambuzi wetu, huwachuna ngozi na kuwafanya vihiyo.

Kwa mlio mafisi wagombea nyama, mwaeza endelea angamiza zizi, lakini hata ujanja wenu kupangusa midomo ardhini kufuta damu, hakusaidii. Mchungaji na wenzake wapembuzi hung'amua ulafi wenu na kuuanika.

Ombi langu kwenu wote mnaonitafuta, fanyeni kazi zenu kwa viapo ili Mchungaji na Kondoo waishi kwa Amani, wakila Asali na Maziwa manono ambayo ni halali na haki yao.

Kuendelea kutupuuza, kutawafanya muendelee kujichanganya mkimtafuta ni nani Mchungaji, ni rafiki wa nani, amejuaje, ana nia gani na maswali mengine kemkem ambayo mngejijibu kama msingekuwa Wazembe na Walafi na kutuumiza siye Wakulima na Wafanyakazi wa Tanzania. Fanyeni kazi zenu kwa Bidii, Juhudi na Maarifa kwa Manufaa ya Mchungaji na Kondoo, nanhyi mtaishi kwa Amani bila wasiwasi au woga.

La mwisho, Uchungaji wangu ni wito, binafsi si wa kuombwa na mtu. Mawazo yenu wengine kuwa kama nitakuja sarandia Miliki na Himaya zenu sahauni, ishini kwa amani kwenye viti vyenu, mimi kazi ya Uchungaji naipenda, nitaendelea kuchambua mchicha na kutoa makapi kwenye nafaka mpaka tupate zao bora na nono kutushibisha.

Jamani mi sijakuelewa, wewe ni mchungaji wa nini? Kondoo (the real kondoo), au mchungaji wa kondoo (Bible kondoo)? Please nielimishe kwanza maana sikuelewi......
 
Unakua kama humjui Shy bana... yaani ndo anakupa taabu ya kuandika yote haya?


Counter Info. And you know it very well unless otherwise you don't mean what you write.....and if it is encrypted...just cycle it....do not smart set.

And in this line of writing I do not know Shy......enh! whats up?
 
Bwa ha ha ha ..Hata mimi nilitaka kusema hivohivo ila nikaamua kum-sare.

Mhmh!!!!Sheikh tupe data.........what makes you ignore Shy's sentiments. At least a detailed one sentence, self explanatory b'se you read not to be a fun of word pools. Au niku-Sare???????? Au utetezi ulioweka kwenye signature unakulinda.......kwa kustahili au?

Lete data tupime uzito........
 
Mhmh!!!!Sheikh tupe data.........what makes you ignore Shy's sentiments. At least a detailed one sentence, self explanatory b'se you read not to be a fun of word pools. Au niku-Sare???????? Au utetezi ulioweka kwenye signature unakulinda.......kwa kustahili au?

Lete data tupime uzito........

Jamaa ni mwanasarakasi wetu hapa JF.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=c6qk1AFH9Y4[/ame]
 
TISS? My foot! What the hell is that? Ni kama Leyland au Bedford ya mwaka 47 itembeayo leo barabarani.
 
Tanzania imeingia katika Millenia mpya ambapo mabadiliko si ya Kiiuchumi pekee, bali hata ya kijamii na kisiasa. Lakini TISS bado wako kule kule kwa mwaka 1947!
 
Nilikuwa kama siamini macho yangu kwa kile nilichikuwa nakisoma. Pole sana Mchungaji, inaonekana hawa jamaa wa TISS wamekukera kupita maelezo. Ni vizuri kutoa dukuduku lako kama ulivyofanya. Nakubaliana nawe kabisaaaa...
 
Nasikia kuna muswada wauanzishwaji wa Balaza la Usalama wa Taifa. Huenda Balaza hilo litafanya mabadiliko ktk chombo hicho muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Wakati mwingine kuwashauri nini cha kufanya ni muhimu sana, na hasa kama watasikia na kuutumia vizuri ushauri huo
 
Mtu mwovu daima hukimbia kivuli chake, ndo maana wanakutafuta! Tutawafuata na kuwatangaza hadi kwenye paa za nyumba zao!
Keep it up!
 
It is about time Preacher! Hivi hilo kanisa lako linaitwaje vile maana naona liko tayari kupokea waumini wengi wa dini ya Uzalendo! Amen brother!
Kanisa lake linaitwa Tanzania na watu wa Tanzania. wote wanaotaka kukutafuta ni watu waoga sana maana huwa unasema ukweli kabisa. Mchungaji ni wa Kondoo sasa wanakutafutia nini?? Utaonana nao Mbinguni na sio Hapa kaa huko huko
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom