Mwamtafuta Mchungaji? Ni Mimi...

Your most welcome back reverand. Tuliku miss sana hapa. Njoo na hoja najua umekuja na vitu vipya toka huko ulikokuwa. Kimya kingi kina mshindo.
 
Mchungaji amekaa na kutafakari sana, anzia enzi za Mzee Sawaya, akaja sijui Sarakikya, Mzena, Kitine, Mahiga, Kombe, Apson na sasa Othman. Angalia mafunzo tuliyopata kutoka kwa CIA, FBI, MI5, MI6, KGB, Surete, Mossad, Shin Bet, BOSS, MSS, DGI-Cuba, Mukhabarat, ISI na kwingineko.

Leo miaka karibu 50 tangu tujitawale, TISS ni kama kichwa cha mwendawazimu, ni Taasisi inayoonyesha ama ni kuchanganyikiwa kwa hali ya juu au imeingiliwa kwa hali ya juu kiasi kuwa hata zile hekaya za kusema walikuwa wakiwabana Makaburu zinaonekana kichekesho!

Nasikitika kusema kuwa katika historia yenu, jambo la maana mlilowahi kufanya na kulipa Taifa letu sifa ni mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika pekee, mengine yote mliyoyafanya ni batili, tupu na bure!

Kama kweli mngekuwa ni chombo makini, basi leo hii Tanzania ingekuwa Taifa kubwa linalojitegemea, lenye uwezo wa kujitosheleza, lenye viongozi wanaojiamini na Watanzania wenye kujiamini, kujituma na Uzalendo wa kweli kwa Taifa!

Mnachekesha sana mnapokazana kutafuta nani kasema nini kuhusu Kiongozi fulani au kuanza kusaili viongozi na wanasiasa nia zao za kuanzisha vyama au kuwa ndani ya siasa. Zaidi mmechekesha pale mlipoanza kuhoji nia ya Watanzania kuchangishana na kuwasaidia waliopata maafa huko Kilosa!

Lakini tatizo langu na nyie si huku kufuatanafuatana kama wajinga na kutaka kujua Mchungaji anakaa wapi au anafananaje.

Tatizo langu ni kuwa nyinyi kama Taasisi pekee iliyokuwa na uwezo mkubwa kuliko nyingine Tanzania kifedha, kiufanisi, kiutendaji na uwezo wa kuwa na nyenzo nyingi, mmeshindwa kulisaidia Taifa letu likaweza kupiga hatua mbele, na badala yake mnafurahia karaha na watu kutaabika.

Je ni vipande vingapi vya fedha mmenunuliwa?

Iweje wakati wa vita vya ukombozzi mliweza kufuatilia kila aina ya uhujumu ambao ulipangwa na Kaburu na Mkowezi Ian Smith, lakini leo mnaifagilia Richmond, EPA, Rites. Rada na hata kina Barrick?

NI vipi leo Taifa letu kila mara linakutwa mguu pande katika mambo mengi ya maana ya kijamii, kisiasa na kiuchumi lakini mlikuwa tayari kupeleka timu nzima Uingereza kumkamata Ze Utamu au kukasirika mliposikia tetesi eti kuna mtu ana picha za Rais akiwa Uchi?

Utaalamu na Ukali wenu mbona ni butu pale Taifa letu linapoendelea kunyonywa na kunyanyaswa na Ukoloni mamboleo na Ubepari Uchwara?

Je nanyi mko njia panda baada ya Azimio la Zanzibar na Mageuzi kuwa hamjui wajibu wenu au ni upande gani muelekee?

Je mnahitaji watu na damu mpya ya kuwapa mawazo mapya na mipango mipya na kufanya msukwe upya ili Tanzania iweze kupiga hatua mbele?

Ikiwa leo hii, kila mtu anaogopa TISS, kisa watakufanyia kitu mbaya au utasota milele, je kweli nyinyi wajibu wenu ni Kumlinda na Kumtumikia Mtanzania au ni chombo cha kuwanyanyasa Watanzania?

Mmejisahau vipi baada ya kuvunjika kwa vita baridi kuwa mpaka leo mmeshindwa kufanya mapinduzi ya ndani na kuleta mabadiliko hata katia mfumo wetu uchwara wa kibepari?

Mchezo wa kufuatilia watu kisa wameongea jambo fulani ambalo hamlipendi ni kitu cha kizamani. Mambo ya kutisha watu, tena wa nchi yenu yamepitwa na wakati!

Tanzania ya leo inahitaji kuwa na chombo kama TISS kinachojua wajibu wake kwa manufaa ya Taifa na si Chama au mtu mmoja. Kiapo chenu (niliwahi kuwauliza mwaka jana au juzi mnaapaje) ni kwa ajili ya Katiba ya Tanzania na si Chama, Kabila, Jinsia, Dini au tabaka la kimapato.

Siogopi wala sijiumiumi nitawaambia ukweli, nyinyi ndio chimbuko la Matatizo ya Tanzania na Kikwazo cha Maendeleo ya Taifa letu.

Mkitaka majadiliano, tuendelee nitumieni maswali yenu rev.kishoka@jamiiforums.com au yaulizeni hapa nitayajibu na kuwapasha namna mpya ya kujifua na kuweza kubadilisha sura ya Taifa letu, tukarudi kwenye ile hadhi tuliyokuwa nayo wakati wa Ukombozi Kusini mwa Afrika.

Kabla hamjaharibu sana, jiulizeni ni kitu gani mnachfanya ambacho kimemfanya Mchungaji aanze kuwaongelea tena!
 
Bravo Reverend,Big Up! Hawa jamaa wamefulia kishenzi,Hawana lolote kwani kazi wanarithishana kama utemi wa urambo!Wametutia hasara na hasira isiyo kifani! Nchi inayumba yumba ni kwa sababu mfumo wetu wa kuwaanda viongozi ni kero tupu.Hawa jamaa hawana la kujivunia ndani ya nchi hii zaidi ya kuwatisha na kuwasuka suka raia waso na hatia.

Wameyasoma ila ndo hawabadiliki kwani mabadiliko kwao ni mwiko!!
 
Mchungaji waambie ukweli wao, kazi wanayoifanya sasa hivi hao TISS inatia kichefuchefu, wamekalia kuwalinda tu viongozi na watuhumiwa wa ufisadi ndo kazi wanyoijua. TISS ya sasa hivi imejaa vibaraka wa viongozi tena wale wasojua kazi, wanaacha kufanya kazi za wananchi kama walivoapa,wamelaaniwa!
 
naamini kinachotafuna nchi ni hii kule SERIKALI kujiona kua ina chama, na chama chake ni CCM, hili ndilo kosa linalotutafuna kila siku, ni hadi pale itakapowaingia watendaji wa Serikali kua Chama huunda serikali na si serikali kuunda chama. tukiliweza hili Rev. Kishoka tutaweza kusonga mbele.

Tatizo hilo ndilo linalowatafuna TISS, TAKUKURU, POLICE, MAHAKAMA na ofisi zingine za UMMA, wao wanadhani kufa kwa CCM ni kufa kwa serikali .
 
Personally nilikuwa nikiwaheshimu sana hawa jamaa,lakini nimegundua ni wakatishaji tamaa tu,hawana ishu.

Hata amani iliyopo si kwa sababu hawa jamaa wanapiga kazi ila ni nature tu ya passiveness tuliyonayo watanzania.Hawa jamaa wangekuwa wanapiga kazi,wangelimulika swala dogo tu la manesi kuwaua wake zetu wajawazito miaka nenda rudi (mpaka wagosi wanatungia nyimbo), Matraffic wanakula rushwa miaka nenda rudi, mpaka jerry Muro alione hilo.Au ndo mnataka kutuambia mnadeal na mambo makubwa yanayohusu nchi yetu,hivi hizi kashfa kama za EPA, MEREMETA, BOT, RICHMOND ziko nje ya majukumu yenu kikazi!?

Maana mnaonyesha weakness kila eneo eg.kuruhusu rais wetu mstaafu apigwe kofi na kijana hasiye hata training ya mgambo(hamna utetezi kwenye hilo).Huku mtaani utasikia tetesi "ah! jamaa usalama yule usimuone vile", misifa kibaoo alafu nchi inaangamia kwenye lindi la umaskini,wasomali wengi wanaishi bila kibali nchini, wanyarwanda na wahindi ndo usiseme,matukio ya kutisha kila kukicha, majambazi wameshika hatamu.

FANYENI KAZI BWANA MNALIPWA KWA KODI ZETU, hatukatai hata failures zipo lakini si kwenye vitu vya mda mrefu kama RUSHWA.
 
Big Up Rev. Kishoka. Ila si unajua wana serve interest za nani?? Hawana sauti hawa, they are dependent not independent. Hii ni Tz bwana, unaweza pata uenda wazimu kama ukijaribu kuchimba mambo mengi maana kila kitu kiko wazi lakini unasikia dana dana tu. Shame.
 
Mchungaji amekaa na kutafakari sana, anzia enzi za Mzee Sawaya, akaja sijui Sarakikya, Mzena, Kitine, Mahiga, Kombe, Apson na sasa Othman. Angalia mafunzo tuliyopata kutoka kwa CIA, FBI, MI5, MI6, KGB, Surete, Mossad, Shin Bet, BOSS, MSS, DGI-Cuba, Mukhabarat, ISI na kwingineko.

Leo miaka karibu 50 tangu tujitawale, TISS ni kama kichwa cha mwendawazimu, ni Taasisi inayoonyesha ama ni kuchanganyikiwa kwa hali ya juu au imeingiliwa kwa hali ya juu kiasi kuwa hata zile hekaya za kusema walikuwa wakiwabana Makaburu zinaonekana kichekesho!

Nasikitika kusema kuwa katika historia yenu, jambo la maana mlilowahi kufanya na kulipa Taifa letu sifa ni mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika pekee, mengine yote mliyoyafanya ni batili, tupu na bure!

Kama kweli mngekuwa ni chombo makini, basi leo hii Tanzania ingekuwa Taifa kubwa linalojitegemea, lenye uwezo wa kujitosheleza, lenye viongozi wanaojiamini na Watanzania wenye kujiamini, kujituma na Uzalendo wa kweli kwa Taifa!

Mnachekesha sana mnapokazana kutafuta nani kasema nini kuhusu Kiongozi fulani au kuanza kusaili viongozi na wanasiasa nia zao za kuanzisha vyama au kuwa ndani ya siasa. Zaidi mmechekesha pale mlipoanza kuhoji nia ya Watanzania kuchangishana na kuwasaidia waliopata maafa huko Kilosa!

Lakini tatizo langu na nyie si huku kufuatanafuatana kama wajinga na kutaka kujua Mchungaji anakaa wapi au anafananaje.

Tatizo langu ni kuwa nyinyi kama Taasisi pekee iliyokuwa na uwezo mkubwa kuliko nyingine Tanzania kifedha, kiufanisi, kiutendaji na uwezo wa kuwa na nyenzo nyingi, mmeshindwa kulisaidia Taifa letu likaweza kupiga hatua mbele, na badala yake mnafurahia karaha na watu kutaabika.

Je ni vipande vingapi vya fedha mmenunuliwa?

Iweje wakati wa vita vya ukombozzi mliweza kufuatilia kila aina ya uhujumu ambao ulipangwa na Kaburu na Mkowezi Ian Smith, lakini leo mnaifagilia Richmond, EPA, Rites. Rada na hata kina Barrick?

NI vipi leo Taifa letu kila mara linakutwa mguu pande katika mambo mengi ya maana ya kijamii, kisiasa na kiuchumi lakini mlikuwa tayari kupeleka timu nzima Uingereza kumkamata Ze Utamu au kukasirika mliposikia tetesi eti kuna mtu ana picha za Rais akiwa Uchi?

Utaalamu na Ukali wenu mbona ni butu pale Taifa letu linapoendelea kunyonywa na kunyanyaswa na Ukoloni mamboleo na Ubepari Uchwara?

Je nanyi mko njia panda baada ya Azimio la Zanzibar na Mageuzi kuwa hamjui wajibu wenu au ni upande gani muelekee?

Je mnahitaji watu na damu mpya ya kuwapa mawazo mapya na mipango mipya na kufanya msukwe upya ili Tanzania iweze kupiga hatua mbele?

Ikiwa leo hii, kila mtu anaogopa TISS, kisa watakufanyia kitu mbaya au utasota milele, je kweli nyinyi wajibu wenu ni Kumlinda na Kumtumikia Mtanzania au ni chombo cha kuwanyanyasa Watanzania?

Mmejisahau vipi baada ya kuvunjika kwa vita baridi kuwa mpaka leo mmeshindwa kufanya mapinduzi ya ndani na kuleta mabadiliko hata katia mfumo wetu uchwara wa kibepari?

Mchezo wa kufuatilia watu kisa wameongea jambo fulani ambalo hamlipendi ni kitu cha kizamani. Mambo ya kutisha watu, tena wa nchi yenu yamepitwa na wakati!

Tanzania ya leo inahitaji kuwa na chombo kama TISS kinachojua wajibu wake kwa manufaa ya Taifa na si Chama au mtu mmoja. Kiapo chenu (niliwahi kuwauliza mwaka jana au juzi mnaapaje) ni kwa ajili ya Katiba ya Tanzania na si Chama, Kabila, Jinsia, Dini au tabaka la kimapato.

Siogopi wala sijiumiumi nitawaambia ukweli, nyinyi ndio chimbuko la Matatizo ya Tanzania na Kikwazo cha Maendeleo ya Taifa letu.

Mkitaka majadiliano, tuendelee nitumieni maswali yenu rev.kishoka@jamiiforums.com au yaulizeni hapa nitayajibu na kuwapasha namna mpya ya kujifua na kuweza kubadilisha sura ya Taifa letu, tukarudi kwenye ile hadhi tuliyokuwa nayo wakati wa Ukombozi Kusini mwa Afrika.

Kabla hamjaharibu sana, jiulizeni ni kitu gani mnachfanya ambacho kimemfanya Mchungaji aanze kuwaongelea tena!

NIMEAMINI WEWE KWELI NI MCHUNGAJI...........MAANA POINT TUPU MPAKA KWENYE VIUNGANISHI KUNA POINT NZITO.

YAANI TISS...NI MUHIMILI MKUBWA SANA WA MAFANIKIO YA ADUI ZETU. HAWA SIYO TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICES TENA....HAWA NI TANZANIA IGNORANCE AND SELFISHNESS SERVICES.

Wanafanya kazi kama robot wa mafisadi. TISS wa nyerere wameshazeeka na ndo walikuwa bomba.....kuna hawa walioanzia kwa mwinyi na kazi zao mnazikumbuka....Kazi ni kuzima mapinduzi ya kweli ya maendeleo ya mtanzania na kuendelea kujenga vitambi vya mafisadi na kuvilinda kwa gharama zozote.
 
Rev. Kishoka,

Umeusoma Muswada wa Sheria ya kuundwa kwa Baraza la Usalama wa Taifa? (sina jina sahihi na kamili ya muswada huo hapa nilipo). Umejadiliwa na Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba wiki hii inayomalizika.

JJ
 
John hebu tunyetishie kama wewe umewahi kuusoma
 
Heshima kwako Mchg,

Umemaliza kila kitu hawa jamaa bado wanafanyakazi utadhani tuko kwenye vita baridi.

TISS wangekuwa makini mikataba yote mibovu ya madini isingekuwepo.Mashirika ya kijasusi ya nchi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo yamejikita zaidi kulinda uchumi wa nchi lakini hapa kwetu hilo halifanyiki kabisa.

TISS yetu ipo kwaajili ya interest ya viongozi waliopo madarakani tu hawana habari na maslahi ya taifa.
 
TISS ni product ya Nyerere!Ilikuwa ni kumlinda yeye na chama tawala,ambapo mpaka sasa ni kuhakikisha SISIEM inakuwa madarakani mpaka mwisho wa dunia.Good ya free media tuna weza kudiscuss hapa. Nafikiri tungekuwa na details zetu hapa,tungefuatiliwa bongo kama mchezo.

Ndio maana kila mtu mwenye akili timamu, anajua mashirika kama PPF, pesa zilivyokuwa zinachotwa na kuifund CCM,hata tangu enzi za Nyerere. Tuna RC, DED, Wabunge ambao at one time walikuwa wameandikwa kwenye taasisi hii.

Tangu enzi ya Tanu,mtu aliyeonyesha kutoa mawazo na Nyerere,alipata cha mtema kuni.walikuwa wamejaa,hata walimu wakuu wa secondary.

Sasa hivi wako waaina mbili.
1.wale wanaofanya kazi za kawaida,still wanaspy wapinzani.lakini ni hopeless sasa.
walikuwa wanapata scholarship kwenda india,australia etc
2.walinzi wa viongozi.hawa ni elite,wanakula perdiem tu.kama waziri,rais anakwenda ulaya wanaandamana na msafara.kupata hii fursa lazima ujuane na mkuu,ukabila na udini upo hapa.
 
Mimi nilidhani taasisi hii ilikufa na mwenyewe Kambarage!
kumbe ipo na inapiga mzigo kinyume nyume!
Daaah hapa timekwisha kabisaaaaaaa.
 
Rev. Kishoka,

Umeusoma Muswada wa Sheria ya kuundwa kwa Baraza la Usalama wa Taifa? (sina jina sahihi na kamili ya muswada huo hapa nilipo). Umejadiliwa na Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba wiki hii inayomalizika.

JJ

Mkuu Kiongozi tuongoze japo kidogo kwenye huo muswaada basi??
 
rev. Kishoka,

umeusoma muswada wa sheria ya kuundwa kwa baraza la usalama wa taifa? (sina jina sahihi na kamili ya muswada huo hapa nilipo). Umejadiliwa na kamati ya bunge ya sheria na katiba wiki hii inayomalizika.

Jj

rev kishoka anapotosha ummah kwa makusudi bila kusoma , rev kishoka soma kwanza ndio uwe unatoa baadhi ya mada na sio kupootosha kama unavyojaribu kufanya sasa , tiss iko imara na itaendelea kuwa imara kama uhai wa taifa ulivyo imara - ole wenu mnaotaka kupeleka jamii hii ambapo sipo
 
Hizi ndo naziita siasa za enzi za Zinjanthropus, ubishi usio na point. Uimara wa TISS uko wapi....au unaongelea tiss kama ulivyoandika. Lakini kama unazungumzia TISS unataka Rev asome kitu gani...hizo saviet paper zinazoandikwa na kunawia mikono na kutupwa jalalani kila siku? Tangu lini uimara ukawa kwenye muswada wakati sheria ya Usalama wa Taifa yenyewe tu tangu iwepo haijawai kufanyiwa kazi kwa manufaa ya Umma wa watanzania.

Whe Shy inabidi uone Shy..... Ole wake nani ...Rev au wewe unayepotosha kwa kusema TISS iko imara...au ndo mana Kikwete kapigwa changa la macho, Mwinyi kapigwa Kereb, EPA, Richmond, TANESCO, TRL, ATCL, Mererani, BOT Scandals, Kuvuja kwa habari nyeti za serikali maana nyingine unakutana nazo baa jamaa wanafukuzia inzi..........yako mengi tu halafu unasema wako Imara.

Na hiyo Ole yako inamaanisha nini...kwamba tuanze kutaja majina ya maelfu ya watu hodari watetezi wa Taifa hili waliopotezwa na TISS??????

Hivi unapomshikia mtu bunduki na kumwamuru anyoshe mikono juu wakati yeye akiwa hana silaha, hivi kati ya wewe na yeye nani anaogopwa. Weka bunduki chini basi tuone.

TISS hii ya sasa hii.......UUUUUUUUUUUUPS!!!!!!!
 
Wakuu,

Taratibu la sivyo hii post itafungwa sasa hivi!!!!

Tiba
 
Unakua kama humjui Shy bana... yaani ndo anakupa taabu ya kuandika yote haya?
 
Back
Top Bottom