Mwamko wa Kuikimbia CCM: CDM inaachwa nyuma...wakati CCM wanajipanga?

maneno machache ya kamanda Sun Tzu kwenye kitabu The Art of War yawe mchango wangu na naomba kunukuu:
Strategy without tactics is the slowest route to victory.Tactics without strategy is the noise before defeat
Kwa muktadha huo hapo juu CDM inahitaji:
KUJITOA NA KUJIKANA kwa wanachama na wapenzi wa mageuzi/mapinduzi
UONGOZI MADHUBUTI kuanzia nyumba kumi hadi taifa
MIKAKATI
MBINU
 
Hakika, tabaka kubwa la wanyonge ndio fimbo ya kuichapia ccm, unyonge wa watanzania ukiwa bega kwa bega na ukwasi wa wachache, umejenga kisasi kikubwa kwa wananchi, ndiyo silaha tosha kabisa kuiondoa ccm madarakani. Chdm inaweza kutumia hii, na itakuwa kama kumsukuma mlevi tu kuingusha ccm.
Swali....
Unyonge huu wa waliowengi unaweza kuondoshwa kwa sera zipi? Chadema wanazo sera hizo? Wanaziishi? Au hadi tuwape madaraka? Kweli tunaweza kumuhadi mnyonge huyu wa tanzania, kuwa tutamuwezesha awe kama Mengi, itamuingia akilini?
Niliwahi kuja na Thread " Natamani Dr. Slaa aje aniambie haya!" sijui mods walikoipeleka! Lengo kuu lilikuwa kumuuliza Dr. Slaa, ni kwa namna gani atazifafanisha hali za raia wake akiingia madarakani? Aishie Manzese hujawa na chuki na kinyongo apitapo Osterbay, haijalishi waishio humo ni fisadi ama laa, anajiuliza ni haki gani ndani ya taifa moja impayo mmoja kumiliki mikate kumi, hali mwingine hana hata mmoja?
Huo ndio UNYONGE wa watanzania walio wengi mbele ya wachache. Ccm imeridhika nao, hawaoneshi nia ya kuondoa unyonge huu. Chadema mnajipanga vip? Watanzania wamechoka kusikia habari kuwa tutawekeza hapa na pale kumnyanyua mnyonge, wanataka kusikia waliojikweza watashushwa vipi ili tuanze hatua sawa! Tusidanganyane kukimbizia nyuma, hali nao wanakimbia kuliko!
Mungu wetu anaita!
 
Nadhani watu bado wanacheza pembezoni mwa hoja yangu; labda niulize hivi:

Mmeona maelfu ya watu wanaandamana, au kuja kwenye mikutano ya hadhara; wapo wanaochanga hata fedha na wamehamasika kabisa katika kile kinachoitwa 'nguvu ya umma'. kwa miaka hii karibu mitatu ya hizi operesheni ni lini mmesikia kesho yake watu wamekusanyika kwenda kujenga shule, kuchimba vyoo, cliniki, kutengeneza barabara, au hata kujitolea kufundisha kisomo cha elimu ya watu wazima? Au nguvu ya umma iko kwenye sauti na kunyosha mikono juu na siyo katika kutenda? Au watu wanafurahia kuona matawi yanafunguliwa na kadi zinatolewa?

Nitatumia mmojawapo wa mifano mizuri tu ambayo inajulikana kwenye pande zote za dini. Mtu akiamua kusilimu kwa mfano, haitoshi tu kusema amesilimu halafu basi. Kusilimu kunaendana na kutenda kama Muislamu safi. Inahusiana na ibada, kujifunza zaidi juu ya Uislamu na hata kujitolea (sadakat na zakat). Sasa, mtu akishawishiwa na baadaye akaingia katika Uislamu akaamini kabisa anataarjiwa kuonesha imani hiyo kwa vitendo vile vile siyo tu kusema Shahda lakini akaendelea tu. Well, anaweza kuwa ni Muislamu lakini hatakuwa hashiki dini.

Hili ni kweli hata kwa Wakristu. Mtu anapokata shauri kuokoka au kuingia ukatoliki anatarajiwa kuonesha kuwa ameamua kweli kuingia imani hiyo. Haitoshi kwa mtu huyo kusema "nampokea Yesu" au "Namkataa Shetani" lakini bado akaendelea na mambo yake kama zamani. Lakini zaidi ni jinsi gani mtu huyo anaweza kuhamasishwa kushiriki katika shughuli za kujenga dini au imani. Mfano mzuri mmemuona yule Masanja Mkandamizaji ambaye nasikia kaokoka siku hizi. Well, watu wa kanisa lake wanamtumia vizuri sana kueneza dini.

Sasa kwa pande zote mbili kueneza dini (iwe Uislamu au Ukristu) kwa aliyeongoka ni jambo linalokuja lenyewe. Vivyo kwa mtu aliyeingia CDM; yeye kuimba sifa za CDM ni jambo kawaida na la msingi lakini kuna zaidi ya kuimba sifa za chama. Kuna kutenda.

Sitaki kuwakumbusha TANU ilivyojengwa kwa kutumia 'nguvu ya umma'. leo hii CDM iko kama TANU isipokuwa kitu kimoja....
 
Je CDM inayo miundo mbinu ya kutosha na ya kisasa... Ukiangalia wizara wote ambazo watu wake wamebadilishwa zote zimewekwa makada wa chama cha Mapinduzi kwa kile ambacho nakiita ni 'strategic preparation before war". Ni sawasawa na vikosi vya majeshi vinavyo amass kwenye eneo kabla ya kuleta mashambulizi.

Come on mwana kijiji, strategic preparation for war!!! Wasingemuweka Hawa Ghasia awe waziri wa Tamisemi. She is such a non-perfomer. CCM haijajipanga kabisa.
 
Back
Top Bottom