Mwamko wa Kuikimbia CCM: CDM inaachwa nyuma...wakati CCM wanajipanga?

Kamanda,Tumaini Makene...hakika nimekukubali! yaani nimesoma coment yako hapo juu na nikakiri
kuwa kweli CDM wanavichwa makini. Kama usemayo hapo juu ni ya kweli,basi CDM ni chama makini
na kina viongozi makini...All the best mikoa ya kusini
 
Tumaini, Arumeru mashariki ni mfano wa hali ilivyowilaya zote nchini au inawakilisha kama asilimia ngapi ya hali ilivyo?

Mzee Mwanakijiji Nakuhakikishia Kabisa hata leo ukifanyika Uchaguzi wa Ubunge Jimbo ambalo CCM alishinda kwa Kishindo 2010 Ataaibika. CCM haipendwi Mpaka na Vitoto Mzee Mwanakijiji, CCM inazungumzwa Vibaya Kila kona na Uzuri People are talking About CCM as entity na si Kingine. Imefikia Wakati sasa Mtu akishabika CCM anakuwa ni Adui na Hakuna tena watu siku wanashabikia CCM kwa Uhuru kama ilivyo zamani. Ukiona Watu wanaimba sifa za CCM ujue hapo kuna Ulinzi wa Vyombo vya Dola. Mwanakijiji kama Huamini Ukienda Tanzania Tafuta Daladala lolote at randomly panda halafu anza kuisifia CCM hakika UTASHUSHWA. CCM haipendwi, Watu wameshagundua kwamba CCM imewanyonya sana.

Kinachotakiwa Kwa Sasa ni Wanannchi waendelee Kukombolewa KICHWANI Basi. Kifo cha CCM NAKIONA KABISA
 
HAYA yanayotokea sasa endapo hayawekewi mikakati basi CDM wasitarajie kwamba yatakuwa na effect kubwa sana kwa CCM kwa strength ile ile inayoonekana wakati wa raia kurudisha kadi za CCM!! Watanzania ni watu wa kukimbilia matukio! Ulitaka kufahamu silika ya Tanzania subiri uone mbio za mwenge...manake mtu unaweza kujiuliza wanaenda kuangalia nini hasa cha maana!! Ukitaka kufahamu silika ya watanzania subiri ajali itokee uone watakavyokimbilia...hiyo ndiyo silika yetu!! Sisi ni watu wa matukio! Tuko easily affected na mob psychology!! Nafahamu watu watapinga hili....!! Lakini ngoja usikie uongozi wa juu wa CCM unapita kulekule walikopita CDM uone wimbi la Watanzania kurudisha kadi za vyama vya upinzani!! Sisi, ndo watanzania bhana, watu wa matukio! Hebu jaribu kukumbuka jinsi ambavyo tuliathiriwa na tukio la Babu wa Loliondo!!!!!

Hivyo basi, nakubaliana na Mwanakijiji kwa 100% kwamba, endapo CHADEMA wasipojipanga na kuridhika kwamba tayari wananchi wameikataa CCM, then NET RESULT haitakuwa sawa na haya yanayotokea sasa!!

Watanzania hawajaanza leo kurudisha kadi za CCM!! Salama ya CHADEMA ni kuwa na matawi hadi mashina yalyoota mizizi ili wawe watetezi wao hapo baadae! Wakati utafika ambao kila kiongozi wa kitaifa atalazimika kupigania nafasi yake!! Zitto atalazimika kujikita zaidi KGM, Mnyika atajikita Ubungo, na wengine sehemu zao kama hao!! Kule walikoikataa CCM sasa watabaki yatima wakati CCM wapo na wajumbe kumi wao! Ofisi zao zitawepo! Weneyeviti wao watakuwepo! Makada wao watakuwepo!

Labda mbadala wa CDM ni kuomba viongozi wa CCM nao waingiwe kiwewe na kuanza kuhamahama hovyo hovyo kiasi cha kusababisha chama kukosa mwelekeo! Otherwise, still CDM has a long way to go!
 
Tumaini, Arumeru mashariki ni mfano wa hali ilivyowilaya zote nchini au inawakilisha kama asilimia ngapi ya hali ilivyo?

Asante MM, nakubaliana na swali lako, Naunga mkono kabisa kuwa Arumeru Mashariki ilidhihirisha kuwa upinzani hata mashambani unakubalika na wanaNchi wameamua kuiondoa ccm madarakani kwa namna yoyote ile, lakini Arumeru SIO true reflection ya maeneo mengi ya Tanzania, na Viongozi wangu CDM tusitumie matokeo ya Arumeru kimakosa, kwa kweli tunahitaji kuwa makini kwani matokeo ya Arumeru yanaweza kuwa chanchu ya kwa maeneo mengine Lakini sio uhalisia wa mambo.

Mkuu Tumaini ulipotoa mfano wa Arumeru hata mm nilishtuka, kwani najua sio hali ilivyo katika maeneo mengi ya nchi yetu. Kumbuka Arumeru Chama chote kilikuwa pale, makada na watu wazito kweli walikuwa wanasaidia... ndio maana tulishuhudia tuliyoyaona wakati ule.... JE CDM ina ubavu wa kumantain hii pace kwenye majimbo mengine na kuhakikisha ushindi unapatikana kama wa Urumeru, jibu liko wazi si Rahisi ila inawezekana kukiwa na mpango madhubuti

Mkuu Makene, umejenga hoja kutuaminisha kuwa kazi inafanyika, well, lakini tuonavyo si ya kiwango ambacho wananchi wanavyokichukia Chama Cha Mapinduzi. Bado kazi inahitajika kufanyika tena kubwa sana.... Operesheni kama za Sangara kwa kanda ya Kusini ni mfano wa mafanikio tuliyoyarecodi... that move should be maintained hasa kuongeza structrures vijijini. Inaogopesha kusikia watu wamekosa kadi, bendera kwa chama kilicho makini kama CDM. Juzi juzi tu kuna mdau alikuja hapa jamvini akiomba kuwezeshwa kadi na bendera kule Mwanga... alishia kuambulia kadi 50 na bendera sijui ngapi... na akishia kuaibika mbele ya waliokuwa wakivihitaji

KAZI ILIYOPO MBELE YETU SI RAHISI KAMA TUNAVYOFIKIRI, NI NGUMU NA INAHITAJI UMAKINI WA HALI YA JUU
 
Kitu kimoja ambacho kiko dhahiri pia ni kwamba, hakuna namna sasa hivi CCM wanaweza kushawishi umma kwa hizi services rahisi rahisi wanazofanya kama sehemu ya mikakati wanayofikiri inaweza kuwafanya watu wageuke nyuma. Nani anataka kuwa jiwe?

Mathalani kama CCM kingekuwa chama makini kinachotaka kuwaaminisha watu kuwa walau bado kina mishipa michache iliyobakia kati mingi iliyokwisha kufa kuweza kuhisi/kusumbuliwa na mahitaji ya watu, mtu kama Ngeleja anapata wapi authority ya kuandaliwa mapokezi makubwa na chama hicho hicho ambacho kimetoka kusema kuwa hafai kutokana na ubadhirifu. Yaani katika tuhuma ambazo serikali ya CCM imelazimika kula matapishi yake, Ngeleja na wenzake wengi, waliotoka na waliobaki, amefanya jambo gani la kishujaa?

Chama makini kinadiriki vipi kuendelea kuwa na wanachama ambao tayari chenyewe kimeridhika kuwa ni wabadhirifu. Kinaruhusu vipi watendaji walioko kwenye serikali yake kuendelea kutamba kwenye nafasi zao watakavyo wkati wanatembea na tuhuma, wengine za kutishia uhai wa taifa hili (mathalani kuruhusu bidhaa za hovyo kupitia TBS).

Hivi chama kinachotaka kuonekana ni makini kinapata wapi uso usio haya wa kuiachia serikali inatupilia mbali maamuzi 23 ya bunge ambayo yalitakiwa kusaidia kufagia uozo serikalini kwa manufaa ya umma. Udhaifu huu unaovuka mipaka hauwezi kusaidiwa kufichwa kwa kubadili mawaziri na kuweka makada na kubadili Sekretarieti inayotokana na watu wale wale...from the same pool. Let them wait for the dawanfall.

It is just a drop of iceberg in the ocean. Lakini inaonesha kuwa kila wakati ambapo CCM wanataka/wanafikiri wamefanya masahihisho ya kitu fulani kisha ijipange kuanza kushambulia inajikuta imefanya makosa mengine makubwa zaidi ambayo yanazidi kualika na kuruhusu mashambulizi ya maana.

Kwenye hali kama waliyonayo CCM sasa ambapo "the centre cannot hold" (Shairi tamu la The Second Coming la William Butler), ni vigumu ku-launch mashambulizi yeyote yenye maana zaidi ya kufanya propaganda nyepesi na kushindwa kuwatumikia wananchi.

Lakini worse enough ikiwa ni moja ya dalili ya wazi ya anguko ambalo haliwezi kuzuiwa kwa any meaningful counterattack, katika hali hiyo ya "the center cannot hold any more", usitegemee kuwa CCM inaweza kufanya lolote la maana katika kuwatumikia wananchi, kwa sababu kila fursa ambayo imekuja miguuni mwao, wameshindwa kuinua mguu na kusukuma...the center cannot hold anymore.

Kitu cha muhimu hatuwezi kuruhusu dawanfall ya CCM iende pamoja na nchi yetu. Ndiyo maana tunajua hatua gani inafuata kila baada ya hatua moja katika mapambano haya. Hatutaki wananchi waseme bora zimwi likujualo...hatutaki wananchi wageuke nyuma, wakumbuke mabakuli ya nyama huko Misri wakati tuko safarini kwenda nchi ya ahadi (mfano tu).
 
Mengi yamesemwa lakini muhimu linabakia kuwa CDM inanufaika na wimbi la watanzania wengi kuichukia CCM, na sio kwa sababu watu wanaipenda (na hata kuchukua jitihada ya kuifahamu) CDM.

Chuki ya CCM inasababisha watu waende CDM, sio kwa sababu wanakipenda CDM au kuwa ni chama 'perfect' ila ni chama pekee ambacho wanaona kitaleta changamoto wa CCM. Cha ajabu CDM imelewa na wimbi hili la kukimbiliwa na haifanyi lolote kubadirisha kuwa chama kinachoaminika kitaifa. Kama CCM hawatarudisha mvuto, na CDM kuendelea na ulevi huu, itakuwa rahisi sana kama kitatokea chama kingine chenye sura ya kitaifa kikanufaika na mtaji huu wa wanachama ambao CDM imefanikiwa kuwahasamisha.
 
CCM haiwezi kujipnga milele kwa sababu kila kukicha wanaibuka na layman solution.
WanaCCM 800 wanaporudisha kadi na kujiunga na CDM, Nape anaibuka na kusema hao waliohamia CDM walikua ni mzigo kwenye chama na baada ya hapo Nape huyo huyo anahonga muandishi wa habari atoe habari za uongo kuwa wanachama 300 wa CDM wamejiunga na CCM, sasa hapo kuna maendeleo kweli au ni kujidanganya na kuzidi kuichimbia CCM kaburi????
 
Mengi yamesemwa lakini muhimu linabakia kuwa CDM inanufaika na wimbi la watanzania wengi kuichukia CCM, na sio kwa sababu watu wanaipenda (na hata kuchukua jitihada ya kuifahamu) CDM.

Chuki ya CCM inasababisha watu waende CDM, sio kwa sababu wanakipenda CDM au kuwa ni chama 'perfect' ila ni chama pekee ambacho wanaona kitaleta changamoto wa CCM. Cha ajabu CDM imelewa na wimbi hili la kukimbiliwa na haifanyi lolote kubadirisha kuwa chama kinachoaminika kitaifa. Kama CCM hawatarudisha mvuto, na CDM kuendelea na ulevi huu, itakuwa rahisi sana kama kitatokea chama kingine chenye sura ya kitaifa kikanufaika na mtaji huu wa wanachama ambao CDM imefanikiwa kuwahasamisha.

Inshort wananchi wana imani na Chadema.
 
Kamanda,Tumaini Makene...hakika nimekukubali! yaani nimesoma coment yako hapo juu na nikakiri
kuwa kweli CDM wanavichwa makini. Kama usemayo hapo juu ni ya kweli,basi CDM ni chama makini
na kina viongozi makini...All the best mikoa ya kusini

Inatia moyo sana kusoma coments za watu wenye kutaka mabadiliko ya kweli, all in all tuna waombea kwa Mungu viongozi wetu wa chadema Mungu awape hekima na ufahamu wajue yawapasayo kufanya ktk nyakati hizi ambazo wananchi wamewaamini UMOJA NA MSHIKAMANO WA KWELI toka viongozi ngazi ya juu mpaka chini wawe na wimbo mmoja wa kuleta mabadiliko ktk nchi yetu na kuondoa huu uchumi unao kua ktk makaratasi ya watawal.
 
Ni namna gani CDM inaweza kujipanga kwa ushindi? Very simple...

CDM iajiri makatibu wa wilaya katika wilaya zote za Tanganyika, I mean Tanzania bara, ambao chama kiwalipe mishahara wawe watendaji wa full time na preferably young graduates. Hawa watafanya kazi za kila siku za chama, hasa uenezi, M4C ijitahidi kuchangisha fedha za kuwalipa hawa jamaa na kuwatafutia usafiri ili mwisho wa siku hawa ndio waje kuwa maafisa wa idara muhimu za serikali ikiingia madarakani. Makatibu hawa wa wilaya wapewe malengo ya kuhakikisha kuwa CDM inasimamisha mgombea katika kila kitongoji kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na mgombea udiwani katika kila kata ktk uchaguzi wa 2015. Kwa kufanya hivyo CDM itakuwa imefika kila sehemu ya nchi na actually hii ndio mbinu ya ushindi wa ccm kwa vile mgombea wao ananadiwa katika kila kijiji na kata. Wenye uchungu na nchi hii tuko tayari kuchangia mabadiliko, tunataka future nzuri ya watoto wetu.
 
Kikubwa ninachokiona ni kweli CDM kuna kazi inafanyika lakini tukubaliane kuwa bado haitoshi na hili si jukumu la viongozi wa kitaifa peke yake. Sawa kama viongozi wa kitaifa wakifika mahali kuna mapokeo hayo mazuri wakiondoka inakuwaje? Ni vema sasa kila mpenda mageuzi viongozi wa kitaifa wakiondoka, tuliobaki huko tuendeleze moto kwa nguvu katika kutoa elimu ya uraia n.k.
Kuna maeneo mengi ambayo kiukweli viongozi wa kitaifa hawajaenda lakini kuna kazi kubwa inafanyika, mf. Iringa, Mh. Nyimbo anafanya kazi kubwa sana, Wilaya ya Mbozi kuna maendeleo makubwa sana, lakini kwa ujumla ni vema mikakati ikaongezeka hasa kuendelea na suala la kuamsha umma kutambua haki zake kama ambavyo CDM wanaendelea kufanya.
Umhimu wa hili jambo ni kwamba vyama vitapita lakini Tanzania itabaki, hivyo CDM wakielimisha umma na watakapochukua madaraka watakuwa na umma ambao kwa kiasi unauelewa, hivyo nao watatakiwa kufanya kazi vizuri wakichemsha umma huohuo utawahukumu.
Kwa wale wote wanaopenda mageuzi huu ni wakati wetu sasa kurudi chini huko tulikotoka ili kusaidia katika ujenzi wa misingi bora kwa watu wa chini, hii kazi tusimwachie Heche, Mbowe, Slaa na viongozi wengine wa kitaifa
 
Tumaini, Arumeru mashariki ni mfano wa hali ilivyowilaya zote nchini au inawakilisha kama asilimia ngapi ya hali ilivyo?

Mkuu MM

Hili ni swali mwafaka kabisa. Fupi lakini kubwa lenye kutaka maelezo, tena si maneno ya juu juu, ya kina. Naweza kusema ungechelewa kuuliza mtu yeyote makini angeuliza, hasa baada ya mchango niliotolea mfano huo wa Arumeru Mashariki. Lakini kutoa exactly computation ya kujibu kwa ufasaha swali hili ni kuanika mikakati muhimu sana ambayo bado iko kwenye pipeline...jikoni bado kuipuliwa. Remember it is a war.

Lakini kwa manufaa ya mjadala, itoshe kusema kuwa hali niliyoitolea mifano iko vile vile katika maeneo mengi sana ya Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (ikiwa ni manufaa ya ile operesheni kali sana ya vijiji vya mikoa 6, Njombe, Katavi, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa). Sitaki kuzungumzia Kanda ya Kaskazini hapa kwa makusudi kwa sababu I dont want to talk about the obvious.

Kiuhalisia, mfano wa maeneo ya vijijini ya Arumeru Mashariki ni reflection ya maeneo mengi sana kwa sasa. Kanda ya Ziwa is as Kanda ya Kaskazini...totally liberated. Juzi nikiwa na Godbless Lema alipotu-join kwenye ziara ya Katibu Mkuu alikiri kuwa Kanda ya Ziwa is so hotter kuliko hata Kanda ya Kaskazini, isipokuwa the latter is advantaged kwenye publicity.

Sasa tunaelekea Kanda ya Kusini, ambako kumekuwa na demand kubwa kweli. Ofcourse mambo yanaweza yasiwe sawa kama mtu akiamua kufanya comparison. Lakini mkoa kama wa Lindi, tuna madiwani. Huwezi kushinda ngazi kama ya madiwani kama chama hakipo strong, kwa maana ya uongozi. Huwezi kushinda wajumbe, wenyeviti wa vitongoji au kumiliki halmashauri ya Kijiji kama ilivyo maeneo mengi ya Kanda ya Ziwa iwapo hakuna uongozi imara katika ngazi ya chini.

Ukiona mahali inafikia hatua DED (huko Sengerema, Buchosa) anaogopa kuitisha uchaguzi kwa sababu katika kitongoji fulani au kijiji fulani CCM wameogopa hata kuchukua fomu kwa sababu wanajua watashindwa kwa sababu wanakijiji na wanakitongoji hawataki kusikia habari yao, hutegemei kuwa mahali hapo hakuna wanachama imara chini ya uongozi wa chama makini, unaowatisha watu wa upande unaotishika.

Niweke wazi kitu kimoja tu kwa sasa. Kuna mwitikio mzuri sana wa kusimika misingi (ndiyo ngazi ya chini kabisa ya CHADEMA, lakini ya muhimu sana kwa sababu ndiko kwenye watu) na matawi (yaliyo hai, uhai ni vikao) kama moja ya masharti ya kupima utendaji kazi wa viongozi wa mikoa, wilaya, majimbo na kata. Nyanda za Juu Kusini wako mbele sana katika hili. Maagizo ya Waraka wa Katibu Mkuu.

Watu wanalazimika kufanya kazi kweli kweli kwa sababu kubwa mbili; ni sifa kubwa kuwa kiongozi wa CHADEMA kisha unachapa kazi kama viongozi wako wa taifa kuwatumikia watu, pili ukizembea unashughulikiwa kweli kweli maana watu wanahisi unawavuta mashati kwenye kasi ya kusaka mabadiliko ya kweli na wanakuona unafanya kama viongozi wa kile chama cha zamani. Nimeiona hii vijijini juzi kwenye ziara ya Katibu Mkuu kujenga na kukagua uhai wa chama.

Poleni kwa majibu marefu.
 
chadema+10.jpg

Kuna kasi ya ajabu tunayoishuhudia ya mwamko wa wananchi waliofunguliwa kuikataa CCM. Karibu kila kona ya nchi makundi ya mamia ya watu wanajitokeza pasi ya hofu wala utata kusema wanaikataa CCM na mambo yake yote. Baada ya mabadiliko nusunusu na hasa baada ya mjadala wa Bungeni kuna watu walitarajia kuwa wananchi watatulia lakini ndio wanazidi. Kuna wimbi la mwamko huo ambalo sasa linatangulia mikutano ya viongozi wa kitaifa wa CDM; viongozi wa mahali (local leaders) na wa sehemu ambazo hata kwenye ramani ni vigumu kuziona wanazidi kuongoza kuchochea mabadiliko.

Umebakia mwezi kama mmoja tu kabla ya kikao cha Bajeti hakijaanza ambapo viongozi wa kitaifa wengi watakuwa wamebanwa Dodoma; je nini kitaendelea wakati huo? Najiuliza mwamko huu yaweza kuwa umetangulia mwendo wa viongozi wa kitaifa - yaani wananchi wameamka na wanatangulia wao kuleta mabadiliko?

Swali la msingi ambalo linahitaji fikara zaidi ni ninihutokea baada ya maandamano na watu kurudisha kadi na shangwe na nyimbo za kufurahia? Nini hutokea baada ya viongozi wa kitaifa kuja na kuondoka; wakifanya mikutano yenye hamasa kubwa? Nini kimetokea Kiteto, Biharamulo, Buchosa, Tarime, Mwanza, Arusha, Songea, Mbeya, Iringa, Mbozi, Magu, Kirumba, Kiwira na kwingine huko kote? Baada ya kurudisha kadi na baada ya viongozi wa kitaifa kuondoka nani anaangalia hawa ambao 'wamekata shauri' kuikataa CCM na kukubali CDM kuwa tumaini leo?

Je CDM inayo miundo mbinu ya kutosha na ya kisasa ya kudumisha (sustain) mwamko huu kabla ya CCM hawajaanza counter attack - na kweli inakuja? Ikumbukwe kuwa baraza la mawaziri lilivyobadilishwa kimsingi limeweka makada mahiri wa chama kwenye nafasi nyeti. Ukiangalia wizara wote ambazo watu wake wamebadilishwa zote zimewekwa makada wa chama cha Mapinduzi kwa kile ambacho nakiita ni 'strategic preparation before war". Ni sawasawa na vikosi vya majeshi vinavyo amass kwenye eneo kabla ya kuleta mashambulizi.

Ninachoweza kukiona kutoka mbali ni kujipanga huku kwa vikosi vya CCM chini ya makamanda wapya na watakapoanza kurudisha majibu kuna watakutwa off guard. Mabadiliko ya Sektretariati ya CCM yanayotarajiwa kuja wiki ijayo utakuwa ni mwendelezo ya kujipanga huku na CDM kama wasipoangalia watajikuta wanajibu (react) na kulazimishwa kwenda kwenye kujitetea (defensive positions).

CCM watakapoanza kujibu mashambulizi hakutakuwa na huruma; hata mtandao wetu huu wa JF na mfumo wake wa kufanya kazi utakiona cha moto kwani watawala hawatoacha waende kwenye uchaguzi mwingine mkuu mitandao kama hii ikiwa kama ilivyokuwa kabla ya 2010. Hili nina UHAKIKA nalo wa kutosha. CDM ikitegemea nguvu ya wananchi tu kuisukuma inaweza - isipoangalia - kujikuta ikiwa imebanwa katika kuzunguka 'mlima huu'.


CDM ifanye nini basi? au isubiri liwalo na liwe kwa sababu 'wananchi wanaipenda'?

Hilo nimeliona mzee mwanakijiji, ninampango ambao ni draft tu, na hivi punde nimeufikisha kwa uongozi wa CDM, ukizingatiwa naamini ni sehemu ya majibu ya swali lako
 
Mengi yamesemwa lakini muhimu linabakia kuwa CDM inanufaika na wimbi la watanzania wengi kuichukia CCM, na sio kwa sababu watu wanaipenda (na hata kuchukua jitihada ya kuifahamu) CDM.

Chuki ya CCM inasababisha watu waende CDM, sio kwa sababu wanakipenda CDM au kuwa ni chama 'perfect' ila ni chama pekee ambacho wanaona kitaleta changamoto wa CCM. Cha ajabu CDM imelewa na wimbi hili la kukimbiliwa na haifanyi lolote kubadirisha kuwa chama kinachoaminika kitaifa. Kama CCM hawatarudisha mvuto, na CDM kuendelea na ulevi huu, itakuwa rahisi sana kama kitatokea chama kingine chenye sura ya kitaifa kikanufaika na mtaji huu wa wanachama ambao CDM imefanikiwa kuwahasamisha.

Pole kamanda.
 
Nadhani hoja ya MM ni kuwa baada ya hamasa hii kuna-follow up ya wale wenye kiu ya mageuzi kuamini kuwa kule walikochagua kwenda ni makini? Unapokuwa na watu maarufu kama Dr Slaa, Tundu, Zitto, Halima wakafanya mkutano na kupokea wanachama 1000, je kuna utaratibu wa kuhakikisha kuwa hao 1000 wanakifahamu chama, wanashiriki katika kukikuza na kukilea chama? Kama hawaoni mabadiliko watajiuliza je wamefanya uamuzi sahihi!

Mkandara: Nakubaliana sana na hoja zako. Ninachoweza kuongezea ni kuwa CDM lazima wafanye kitu. Kitu hicho ni kuzidi kujiimarisha huko vijijini na kuhakikisha wale walioona mwanga basi wanakuwa sehemu ya mabadiliko ili wabadili wengine.

Ngaliba Dume: Hakika umesema kitu ambacho wengi hawataki kukisikia. Nashukuru umekiona hicho kama ninavyosema siku zote. Mtandao wa CDM kitaifa una walakini. Kuna 'disorganization' na hili lazima walifanyie kazi. Nadhani kuna mtafaruku uliojificha na ni lazima waufanyie kazi. Vinginevyo shangwe za NCCR tunazikumbuka, CUF tunazikumbuka mengine ni hadithi.

Tumaini: Sikubaliani kuwa kuna mtandao katika wilaya zote. Sample yako ya Arumeru si nzuri. Tayari ina bias kwasababu Arusha ni ngome ya upinzani kama ilivyo Mbaya na Mwanza au Mara.
Jiulize kama utachukua sample Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani na Mtwara utapata matokeo unayotueleza?
 
Ni namna gani CDM inaweza kujipanga kwa ushindi? Very simple...

CDM iajiri makatibu wa wilaya katika wilaya zote za Tanganyika, I mean Tanzania bara, ambao chama kiwalipe mishahara wawe watendaji wa full time na preferably young graduates. Hawa watafanya kazi za kila siku za chama, hasa uenezi, M4C ijitahidi kuchangisha fedha za kuwalipa hawa jamaa na kuwatafutia usafiri ili mwisho wa siku hawa ndio waje kuwa maafisa wa idara muhimu za serikali ikiingia madarakani. Makatibu hawa wa wilaya wapewe malengo ya kuhakikisha kuwa CDM inasimamisha mgombea katika kila kitongoji kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na mgombea udiwani katika kila kata ktk uchaguzi wa 2015. Kwa kufanya hivyo CDM itakuwa imefika kila sehemu ya nchi na actually hii ndio mbinu ya ushindi wa ccm kwa vile mgombea wao ananadiwa katika kila kijiji na kata. Wenye uchungu na nchi hii tuko tayari kuchangia mabadiliko, tunataka future nzuri ya watoto wetu.

Good idea. Ndiyo maana nilisema mapema kabisa kuwa hii itakuwa topic nzuri. Any constructive comments (constructive si lazima ile unayopenda kusikia tu) itafanyiwa kazi. Hiki ni chama cha watu kwa ajili ya maendeleo ya watu.

Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe mara kadhaa amesikika akiwaongoza makamanda katika kusisitiza kuwa chama hiki kiko mikononi mwa Watanzania. Chama cha watu. Ndiyo tumaini pekee kwa sasa kwa Watanzania. Tumaini la wananchi dhidi ya wala nchi.

Tumaini la wanyonge dhidi ya watawala wanyonyaji, tumaini la wapigania haki dhidi ya wanyanyasaji, tumaini la wanaodai uwajibikaji dhidi ya wazembe, tumaini la wapinga ufisadi dhidi ya mafisadi, tumaini la wapinga ubadhirifu dhidi ya watafuna nchi, tumaini la wapinga mfumo na utawala mbovu. Ni tumaini la wataka mabadiliko.

Kucheza na tumaini hili ni kuchezea mstakabali wa wananchi. HAIKUBALIKI. Juzi nikiwa kanda ya Ziwa, Geita, watu wamekataa gari isiwashwe, wanataka wamsukume Dkt. Slaa akaja mtu mmoja karibu na kioo, kutuma ujumbe mzito. "Hiki ni chama chetu, huku usukumani na uzinzani tunaambiwa eti chama cha kabila fulani, hatutaki kusikia habari hizo, atakayekichezea au kutunyang'anya...tutaua mtu." Maneno ya Mwanakijiji wa Kijijini (si wa hapa JF).

Nitawawekea nukuu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa akiwa katika ziara ya kujenga chama na kukagua uhai wa chama katika mikoa mitano, hivi karibuni. Alikuwa akirudia mara kwa mara, almost the same words kwa viongozi wa chini;

“Viongozi wangu naomba mtambue, chama hiki si mali ya mtu, wala si chama cha viongozi, ni chama cha wananchi, ni chama cha watu, ni chama cha Watanzania. Hiki si chama cha kukaa siku nzima kutatua migogoro, ni chama cha kutafakari suluhisho la matatizo mbalimbali yanayowakabili Watanzania. Chadema ni tumaini pekee la Watanzania kwa sasa.

“Hatutavumilia ufisadi, hatutavumilia uzembe, hatutakubali viongozi wanaojali maslahi yao badala ya wananchi, katika hili CHADEMA tutakuwa wakali kwa yeyote hata kama angekuwa ni katibu mkuu, hatuwezi kujifungia kuzungumzia migogoro inayosababishwa na ubinafsi wa watu badala ya kutumia muda huu kuzungumzia kero na maendeleo ya watu."

 
Kwa watu walioishi enzi ya chama kimoja watakubaliana nami jinsi CCM ilivyokuwa ikipendwa na kuaminiwa na jamii. Watu walikuwa tayari kukilinda chama, kilikuwa mioyoni mwa watu. Chama kiliwajali wananchi wa hali ya chini kiliwasikiliza na kuwaheshimu. Kifupi chama kilikuwa ni cha wananchi na wananchi walikuwa ni wa chama, ilikuwa vigumu kuwatenganisha wananchi na CCM.

CCM ya leo si ile ya miaka ya 80s, leo kimejitenga na wananchi (makabwela) ambao ni wengi chama hakiwaheshimu tena kimejiunga na matajiri (mabwanyenye) wachache. Makabwela wanajiona kama yatima hawana msemaji wa kuwasemea matatizo wao. Polisi wanawabambikizia kesi, watoto wanakosa karo, hospitali hakuna dawa, watu wananyang'anywa ardhi yao, hakuna mtu anayeona machozi yao. Wamebaki hawana kitu cha thamani, walichobaki nacho ni mapenzi yao ambayo CCM hawawezi kuwapoka. Wanajiuliza wampe nani, wametafuta chama ambacho angalau kitawasikiliza na kuwasemea matatizo yao wamegundua ni Chadema.

Nina hakika CCM wanajua walipokosea wanaweza kuparekebisha kama wakitaka, ila kwa hali ilivyo sasa ndani ya chama ni ngumu sana kwao kuweza kujikosoa wenyewe lazima wakosolewe. Kama tulivyoona juzi kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri bila shinikizo kutoka nje wasingejikosoa. Kwa bahati mbaya sana nikiangalia ndani ya CCM hakuna mwenye utashi huo kama waliokuwa nao kina Nyerere, Sokoine nk, utashi wa kuwaonea huruma makabwela kwa njia ya kukosoana. Kila aliyemo ndani yupo kwa maslahi yake na watu wake. Unaweza kusema Kikwete anaweza kuwa na mawazo hayo lakini hana uwezo akisimama kama yeye.

Kwa hiyo hili wimbi la wanachama kukikimbia chama litaendelea si kwa sababu Chadema kimewafanyia nini wananchi bali CCM haifanyi inachotakiwa kuwafanyia wananchi. Vuguvugu hili halitarudishwa nyuma kwa vitisho, wala kwa CCM kuwabeza CDM waonekane hawafai bali ni kwa CCM kujiangalia walipokosea na kurudi kwa wananchi.
 
Mh. Mwanakijiji,

Kujipanga kwa CCM:
Leo hii (currently) tunasoma na kusikia "wasifu" wa wateuliwa mbalimbali wa Rais. Mfano wale ma-DC wapya wawili toka Singida aliowataja Mh. Lissu. Humu tumesoma (tutaendelea kusoma) watu wa hovyo kabisa ambao wamepewa fadhila kwa MFUMO na UTAMADUNI wa CCM. You know pretty well kuwa Serikali hii iko kwa ajili ya CCM and not vice versa.

Ninavyo yaangalia makundi haya matatu:-

1) CCM - they have everything to loose. Not only power (the means to national cake) but it's very life. Potentially CCM is aware that outside "that pond" stands no chance of them staying alive.

2) CDM - of coz they have everything to win simply because both history and factors on ground states so.

3) Wananchi - they're the most important players. The thing is they've come of age and realized their importance not only to an outcome but to their very wellbeing. So they have massive interests in it and have resonated to put their mark.


I agree with us going critic in constructive way. Only we need to balance with a bit realism....and of coz patience.
 
I salute you guys who by one way or another have contributed to this thread.....Hakiki Jf ina great thinker....of course kadri nilivyo kuwa ninasoma ndiyo nilijikuta kuwa I HAVE NOTHING TO ADD. ALMOST guys have said all of what I would expect to say......Big up.....!!!!!!
 
Back
Top Bottom