Mwamasika:Kanisa liligomboa Watumwa Bagamoyo kwa fedha zake.

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,663
..I never knew about this.

..hivi kuna wana-Historia wanaoweza kutuhabarisha zaidi kuhusu matukio kama haya ktk maeneo mengine ya Tanganyika.

Askofu Mwamasika said:
Kanisa likiona watu wanataka kurudi kwenye utumwa katika nchi yao lazima liseme, nawataka wanasiasa waelewe kwamba hata utumwa katika nchi hii pale Bagamoyo haukuondolewa na wanasiasa, utumwa uliondolewa na wamisionari waliokuja kufundisha neno la Mungu, tena walifanya mambo ya ajabu kwa kununua watumwa kwa fedha zao ili waachiwe huru, na wao wakaenda kuwafundisha kusoma na kuandika na baadaye wakawa maketekista waliorudi kufundish watu, lazima tujue historia,
 
Joka kuu, mbona hii ni common knowledge nadhani tulikuwa tunafundishwa katika historia kama si darasa la sita na la saba basi ni mwanzoni mwa sekondari kwa sie tuliosoma zamani. Nikifikiri sana naweza hata kukumbuka baadhi ya majina ya wamisionari waliohusika. Lakini cha muhimu hapa ni kuangalia context aliyoukuwa akiizungumzia askofu, tuna hiyo sehemu tu lakini hatujui nia ya hayo mazungumzo ilikuwa ni nini, kama nia ni kuleta makanisa na misikiti kuchangia katika kuweka mikakati serikalini, binafsi nasita kidogo maana kuna watu wegine ambao hawamo katika misikiti wala makanisa hivyo haitakuwa vyema kuchanganya dini na serikali.

Nimekumbuka mmoja wao ni William Wilberforce, alikuwa ni evangelist tajiri hivi.
 
Last edited:
Sisi enzi zetu tulifundishwa kuwa wamissionari waliamua kukomesha biashara ya utumwa kwa sababu biashara hiyo ilikuwa imepitwa na wakati baada ya mapinduzi ya viwanda (industrial revolution). Utaratibu ukawa badala wa watu weusi kufanya kazi huko ulaya waafrika walime mazao afrika na ulaya ziende bidhaa. Ndio maana baada ya biashara hiyo kukoma tukapata akina carl peters waliowadanganya akina chief mangungu na mikataba yao feki ( ambayo injirudia sasa hivi) na baadaye kuanzaishwa dutch ost africa company( not sure about the spelling) na eventually kuja kwa serikali (colonisation)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom