Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Polisi wa tanzania wana leseni ya kuua.
Hata usipokuwa jambazi wanakuunganishia tu kuwa ulikuwa jambazi na wamekufukuza toka posta hadi mbezi kwa msuguri huku mkirushiana risasi,
wakati ukweli ni kuwa wewe ulikuwa umetoka kibaruani na polisi wamekuvizia ili wamwage damu yako.
Mwaka jana miezi karibuni na mwishoni, mfanya biashara maarufu tundduma aliuawa na polisi kwa kusingiziwa kuwa ni jambazi.
Baada ya kifo chake wananchi wa tunduma walifanya sana fujo hadi kikosi maalum kutoka mbeya mjini kikatumwa tunduma.
Baada ya mazishi hamna hatua yoyote polisi waliyoichukua dhidi ya wauaji na huo ukawa ni mwisho wa mchezo.
Police need to be extra careful katika hili, still polisi wa Tanzania siwaamini intelijinsia yao.
Hawa jamaa nitawaamini tu wakifumua fumua mifumo yao ya zamani na kuongeza nguvu kwenye upelelezi wa kisasa.
Ok, how do we know those guys were robbery? if were robbery, si ni kazi yao wanalipwa mshahara , sherehe ya nini????
manesi wote nao wakichoma sindano wafanya sherehe!