Elections 2010 Mwalimu wa Nyerere ataka CCM iadhibiwe

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234


Mwalimu wa Nyerere ataka CCM iadhibiwe

Na George Marato

Mwalimu aliyemfundisha baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika shule ya msingi, amesema adhabu pekee ya kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kuendesha nchi katika mazingira ya rushwa na kutojali wazee ni kukinyima kura katika uchaguzi wa mwishoni wa mwezi huu.

Mwalimu huyo, James Irenge, mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 120, anasema CCM imekumbatia rushwa na kwamba haijalai hata wazee waliotumikia taifa kwa uadilifu.

“Kukinyima kura ndiyo itakuwa njia sahihi ya kumuenzi Nyerere,” anasema Mwalimu Irenge alipohojiwa na mwandishi wa makala hii, nyumbani kwake mjini Musoma, huku akichuruzika machozi.

“Kwa vile dunia nzima sasa inatambua kuwa CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi tena: kwamba hakijali watu wake; ni vema wanaojiita wazee wenye busara, ambao hawajapata doa la wizi wa mali za umma, wakajiondoa ndani yake mapema,” anasema Mzee Irenge.

Mzee Irenge alikuwa mwalimu wa Nyerere katika shule ya msingi Mwisenge ya mjini Musoma, mkoani Mara.

Anasema alimfahamu Nyerere mwaka 1934 wakati alipokwenda kuanza darasa la kwanza katika shule hiyo, na mwaka 1935 alimfundisha darasa la tatu ikiwa ni baada ya kuvukishwa darasa moja kutokana na ufahamu wake mzuri darasani.

“Alikuwa na ufahamu mkubwa sana, sema akili, mpaka wakamvusha darasa na mimi nikaanza kumfundisha darasa la tatu mwaka 1935,” anakumbuka Mwalimu Irenge.

Mwalimu Irenge alistaafu mwaka 1970. Ana watoto 12 na wajukuu 27. Kwa sasa anaishi Mwisenge, mjini Musoma. Anasema serikali imeshindwa kumlipa kiinua mgongo stahiki kwani tangu alipostaafu, amekuwa akilipwa pensheni ya sh 200 kwa mezi.

Amesema anashangaa kuona viongozi wa siku hizi hawathamini hata wazee wakati Baba wa Taifa alikuwa anapenda sana kuongea na wazee ili kujua matatizo yao na hata kuelewa ni wapi anakosea katika utawala wake.

“viongozi wetu siku hizi wamekuwa na tama, tofauti na wakati wa Mwalimu Nyerere. Kwa mfano, wizi wa mamilioni ya shilingi uliotokea Benku Kuu na mikataba mibovu inayofanywa na serikali, ni kipimo tosha kuwa serikali haiku makini,” ameeleza.

Mzee Irenge anasema lengo la CCM lilikuwa kwasaidia wakulima na wafanyakazi katika kuendeleza taifa lao, lakini kwa sasa chama hicho kimekuwa cha wafanyabiashara, kitu ambacho Mwalimu hakukipenda.

Anasemmma kwa sasa hakitaki tena chama hicho kwani siyo chama alichokitaka Baba wa Taifa. “Enzi za Nyerere hakukuwa na matumizi ya fedha wakati wa kutafuta uongozi, lakini hivi sasa sifa kubwa ni fedha,” anasema kwa sauti ya kusikitisha……………………


…….Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo.
 
Na JK anapokutana na wazee, kikubwa ni kwamba yeye ndiye anakuwa mzungumzaji mkuu na kutukana wafanyakazi. Hivi huyu hawezi kukaa na wazee kupata mawazo na busara zao? Yeye daima na wahindi tu?
 
...Mzee Irenge anasema lengo la CCM lilikuwa kwasaidia wakulima na wafanyakazi katika kuendeleza taifa lao, lakini kwa sasa chama hicho kimekuwa cha wafanyabiashara, kitu ambacho Mwalimu hakukipenda.

Anasemmma kwa sasa hakitaki tena chama hicho kwani siyo chama alichokitaka Baba wa Taifa. “Enzi za Nyerere hakukuwa na matumizi ya fedha wakati wa kutafuta uongozi, lakini hivi sasa sifa kubwa ni fedha,” anasema kwa sauti ya kusikitisha……………………


…….Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo.

Mwl. Nyerere alikuwa ni mjenga hoja hakuwapa mwanya watu wenye uwezo wa pesa kushika madaraka na ukihitaji madaraka na unapesa zako lazima ujieleze umepatawapi hiyo pesa? na hapo ndipo wenyepesa hawakutaka kabisa kujiingiza kwa siasa aliliona hili and that was only way kupunguza mianya ya rushwa na kuwepo uongozi na viongozi kutimiza wajibu wao kama viongozi na hapo ndipo miiko ya uongozi inakuwepo kwani hamjiulizi kwani Azimio la Arusha lilipingwa kwa hali na maali?
 
Swala msingi Shemeji wazee anaokutana nao wanakuwa wameshachakachuliwa na system hiyo ndio so... wapo wazee ambao walikubali kuwa maskini mpaka leo kwa kuwa waadilifu kwa matumaini ya pensheni zao za haki zingewasubirishia mauti zao lakini wapi....pensheni inaliwa na mchwa...wapiiii....heshima yao imporwa na kuonwa wazembe ambao hawakujua kutumia nafasi......wapiiii lazima waon'jeshwe misaada ya maji ya pilipili kutoka ulaya kwenye yali magari ya kina muraaaa......wapiiii lazima waone vijana wasivyo na nidhamu kuwapiga babu zao virungu kumbe wao ndio waliowawekea mazingira ya kusoma na kuupata umuraaaaaaaa.
Kuna jambo moja lilobaki ni kurudi pale tulipokosea njia na kugeuka!!!! Hata yeye Genius Mwalimu Professor, Dr Nyerere Nyerere aliliona hili CCM sio baba yake wala mama yake siku yeyeyote angeweza kuibwaga....
 
Back
Top Bottom