Mwalimu v/s nesi

Marandura

Senior Member
Jul 21, 2011
105
11
Wana JF naombeni ushauri wenu kati ya hawa (mwalimu,nesi) ni yupi anafaa kuoa? & why?
 
Wana JF naombeni ushauri wenu kati ya hawa (mwalimu,nesi) ni yupi anafaa kuoa? & why?

Kwani unaoa kazi zao!? Si unamuoa yule uliyempenda kimaumbile na tabia zake pia unaziona zinaendana na maadili yako? au ni aje Mkuu?
 
Angalia tabia kaka na wala siyo unaangalia cheo
 
Nimeshindwa kupata connection kati ya professional na kuoa
Sijui kama jamaa anaoa professional au anaona mtu kwa mapenzi yake na upendo wa wake kwa muhusika
 
Siyo ivyo wanajamii mm nina mchumba ambaye ni nesi ila izi shift zake za night zinaniboa kweli. Na ndo maana nikaomba msaada wenu au ni mtafute teacher
 
Kwani si maelewano ndani ya nyumba na kazi zake mkuu. We tulia nae uone ni nini mnajipanga kwa ajili ya maisha yenu achana na masuala ya shifti
 
Siyo ivyo wanajamii mm nina mchumba ambaye ni nesi ila izi shift zake za night zinaniboa kweli. Na ndo maana nikaomba msaada wenu au ni mtafute teacher

Hilo ni tatizo, wanaume wengi hawapendi wake zao wafanye kazi za shift ambazo zitasababisha baadhi ya siku wasilale nyumbani. Jaribu kukaa chini na mhusika kulijadili hili kwa kina ili muone mtalitatua vipi.
 
Imagine na upande wa pili kama wewe ungekuwa uko shifti si angelala nyumbani peke yake.
 
chagua nessy maana huyo mwalimu hana msaada huyo nessy ndiyo akitaka kujifungua hamtapata gharama
 
Ingelikuwa wanaume wote wanakataa manesi kisa shift za usiku ingekuwaje? Acha ubinafsi kaka, hata mwalimu kuna wakati atakwenda kusahihisha mitihani utamkataza kisa baridi ya usiku? Labda kama hujampenda kiukweli unamdanganya tu.
 
Mwana cha kukushauri sababu unateseka na baridi
piga chani oa mama wa nyumbani aka goli kipa
shida za baridi zitaisha lkn hao wengine hawakufai
<br />
<br />
Muda huu naandika hii thread yupo job. Napigwa na barid mbaya mablanket hayanisaidii. We unasema sio issue
 
Back
Top Bottom